Tunasoma kutoka Injili ya Luka 2:52 hivi:
" Naye Yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu."
Hekima inafunua wazo la maarifa. Je,maarifa hayo aliyapata wapi Yesu? Kuna namna mbili Yesu alifundishwa:
1. Na wazazi wake kama ilivyokuwa desturi ya watoto Wa kiume Wa Kiyahudi kufundishwa Maandiko Matakatifu,Agano la Kale
2. Watoto Wa Kiyahudi katika Karne ya Kwanza AD walikuwa wanasomeshwa bure.
Ukiachana na suala la Yesu kufundishwa nyumbani na wazazi wake, vile vile Yesu kama mtoto Wa kiume Wa Jamii ya Kiyahudi alipata fursa ya kusoma bure. Watoto wote Wa Kiume Wa jamii ya Kiyahudi katika Karne ya kwanza walikuwa wanasoma bure. Walisomeshwa Scripture na law. Walifundishwa pia kusoma, kuandika, historia, elementary sciences and mathematics. Na Fursa hii ilitolewa kwa kila mtoto wa kiume wa Kiyahudi bila kujali hadhi ya familia anayotokea au social standing.
Kwa hiyo,ile pointi kwamba wazazi wake YESU walikuwa maskini na hivi wasingaliweza kumudu gharama za masomo sio kweli. Na kupitia fursa hii Paulo na Timetheo nao walisoma.
Ushahidi kwamba Yesu alisoma.
"6 Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome.
17 Akapewa chuo cha nabii Isaya, akakifungua chuo, akatafuta mahali palipoandikwa," (Luke 4:16)
"7 Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe. 8 Akainama tena, akaandika kwa kidole chake katika nchi." (Yohana 8: 7-8).
Kwa hiyo haya yote yanathibitisha kwamba Yesu aliingia darasani na ndio kisa alijua kusoma na kuandika na hata kutafsiri maandiko mbalimbali Matakatifu.
#
Kwa wayahudi Jukumu la kwanza kwa Elimunya Dini sio shuleni bali Nyumbani tangu akiwa mdogo.
Na Kusoma na Kuandika walijifunza Nyumbani, maana Agizo linasema wazazi wawafundishe watoto.
Utamfundishaje mtoto kama hujaanza kumfundisha kusoma na Kuandika. Tusifikiri kitanzania tufikiri Oriental mkuu.
Mstari. kumbukumbu la torati 6:6-9
6 Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako;
7 nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo.
8 Yafunge yawe dalili juu ya mkono wako, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yako.
9 Tena yaandike juu ya miimo ya nyumba yako, na juu ya malango yako.
Ndio maana nikakupa mfano wa stephano ambaye Paulo anamshuhudia amejifunza kwa Mama na Bibi yake. Maana hata hivyo huko Listra walikukwa wanaishi hakukuwa na sinagohi walamhao wakufunzi, na ulikuwa ni mjimwa kipagani hadimwaliwaita paulo na barnaba kwa majina ya miungu yao.
##
Pia elimu nyingine ya dini kwa watoto ilitolewa kwa maswali na majibu siku ya sikukuu za dini, ni mkakati maalum.
Kutoka 12:26 Kisha itakuwa,
hapo watoto wenu watakapowauliza, N'nini maana yake utumishi huu kwenu?
###
Kwa masimulizi nje ya BIBIBLIA maana mistari uliyotoa haionyeshi kama alipita katika rabbinical schools.
kulikuwa na mafunzo ya kawaida tu, kwenye masinagogi hasa kwa watoto wa miaka sita/saba .
Ila hapa nazungumzia zile Rabinical schools mfano enzi za Paulo kulikuwa na shule mbili maarufu na pinzani Shule ya Hillel na Shule ya Shammai (schools of theology) ambazo walihudhuria vijana miaka 13+ sio watoto na moja wapo alihudhulia Paulo.
Ila Uthibitisho wa Maandiko kuwa Yesu Hakupitia kwenye hayo mashule ya mascholers wa kiyahudi kama Paulo anavyosema.
Matendo ya Mitume 22:3
Mimi ni mtu wa Kiyahudi, nalizaliwa Tarso, mji wa Kilikia, ila nililelewa katika mji huu, miguuni pa Gamalieli,
nikafundishwa sheria ya baba zetu kwa usahihi, nikawa mtu wa jitihadi kwa Mungu kama ninyi nyote mlivyo leo hivi;
Yesu alikuwa anapinga Sheria za mababa na mdesturi zote ambazo ndizo zilikuwa Core courses za shule hizo za mayahudi.
mfano
Mathayo 15:3,6
Akajibu, akawaambia, Mbona ninyi
nanyi huihalifu amri ya Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu?
basi asimheshimu baba yake au mama yake.
Mkalitangua neno la Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu.
Wanafunzi waliopitia Mfumo wa shule ya dini kama aliyowaachia wanafunzi wake, ni wale watoto wa wa vuvi vilaza ila waliposimama kutamka mambo ya Mungu walionekana Bora kuliko waalimu wa sheria na scholars wote wa wakati huo.
Basi walipoona ujasiri wa Petro na Yohana, na kuwajua ya kuwa ni watu wasio na elimu, wasio na maarifa, wakastaajabu, wakawatambua ya kwamba walikuwa pamoja na Yesu.
Matendo 4:13