Karibuni kwenye Kituo cha biblia cha Kanisa Katoliki (KBKK)

Karibuni kwenye Kituo cha biblia cha Kanisa Katoliki (KBKK)

mngefanya hilo enzi za zama za giza ambapo bibilia ilisomwa na makasisi na viongozi wa dini tu huku waumini wakisubiri kulishwa bila kuhakiki wanacholishwa ni sasa hivi mngekuwa mbali.

Nawatakia Shule njema,
Tungekuwa mbali kivipi, kwenye nini..? Kuna anayeweza Shindana kwenye dunia hii na Kanisa Katoliki kwenye mambo ya Biblia...??


Biblia ni mali ya Kanisa Katoliki....utaaanzia wapi kushindana nalo...? Tupo mbele kwenye kila kitu...

Elimu, Afya, Huduma, Mambo ya Kiroho....sisi ndip tunaongoza
 
Hata huyo Yesu kabla ya kimleta Roho Mtakatifu aliwafundisha kwanza wanafunzi wake kwa miaka mitatu....

Unafikiri alikuwa hana uwezo wa kuwashishia siku anaanza ministry yake...?

Roho Mtakatifu kimeshakuwa kichaka au anachukuliwa kwamba yeye ni zaidi ya zile nafsi mbili,Baba na Mwana.

Wameona sasa wameanza kubanwa juu ya mafundisho yao kukosa ukweli wakaona wakimbilie kwa Roho Mtakatifu. Huyo kimekuwa kichaka cha watu kujificha.
 
Hivi, una vyanzo vya kutosha kwamba Yesu hakupitia shule?
kwa sababu wewe ni mpenzi wa mantiki.
1:Familia ya Yesu ilikuwa masikini mno, hivyo wazazi wake wasingeweza kuwa na uwezo wa kulipia shule za marabbi.
2:Elimu ya kiyahudi ya kwanza hufundishwa na wazazi nyumbani hata basics za kidini. Torati 6:7 (Uwafundishe watoto wako), Mfano ni Timotheo mkazi wa mji wa kipagani Listra ambao haukuwa hata na sinagogi na baba yake alikuwa mgiriki lkni Bibi yake mzaa mama Loisi na mama Yake mzazi Eunike. Hivyo maandiko Yesu atakuwa alijifunza kwa wazazi tu.
3😛ia Yesu amekulia nazareti, pale kulikuwa na sinagogi, na kwenye masinagogi kulikuwa na magombo, hivyo kwa mujibu wa kitabu Manners and Customs of Bible time Kuna uwezekano alikuwa anakwenda kujifua pale au anaazima magombo kwenye sinagogi na kwenda kujifua nyumbani.
4: Hii ndiyo Muhimu, Siku alipoenda hekaluni akiwa na miaka 12, Walimu walimshangaa hekima yake na ujuzi wa maandiko kuliko sio tu wanafunzi wa shule ya marabbi hapo bali hadi wakufunzi wenyewe walimshangaa.

karibu kwa maoni
 
Matendo 5.
Kinapingana na maamuzi ya wazazi wa Paulo walioamua kumpeleka mtoto wao kitokea huko Tarso kwenda Yerusalem kufunzwa miguuni kwa mkufunzi na FARISAYO MBOBEZI GAMALIELI, Kiasi cha Kumfanya Paulo naye Kuwa Mbobezi wa maandiko hayo na FARISAYO Sugu mwenye roho mbaya dhidi ya wafuasi wa Kristo.
je , GAMALIELI alikuwa ni muandishi au mfarisayo ?? au alikuwa ni mwandishi na farisayo vyote pamoja ?

je, kila aliyekuwa FARISAYO alikuwa ni mbobezi wa maandiko kwa maana ya kuwa na sifa ya kuitwa muandishi/mwalimu ??

nianakuelewa vizuri sana na ninafahamu unapokwama ni wapi. ninachokizungumzia mimi ni uhalisia kadiri ya taratibu na sheria walizokuwanazo na walizojiwekea wayahudi katika wakati huo.

na unachokizungumzia wewe ni kile tu unachokiana katika maandishi ya biblia yako kitu ambacho uhalisia wake ni mdogo kwa mtu anaetegemea anachokiana tu kwenye mandishi ya biblia.

