Karibuni kwenye Kituo cha biblia cha Kanisa Katoliki (KBKK)

Karibuni kwenye Kituo cha biblia cha Kanisa Katoliki (KBKK)

Wapendwa Wanafamilia ya Mungu, *CBC I* na *CBC II* karibuni sana tuweze kusoma somo hili la tatu, juu ya *MWANDISHI WA BIBLIA* kama liletwavyo kwako na Admin wetu, Fr Amigu. Kisha lisoma tena na tena, tunaalikwa kwa maswali, na michango mingine. Karibuni sana.
NDIMI MWASILISHAJI,
Frt Leonard Sing’ambi,
Seminari Kuu Peramiho
[email protected]👇👇👇
 
*CATHOLIC BIBLICAL CENTRE - SOMO LA TATU - MWANDISHI WA BIBLIA: MWANDISHI PACHA*

_*MAANA YA MWANDISHI PACHA*_
Biblia ni maktaba ya vijitabu vilivyoandikwa kwa ushirikiano wa Mungu na wanadamu. Kwa namna hii kuna Mungu na wanadamu waliohusika kutukamilishia neno la Mungu. Ukweli huu ndio unaotufanya tujibu swali la nani mwandishi wa Biblia kwa kusema ni mwandishi pacha, Mungu na wanadamu.

_*WANADAMU WALIANDIKA KWA KUVUVIWA, UVUVIO*_
Waandishi wanadamu waliandika kwa msaada wa Roho Mtakatifu. Yaani walisaidiwa mwangaza wake.
Kuhusu idadi yao, jibu ni kwamba walikuwa wengi. Kabla ya Yesu waliandika vijitabu mbalimbali vya Agano la Kale na baada ya Yesu waliandika vitabu vya Agano Jipya. Waandishi hao wengi waliandika katika mazingira mbalimbali wakiwalenga watu mbalimbali. Turudie. Waliandika maandishi hayo ya Biblia Takatifu wakiangazwa na mwanga wa Roho Mtakatifu. Walivuviwa ndiyo maana kweli walizoandika ni za kina kweli kweli na wala hazipitwi na wakati.
Najumlisha. Biblia ni kitabu kilichoandikwa kwa ushirikiano kati ya Mungu na mwanadamu. Hii ni maana yake ni kwamba Mwenyezi Mungu alishiriki kikamilifu katika zoezi la uandishi wa Biblia ambapo licha ya ushiriki wake bado mwanadamu alibaki huru katika matumizi ya vipaji vyake na nyenzo mbalimbali za uandishi.

_*UVUVIO NI NINI?*_
Uvuvio ulikuwa ni ushirikiano wa pekee wa Mungu kwa wanadamu waandishi. Ushirikiano huo HAUKUWA mambo mawili yafuatayo. Haukuwa imla wala usahihishaji na uidhinishaji wa yaliyoandikwa baada ya kuandikwa.
i. _*Ushirikiano huo haukuwa imla*_ eti labda kwamba Mungu aliwaandikisha waandishi wanadamu kwa kuwatamkia maneno ya kuandika. La hasha!
ii. _*Ushirikiano huo haukuwa usahihishaji na uidhinishaji wa yaliyoandikwa*_ baada ya kuandikwa yaani kwamba Mungu aliwaacha waandishi wanadamu waandike yote na kisha ayakubali mambo waliyoandika au la.
Badala yake, _*uvuvio ulikuwa msaada wa pekee kutoka kwa Mungu ambao kwao wanadamu waandishi waliachwa waandike yale tu ambayo Mungu aliyaona yanawafaa watu katika imani na fadhila mbalimbali.*_ Biblia yenyewe inatangaza kwamba yaliyoandikwa yaliandikwa kwa uvuvio (rej. 2Pet 1:19-21).



_*MAPATO YA UVUVIO YAKO PANDE MBILI*_
Tumeshasema mwandishi wa Biblia ni pacha, Mungu na wanadamu kwa hiyo kuna pia mapato ya pande mbili.

*_MAPATO KUTOKANA NA MWANDISHI MUNGU*_
_Upande wa kwanza:_ Kwa sababu ya mwandishi Mungu kuna mambo matano. Biblia ni ufunuo, moja, kamilifu, yenye hali ya kisakramenti na kweli.

