Karim Mandonga Mtu Kazi azawadiwa gari

Karim Mandonga Mtu Kazi azawadiwa gari

Bondia Mtanzania Karim Mandonga amekabidhiwa gari aliyoahidiwa endapo angeshinda pambano lake nchini Kenya, amepewa zawadi ya gari hilo aina ya Nadia na Mfanyabiashara Dick Sound bila mashariti yoyote ikiwa ni sehemu ya kutimiza ahadi aliyokuwa ameahidiwa endapo angeshinda pambano hilo.

Tukio hilo limefanyika leo hii katika Ofisi za DickSound Mall @dicksoundmall maeneo ya Magomeni Dar es salaam ambapo Dick amesema “Nimempa kama zawadi siyo kwa ajili ya Ubalozi, alikuja kwangu wakati anaenda kupambana nikamuahidi akishinda nitaweza kumpa gari, wakati akiwa Kenya nikaona video nikamtumia kumwambia umeniangusha ushapigwa, akasema hapana sio kweli Mimi ndio napanda kupambana, hivyo leo tumemkabidhi kumpongeza na kutimiza ahadi”

Kwa upande wa Mandonga “Namshukuru sana DickSound Kwa hili leo ndoto yangu imetimia, Mandonga anaondoka na usafiri Mungu mkubwa
Betting inalipa wazee sio utani, betting inalipa sana, alienielewa kanielewa
 
Toyota Nadia ni gari ya kumpa mtu kweli in 2023? Nadia ilikuwa discontinued in 2003 maanake huwezi kupata Nadia ambayo haina miaka si chini ya 19 at least. Hili gari bora akalitupe azawaizi ni tripu za shamba, gereji, shamba, gereji
Shukuruni kwa kila jambo. Usipoweza kushukuru kwa jambo dogo utaweza kwa jambo kubwa?
 
Hata angepewa range rover iliyotoka 20 years ago ni upumbavu. Next time usiwe kama ling’ombe. Ishu sio brand wala model ya gari. Ishu ni for how long that car has been in use. Usitumie kichwa kama mfuko wa kubebea meno pekee.
Amiii punguza munkali weyee
 
Kibongo bongo, watu wanaopata umaarufu wa ghafla huwa kwenye peak kwa miezi kama 6 tu, baada ya hapo umaarufu hupotea...wako wapi sasa watu kama Pierre, Uchebe, Chikumbalaga aka Sukari yao, yule dogo wa Irudiweee...
 
Na kweli jamaa inaonesha aliweka mzigo mrefu kwa mandonga.
Ndio kaweka ndefu kapiga ndefu kwenye 100 akampa 20 anapata hasara gani? Betting inalipa hii michezo watu wanapiga pesa, anaweza akacheza jingine akaambiwa apigwe yaan apoteze pambano na akipoteza watu wanaingiza pesa, betting inalipa wenye akili ya pesa
 
Bondia Mtanzania Karim Mandonga amekabidhiwa gari aliyoahidiwa endapo angeshinda pambano lake nchini Kenya, amepewa zawadi ya gari hilo aina ya Nadia na Mfanyabiashara Dick Sound bila mashariti yoyote ikiwa ni sehemu ya kutimiza ahadi aliyokuwa ameahidiwa endapo angeshinda pambano hilo.

View attachment 2485210

Tukio hilo limefanyika leo hii katika Ofisi za DickSound Mall @dicksoundmall maeneo ya Magomeni Dar es salaam ambapo Dick amesema “Nimempa kama zawadi siyo kwa ajili ya Ubalozi, alikuja kwangu wakati anaenda kupambana nikamuahidi akishinda nitaweza kumpa gari, wakati akiwa Kenya nikaona video nikamtumia kumwambia umeniangusha ushapigwa, akasema hapana sio kweli Mimi ndio napanda kupambana, hivyo leo tumemkabidhi kumpongeza na kutimiza ahadi”

Kwa upande wa Mandonga “Namshukuru sana DickSound Kwa hili leo ndoto yangu imetimia, Mandonga anaondoka na usafiri Mungu mkubwa
Imenikumbusha zile Noah tulizoahidiwa Watanzania.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Bora umpe ushauri huo maana hela mwanaharamu.

Mastaa wengi duniani huona ufahari kuwa wahuni na wavuta Unga pindi wanapozipata.

Unashangaa jitu kubwa likipata hela linarudi utoto.
Pata hela tujue tabia yako,

Mkuu hela haimbadili mtu tabia bali ule ndio uhalisia wake,sema tu uhalisia wake ulikua umefichwa na umasikini wake.
 
Back
Top Bottom