Memtata
JF-Expert Member
- Jul 27, 2013
- 587
- 1,863
Nilishawahi kuumizwa sana kimapenzi enzi hizo lakini kuna hawa wawili hadi leo sijawahi kuwasahau, Spice na Cathe (si majina halisi)
Huyu Spice alinionyesha kunipenda sana lakini alikuja kunikimbia kila alipokuwa ananiona, hakutaka hata kusimama na mimi japo kusalimiana kumbe aliambiwa na watu mimi ni HIV+. Kilichoniuma ni kwanini alipopata taarifa hizo asiniambie tupime yeye akaanza kunikimbia?1. Baadae alikuja kuolewa na jamaa mmoja nchi za Ulaya huwa nachat nae mara moja moja fb na inaonekana anaishi maisha mazuri tu japokuwa sifahamu kwa undani wake.
Cathe tulianza mahusiano baada ya kumaliza kidato cha nne alikuwa anaishi vijijini huko alipokuja mjini kwa mama yeke mi nikadaka. Alikuwa mshamba nikambadilisha hadi kuwa sister du, nilimsaidia kwa mengi hasa matumizi akiwa chuo hadi maza alinijua na kwao nilienda bila kipingamizi. Alipomaliza certificate pale mjini akakomaa ahame mkoa kwenda kusoma diploma. Nilimshauri asomee hapo nilipo akagoma basi nikamruhusu. Siku chache kabla ya safari yake akanitumia sms... 'Naona sitaweza kuendelea kuwa na wewe' can you imagine?! Niliachwa kwa meseji! 🤣
Cathe aliniuma sana maana tulikuwa na mpango wa kuoana hadi wazazi wa pande mbili walijua hivyo, nilibembeleza hakukubali kabisa nikamuacha aende lakini nilimlaani na kujisemea "She must regret!"..... Regret my foot! Miezi michache baada ya kumaliza chuo akanitaarifu kwamba anaolewa, nilikuja kujua huyu mume wake alikuwa anaishi huku kwetu kabla ya kuhamishwa kikazi mkoa. Huyu naye kwa muonekano ana maisha mazuri baada ya kuachana na mimi jamaa aliyemuoa anaonekana kuwa na kipato zaidi yangu.
Je hawa walionitenda walikuja kwangu kulipiza niliowahi kuwaumiza tu na wao hawana hatia ya kulipiziwa?! Ni mawazo tu kwa sasa nawaombea mema sina kinyongo nao kabisa japokuwa roho iliniuma haswa🤣 🤣 🤣