Karibuni kwenye Kituo cha biblia cha Kanisa Katoliki (KBKK)

mpendwa katika kristo "kumcha Mungu /wacha Mungu" na "elimu ya biblia/Mungu" ni vitu viwili tofauti sana. japo vinaweza kukalibiana kadili ya maisha na matamani ya mtu.

kilichopo kwenye uzi sio habari za kumcha Mungu. kama ni kumcha Mungu kuna waisilamu nk wasiomjua roho mtakatifu wala biblia ila ni wacha Mungu kwelikweli kuwazidi wakristo lukuki hiyo ni kwa neema ya Mungu tu. ila kilichpo kwenye uzi ni elimu ya biblia kama zilivo elimu zingine yaani udaktari, enginiering, ualimu nk
amina, ubarikiwe...
 
jaribu kutofautisha kutofautisha uchafu/usafi wa moyo wa mtu na bible knowlege/kilichopo mezani ni vitu viwili tofauti na nikkilichopo mezani ni icho namba mbili
Kama wapo wasabato, wakatoliki au yoyote yule ambaye amegotea kwenye bible knowledge au head knowledge au bibilia kwake ni kama desa Huku Moyoni ni Mchafu
 
Mabingwa wa Bible knowledge walikuwa mafarisayo, na Masadukayo, waalimu na waandishi lakini hawakuona mpango mkubwa wa Wokovu ndani yake wakabaki na Head Knowledge.
hapo kwenye bold naona umeteleza kidogo so ninaomba nikurekebishe ili na wengine wasijifunze makosa.

wafarisayo, wasadukayo na wengine kama waeseni, wazeloti nk hawakuwa na wala hawajawahi kuwa wabobezi au wataalamu wa maandiko kwa maana ya kukaa darasani A to Z mpaka kuhitimu na kuitwa mwalimu/rabbi na wala hawakurusiwa kujihusisha na habari zozote za kufafanua/kuelezea/kunakili maandiko isipokuwa kama ulikuwa umesomea huo utaalamu tu ndio uliweza kuruhusiwa kuelezea/kunakili kumbe ivo vilikuwa ni vikundi vya kawaida tu vya kidini kwetu tungeviita madhehebu.

"waandishi na walimu wa sheria" hayo sio makundi mawili kama ulivoonesha ila ilo ni kundi moja tu. kimsingi hao ndio walikuwa wabobezi/wataalamu wa maandiko kwa maana ya kusoma A to Z mpaka kuhitimu na kuitwa rabbi. mmoja aliweza kuitwa mwalimu au muandishi kadiri ya majukumu yake/kazi yake na sio kundi lake. kwa sababu wao pia kama wengine walikuwa na vikundi vyao vya kidini yaani wafarisayo, waeseni, wasadukayo nk.

hivyo ni makosa kwa vikundi hivyo kuwekwa kundi moja kama wabobezi wa maandiko matakatifu.

AHSANTE NA KARIBU TUSAIDIANE PALIPO NA HAJA YA KUSAIDIANA NA KUREKEBISHANA.
 
Matendo 5:34
Lakini Mfarisayo mmoja aitwaye Gamalieli ambaye alikuwa mwalimu wa Sheria na aliyeheshimika sana mbele ya watu wote, alisimama mbele ya lile Baraza, akataka wale mitume watolewe nje kwa muda mfupi.

Gamalieli alikuwa farisayo.
Sauli/Paulo alikuwa farisayo.
na wote walikuwa ni wabobezi wa maandiko ya Kiyahudi.

Masadukayo wana wa Sadoki, nao walikuwa wabobezi wa maandiko na ndio maana walikuwa na theolojia yao ya '' kutokuwepo kwa Ufufuo wa wafu'', Pia ukizingatia ni wazao wa kikuhani ambao makuhani walikiwa watu wa maandiko. Huku mafarisayo wakiwa na yao ya '' ufufuko wa wafu''.
Wazeloti sawa, hawa nakubali walikuwa wafia uyahudi tu, ila pia nakubali waalimu, wanasheria na marabi nao walikuwa wajuzi wa maandiko. Japo Yesu naye alikuwa mjuzi na kuitwa rabbi ila hakupitia kwenye shule zao kukidhi viwango vyao vya kirabbi.
 
