SANCTUS ANACLETUS
JF-Expert Member
- Mar 5, 2016
- 3,336
- 4,694
Tatizo hamko serious, mmevaki kuwalalamikia wasabato!.. Anzisheni mfumo was kuwafundisha waumini ndani ya makanisa yao... Sasa wewe unafikiri kwenye hivyo vituo wangapu mtafika?.. Yaani waumini wamejaa tele makanisani kwenu lakini hawajui maandiko kabisa!.. Wenzenu wasabato, kila jumamosi wana vipindi Vingi vya mafundisho na pia wana mwongozo was kujifunza biblia kila siku asubuhi na jioni kabla ya kulala.. Sasa unadhani mtalinfana nao...
Karibu kwenye Sinagogi ushiriki na Wafarisayo....,asante kwa maoni.
A little bit error "Wafarisayo=Mafarisayo"Karibu kwenye Sinagogi ushiriki na Wafarisayo....,
Asante sana kwa Ukaribisho huu,lkn pia wanakaribishwa Wakristo wote wanaopenda kujifunza na naamini elimu ya biblia huishia pale nafsi inapoingia mautini...*MASOMO MAWILI YA UTANGULIZI – SOMO A*
*SOMO A LA UTANGULIZI - UHALALI NA WAJIBU WA WAKRISTO KUFUNDISHANA BIBLIA*
Hivi karibuni tutaanza kurusha masomo ya Biblia na kujadiliana juu yake moja baada ya jingine. Tunataka nini? Tunataka kufundishana ili Mungu akiridhia yeye azidi kutukuzwa, Kanisa lake likue na hatimaye sisi wenyewe tujipatie uzima wa milele. Pamoja na kuonekana rahisi kufahamu uhalali na umuhimu wa shughuli tunayokusudia kuifanya, wapo watu wanaweza kutubeza. Lakini, hapana, Wakristo wote tuna wajibu wa kufundishana Biblia. *Jibu kwa swali kwa nini tufundishane Biblia ni hoja kuu NANE zifuatazo:*
*MOSI, NI HAKI KWA MAJALIWA TULIYOPEWA*. Wanadamu tumeumbwa kwa mfano na sura ya Mungu Mwenyezi maana yake tuna akili na utashi (Mwa 1:26-27). Kujifunza Biblia kunaendana na jinsi ya kuumbwa kwetu yaani kuipatia akili mahitaji yake. Akili inahitaji mambo ya akili, kumbe, kujifunza kitu ndiko kuilisha akili. Chakula cha akili ni elimu. Ndiyo maana Yesu alipoulizwa amri ipi ni kuu kati ya 613 za Wayahudi (248 za kuhimiza kufanya na 365 za kukataza kufanya), aliwajibu kwa msisitizo kwamba Mungu ni sharti apendwe KWA AKILI YOTE vile vile. Hivi Yesu alifanyia maboresho kile kichoandikwa katika Kum 6:4-9 kwa kuliweka bayana neno AKILI.
Tunasoma: “Mafarisayo waliposikia kwamba Yesu alikuwa amewanyamazisha Masadukayo, wakakutana pamoja. Mmoja wao, mwanasheria, akamuuliza Yesu kwa kumjaribu. ‘Mwalimu ni amri ipi iliyo kuu katika sheria? Yesu akamjibu, ‘Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote na KWA AKILI YAKO YOTE. Hii ndiyo amri kuu na ya kwanza. Ya pili inafanana na hiyo. Mpende jirani yako kama unavyojipenda wewe mwenyewe. Sheria yote ya Musa na mafundisho ya manabii vinategemea amri hizi mbili’” (Mt 22:37-40).
Hivi kufundishana kulisha akili zetu ni haki yetu sote. Ndiyo maana lazima tuigundue elimu na tuing’ang’anie sana (Mit 4:13) kwa sababu kama hatunayo tutaangamia. Watu huangamia wakikosa elimu (Hos 4:6).
