KARMA: Tulishangilia wakati wengine wanalazimishwa kulipa kodi za dhuluma, sasa yameturudia inabidi tushangilie

KARMA: Tulishangilia wakati wengine wanalazimishwa kulipa kodi za dhuluma, sasa yameturudia inabidi tushangilie

escrow one

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2014
Posts
1,473
Reaction score
2,868
Kwa miaka takribani sita iliyopita matajiri hawakupumua nchi hii, kodi za dhuluma ziliwaelemea. Kesi za uhujumu uchumi ziliwazunguka, akaunti zao zilifungwa na wengine ilibidi wahame nchi.

"Wanyonge" walishangilia kwa vifijo, miluzi na tarumbeta. Hawakujua nao yangekuja kuwatokea.

Hivi sasa wameongezewa kodi kidogo tu wamehamaki, wanalia na kuomboleza. Acha yatupate tuone uchungu wa kile tulichokuwa tukishangilia kwenye mikutano na vijiweni. Tujue ilivyo ngumu kulipa kodi ya dhuluma.
 
Wewe ni mwongo mnafiki mzandiki na kizabizabina. Hakuna aliyefurahia kuwekwa ndani kwa dhuluma hao waliobambikiwa kesi za kodi.

Badala yake wapinzani na ma ccm wanafiki na wana ccm wapenda haki wote waliungana kumpongeza mama kwa kuwaondolea vifungo hao wafanyabiashara sambamba na kurejeshewa kodi zao.
 
Kinachosikitisha,
Kwenye ishu Kama hizi zinazogusa wananchi moja kwa Moja.

Huwezi kuwasikia YANGA wakikemea ilo.

Sijajua Hii timu inayojiita Ni ya wananchi,
Inahusika na wananchi wa nchi gani[emoji3525]
 
Kinachosikitisha,
Kwenye ishu Kama hizi zinazogusa wananchi moja kwa Moja.

Huwezi kuwasikia YANGA wakikemea ilo.

Sijajua Hii timu inayojiita Ni ya wananchi,
Inahusika na wananchi wa nchi gani[emoji3525]
Tunako elekea mpaka IHEFU fc nayo italaumiwa sasa kwa kukaa kimya!!
 
Wewe ni mwongo mnafiki mzandiki na kizabizabina. Hakuna aliyefurahia kuwekwa ndani kwa dhuluma hao waliobambikiwa kesi za kodi.

Badala yake wapinzani na ma ccm wanafiki na wana ccm wapenda haki wote waliungana kumpongeza mama kwa kuwaondolea vifungo hao wafanyabiashara sambamba na kurejeshewa kodi zao.
Hela iliondoka serikalini, je itarudije? Ni tozo tu. Mwaka huu michadema itajificha wapi
 
Ungetaja hata mmoja aliyebambikiwa kodi hapo kabla ingekuwa poa sana
 
Back
Top Bottom