Nafuu kwani inasemekana wakatoliki hawaijui biblia . Akishabeba misale ya waumini mkononi basi .
 
Sauli alikiwa farisayo.

matendo 5:34 ndicho ambacho nimekielezea hapo juu kwa kirefu kidogo.
kwa sababu wao pia kama wengine walikuwa na vikundi vyao vya kidini yaani wafarisayo, waeseni, wasadukayo nk.
ulipoteleza ni kule juu kwa kudai kuwa "wafarisayo, wasadukayo yalikuwa ni moja ya makundi maalumu ya utaalamu wa biblia kitu ambacho ni makosa.

na pili ni kwa kitendo cha kuwaweka waandishi na walimu kama makundi mawili tofauti kitu ambacho sio kweli ila hilo ni kundi
 
Nafuu kwani inasemekana wakatoliki hawaijui biblia . Akishabeba misale ya waumini mkononi basi .
sio kweli kwamba wakatoliki hawajui biblia na wala sio kweli kwamba wakatoliki hawasomi biblia. hayo ni maneno ya mitaani tu

misale yenyewe yote ni maneno ya biblia yaliopangwa katika masomo ya kila jumapili ambapo kwa muda wa miaka mitatu mwaka A mpaka mwaka C utakuwa umesoma zaidi ya robo tatu ya biblia. na bado taasisi inayochapisha na kusambaza biblia zaidi ni kanisa katoliki. sasa kama linachapisha, linaandika na kusambaza linamuuzia nani au zinaishia wapi ?. na kuhusu kituo ni huku kwetu tu tanzania wenzetu waishaendelea zamani sana.

usishugulike na watu wanasema nini utateseka.
 
wafarisayo, wasadukayo na wengine kama waeseni, wazeloti nk hawakuwa na wala hawajawahi kuwa wabobezi au wataalamu wa maandiko kwa maana ya kukaa darasani A to Z mpaka kuhitimu na kuitwa mwalimu/rabbi na wala hawakurusiwa kujihusisha na habari zozote za kufafanua/kuelezea/kunakili maandiko isipokuwa kama ulikuwa umesomea huo utaalamu tu ndio uliweza kuruhusiwa kuelezea/kunakili kumbe ivo vilikuwa ni vikundi vya kawaida tu vya kidini kwetu tungeviita madhehebu.
Hiki ndicho ulichoandika kinachopingana na Matendo 5.
Kinapingana na maamuzi ya wazazi wa Paulo walioamua kumpeleka mtoto wao kitokea huko Tarso kwenda Yerusalem kufunzwa miguuni kwa mkufunzi na FARISAYO MBOBEZI GAMALIELI, Kiasi cha Kumfanya Paulo naye Kuwa Mbobezi wa maandiko hayo na FARISAYO Sugu mwenye roho mbaya dhidi ya wafuasi wa Kristo.

Hivyo ukosoaji wako umekuwa jumla kiasi cha kuruka kweli kadhaa za maandiko na kuufanya kuwa ufafanuzi potoshi.

Na kuthibitisha kuwa MAFARISAYO Walikuwa WABOBEZI Hadi kuwa na Wanafunzi pia kama Marabbi wengine na sio Gamalieli tu.
Pitia

Marko 2:18
Nao wanafunzi wake Yohana na Mafarisayo walikuwa wakifunga; basi walikuja, wakamwambia, Kwani wanafunzi wa Yohana na wanafunzi wa Mafarisayo hufunga, bali wanafunzi wako hawafungi?

Pia Mafarisayo Wametokana na Uzao wa Kikuhani Kama Masadukayo pia, Hivyo ni vigumu kutenganisha gombo na hao mafarisayo na sio swa kuwaunganisha na Zealots, maana hata katika bibilia hawaunganishwi isipokuwa Mafarisayo, Masadukayo, Kuhani, scribes (waandishi wa maandiko tangu enzi za Ezra) walikuwa wanatamkwa kwa pamoja.
 