Elimu imesifiwa katika Biblia tena na tena kama tunu ya maana sana (rej. Mit 8:33, 9:9, 19:20.27. 23:12. 23, Hek 6:25, YbS 23:7, 30:3, 51:23 na kadhalika). Ni jambo la heri kubwa kama nasi tutafundishana vyema. Musa alisoma (Mdo 7:22), Paulo alisoma (Mdo 22:3) na kadhalika. Sasa ni zamu yetu.
*PILI, NI AGIZO LA MUNGU MWENYEZI KWAMBA TUFUNDISHANE BIBLIA.* Mungu hataki tumfuate kwa umbumbumbu. Agizo hilo alilitoa kwa Wayahudi na wao walilipokea kwa niaba ya wanadamu wote. Imeandikwa, “Sikiliza, ee Israeli, Mungu Mwenyezi, Mungu wenu, ni Mungu Mwenyezi mmoja. Mpende Mungu Mwenyezi, Mungu wenu kwa moyo wenu wote, kwa roho yenu yote na kwa nguvu yenu yote. Wekeni moyoni mwenu maneno hayo ninayowaamuru leo na KUWAFUNDISHA KWA UANGALIFU WATOTO WENU. Mtawasimulia mwapo mmekaa nyumbani au mlipo safarini au mnapolala au mnapoamka. Yafungeni katika mikono yenu na kuvaa katika paji za nyuso zenu kama ukumbusho. Yaandikeni kwenye miimo ya milango yenu na malango ya miji yenu” (Kum 6:4-9).
Jambo hili la Wayahudi kuwafundisha watoto wao dini na elimu kwa ujumla, hawakulifanyia uzembe. Ndipo, hata kabla ya Yesu kuzaliwa, Wayahudi walikuwa na chekechea na mfumo rasmi wa kujifunza Torati na mengineyo kutoka kwa marabi kwa muda mrefu takribani miaka 38. Yesu kama mwanadamu alipitia mfumo wa elimu wa Kiyahudi, akajifunza kuandika (Yn 8:6) na kusoma (Lk 4:16), isipokuwa hakuhitaji kujifunza kwa rabbi fulani kwa miaka 38 kwa sababu kama Mungu alijua mambo yote. Kumbe, sisi nasi tunahitaji kujifunza.
*TATU, NI KUFANYA KAZI YA YESU MWENYEWE.* Yesu alitumia miaka mitatu kwenda huko na huko akiwafundisha watu. Aliwafundisha ili watu waipokee Injili kwa uelewa. Yesu hakuja duniani kujenga ufalme wa Mungu juu ya tofali la barafu. Asiyejua kitu anaweza kuvuruga mengi na kuwa mkaidi sugu kwa vile hajui kwamba anakosea. Kumbe, mafundisho sahihi ndiyo msingi wa imani na utendaji sahihi. Mtu akielewa vizuri anaweza kuamini vizuri na vivyo mtu aliyeamini vizuri anaweza akaelewa vizuri. Ndiyo maana alisema Maria aliyechagua kusikiliza kabla ya kutenda alichagua fungu bora zaidi ya Marta alijitosa katika kutenda pasipo kusikiliza (Lk 10:38-40). Kumbe, Yesu kuanza kufundisha kabla ya kuwapelekea mitume wake Roho Mtakatifu haikuwa kupoteza muda.
Mwanadamu kutia bidii katika kujifunza ya Mungu ni sawa sawa. Si sawa kudhani Roho Mtakatifu atatufanya tujue yote pasipo mchango wetu wa kujifunza imani yetu. Roho Mtakatifu hajengi nyumba hewani bali anategemea msingi fulani. Narudia. Ndiyo kisa, Yesu aliwafundisha watu kwanza kabla ya kumgawa Roho Mtakatifu. Pentekoste ilikuja baada ya miaka mitatu ya “shule”.
