Karibuni kwenye Kituo cha biblia cha Kanisa Katoliki (KBKK)

Hizi zama ni muhimu Kanisa liwekeze elimu ya Biblia kwa waamini ili waweze kujisimamia. Wakatoliki wengi wanayumbishwa mno kwa kutoijua kweli.

Lakini watu watajitokeza kusoma? Watu wanataka kusoma mambo au kozi ambazo zitawawezesha kuajiriwa.
 
za masiku ni salama kabisa ni salama TUNAMSHUKURU MUNGU

1: ni kama shule/chuo, iyo whatsap ni njia ya kurahisisha mawasiliano na taarifa tu. zaidi kuna namba hapo juu ya muhusika mkuu unaweza itumia ili kujua mengi zaidi.

2: biblia ni kwa wote hivyo wote wanakaribishwa. taifa la Mungu lote bila kujali chochote
 
Hata kama wakiniruhusu nijiunge bure siwezi; hawa ndio waharibifu wa maandiko matakatifu!
ndugu yangu katika kristo kwa nini uneamua kufikiri ivyo ?? au ni nini chanzo cha wewe kujenga mawazo kama hayo ??

tangu lini kutoa elimu juu ya jambo/kitu fulani kukatafsiriwa kuwa ni uharibifu wa jambo/kitu icho ??. au umevumbua definition mpya ya elimu ??
 
Kwa nini unadhani tunastahili kuomba kazi kwenye hiyo taasisi inayofundisha bibilia KIKATOLIKI.
Lengo la Bibilia sio Kujipatia kipato bali Badiliko la Moyo.
Mabingwa wa Bible knowledge walikuwa mafarisayo, na Masadukayo, waalimu na waandishi lakini hawakuona mpango mkubwa wa Wokovu ndani yake wakabaki na Head Knowledge.

Roho mtakatifu mwalimu kiongozi anatosha.
 
Mabingwa wa Bible knowledge walikuwa mafarisayo, na Masadukayo, waalimu na waandishi lakini hawakuona mpango mkubwa wa Wokovu ndani yake wakabaki na Head Knowledge.

Kwa hiyo hivi ninyi Roho Mtakatifu anavyowajalia kuielewa Biblia vilivyo namna hii hamjafikia ubingwa kama Wa Mafarisayo na Madukayo?
 
Hiyo sio taasisi ya kutoa ajira bali ni ya kufundisha Bible...,

Na watakuwepo wabobezi ambao huwezi wakuta humu JF,na hakuna biblia Katoliki hii nimeisikia kwako leo.
 
Kwa hiyo hivi ninyi Roho Mtakatifu anavyowajalia kuielewa Biblia vilivyo namna hii hamjafikia ubingwa kama Wa Mafarisayo na Madukayo?
Yesu aliahidi roho mtakatifu atawaongoza kuishika kweli Yote. Ukuaji wa kiroho wa mtu yoyote sio msabato tu nje ya utegemezi wa roho mtakatifu haishii tu kuwa farisayo bingwa bali akageuka kuwa mwerevu mno lkn moyo bado uko gizani.
Professor wa Bible knowledge sio tu mafarisayo, bali IBIRISI, Aliyatumia kutaka kumuangusha Bwana Yesu Bila hata Kufungua Gombo yalikuwa kichwani.

Sisi tunaamini, Bible knowledge, Kigiriki na Kiebrania au uchimbuzi wowote wa maandiko ni hatua ya hawali kabisa ya Kumfahamu Mungu. Application of truth, Unwavering Obedience of Truth obtained in scripture while dropping down all human opinions and dry religious rituals ndio inaleta tofauti kati ya wacha Mungu na wajuzi wa elimu ya Mungu.
Kama wapo wasabato, wakatoliki au yoyote yule ambaye amegotea kwenye bible knowledge au head knowledge au bibilia kwake ni kama desa Huku Moyoni ni Mchafu anapaswa kutambua bado anasafari ndefu ili haki yake izidi haki ya mafarisayo na masadukayo.
 
Kujifunza kwa biblia kiufasaha...,
mngefanya hilo enzi za zama za giza ambapo bibilia ilisomwa na makasisi na viongozi wa dini tu huku waumini wakisubiri kulishwa bila kuhakiki wanacholishwa ni sasa hivi mngekuwa mbali.

Nawatakia Shule njema,
 
Hiyo sio taasisi ya kutoa ajira bali ni ya kufundisha Bible...,

Na watakuwepo wabobezi ambao huwezi wakuta humu JF,na hakuna biblia Katoliki hii nimeisikia kwako leo.
Katikati ya mwezi ujao, tutaanza kufundisha Biblia Kikatoliki cc mleta uzi
#8
mitale na midimu Aroon 3Angels message na wasabato wengineo mnaojiita wajuzi wa Maandiko matakatifu na wajuzi Wa maandiko ya Daniel na Yohana kuomba Kazi kwenye Chuo husika. Nendeni mkaombe Kazi hata kama ni Part-time kupiga Lectures hapo. Ndiyo nafasi yenu sasa kuonyesha ubingwa wenu katika Teolojia na historia ya Biblia.

cc mchangiaji mwenza.

sio maneno yangu mkuu wangu. hata mimi nimeyaokota humu humu.
Shule njema.
 
ndio inaleta tofauti kati ya wacha Mungu na wajuzi wa elimu ya Mungu.
mpendwa katika kristo "kumcha Mungu /wacha Mungu" na "elimu ya biblia/Mungu" ni vitu viwili tofauti sana. japo vinaweza kukalibiana kadili ya maisha na matamani ya mtu.

kilichopo kwenye uzi sio habari za kumcha Mungu. kama ni kumcha Mungu kuna waisilamu nk wasiomjua roho mtakatifu wala biblia ila ni wacha Mungu kwelikweli kuwazidi wakristo lukuki hiyo ni kwa neema ya Mungu tu. ila kilichpo kwenye uzi ni elimu ya biblia kama zilivo elimu zingine yaani udaktari, enginiering, ualimu nk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…