_*Ufunuo:*_ Kwa sababu ya mwandishi Mungu, Biblia ni ufunuo. Ufunuo maana yake Mungu kujibainisha au kujionesha mwenyewe kwa watu. Mungu alijibainisha mwenyewe kwa watu katika Agano la Kale kwa kujitokeza na kuisimamia historia ya Waisraeli, tangu uumbaji hadi kuitwa kwa Abrahamu, hadi Wayahudi kwenda na kutoka utumwani Misri, hadi Wayahudi kwenda na kurudi utumwani Babiloni, hadi kujijenga upya katika nchi ya ahadi na kadhalika. Hata hivyo, kujifunua kwake katika enzi ya Agano la Kale kulikuwa kwa nusu nusu akitumia maono, ndoto na kunena na manabii na watu kwa namna mbalimbali (Ebr 1:1-4). Kwa kiasi hicho Mungu hakufahamika kikamilifu.
Kujifunua kwa Mungu katika Agano Jipya ndiko kukamilifu zaidi kwa sababu amejifunua mwenyewe kwa watu kwa kupitia Nafsi yake ya pili, ndiye mwanawe wa pekee Yesu Kristo (rej. Yn 1:1-14. 3:16, Mk 9:7-8 na Ebr 1:1-4). Yesu ndiye aliyekuja kuyafafanua kikamilifu mafundisho ya Agano la Kale. Hiyo ndiyo maana ya kujitangaza hakuja kuyatangua mambo ya Agano la Kale isipokuwa kuyatimiza (= kuyafafanua kikamilifu, kuonesha maana yake kamilifu, rej. Mt 5:17-20). Na huu ndiyo msingi wa kuyapa maneno na matendo ya Yesu nafasi ya kwanza mbele ya maneno na matendo ya watu wa Agano la Kale.
Kwa maelezo haya, kitu alichosema Yesu Kristo ni cha kipaumbele kuliko kilichotamkwa au kutendwa na nabii fulani katika Agano la Kale. Kwa hiyo, si halali kufuta kauli ya Yesu Kristo kwa maneno au matendo ya Abrahamu, Musa, Daudi, Sulemani, Ayubu, Eliya, Elisha, Yehu, Ahabu, Yezebeeli na kadhalika. Kwa mfano, kama Yesu alisema watu waliooana wasiachane (Mt 19:1-12), mtu asiponde kauli hiyo kwa kunukuu mahali Musa alipotoa ruhusa ya talaka (Kum 24:1-4). Kama Yesu alisema vyakula vyote ni halali (Mk 7:19-23), mtu asifute kauli hiyo kwa kunukuu mahali panapobagua nyama fulani fulani kama haramu (Law 11). Kama Yesu alisema watu wasali kwa nidhamu kubwa (Mt 6:5-8), mtu asitangue kauli hiyo kwa kitendo cha mara moja cha kuserebuka Daudi (2Sam 6:16-21). Kama Yesu alisema kila mume awe na mke mmoja (Mt 19:1-12), mtu asinukuu tabia ya Sulemani kuoa wanawake wengi (1Fal 11:1-3) na kadhalika.

_*Umoja wa Biblia:*_ Kwa umoja wa Biblia tunamaanisha Biblia ni moja. Vitabu vinaungana kwa namna ya pekee kama kete za mkufu. Vitabu vya Agano la Kale ni maandalizi au utangulizi wa ahadi ya ujio wa Yesu Kristo wakati Agano Jipya ndiyo ukamilifu wa ahadi yenyewe. Hivi msomaji wa Biblia asiisome Biblia kwa kuitenganisha tenganisha bali aisome katika mnyororo ulioungana. Si mara haba jambo lisiloeleweka katika kitabu kimoja kuwa limefafanuliwa vyema katika kitabu kingine, au swali linalopatikana katika kona fulani ya Biblia kuwa na jibu nzuri katika kitabu kile kile au katika kitabu kingine cha Biblia. Mfano, swali kama Bikira Maria alikuwa na watoto wengine mbali ya Yesu linaloanzishwa na Mk 6:1-6 linajibiwa kwa kukanushwa katika Mk 15:40.47 na 16:1.

