#COVID19 Karma ni hatari: Mzanzibar aliyebeza COVID-19 huko ughaibuni, imempata

#COVID19 Karma ni hatari: Mzanzibar aliyebeza COVID-19 huko ughaibuni, imempata

Uchanje, usichanje utakufa tu! Siku za kuishi binadamu ni chache sana.
 
Huyo dada anavyoongea...

Huku kitaani kwetu huwa kibaka hapigwi bali huitiwa wadada wanaoongea kama huyo, wanamsuuuta weeee kibaka hadi anaanza kulia na akiyoka hapo anaachana kabisa na udokozi
Huko kwenu vyumba bado vipo? Ninahitaji kimoja.
 
Kwani ukichanjwa ndio hupati huo ugonjwa? uchanje au usichanje ikifika utaupata tu
Ukichanja unaimarisha kinga mzee.
Kuchanja ni sawa na kufunga milango wakati unaenda kulala. Si kwamba ukifunga mlango huwezi ibiwa, bali inapunguza urahisi wa kuibiwa.

Huwezi sema ulale milango wazi kwakuwa mwizi anaiba hata ukiwa umefunga milango.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Kwani ukichanjwa ndio hupati huo ugonjwa? uchanje au usichanje ikifika utaupata tu

Nilivyockia kuambukizwa unaambukizwa ata kama umepata chanjo, but haitakusumbua. Tofauti na ambae hajapata chanjo ikimpata itamsumbua na hata kufa.
 
Baada ya kuchanjwa ndio hawataugua tena?? Mbona tumeamua kuacha kufikiri? Kwani wanaokufa wote hawana chanjo?
Kwa logic yako ni kwamba hata hospitali hazina haja kuwepo kwani ni watu wengi tu wanapelekwa hospitali lakini bado wanakufa.

Jiangalie kama unafikiria vema.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Mwendazake aliikandia na kuikebehi ikaamua kusepa naye na kijiji, hilo Dude ni kuomba tu lisikukute ni suala lingine kabisa hilo Jombaa
 
Back
Top Bottom