Nasisitiza. Kwa kuweka msingi imara wa imani na utendaji, Yesu alikaa na mitume miaka mitatu ili kuwafundisha “wajue” na hata aliwapa fursa ya kujaribia wenyewe kufundisha kwa vitendo. Kwa lengo hili, aliwatuma mitume na kishapo wafuasi 72, wawili wawili, sehemu mbalimbali wakajaribie namna ya kufundisha. (Kwa Kiingereza aliwatuma katika ufundishaji wa majaribio, BTP, yaani Block Teaching Practice).
Kumbe, kila mwamini anahitaji kujifunza vyema. Wengine wetu, wakitaka kubeza elimu ya dini, huzoea kujitetea wakisema, “MITUME HAWAKUSOMA hata hivyo walifanya kazi vizuri sana.” Utetezi huu si kweli na si halali. Mitume walisomeshwa tena walipata elimu bora kabisa kwa sababu walifundishwa na mwalimu bora kabisa, mwalimu wa walimu, ndiye Yesu Kristo, NENO mwenyewe (rej. Mk 9:7-8, Ebr 1:1-4).
Wala tusizoee kusema akina Petro na mitume hawakuwa na elimu. Tusizoe kusema walikuwa maamuma. Hata kama hawakusomea Torati kutoka kwa marabbi, Yesu alipowachagua hakuwatuma kama alivyowaita. Badala yake, kabla ya kutumwa, aliwafundisha teolojia halisi kutoka kwa Mungu kwa vile yeye mwenyewe Yesu ndiye aliyekuwa mwalimu na NENO mwenyewe (Yn 1:1-14, Mk 9:7-8, 1Yoh 1:1-4). Wao walikaa na kusoma kutoka kwa Yesu moja kwa moja, ndiyo maana ya kuchaguliwa ili “wakae” naye kisha awatume (Mk 3:13-14). Kama mitume waliokaa na Yesu walisomeshwa hivyo, hitaji hilo linaendelea kwetu pia. Walitumwa baada ya kuiva kiuelewa na Roho Mtakatifu alitumwa kwao kuwakumbusha waliyofundishwa na kuwaimarisha katika hayo (Yn 14:26). Hivi, tukifundishana tutakuwa tunashiriki kazi ya Yesu mwenyewe.
*NNE NI KUTIMIZA AGIZO LA UTUME WA KANISA.* Yesu alipotoa agizo la utume alisema hivi: “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Nendeni, basi, mkawafanye watu wa mataifa yote kuwa wanafunzi wangu, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu. WAFUNDISHENI kushika maagizo yote niliyowapeni. Nami nipo pamoja nanyi siku zote, naam, hata mwisho wa nyakati” (Mt 28:18-20). Hivi tukifundishana Biblia tutakuwa tunawapa wenzetu fursa ya kuyashika tuliyoagizwa wenyewe tuyashike. Kufanya hivyo kutakuwa sehemu ya kutimiza utume wa kimisionari kwa zamu yetu.
*TANO NI KUUTIMIZA WAJIBU WETU WA UBATIZO*. Mitume na wafuasi wa Yesu walipokea kijiti cha kufundisha kutoka kwa Yesu, wakawafundisha watu pasipo masihara. Mfano mzuri ni Shemasi Filipo aliyemkuta towashi wa Kandake akimangamanga na Maandiko Matakatifu.