kiujumla vikundi vilikuwa vingi sana lakini ni vikundi vichahe tu vinavoonekena kwenye biblia.

waandishi/waalimu hilo halikuwa kundi la kidini yaani dhehebu kama hayo mengine ulioyataja isipokuwa mtu yeyote yule awe mfarisayo, awe msadukayo, awe zeloti, awe mueseni nk hata asiyekuwa na kikundi cha kidini aliweza kuitwa mwandishi/mwalimu/rabbi iwapo aliamua kusomea kazi hiyo mpaka kuhitimu na wengi wao walitunukiwa heshima hiyo ya juu wakiwa na umri wa miaka karibu 40 (ndivo ilivokuwa sheria).

hivyo mpendwa ulipaswa kutambua kuwa kulikuwa kuna kundi kubwa sana la wafarisayo lakini ni wachache sana miongoni mwao waliokuwa na elimu ya kuitwa waalimu/waandishi, kulikuwa kuna kundi la wasadukayo lakini ni wachache sana miongoni mwa hao wasadukayo waliokuwa na elimu ya kuitwa waalimu/waandishi, vivo ivyo kwa waeseni, wazeloti na vikundi vingine.

kwa lugha nyingine ninamaanisha kuwa mtu kuwa mfarisayo, msadukayo, zeloti, mueseni haimzuii yeye kuwa mwandishi/mwalimu/rabi kwa sababu uandishi/ualimu/urabi ilikuwa sio kazi ya kikundi cha kidini ila yeyote aliyakuwa na sifa haijalishi kikundi chake aliweza kuwa mwalimu/muandishi.
Marko 2:18
Nao wanafunzi wake Yohana na Mafarisayo walikuwa wakifunga; basi walikuja, wakamwambia, Kwani wanafunzi wa Yohana na wanafunzi wa Mafarisayo hufunga, bali wanafunzi wako hawafungi?
ndugu yangu katika kristo hao wanaotajwa ktk marko 2:18 kama "wanafunzi wa mafarisayo" ni wanafunzi wa kawaida au wanachama wapya/wachanga katika muktadha wa malengo ya kikundi chao tu kwa maana ya kuwa unapokuwa na kundi fulani lazima uwe na viongozi/wakufunzi wa sheria na taratibu za kikundi husika kwa wanachama wapya. na sio katika muktadha wa kwamba hao wanafunzi wa mafarisyo ni wanafunzi kwa ajili ya ubobezi wa sheria. kwa madai yako itabidi ukiri kuwa hata hao wanaotajwa kama "wanafunzi wa yohane" ni wanafunzi katika muktadha wa ubobezi na utaalamu wa maandiko. na wanaotajwa pia kama "wanafunzi wa yesu" ni wanafunzi katika muktadha wa ubobezi na utaalamu wa maaandiko. kwa maana hiyo wasadukayo walikuwa na wanafunzi/wanacha wapya na walimu wao, wazeloti, waeseni vile vile nk

kwa wafarisayo na waandishi katajwa kwa pamoja mara nyingi: ni kwa sababu idadi kubwa sana ya waandishi /walimuwa sheria walikuwa ni wanachama wa mafarisayo na ambao ndilo lililokuwa kundi kubwa sana na lenye nguvu kubwa na ushawishi (nazungumzia ushawishi wa kidini sio wa kisiasa)

mpendwa sio kila unapoona kwenye bible kumeandikwa wanafunzi basi wewe uelewe kuwa waalimu wao ndio wabobezi/wataalamu wa maandiko matakatifu wanaotajwa kwenye biblia hapo unakosea.

"waandishi " na "waalimu wa sheria" hi kundi moja au ni makundi mawili tofauti ??
 
Hata kama wakiniruhusu nijiunge bure siwezi; hawa ndio waharibifu wa maandiko matakatifu!

Naomba nideclare interest kwanza mimi ni mkatoliki, lakini biashara ya injili wakatoliki ilishatushinda tuwaachie pentecoste na waprostentant! Sisi biashara za shule,vyuo, hospital I n.k ndizo tunazoweza. Kusema ukweli biblia hatuisomi wala hatuijui
 
Hata huyo Yesu kabla ya kimleta Roho Mtakatifu aliwafundisha kwanza wanafunzi wake kwa miaka mitatu....

