GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Okrah ndiyo kwa 99% alisababisha Mzungu Wetu Dejan asiwe na Furaha ndani ya Simba SC mpaka Kukereka na kufikia Kuchukua yale Maamuzi aliyoyachukua ya Kuondoka.
Okrah huyu huyu ndiyo alikuwa akimtukana Mzungu wa Watu Dejan na Kubwa zaidi akiwashawishi Wachezaji wenzake Waswahili wamtenge, wambague na kubwa zaidi wasiwe wanampa Pasi Uwanjani kitu ambacho kilitokea mno tu.
Mzungu wa Watu Dejan alililalamikia zaidi hili hasa kwa Uongozi na Benchi la Ufundi ila hakupata Ushirikiano wowote ule sana sana alizidi tu Kunyanyasika ukichanganya na hata Lugha zenyewe tu za Kiswahili na Kiingereza Kwake zilikuwa tatizo ndiyo balaa tupu.
Baada ya Mzungu wa Watu Dejan Kuondoka zake Simba SC sasa yule yule Okrah aliyekuwa Akimfitini nae Kibao Kimemgeuka na hana tena Furaha Kikosini Simba SC kwani kuanzia Benchi la Ufundi, Uongozi na hata Wachezaji wenzake ( baadhi na Waandamizi ) hawamkubali tena kutokana na tabia yake ya kupenda Majungu, Kusengenya na Dharau ya Kiasili aliyonayo huku akitamba kuwa ana Kipaji na anatokea Taifa la Ghana ( Brazil ya Afrika) hivyo hakuna wa Kumtisha Tanzania na hata kwa Wachezaji Wengine wa Ukanda Wetu huu wa EAC na COSAFA.
Wanadamu tujitahidi sana kutokuwa Wafitini kwa Wenzetu na Kuwaharibia Maisha yao kwani hakuna Dhambi ambayo utaifanya hapa duniani kwa Mtu isiyemstahili au unayemuonea halafu isikurudie tena mara mbili yake.
Pole sana Okrah na hapo bado!!!!!