Karibuni Dodoma wajumbe wa mkutano mkuu maalumu wa CCM Taifa , 29-30 Mei 2025

Karibuni Dodoma wajumbe wa mkutano mkuu maalumu wa CCM Taifa , 29-30 Mei 2025

Karibuni Dodoma wajumbe wa mkutano mkuu maalumu wa CCM Taifa , 29-30 Mei 2025

KILIO MAKATIBU WA CCM WILAYA YA MKURANGA.

Chama Makao Makuu, mtusaidie SISI makatibu wa CHAMA na Jumuiya zake wilaya ya Mkuranga. Tumechoka kutumika.

Mbunge wetu anatulazimisha kufanya mambo kinyume na utaratibu wa Chama Chetu ili kumtafutia kura.

Mara kadhaa amekua anatulazimisha Kuwaita wajumbe kutumia kivuli cha semina elekezi, kumfanyia kampeni (yeye au mkewe) na kuwatisha kua atawashughulikia wanaompinga kutumia mamlaka yake.

Sasa TAR_*EHE 03.06.2025, Ametulazimisha, kuwaita wajumbe wote wa kamati za Utekelezaji kaka zote 25 na matawi yote 247 ya wilaya ya Mkuranga, watakua wajumbe zaidi ya 5000*_, kwa ajili ya semina elekezi, zote zifanyike siku moja na kila jumuiya ktk ukumbi wao. Lengo Kuu ni kuwapa maelekezo wamchague yeye uchaguzi ujao wa 2025, na apate fursa ya kuongea nao na kuwapa pesa ili awashawishi wamchague tena.

Mafunzo gani ya watu zaidi ya 5000?

*Kama hiyo haitoshi amekua anatulazimisha kupeleka viongozi na wanachama wale anoahisi hawamuungi mkono takukuru*_. Hadi sasa tushapeleka zaidi na wanachama/viongozi wa Chama Chetu zaidi 50 takukuru, kinachofanyika huko ni kutishwa na kutakiwa wamuunge mkono mbunge uchaguzi ujao, kwani yeye kiongozi Mkubwa na atawashughulikia wale wote wasiomuunga mkono.

Hali hii inaleta MPASUKO NA CHUKI KWA CHAMA CHETU WILAYA MKURANGA.

Mtusaidie.
 

Attachments

  • IMG-20250529-WA0002.jpg
    IMG-20250529-WA0002.jpg
    33.4 KB · Views: 19
Janja janja ya chama dola kongwe watu wamesombwa kujaribu kurekebisha makosa ya tarehe 19 January 2025

29 Mei 2025
Yaleta mazingaombwe ya kijiditali

Ukiachana na wasanii maarufu walioanza kupanda kwenye jukwaa kuburudisha wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ulioanza leo Alhamisi, Mei 29, 2025 jijini Dodoma, kivutio kingine kilichowapagawisha wajumbe wa mkutano huo ni uwepo wa maroboti mawili nje ya ukumbi.Maroboti hayo yaliyonakshiwa kwa rangi za kijani na njano zinazoakisi rangi za chama hicho tawala, huku kifuani yakiwa yameandikwa Kauli Mbiu ya ‘Kazi na utu. Tunasonga mbele’. Ambayo ndio itatumika wakati wa kunadi sera za kuomba ridhaa ya Watanzania kwenye uchaguzi mkuu wa 2025

View: https://m.youtube.com/watch?v=7xFAN6pv6V4
 
Mbona Mkutano Mkuu uliompendekeza mgombea Urais ulikwishafanyika tena Mkutano Mkuu wa nini tena?.