Imeandikwa, “Filipo akakimbilia karibu na gari akamsikia huyo mtu akisoma katika kitabu cha nabii Isaya. Hapo Filipo akamwuliza. ‘Je, unaelewa hayo unayosoma?’ Huyo mtu akamjibu, ‘Nitawezaje kuelewa bila mtu kuniongoza?’ Hapo akamwalika Filipo apande juu, akaketi pamoja naye…. Hapo Mwethiopia akamwambia Filipo, ‘Niambie huyu nabii anasema juu ya nini? Anasema mambo haya juu yake yeye mwenyewe au juu ya mtu mwingine?’ Basi, Filipo akaanza na sehemu hiyo ya Maandiko Matakatifu, akamweleza Habari Njema juu ya Yesu. Walipokuwa bado wanaendelea na safari walifika mahali penye maji na huyo afisa akasema, ‘Mahali hapa pana maji, je, kuna chochote cha kunizuia nisibatizwe?’ Basi, huyo ofisa akaamuru lile gari lisimame, na wote wawili, Filipo na huyo towashi wakashuka majini, naye Filipo akambatiza” (Mdo 8:30-31.34-38).
Sasa sikilizeni. Kwa ubatizo tumefanywa taifa la makuhani, manabii na walimu (1Pet 2:9). Kwa mujibu wa sakramenti ya Ubatizo, sisi sote tuna ukuhani wa ujumla lakini wengine huongezea juu yake ukuhani wa huduma (upadre). Wajibu wetu wa kufundishana na hivyo kuitumikia Injili unalala katika cheo chetu cha kuwa MANABII au WALIMU kwa mujibu wa sakramenti ya Ubatizo. Lakini, ni dhambi mtu kutotimiza wajibu aliopewa dhamana nao. Basi, ole wetu tusipoihubiri Injili (1Kor 9:16).
*SITA NI AGIZO LA MITUME WALIOPOKEZWA KIJITI KUTOKA KWA YESU MWENYEWE*. Mambo ya kufundishana neno la Mungu yatakoma siku ya mwisho wa dunia. Kabla ya hapo ni kama mbio za kupokezana vijiti. Mitume walifundisha kama Bwana alivyowaagiza na wao wakatupasia sisi kazi hiyo. Mtume Paulo, kwa mfano, alimwagiza kijana Timoteo afundishe, na maagizo hayo ni kwa niaba yetu sisi sote.
Tunasoma hivi, “Nakuamuru mbele ya Mungu na mbele ya Kristo Yesu atakayewahukumu watu walio hai na wafu, na kwa sababu anakuja kutawala akiwa Mfalme, hubiri huo ujumbe, sisitiza kuutangaza, iwe ni wakati wa kufaa au wakati usiofaa, karipia, onya na himiza watu ukiwafundisha kwa uvumilivu wote. Utakuja wakati ambapo watu hawatasikiliza mafundisho ya kweli, ila watafuata tamaa zao wenyewe na kujikusanyia walimu tele watakaowaambia mambo yale tu ambayo masikio yao yako tayari kuyasikia. Watakataa kuusikia ukweli, watageukia hadithi za uongo. Wewe, lakini, uwe macho katika kila hali, vumilia mateso, fanya kazi ya mhubiri wa Habari Njema, timiza kikamilifu utumishi wako” (2Tim 4:1-4). Basi, tutekeleze agizo la walioagizwa na Bwana mwenyewe.
*SABA, NI KUKOMBOANA KUTOKA GIZANI NA VIFUNGONI.* Kristo alikuja ulimwenguni kutuweka huru na aina zote za upofu na hofu. Yesu aliitangaza kazi yake akisema, “Roho wa Bwana yu juu yangu kwani amenitia mafuta niwaletee maskini Habari njema. Amenituma niwatangazie mateka uhuru wao na vipofu wapate kuona tena. Amenituma niwakomboe wanaoonewa na kuwatangazia mwaka wa neema ya Bwana.” Kumbe, kifundishana neno la Mungu ni kukomboana. Aidha, Mwinjili Yohane anamtambulisha Yesu kama mwanga uliokuja kuwaangazia watu. Nuru au mwanga kwa watu wakaao gizani na katika uvuli wa mauti hufikishwa kwa watu kwa kufundishana. Hivyo, acha tutiane nuru; acha tupelekane mwangani.