Unafikiri alikuwa hana uwezo wa kuwashishia siku anaanza ministry yake...?
ahsante
jibu zuri sana ......

la sivyo hata hizi taaluma zetu kama ualimu, udaktari nk au masomo kama physics, math na kemia tungekuwa tunajifungia chumbani na kusubiri nguvu ya roho mtakatifu kama ile ya pentekoste.
 
Jiunge na semina acha kusemea nyuma ya mlango,niliwahi kukuambia kuwa kuna wabobezi wa maandiko matakatifu ambao kamwe huwezi wakuta humu JF au popote pale kwenye mitandao ya kijamii.
wabobezi ndio watu gani mkuu. siwezi kujiunga shule mbili, mimi niko shuleni mwa kristo tangu nilipoamini, graduation ni siku ya kulala mavumbini.
wanatafutwa ambao hawako shuleni.
 
wabobezi ndio watu gani mkuu. siwezi kujiunga shule mbili, mimi niko shuleni mwa kristo tangu nilipoamini, graduation ni siku ya kulala mavumbini.
wanatafutwa ambao hawako shuleni.
We jamaa huwa ni kigeugeu sana,alafu unenavyo sivyo utendavyo...,
Unasema huwezi kujiunga shule mara mbili lkn wkt huo huo unasema elimu ya biblia haishi mpaka utakapoingi kaburini(graduation ni siku kulala mavumbini) you mean bado tunajifunza,unaona ugumu gani wa kwenda kuwasikiliza wakatoliki..????au kwa kuwa ni Wakatoliki...???je zingekuwa zile kambi za wasabato ungeenda ee...????
Wewe unatofauti gani na Mafarisayo..????
 
Kanisa limepitia Nyakati nyingi katika historia yake na kila nyakati ilikuwa na mahitaji yake.

Wakati imani ya Kikristo inaingia miongoni mwa jamii wkt ule wa karne ya kwanza sio kila mtu alijua kusoma na kuandika,kwahyo ilibidi wasomewe na kutafisiriwa na wanaojua kusoma ili Injili ienee kwa kwao,na hata wkt ule wamisionari wanaingia Afrika hususani Tz sio kila mtu alijua kusoma na kuandika na pia ukumbuke kuwa Missionaries walikuja na Injili ikiwa katika lugha ya kigeni kwahyo iliwabidi wasambaze shule kwanza ili kujifunza lugha zao pamoja na mengine kama geography,mathematics nk, ili kuwapa elimu dunia kisha kuwapa elimu ya Mungu.

Mitale siamini kama bibi yako alijua kusoma na kuandika,kwahyo ili kuipata Injili ilibidi atumike mtu kuwasomea na kutafasiri na ukumbuke utafasiri huo ulitoka kwenye lugha ya kigeni kwanza na kuja kwenye lugha za asili,ndio maana nyakati zile walitumika makuhani wa asili ambao tayari walikuwa wameshapata elimu toka kwa missionaries katika kufundisha bible.

Lkn pia sio kosa lako kuandika hivi kwa sababu Usabato umeingia juzi kukiwa tayari watu washaujua Ukristo na pia wengi wao wakiwa wanajua kusoma na kuandika.
Leo Kanisa Katoliki linatimiza miaka 150 ya Uinjishaji hapa Tz yani Missionary wa kwanza aliingia nchi 1868 ambapo ni miaka michache tangu kuasisiwa kwa SDAC duniani.
wasabato hata kama wangeanza juzi.
wanasisitiza na kufundisha yale yaliyopo tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu mkuu.
Wanasisitiza kweli za bibilia zenye umri mkubwa kuliko hata Dunia.

Bibilia inasisitiza watu wasome, ila ikitokea taasisi inataka wasomewe na viongozi ni kinyume na bibilia ndio maana napongeza juhudi hizi za Sala na Kazi za kuwataka msome bibilia kikatoliki angalau.

