Karma inaniumiza sana mwenzenu

Karma inaniumiza sana mwenzenu

Nawasalimu kwa dhati wanajamii wenzangu.Mara zote nimekuwa nikijifunza kutoka kwa wanajamii wenzangu humu na hata juu ya hili ninaamini nitapata suluhisho lake humu .Nimekuwa mkimya kwa muda sasa kutokana na kupata sononeko kuu linalotokana na mashindano kati ya mwili na roho.
Ninaamini humu kuna wataalamu wa "karma"naombeni mnishauri nifanye nini maana ni kama nahisi kuna kitu nakosea na sijakifanya lakini bado kitu hicho ni muhimu nikifanye.
Natanguliza shukrani.
Wewe mlakimtoto ukiacha tu kula huyo mdudu mambo yatakunyookea vibaya mno.
 
Tuambie nini kimekukuta, au wewe ndo yule askari magereza aliewapiga wabunge wanchada hadi kuwavunja mikono?
 
Binadamu wamejawa na kumbukumbu katika mawanda yake yote.Hakuna tunachokifanya nje ya kumbukumbu tukio nazo kwa kujua au kutokujua.
Mathalani hata kumbukumbu ya muonekano wa mtu inatunzwa kwenye D.N.A. n.k.."we are full of memories"..tatizo ni kwamba inanisumbua sana.

Unaweza kuistopisha karma,ngoja Akina Mshana jr wakushauri kwanza,ukishindwa nimtafute ntakupa njia sahii ya kuescape au kuondoa karma.
 
Uongo. Hito siyo maana ya karma mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Nisaidie na wewe kwa maana nielewavyo Mimi karma ni jumla ya kumbukumbu ya kila unachofanya na ulichofanya na walichofanya watu wa karibu yako ambacho hitback yake humuandama mtu.
Ukisikia utavuna ulichopanda=karma.
Karma haikosei.
Nipe maana nyingine zaidi
 
Unaweza kuistopisha karma,ngoja Akina Mshana jr wakushauri kwanza,ukishindwa nimtafute ntakupa njia sahii ya kuescape au kuondoa karma.
Hapo ndiyo haswaa nilikuwa nahitaji.
 
Back
Top Bottom