Janja janja ya chama dola kongwe watu wamesombwa kujaribu kurekebisha makosa ya tarehe 19 January 2025

Maboresho ya katiba ya CCM
TOKA MAKTABA:

29 Mei 2025

Samia - mikutano ile isikiuke katiba ya chama isiwe mikutano kinyume na katiba ya Chama cha Mapinduzi​

Katika siku ya kwanza ya mkutano mkuu maalum wa Chama cha Mapinduzi Mei 29, 2025, chama hicho kimefanya mabadiliko mengine ya Katiba yake:

View: https://m.youtube.com/watch?v=ZGdxUSCJLcA

transcript/ neno kwa neno:


Rais Samia: CCM Oyee ! Haya waheshimiwa wajumbe sasa tunaendelea kwenye kipengelee kama inavyoonekana kwenye ratiba marekebisho madogo sana ya katiba yetu. tumeleta marekebisho madogo ya katiba yetu ya chama cha mapinduzi ya mwaka 1977 toleo la Januari mwaka huu 2025 yanayopendekezwa katika waraka huu na yamelenga mambo yafuatayo. La kwanza kama mnavyojua kwamba Chama chetu cha Mapinduzi kina kinaendelea jinsi dunia inavyoendelea.

Ndani ya chama chetu cha mapinduzi sasa tunafanya kazi kidigitali pia na tumefunga mitambo ya kuweza kuwasiliana na mikoa na wilaya au mikoa kuwasiliana wilaya kuwasiliana ah ili kurahisisha utendaji wa kazi.

Kwa hiyo tumekuja na wazo la e-meetings mikutano ya kimtandao ambayo idara ya organizesheni inapendekeza vikao vifuatavyo kwa njia ya mtandao;

  • Kikao cha kwanza ni sekretariati ya wilaya
  • Kamati ya siasa wilaya
  • Sekretarieti ya mkoa
  • Kamati ya siasa mkoa
  • Sekretarieti ya kamati maalum ya halmashauri kuu ya CCM taifa
  • Sekretarieti ya halmashauri kuu ya CCM taifa
  • Kamati maalumu ya halmashauri kuu ya CCM taifa
  • Kamati kuu ya halmashauri kuu ya CCM
  • Halmashauri kuu ya CCM taifa
  • Mkutano mkuu wa taifa.
Sasa hivi vikao vingine tumeviweka kwa kujua kwamba jinsi tunavyoendelea huko mbele tutakuwa tunaendelea kiteknolojia na kwamba katiba yetu inatupa fursa ya kutunga kanuni za vikao hivi.

Lakini kwa sasa tumeanza mikutano na kamati za siasa au halmashauri kuu za siasa za mikoa au za wilaya. Lakini mikutano ile haimo katika maelekezo ya katiba ya chama chetu.

Kwa hiyo tumeamua kuiingiza ili mikutano ile isikiuke katiba ya chama isiwe mikutano kinyume na katiba ya Chama cha Mapinduzi. Kwa hiyo hilo ni pendekezo la kwanza tunalokwenda kulileta kwenu.

Lakini vikao husika hivi vinavyozungumzwa vitafanyika kwa njia ya mtandao endapo tu kuna ulazima au udharura. Vikao husika kwa ngazi ya wilaya na mkoa vitafanyika kwa idhini ya katibu mkuu. Watamjulisha katibu mkuu kwa nini wanafanya kikao kwa mtandao na hii ni kuepusha kutumika vibaya mitandao hii. Hilo ni swala la kwanza.

Lakini swala la pili ni swala la baraza la wadhamini. Sheria ya vyama vya siasa sura ya 258 rejeo la 2019 imetutaka idadi ya mabaraza ya wadhamini wa vyama vya siasa iwe namba isiyogawanyika kwa mbili yaani iwe 3,5, 7, 9,11, sasa baraza letu la wadhamini lina watu wanane.

Kwa hiyo tunapaswa kumwongeza mtu mmoja wawe tisa na hii inakwenda kwa mujibu wa katiba yetu. Kwa hiyo tunaleta ili kuiweka kwenye katiba ili tuweze kuwa na namba kama inavyotakiwa kwenye baraza la wadhamini.