Maandiko yanapaswa kufundishwa kuanzia nyumbani, Ndilo agizo la Mungu Torati 6, Hutakiwi kuhadithiwa bibilia unatakiwa usome bibilia kuhakiki unachofundishwa na makasisi (waberoya wa kitabu ca matendo)
Timotheo anaandikiwa na Paulo afanye Bidii katika KUSOMA.
Ufunuo inaanza na '' HERI ASOMAYE''.

hivyo nawapongeza kwa juhudi ila mmechelewa, hiyo misisitizo ilianza tangu watunwa Mungu wako Jangwani. Ndio maana hadi kesho sisi wakosefu huwa tunashangaa ni kifungu gani mlitumia kuchoma bibilia na kushughulikia kila aliyeonyesha juhudi kutafsiri bibilia katika lugha za watu husika ili kuongeza spidi ya uinjirishaji. Isingekuwa Bidii za reformers kusingekuwa hata na hiyo Douay .
 
Wazungu walioleta ukristo kuanzia Ukatoliki Na uprotestant na kufundisha Mapadri Na wachungaji wenye PhD za Bible knowledge wanaojua kigiriki na kiebrania kwao ndio wameruhusu ushoga.Nadhani kwa Waafrika Biblia tujisomee tu wenyewe tuielewe tutakavyo Kila mtu kivyake kama wanigeria Na waghana ambao walisusa miaka mingi iliyopita kufundishwa elimu ya Biblia Na wazungu au waliosomeshwa Na wazungu kuwa wanafundisha head knowledge sio spiritual knowledge.Kumjua Mungu Na kujua Biblia ni vitu viwili tofauti.Wazungu wengi wanajua Biblia hawamjui Mungu Na hawana haja naye ndio maana ulaya makanisa yanafungwa watu hawaendi kanisani kabisa pamoja Na elimu ya Biblia kubwa waliyonayo.Kwa anayetaka kuongeza head knowledge ajiunge tu aongeze mistari ya kigiriki na kiebrania kichwani ili apanue head knowledge yake
 
We jamaa huwa ni kigeugeu sana,alafu unenavyo sivyo utendavyo...,
Unasema huwezi kujiunga shule mara mbili lkn wkt huo huo unasema elimu ya biblia haishi mpaka utakapoingi kaburini(graduation ni siku kulala mavumbini) you mean bado tunajifunza,unaona ugumu gani wa kwenda kuwasikiliza wakatoliki..????au kwa kuwa ni Wakatoliki...???je zingekuwa zile kambi za wasabato ungeenda ee...????
Wewe unatofauti gani na Mafarisayo..????
Nimeamua Kujifunza Bibilia kupitia kwa Mwalimu mkuu sio scholars na Marabbi unaodhani ni wabobezi. Ila Maoni yao ninayafuatilia sionhao tu waislam, wabudha wasabato wenzangu, wayahudi, etc.

Kuhusu kunifananisha na mafarisayo, ni maoni yako mazuri pia, mjuzi wa mioyo ya mwanadamu anafahamu.
 
Hata huyo Yesu kabla ya kimleta Roho Mtakatifu aliwafundisha kwanza wanafunzi wake kwa miaka mitatu....

Unafikiri alikuwa hana uwezo wa kuwashishia siku anaanza ministry yake...?
Sasa kwa nini wawe na hitaji la roho mtakatifu wakati wako na Bwana harusi na Neno mwenyewe?
Ndio maana alisema inanipasa mimi niondoke ili huyo msaidizi aje.
 
Tungekuwa mbali kivipi, kwenye nini..? Kuna anayeweza Shindana kwenye dunia hii na Kanisa Katoliki kwenye mambo ya Biblia...??


Biblia ni mali ya Kanisa Katoliki....utaaanzia wapi kushindana nalo...? Tupo mbele kwenye kila kitu...