_*Kukamilika kwa Biblia:*_ Kwa kukamilika Biblia tunamaanisha Biblia imetimia wala hahitaji nyongeza yoyote. Vitabu vinapokezana taarifa tangu ukurasa wa kwanza hadi wa mwisho. Kwa kutimia huko Biblia hahitaji nyongeza yoyote. Hakuna kitu cha kuboreshwa wala cha kuandikwa upya. Yote yamekamilika. Mtu asipoelewa sehemu fulani ya Maandiko si kwamba pana upungufu, la hasha, isipokuwa kwamba msomaji mwenyewe “ajiongeze” aelewe jambo hilo kwa kuunganisha na sehemu nyingine. Ndiyo kisa basi, si vyema mtu kusoma neno au aya moja ya Biblia na kuchomoka nayo huku akiacha kufanya juhudi ya kujifahamisha kimeandikwa nini kingine kuhusu neno lile lile.
Waaidha Biblia haijakosewa. Maneno na aya zote zina uwezo wa kutoa ujumbe. Ugumu wa baadhi ya maneno au aya haimaanishi kuwa ni uongo. Ukweli hautegemei kuelewa kwa msomaji. Ukiona jambo la kushangaza au la kukwaza maana yake ni onyo na ukiona jambo la kufurahisha au kutia moyo maana yake kuhimizwa. Hivi, kwa kukamilika huko, leo hata mtaalamu fulani aandike kitabu kizuri na cha kitaalamu kiasi gani hakiwezi kupata nafasi katika Biblia. Kifupi, kitabu cha namna hiyo hakitaleta ufunuo mpya isipokuwa kufafanua vyema kilichoko tayari kwenye Biblia. Ufunuo ulikamilishwa na Yesu anayetangazwa kama kilele cha kujifunua kwa Mungu kwa wanadamu (Ebr 1:1-4).

_*Hali ya kisakramenti:*_ Kutokana na mwandishi Mungu, maneno ya Biblia yana nguvu ya kumletea mtu neema, baraka na mabadiliko. Mambo haya ndiyo yanayojumlishwa kwenye ukweli kwamba Biblia ina hali ya kisakramenti. Hii maana yake hata neno moja au aya moja inaweza kumbadili mtu. Mtakatifu Francis ni kati ya watu waliobadilishwa na aya moja tu: “Nenda ukauze mali zako, kisha njoo unifuate” (Mk10:21). Hivi kusudi mwanadamu abadilishwe na Biblia msomaji hahitaji kusoma kitabu kizima, neno au hata aya moja inatosha sana.

_*Ukweli wa Biblia:*_ Kutokana na mwandishi Mungu, Biblia ni kweli. Mungu aliyehusika katika kuandika Biblia hana hulka ya uongo. Mungu hana maslahi na uongo wowote. Hivi jambo lolote aliloruhusu liandikwe ni kweli na linapaswa kusadikiwa. Mungu hana nia ya kumdanganya yeyote. Mchonga sanamu hawezi kuzidanganya sanamu zake mwenyewe. Sisi tulioumbwa kwa mfano na sura ya Mungu Mwenyezi ni sanamu zake hivi hawezi kutudanganya (Mwa 1:26-28).



_*VITU TUSIVYOWEZA KUVIKOSOA KWENYE BIBLIA*_
Vitu tusivyoweza kukosoa sisi wanadamu kwenye Biblia ndiyo hayo matano: ufunuo, umoja wa Biblia, kukamilika kwa Biblia, hali ya kisakramenti na ukweli wa Biblia kwa sababu ni mapato ya ushiriki wa mwandishi Mungu na yeye ni mkamilifu.

_*MAPATO KUTOKANA NA WAANDISHI WANADAMU*_
Kwa upande wa pili, kwa sababu ya mwandishi mwanadamu kuna mambo yafuatayo kwenye Biblia: _*historia, uchumi, siasa, jiografia, utamaduni*_ na kadhalika.
Tumeshasema, wanadamu walikaribishwa na Mungu katika kuwaandikia wenzao mambo ya kuwafaa kiimani na kimaadili. Kwa ushiriki huo “nyayo” za binadamu zinaonekana katika masuala yafuatayo: historia, utamaduni, jiografia, lugha, uchumi na kadhalika.
Hivi masuala ya kama nani alikuwa mtawala wakati huu au ule, nani alifanya vita na nani na kadhalika, maelezo yake yatategemea uelewa wa wanadamu walioandika. Hayo ni masuala ya historia tu. Masuala ya watu walichumbianaje, walifungaje ndoa, ujauzito ulitunzwaje, mtoto mchanga alitunzwaje, maiti alizikwaje na kadhalika ni masual ya kiutamaduni ambayo ugumu na kueleweka kwake kunawategemea waandishi wanadamu.
Kana iko wapi, Nazareti kilikuwa kijiji cha aina gani, Sioni ilionekanaje, Bahari ya Shamu ilivukwa wapi na kadhalika maelezo yake ya kijiografia yanategemea uelewa wa kijiografia wa waandishi wanadamu. Neno ndugu au dada, tamathali za semi, nahau, methali na kadhalika vilimaanisha nini, maelezo yake yanategemea uelewa wa waandishi wanadamu. Dinari, shekeli, talanta na kadhalika zilikuwa pesa za thamani gani maelezo yake ya kiuchumi yanategemea uelewa wa kiuchumi wa waandishi wanadamu.