Lakini sehemu ya pili ya baraza la wadhamini katika jitihada zake za kuimarisha uchumi wa kisiasa. Tunatazamia kutumia ushauri wa kitaalamu katika shughuli zake za uwekezaji kwa lengo la kuongeza tija. Kama mnavyojua chama chetu sasa hivi tunazipa nguvu kubwa kampuni zetu za chama ili ziweze kuzalisha kwa manufaa ya chama. Tunajielekeza zaidi kwenye uwekezaji na uchumi. Kwa maana hiyo kwa mtazamo huu ni wakati muhimu wa baraza la wadhamini kuiona, kujiridhisha na kutoa maelekezo kwa miradi itakayobuniwa na ngazi za mikoa na taasisi nyingine kwa manufaa ya chama.

Katika kutekeleza jukumu hilo, baraza la wadhamini la Chama cha Mapinduzi litatoa idhini kwa maandishi. Katiba inavyosomeka sasa, Baraza la wadhamini litatoa idhini, itakasimu imeandikwa itakasimu madaraka hayo kwa kamati za siasa. Sasa ile imechukuliwa kwamba ni automatic kamati za siasa mikoa huko wakiwa na miradi wanamaliza kila kitu bila kuja kwa baraza la wadhamini. Kwa hiyo sasa tunaweka neno kwa maandishi hilo tu basi maneno mengine mantiki iko vile vile. Watakasimu kwa maandishi hii ina maana kamati za siasa sasa bidi ziombe ruhusa kwa baraza la wadhamini na wajibiwe kwa maandishi.

Kwa hiyo marekebisho matatu ni hayo. La kwanza la mikutano kidigitali, la pili namba ya baraza la wadhamini na ya tatu ni kwamba kukasimiwa yale madaraka ya miradi ni kwa maandishi waheshimiwa wajumbe wa mkutano mkuu hayo ndio marekebisho tunayoyawasilisha na kuomba ridhaa ya wajumbe wa mkutano mkuu.

Ridhaa imetolewa? [Anauliza Rais Samia]

Wajumbe: Ndiooo!

Ridhaa imetolewa? [anauliza tena]

Wajumbe: Ndiooo!

Rais Samia: Tunawashukuru sana.

Wajumbe
 
Maboresho ya katiba ya CCM
TOKA MAKTABA:

29 Mei 2025

Samia - mikutano ile isikiuke katiba ya chama isiwe mikutano kinyume na katiba ya Chama cha Mapinduzi​


WaTanzania mlikuwa mnafuatilia Derby ya Kariakoo Simba Vs Yanga, MaCelebrity waliojazana Dodoma 29 Mei 2025 mkashindwa kuona mchezo wa kuigiza wa mwaka uliochezwa ktk Mkutano Mkuu Maalum wa Tarehe 29 Mei 2025 kwa mtindo huu wa kiini macho :

USIPITWE TAZAMA KIPINDI AGENDA | MADA : FAIDA NA ATHARI ZA PROPAGANDA KWA TAIFA
  • White propaganda kutafuta heshima kupitia taarifa za kweli
  • Black propaganda chanzo hakitambuliki na pia taarifa siyo za kweli
  • Grey propaganda ipo katikati baina ya ukweli na uwongo

View: https://m.youtube.com/watch?v=OwLNl_fv_CY

Source : Star TV Habari
 
TOKA MAKTABA:

29 Mei 2025

Samia - mikutano ile isikiuke katiba ya chama isiwe mikutano kinyume na katiba ya Chama cha Mapinduzi​

Chama cha Mapinduzi Mei 29, 2025, chama hicho kimefanya mabadiliko mengine ya Katiba yake:

View: https://m.youtube.com/watch?v=ZGdxUSCJLcA

transcript/ neno kwa neno:


Rais Samia: CCM Oyee ! Haya waheshimiwa wajumbe sasa tunaendelea kwenye kipengelee kama inavyoonekana kwenye ratiba marekebisho madogo sana ya katiba yetu...


25 JULAI 2025
MAKALLA AITA WAANDISHI WA
HABARI

View: https://m.youtube.com/watch?v=Ys036uGy8BM
 
Back
Top Bottom