Karibuni tuijadili hii Biashara

Karibuni tuijadili hii Biashara

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
14,588
Reaction score
32,361
Wakuu nilikuwa nataka ninunue hii mikeka mbao (SPC Flooring) kwa ajili ya nyumbani kwangu ila kwenye mchakato ndo nikaona mbona hii kitu inataka kuwa fursa ya biashara?

Hii PVC flooring huambatana na vitu kama Wall Panels zinazotumiwa sana kama decoration kwenye majumba. Kimsingi kuna items nyingi zinauzwa pamoja na mikeka mbao. Picha kadhaa nimekuwekea.

Nini changamoto kubwa ya hii biashara? Karibuni tujadili.

1741262826062.png
1741262793266.png
1741262758548.png
1741262753430.png
1741262748935.png
1741262744313.png
1741261235286.png
 
Umenikumbusha mbali sana kuna nyumba nilipanga mwenye nyumba akasema hataki nyumba yake itobolewe hata kuweka tv ukutani hakuna
Yupo sahihi unaanzaje kutoboa ukuta, ukihama umwachie matobo aikija mwingine atopoe kwa engo yake... Marufuku!
 
Kuna mwenye nyumba mpuuzi, nilihama ghafla nikamuachia kodi ya miezi miwili (600k).

Alivyo hana aibu ananipigia simu eti kwanini ulitoboa nyumba yangu..... Nikamwambia mzee em kwa hiyo kodi niliokuachia toa fungu dogo repair hapo nilipotoboa, akakata simu.
 
Mimi naona wenye nyumba wangekuwa wanaongeza kodi kidogo kwaajili repairing pale mpangaji atakapohama

Mpangaji hapangishi kuja kumtunzia mwenye nyumba nyumba yake.

Mpangaji anataka chumba chake aninginize frames za picha (lazima atatoboa ukuta), mpangaji anataka aninginize TV (lazima atatoboa ukuta)
 
Bado hii biashara kwa Tanzania inafanywa kijima mno.
 
Kuna mwenye nyumba mpuuzi, nilihama ghafla nikamuachia kodi ya miezi miwili (600k).

Alivyo hana aibu ananipigia simu eti kwanini ulitoboa nyumba yangu..... Nikamwambia mzee em kwa hiyo kodi niliokuachia toa fungu dogo repair hapo nilipotoboa, akakata simu.
Pole huyo alikuwa mpuuzi pro max
 
Hata kama ni ww huwezi kukubali nyumba Yako itobolewe labda ukapange zile za uswahilini za bei ya chini mkuu
Kutoboa kuweka tv mimi sioni kama hiyo ni shida mkuu ila kwenye kuweka picha na makorokoro mengi huko ndiyo shida
 
Mkuu ukitoboa ukuta wa nyumba, ni kama umetoboa roho yake mwenye nyumba. haujui tu ni namna Gani wanavyofeel, yani hapo kurepair ukihama inamchukua ghalama sana haujui tu siku tukijaaliwa ukajenga utagundua mwenye nyumba alikuwa sahihi
 
Tena nyumba ikiwa mpya ndiyo hatari zaidi
 
Back
Top Bottom