_*VITU TUNAVYOWEZA KUVIKOSOA KWENYE BIBLIA*_
Vitu tunavyoweza kukosoa sisi binadamu katika Biblia ni masuala yote yanayowahusu waandishi wanadamu wenzetu. Hayo ndiyo yanayohitaji na yanayoruhusiwa kukosolewa na siyo yale yanayosababishwa na mwandishi Mungu. Hivi sisi wanadamu tukitaka kuikosoa Biblia na kuibanisha usahihi au mapungufu tunayoruhusiwa kuyachambua ndiyo hayo ya historia, utamaduni, jiografia, lugha, uchumi na kadhalika.

Mwisho wa somo la tatu.
Admin. Titus Amigu
 
*SOMO LA NNE – AINA YA VITABU AU UANDISHI*

_AINA YA VITABU_

Tuendelee na masomo yetu. Baada ya somo letu la tatu, nilipata maswali muhimu kadhaa. Baadhi nilishayajibu lakini nikashtuliwa kwamba kuna mengine ambayo sikuyagusa. Nisiyoyagusa yalikuwa manne. Tangu wakati ule hadi leo maswali hayo manne sijayajibu bado. Sijayajibu kwa sababu nilikuwa nafikiria jinsi ya kuyafikisha kwenu pasipo kuharibu darasa letu. Hivyo si kwamba sina majibu yake, la hasha! Majibu yake yana ugumu unaopaswa kuondolewa kwanza. Basi, nikawa natafuta namna ya kuyaleta katika sura laini kwa wote. Nimechelea sana kuyaleta uwanjani na kuchokoza maswali mengine mia na ushehe kwa sababu ya kuwavurugeni. Hatimaye, kwa kusudi la kuzuia mkasa wa kulivuruga darasa, nimeona vyema nilete kwanza somo maalumu, somo la nne.
Somo hili linaeleza kitu kimoja tu: *mitindo au aina za uandishi zilizomo katika Biblia.* Aina za uandishi ni kitu kinachokuja kufuatia ushiriki wa mwandishi mwanadamu. Ni hivi, aina za uandishi zilizomo kwenye Biblia si aina moja. Aina, au mtindo, au tukitaka fani, kwa kizungu ni “genre”. Neno hili ni la Kifaransa lakini linatumika kama lilivyo katika Kiingereza.
Ni hivi, kusudi Mungu afanikishe nia yake ya kuwaletea wanadamu ujumbe wake mzito, aliwaruhusu na aliwasaidia waandishi wanadamu watumie aina au mitindo mbalimbali za uandishi.
Katika Biblia kuna walau aina kumi na nane za uandishi:
i. *Hadithi* – mfano masimulizi ya kuumbwa ulimwengu na vitu vilivyomo (katika kitabu cha Mwanzo)
ii. *Historia* – matukio ya Misri na masimulizi yote ya Kutoka (katika vitabu vya Torati na vitabu vya historia)
iii. *Usimuliaji wa mtiririko* – masimulizi ya maisha ya Abrahamu, Isaka, Yakobo n.k
iv. *Hekima* - vitabu vya Ayubu, Zaburi, Mithali, Hekima ya Sulemani, Wimbo Ulio Bora, Mhubiri na Yoshua bin Sira
v. *Zaburi (mashairi)* – mfano wimbo wa Musa (Kut 15), kitabu cha Zaburi, wimbo wa Zakaria (Lk 1:68-79), wimbo wa Bikira Maria (Lk 1:46-55), wimbo wa mzee Simeon (Lk 2:29-32)
vi. *Misemo ya kinabii* – katika vitabu vya manabii (vitabu vya Isaya mpaka Malaki)
vii. *Nyimbo* – mfano wimbo wa kuusifu utii wa Yesu (Flp 2:6-11)
viii. *Sala* – mfano sala ya Sulemani katika kulitabaruku hekalu (1Fal 8:22-61), sala ya Baba Yesu (Mt 6:9-13)
ix. *Injili* – mfano Injili za Mathayo, Marko, Luka na Yohane
x. *Mifano* – mfano katika Mt 13:1-50 na Mk 4:1-34
xi. *Miujiza* – masimulizi ya makuu ya Mungu (mfano katika Mk 1:21-34, Yn 2:1-12 n.k.)
xii. *Methali* – mfano katika vitabu vya Mithali na Hekima ya Sulemani
xiii. *Barua au nyaraka*: mfano barua au nyaraka 21 za Agano Jipya
xiv. *Uandishi wa kiapokaliptiko (ufunuo)* – Danieli 8-9, Mt 25, Mk 13 na kitabu cha Ufunuo
xv. *Lugha ya picha au isitiari* – mfano katika kitabu cha Mwa 1-3 na
xvi. *Lugha ya mafumbo* – mfano katika kitabu cha Ufunuo
xvii. *Lugha ya chuku (ndiyo kutilia chumvi)* – mfano habari ya mtu kukata miguu au mikono yake mwenyewe (Mt 18:6) au ngamia kupita kwenye tundu la sindano (Mk 10:25) na
xviii. *Lugha ya kinyume* – mfano katika Mk 4:12.