Katikati ya mwezi ujao, tutaanza kufundisha Biblia Kikatoliki cc mleta uzi
#8
mitale na midimu Aroon 3Angels message na wasabato wengineo mnaojiita wajuzi wa Maandiko matakatifu na wajuzi Wa maandiko ya Daniel na Yohana kuomba Kazi kwenye Chuo husika. Nendeni mkaombe Kazi hata kama ni Part-time kupiga Lectures hapo. Ndiyo nafasi yenu sasa kuonyesha ubingwa wenu katika Teolojia na historia ya Biblia.

cc mchangiaji mwenza.

sio maneno yangu mkuu wangu. hata mimi nimeyaokota humu humu.
Shule njema.
Kuomba kazi haimaanishi ni kazi kweli kama alivyoandika mwandishi bali unatokana na ule utafasiri wenu wa kitabu Daniel na Yohana na kuvihusisha na Kanisa Katoliki.

Ndio maana mwandishi amekuwa specific katika kutaja vitabu lkn sio biblia nzima.
 
Hiki ndicho ulichoandika kinachopingana na Matendo 5.
Kinapingana na maamuzi ya wazazi wa Paulo walioamua kumpeleka mtoto wao kitokea huko Tarso kwenda Yerusalem kufunzwa miguuni kwa mkufunzi na FARISAYO MBOBEZI GAMALIELI, Kiasi cha Kumfanya Paulo naye Kuwa Mbobezi wa maandiko hayo na FARISAYO Sugu mwenye roho mbaya dhidi ya wafuasi wa Kristo.

Hivyo ukosoaji wako umekuwa jumla kiasi cha kuruka kweli kadhaa za maandiko na kuufanya kuwa ufafanuzi potoshi.

Na kuthibitisha kuwa MAFARISAYO Walikuwa WABOBEZI Hadi kuwa na Wanafunzi pia kama Marabbi wengine na sio Gamalieli tu.
Pitia

Marko 2:18
Nao wanafunzi wake Yohana na Mafarisayo walikuwa wakifunga; basi walikuja, wakamwambia, Kwani wanafunzi wa Yohana na wanafunzi wa Mafarisayo hufunga, bali wanafunzi wako hawafungi?

Pia Mafarisayo Wametokana na Uzao wa Kikuhani Kama Masadukayo pia, Hivyo ni vigumu kutenganisha gombo na hao mafarisayo na sio swa kuwaunganisha na Zealots, maana hata katika bibilia hawaunganishwi isipokuwa Mafarisayo, Masadukayo, Kuhani, scribes (waandishi wa maandiko tangu enzi za Ezra) walikuwa wanatamkwa kwa pamoja.
Jiunge na semina acha kusemea nyuma ya mlango,niliwahi kukuambia kuwa kuna wabobezi wa maandiko matakatifu ambao kamwe huwezi wakuta humu JF au popote pale kwenye mitandao ya kijamii.
 
mngefanya hilo enzi za zama za giza ambapo bibilia ilisomwa na makasisi na viongozi wa dini tu huku waumini wakisubiri kulishwa bila kuhakiki wanacholishwa ni sasa hivi mngekuwa mbali.

Nawatakia Shule njema,
Kanisa limepitia Nyakati nyingi katika historia yake na kila nyakati ilikuwa na mahitaji yake.

Wakati imani ya Kikristo inaingia miongoni mwa jamii wkt ule wa karne ya kwanza sio kila mtu alijua kusoma na kuandika,kwahyo ilibidi wasomewe na kutafisiriwa na wanaojua kusoma ili Injili ienee kwa kwao,na hata wkt ule wamisionari wanaingia Afrika hususani Tz sio kila mtu alijua kusoma na kuandika na pia ukumbuke kuwa Missionaries walikuja na Injili ikiwa katika lugha ya kigeni kwahyo iliwabidi wasambaze shule kwanza ili kujifunza lugha zao pamoja na mengine kama geography,mathematics nk, ili kuwapa elimu dunia kisha kuwapa elimu ya Mungu.

