Ngongo
Platinum Member
- Sep 20, 2008
- 20,654
- 35,887
Heshima sana wanajamvi,
Tanzania ilipata uhuru wake zaidi ya miaka 60 iliyopita.Tumepitia awamu mbali mbali kuanzia awamu ya kwanza ya Mwl Nyerere hadi sasa awamu ya sita ya Mama Samia Suluhu.
Nimekuwa nikitatizwa na namna tunavyojitawala,hasa katika suala la zima la mamlaka ya uteuzi wa nafasi mbali mbali kama RC au DC.
Hizi nafasi za RC or DC zinahusika moja kwa moja na maisha ya wananchi wengi.Nimejaribu kufuatilia mamlaka ya Wakuu wa Mikoa au Wakuu wa Wilaya katika maeneo yao ya kazi nikaona wamekuwa na nguvu kuliko viongozi wanaochaguliwa na wananchi kama Wabunge au Madiwani.
Wakuu wa Wilaya na Mikoa wana uwezo wa kuwaweka ndani wananchi pia ni wenyeviti wa ulinzi na usalama katika maeneo yao ya kazi.
Wakuu hawa wapo katika maeneo ya kazi kwa maana ya Wilaya na Mikoa kwa ridhaa ya Rais na si wananchi !.
Hapa ndio mgogoro unapoanza,mfano mzuri ni Mkuu wa Wilaya ya Hai kama wananchi wangekuwa na uwezo wa kumwadhibu wengefanya hivyo siku nyingi.Matokeo yake Wakubwa hawa wanajitahidi kwa kadri ya uwezo wote kimfurahisha Rais au kutenda mambo ambayo yatampendeza Rais na si wananchi.
Utaratibu huu uliopitwa na wakati unasababisha wananchi wa maeneo mbali mbali kuongozwa na viongozi ambao hawana ridhaa nao.
Leo hii wananchi wa Mkoa wa Manyara wameletewa Makongoro Nyerere kuongoza Mkoa wao pasipo kuhusika kwa namna yoyote katika uteuzi wake.Mambo ni hayo hayo katika Mikoa yote na Wilaya zote.
Naomba kuwasilisha,
Ngongo Safarini Zanzibar kwa mapumziko mafupi na kusheherekea sikukuu ya Idd.