_UMUHIMU WA KUJUA AINA ZA UANDISHI_
Kuzijua na kuzipambanua aina za uandishi zilizomo kwenye Biblia ni muhimu, tena muhimu sana. La sivyo, Biblia inaweza kusomwa vibaya. Kwa maneno mengine, kujua aina za uandishi ndiyo msingi mmojawapo wa kujua kusoma na kutafsiri vizuri Biblia. Mfano, katika Agano la Kale, usisome wala kutafsiri vitabu vya Torati (ambavyo ndani yake kuna uandishi wa kihadithi, kihistoria, usimuliaji wa mtiririko, miujiza na sala) kama vitabu vya hekima. Wala usisome vitabu vya historia kama vitabu vya kinabii. Usisome zaburi (ambazo ni mashairi na sala) kama hadithi wala usisome vitabu vyenye hadithi kama vitabu vya nyimbo au sala na kadhalika.
Hali kadhalika, katika Agano Jipya mtu asisome Injili kama barua au barua kama kitabu cha kiapokaliptiko. Aidha, ndani yake mtu asisome sehemu zilizoandikwa kama zaburi au sala kama anasoma mambo ya kiapokaliptiko.
Basi, aina za uandishi ndizo zinazotofautisha vitabu vya Biblia. Lakini, wala si katika Biblia tu bali ndicho kinachotofautisha hata leo hii, barua za serikali na zile za kirafiki au na zile za mapenzi, matangazo ya kifo redioni na matangazo ya biashara, hotuba za kwenye mazishi na hotuba za kwenye sherehe za ndoa, magazeti ya dini na magazeti mengineyo kama MWANANCHI, MAJIRA, NIPASHE, TANZANIA DAIMA, MZALENDO, UHURU, MWANA SPOTI, DIMBA, IJUMAA, TANZANITE, TIMES, THE NEW AFRICAN ama NEWSWEEK, vitabu vya dini na vitabu vya hadithi, vitabu vya sayansi na vitabu vya lugha na kadhalika.

_NIA YA KUTUMIA AINA NYINGI ZA UANDISHI_
Mungu aliwaruhusu waandishi wanadamu watumie aina mbalimbali za uandishi ili wawaeleweshe wanadamu wenzao mambo mazito aliyokusudia wayaelewe vyema. Ni kama darasani, kusudi mwalimu awaeleweshe wanafunzi mambo magumu anaweza kutumia picha, nyimbo, hadithi, mifano na kadhalika. Mwalimu asiye mbunifu katika hayo mara nyingi huishia kujielewa mwenyewe tu.
Kumbe, msomaji wa Biblia hawezi kuufahamu vyema ujumbe wa Mungu pasipo kuelewa aina, fani au miundo ya vitabu vilivyo ndani yake. Kifupi, aina za uandishi zimetumika kama nyenzo za kubebea ujumbe wa Mungu asiyeonekana na asiyezungumza lugha za binadamu kwa midomo yenye mate kama yetu. Mungu hakutaka wanadamu wapokee ujumbe wenye utata isipokuwa unaoeleweka kama maji. Kwa kisa hicho akaruhusu hata waandishi wanadamu watumie hadithi za watu wao wenyewe kubebea ujumbe wa Mungu.
Mfano wa ruhusa hii unaonekana wazi katika sura za mwanzo za kitabu cha Mwanzo, sura 1-3, ambapo hadithi vya visasili vya watu wa Mashariki ya Kati zimetumika kuwaeleza watu kwamba kila kitu mwanzo wake ni Mungu, mamoja uwe ulimwengu na magimbe yake, dunia na vilivyomo ndani yake na hata wanadamu wenyewe. Hapo hadithi zimetumika kubebea vitu kama vikapu, magunia, viroba na rambo vinavyotumika kubebea vitu vyenye thamani kubwa. Ukipokea vitu hivyo unaweza kutenganisha kikapu, gunia, kiroba au rambo na kitu kilichobebwa. Usipoweza kutenganisha mambo kwa namna hiyo, ndiyo umeyakoroga mambo.