Mitale siamini kama bibi yako alijua kusoma na kuandika,kwahyo ili kuipata Injili ilibidi atumike mtu kuwasomea na kutafasiri na ukumbuke utafasiri huo ulitoka kwenye lugha ya kigeni kwanza na kuja kwenye lugha za asili,ndio maana nyakati zile walitumika makuhani wa asili ambao tayari walikuwa wameshapata elimu toka kwa missionaries katika kufundisha bible.

Lkn pia sio kosa lako kuandika hivi kwa sababu Usabato umeingia juzi kukiwa tayari watu washaujua Ukristo na pia wengi wao wakiwa wanajua kusoma na kuandika.
Leo Kanisa Katoliki linatimiza miaka 150 ya Uinjishaji hapa Tz yani Missionary wa kwanza aliingia nchi 1868 ambapo ni miaka michache tangu kuasisiwa kwa SDAC duniani.
 
Lakini watu watajitokeza kusoma? Watu wanataka kusoma mambo au kozi ambazo zitawawezesha kuajiriwa.
Watu wana kiu ya kujua mengi. Hizi elimu hazikupaswa kukaziwa kwa mapadre na kuwalea waamini kama watoto wasiokua.

Watu watasoma tu, nimeona mafanikio makubwa kwenye vituo vya makuzi ya kiroho vya Karistimatiki Katoliki ambavyo hadi usiku watu wanaenda kusoma. Kama itakuwa wazi ni nini mtu atajifunza itavutia kila muhitaji.
 
Matendo 5:34
Lakini Mfarisayo mmoja aitwaye Gamalieli ambaye alikuwa mwalimu wa Sheria na aliyeheshimika sana mbele ya watu wote, alisimama mbele ya lile Baraza, akataka wale mitume watolewe nje kwa muda mfupi.

Gamalieli alikuwa farisayo.
Sauli/Paulo alikuwa farisayo.
na wote walikuwa ni wabobezi wa maandiko ya Kiyahudi.

Masadukayo wana wa Sadoki, nao walikuwa wabobezi wa maandiko na ndio maana walikuwa na theolojia yao ya '' kutokuwepo kwa Ufufuo wa wafu'', Pia ukizingatia ni wazao wa kikuhani ambao makuhani walikiwa watu wa maandiko. Huku mafarisayo wakiwa na yao ya '' ufufuko wa wafu''.
Wazeloti sawa, hawa nakubali walikuwa wafia uyahudi tu, ila pia nakubali waalimu, wanasheria na marabi nao walikuwa wajuzi wa maandiko. Japo Yesu naye alikuwa mjuzi na kuitwa rabbi ila hakupitia kwenye shule zao kukidhi viwango vyao vya kirabbi.

Hivi, una vyanzo vya kutosha kwamba Yesu hakupitia shule?
 
Hii kitu ingekuwa Dar ningejiunga. Nina maswali mengi mno ambayo natamani nipate majibu ya kina na najua ni wanazuoni wa Kikatoliki tu ndio wanaweza kuja na facts na kuondoa sintofahamu yangu maana wale wengine maswali yakiwa magumu wanakwambia okoka kwanza ili uelewe maana mambo mengi ni ya kiroho sana!

Yani swali likiwa gumu linahamishiwa kwenye state ya "kiroho" na hoja inafia hapo.
Kumbe nawe umeliona hilo
 
Yesu aliahidi roho mtakatifu atawaongoza kuishika kweli Yote. Ukuaji wa kiroho wa mtu yoyote sio msabato tu nje ya utegemezi wa roho mtakatifu haishii tu kuwa farisayo
Hata huyo Yesu kabla ya kimleta Roho Mtakatifu aliwafundisha kwanza wanafunzi wake kwa miaka mitatu....

Unafikiri alikuwa hana uwezo wa kuwashishia siku anaanza ministry yake...?
 
Back
Top Bottom