*NANE, NI KUJIEPUSHA WENYEWE NA HATARI YA KUTUMBUKIA SHIMONI. *Yesu alisema watu wasioona wakiongozana wataishia shimoni. Mtaalamu wa Maandiko, Mt. Jerome, alisema kutoyajua Maandiko ni kutomjua Yesu. Kumbe, kufundishana ni kupeana sisi sote uwezo wa kuiona njia vizuri. Watu wasiojua Maandiko hawatamjua Yesu ambaye ni njia, ukweli na uzima (Yn 14:6). Watu kama hao watakuwa hawajui wanatoka wapi seuze wanaelekea wapi. Watu hao siyo tu watapeperushwa na kila upepo bali pia watapotoshana. Na mambo haya mawili ndiyo kupelekana na kuishia shimoni wote. Kwa maneno yake mwenyewe, Yesu alisema: “Akawaambia mfano, je, kipofu anaweza kumwongoza kipofu mwenzake? La, wote wataangukia shimoni” (Lk 6:39).
Kumbe, kufundishana neno la Mungu ni kupeana macho tuione vyema njia iendayo uzimani na hivyo kujiepusha na hatari ya kuishia shimoni sisi sote. Hivi, tukifundishana neno la Mungu, tukaukosa uzima wa milele hatutakuwa na wa kumlaumu isipokuwa ukaidi wetu wenyewe.
*MWISHO WA SOMO A LA UTANGULIZI.*
Wewe ni Mkristo wa dhehebu gani? Una elimu gani juu ya Biblia? Sitaki uniambie hilo ni swala la kiroho nataka majibu clear and very direct. Twende kazi!maswali gani mkuu ninawwza nikakusaidia
Aisee sikujua kuna kazi hii nzuri inaendelea kupitia hapa JF. Mbarikiwe sana*MASOMO MAWILI YA UTANGULIZI – SOMO A*

usijali masomo mengine tutashare hapa hapa jukwaani kadiri itakavowezekana kwani kule whatsap group lishajaa ila wanatengeneza magroup mengine na baadae watahamia tele. cha msingi Tumshukuru Mungu kwa yote na tombe uzima.Aisee sikujua kuna kazi hii nzuri inaendelea kupitia hapa JF. Mbarikiwe sana
Ndugu zangu *WanaCBC* karibuni leo tuone sehemu ya mwisho ya UTANGULIZI wa masomo yetu ya Biblia hapa CBC Whatsapp, kama iletwavyo naye Mtawala wetu wa Kundi(Admin), Pd Titus Amigu. Hivyo tutaona *SOMO B LA UTANGULIZI – KIPANDE CHA PILI – SHUGHULI ZA UTUME WA BIBLIA*
Hapo Baba Amigu atatupitisha katika maeneo yafuatayo:
1. _*Shughuli za Utume wa Biblia katika sura yake halisi.*_
2. _*Shughuli Zingine Maalumu za Utume wa Biblia*_
3. _*Matatizo na Changamoto za Utume wa Biblia Ulimwenguni*_
4. _*Uamuzi Binafsi wa Kujisomea Biblia*_
5. _*Mkristo na Biblia - Biblia na Kila Mkristo*_
Karibuni tujipatie maarifa haya adhimu. MASWALI, MAONI, MAPENDEKEZO, NA MICHANGO MINGINE kutoka kwetu Wanadarasa itakuwa ni fursa yetu kuitoa.
*KARIBUNI SANA!*[emoji116][emoji116][emoji116]
MTAZAMO
usijali masomo mengine tutashare hapa hapa jukwaani kadiri itakavowezekana kwani kule whatsap group lishajaa ila wanatengeneza magroup mengine na baadae watahamia tele. cha msingi Tumshukuru Mungu kwa yote na tombe uzima.
group la kwanza limejaa ila wanatengeneza magroup mengine zaidi so rejea maelezo ya uzi yaani post namba moja kabisa.Napenda kujiunga na hili group, unafanyaje?