_UWEZEKANO WA KITABU KUWA NA AINA KADHAA ZA UANDISHI NDANIMWE_
Kwenye kitabu kimoja kunaweza kuwa na aina kadhaa za uandishi. Ufundi au umahiri wa waandishi wanadamu waliovuviwa na Roho Mtakatifu katika kuyaandika Maandiko Matakatifu ni mambo yanayotofautisha kitabu kimoja cha Biblia na kingine. Kila mwandishi aliandika kadiri ya wasikilizaji au wasomaji wake na hata lengo lake. Kwa kukidhi haja yake, wakati mwingine ilimpasa achague mara hadithi, mara usimuliaji wa mtiririko, ama shairi, mara wimbo au zaburi, mara mfano, mara isitiari, mara methali, mara lugha ya picha au lugha ya mafumbo au mtindo wa kiapokaliptiko na kadhalika. Mwishowe, kitabu chake kimoja kiliweza kuwa ndani yake na aina kadhaa za uandishi. Hivi ndani ya Injili, kwa mfano, kunaweza kuwa na historia, masimulizi ya miujiza, mifano, mithali, sala, sehemu ya kiapokaliptiiko na kadhalika. Mfano, chukua Injili ya Marko, ndani yake kuna sura za usimuliaji wa mtiririko, miujiza na mifano, ndiyo sura 1-12 na sura 14-16 na pia sura ya kiapokaliptiko, ndiyo sura 13. Ni lazima msomaji atambue jambo hili kusudi atafsiri atakayoyasoma kwa namna tofauti tofauti.
*Hatima:* Basi, maswali nitakayoyajibu yatahusika na aina tatu za mwanzo za uandishi: hadithi, historia na usimuliaji wa mfululizo.
Mwisho wa somo la nne (maandalizi ya kujibu maswali nisiyoyajibu bado).
*Admin: Fr. Titus Amigu*
 
Kwa UPENDO napenda kukualika Mitale na midimu katika semina hii ili tujifunze pamoja,tusiishie JF tuu tupige hatua nyingine katika kupata elimu zaidi ya biblia.

Ndani ya semina kuna muongozo,moja ya dhumuni ni kujidili biblia tuu na wala sio kundi au mtu yoyote yule.

Karibu bwana Mitale kupitia namba 0788462833 whatsup.
Huyu yupo sana....Sema anafyonza tartiib madini....
 
Ahsante Mkuu SALA NA KAZI kwa kutuwekea masomo yote humu
ahsante pia nikipata nafasi nzuri nitayapanga katika mtiririko mzuri pamoja na maswali yalioylizwa na majibu yake, na maswali yatakayoulizwa humu nitayapeleka sehemu husika halafu majibu nitayarudisha humu.

nafikiri nikakamilisha vizuri uzi nitaupeleka jukwaa la dini sababu hili ni jukwaa la matangazo sio darasa.
 
Ahsante Sana ila ukiuhamisha jukwaa,wengine hatuna access ya jukwaa la Dini na pia bado hatujaungwa kwa group ,je utatusaidiaje hapo
ahsante pia nikipata nafasi nzuri nitayapanga katika mtiririko mzuri pamoja na maswali yalioylizwa na majibu yake, na maswali yatakayoulizwa humu nitayapeleka sehemu husika halafu majibu nitayarudisha humu.

nafikiri nikakamilisha vizuri uzi nitaupeleka jukwaa la dini sababu hili ni jukwaa la matangazo sio darasa.