Elimu, Afya, Huduma, Mambo ya Kiroho....sisi ndip tunaongoza
Kanisa la kwanza lilianzia Israel alikozaliwa Yesu sio Roma Italia.Na Biblia walioandika ni wayahudi sio warumi.Kipindi Biblia inaandikwa warumi walikuwa wapagani.Waroma ndio walimhukumu Yesu kusulubiwa mtoa hukumu alikuwa ponsio pilato mroma.Na Yesu hakusulubiwa Na kuuawa Na wayahudi.Waliompiga Yesu Na kumgongomelea msalabani Na kumuuua kwa kumchoma mkuki ubavuni ni askari wa Kiroma.Yesu waliua wao .Ndio maana wasio wakatoliki wana mshikamano mkubwa Na wayahudi kuliko wakatoliki.Na huenda kuhiji Israel sio Roma sababu kule ndiko kanisa la kwanza Na huduma ya Kristo lilianzia.Wakikusanyika nyumba kwa nyumba Na siku ya Pentecost roho akawashukia kanisani ghorofani Israel sio Roma Italia.Hawaendi kuhiji Roma huenda Israel kwa wayahudi ambao hawakumpiga,kumtesa wala kimsulubisha Na kumuua Yesu.Wauaji wakuu wa Yesu ni Waroma.Hiyo Biblia wanayoijua ni ipi?
 
Wazungu walioleta ukristo kuanzia Ukatoliki Na uprotestant na kufundisha Mapadri Na wachungaji wenye PhD za Bible knowledge wanaojua kigiriki na kiebrania kwao ndio wameruhusu ushoga.Nadhani kwa Waafrika Biblia tujisomee tu wenyewe tuielewe tutakavyo Kila mtu kivyake kama wanigeria Na waghana ambao walisusa miaka mingi iliyopita kufundishwa elimu ya Biblia Na wazungu au waliosomeshwa Na wazungu kuwa wanafundisha head knowledge sio spiritual knowledge.Kumjua Mungu Na kujua Biblia ni vitu viwili tofauti.Wazungu wengi wanajua Biblia hawamjui Mungu Na hawana haja naye ndio maana ulaya makanisa yanafungwa watu hawaendi kanisani kabisa pamoja Na elimu ya Biblia kubwa waliyonayo.Kwa anayetaka kuongeza head knowledge ajiunge tu aongeze mistari ya kigiriki na kiebrania kichwani ili apanue head knowledge yake
Mkuu umeandika mambo makubwa mno.
Ubarikiwe.
Binafsi nimefuatilia wanataalimungu na wanaojiita wabobezi wa bibilia wanamatatizo makubwa.
Mbaya zaidi ni Yule ambaye anatumia theology ya '' Historical critical"
Hawa ndio chanzo cha uptofu mkubwa makanisani karibu kila dhehebu.
#Japo wengi hawatasema ila wanafundisha bibilia rationally na kuziinua human opinions na kuzilevel au kuzikubwisha beyond neno.
#Hawa ndio watetezi wa wazi U siri wa homosexuality makanisani maana wanaanza kwa kusema kitabu cha mwanzo ni stori sio live events kisha wanasema Mungu hakuumba adam na hawa tu bali aliumba watu wengi, hivyo kutoa room ya ushoga.
#Wengi hawaamini kabisa bibilia japo wanaishika mikononi na kuifundisha, wala uwezo wa Mungu hawauamini kabisa kabisa na ili ujui inakubidi uwe makini sana na kauli zao.


Umakini mkubwa unahitajika sana katika kusikiliza MZUNGU au mtu yoyote anayedai ni Mbobezi wa Maandiko jnaweza kuishia kuwa mpagani kuliko hata mwanzo.


angalizo
 
Tungekuwa mbali kivipi, kwenye nini..? Kuna anayeweza Shindana kwenye dunia hii na Kanisa Katoliki kwenye mambo ya Biblia...??


Biblia ni mali ya Kanisa Katoliki....utaaanzia wapi kushindana nalo...? Tupo mbele kwenye kila kitu...

Elimu, Afya, Huduma, Mambo ya Kiroho....sisi ndip tunaongoza
Ujivuni wa elimu, afya, huduma, huku waumini wakiwa na njaa ya neno la Mungu ni kama kuwatoa muhanga katikati ya Vita kati ya uovu wa wema.
ndio maana napongezanhizi juhudi, wenda wengi wakawa na uelewa na kuupdate maamuzi yao ya kiroho, wenda wakauona ukweli kwa karibu zaidi na kupunguza mabishano ya Truth v/s church traditions.


Watu waandike maandiko kwa Bidii kwa Uongozi wa Roho mtakatifu miaka zaidi 1500 kabla na baada ya Yesu, kiibuke kikundi cha dini kijimilikishe hii ni KUFURU kwa MWENYEZI MUNGU.
 
Back
Top Bottom