MTC | 101| [emoji769]
 
Hii kitu ingekuwa Dar ningejiunga. Nina maswali mengi mno ambayo natamani nipate majibu ya kina na najua ni wanazuoni wa Kikatoliki tu ndio wanaweza kuja na facts na kuondoa sintofahamu yangu maana wale wengine maswali yakiwa magumu wanakwambia okoka kwanza ili uelewe maana mambo mengi ni ya kiroho sana!

Yani swali likiwa gumu linahamishiwa kwenye state ya "kiroho" na hoja inafia hapo.
Mkuu umenichekesha sana, hiyo mambo nimekutana nayo kama wiki mbili zilizopita kuna nabii kila akija daily tunajadili mambo mbalimbali. Sasa nikaanza ku'apply u'Kiranga kilichoambulia nikuambiwa niokoke ndio nitapata majawabu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ahsante Sana ila ukiuhamisha jukwaa,wengine hatuna access ya jukwaa la Dini na pia bado hatujaungwa kwa group ,je utatusaidiaje hapo

MTC | 101| [emoji769]
basi kama ni ivo nitauweka jukwaa la habari na hoja mchanganiko au jamii intelligence. ikitokea wameuhamishia jukwaa la dini basi tutaendelea huu uzi
 
Huyu yupo sana....Sema anafyonza tartiib madini....

Kuna Group la WhatsApp la Wasabato nipo humo, wengi wao wanakunwa na hoja za mafundisho ya Kikatoliki kimyakimya kama ulivyosema na wengine wanakiri hadharani. Na wengine ma-fundamentalist wanajiondoa katika Group wanapoona ukweli fulani. Sasa ili kukwepa kujikuta wanauongokea Ukatoliki wanaona bora "wausepe" ukweli.
 
Mkuu umenichekesha sana, hiyo mambo nimekutana nayo kama wiki mbili zilizopita kuna nabii kila akija daily tunajadili mambo mbalimbali. Sasa nikaanza ku'apply u'@Kiranga kilichoambulia nikuambiwa niokoke ndio nitapata majawabu.

Msabato mmoja katika Group la WhatsApp la Kisabato aliulizia maana ya WANEFILI wanaoongelwwa katika Kitabu cha Mwanzo 6:1-4 akajibiwa aende akanunue Bible Commentary asome. Muuliza swali alipodai yuko remote area kiasi kwamba hawezi kuipata bado akalazimishwa atoke akaitafute. Mimi nilitoa majibu na mpaka Leo sijapata mtu Wa ku-challenge ishara ya kwamba walikubaliana na tafsiri ya Kanisa Katoliki.

Kwa hiyo,ninachojifunza ni kwamba hawa watu wanajibu tu waliokaririshwa,na nje ya hapo hugeuka wapole mithili ya Kuku Wa Kichina walioshikwa na mdondo.
 
Kuna Group la WhatsApp la Wasabato nipo humo, wengi wao wanakunwa na hoja za mafundisho ya Kikatoliki kimyakimya kama ulivyosema na wengine wanakiri hadharani. Na wengine ma-fundamentalist wanajiondoa katika Group wanapoona ukweli fulani. Sasa ili kukwepa kujikuta wanauongokea Ukatoliki wanaona bora "wausepe" ukweli.
Ni kweli kabisa....

Hii ni plat form yetu kuwapa elimu....

Wataelimika tuu....ni swala la muda
 
Kwa hiyo,ninachojifunza ni kwamba hawa watu wanajibu tu waliokaririshwa,na nje ya hapo hugeuka wapole mithili ya Kuku Wa Kichina walioshikwa na mdondo.
Ni kweli kabisa...wapo kama programmed machines....Hicho kilichokuwa installed kwenye bongo zao, ni hicho hicho....ukiwatoa nje ya box wanabaki kuduwaa kama maduwanzi
 
Mkuu nilipoteza namba niliyokua nimeungwa kwenye group!
Naomba unipm tuone utaratibu wa kunirudisha..!!
Kwanini ulibadirisha ID?

Sent from my GT-I9300 using Tapatalk
Sikubadilisha ni baada JF kufungiwa mwaka jana ilipofunguliwa id yangu ilishindwa kudisplay na nimejaribu sana kuirudisha lkn imeshindikana.

Nakutumia namba za admn Mkuu Fr Titus Amigu pm.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom