Karne 21 bado ni sahihi DC & RC kuteuliwa na Rais?

Kile kiti sijui huwa kina nini! Wimbo ni huo huo toka enzi za Nyerere!
Jk aliuanzisha mchakato wa katiba mpya,ila shida naona ilikuwa ni wazalendo maslahi ndio waliouteka mchakato ule na kuuchelewesha

Hadi muda wake haukutosha kuukamilisha,na mtazamo wangu ni kuwa wenye maslahi yao walihakikisha aliyefuata ni mtu siyetayari kuuendeleza mchakato ile malengo yao yatimie,japo hali haikuwa kama matarajio yao.
 
Kwa mamlaka aliyopewa Rais kwa mujibu wa katika hakuna tatizo...
 
Pengine swali lingekuwa...upo umuhimu was kuwa na maRC na maDC??
 
Kama bado wakuu wa wilaya na mikoa hawawajibiki kwa wapiga kura, tuna kazi ngumu ya kupata maendeleo!!

Kama tunavowashutumu wabunge kwa kutoleta maendeleo, wakuu wa mikoa wawe na wajibu pia. Kama vipi watoke tu. Maendeleo hayajawahi kuwa jambo la level ya mkoa. Ni jimbo!!!
 
Pengine swali lingekuwa...upo umuhimu was kuwa na maRC na maDC??
Kamanda: mbona mambo unaishia nusunusu? Askofu wako anateuliwa Roma, Headmaster anateuliwa na Ndalichako Dodoma, na Mkurugenzi wa Fedha anatokea NBAA Dar es Salaam? Kweli bwana, sasa tumesoma vya kutosha kila Kijiji tuwe na Mganga wetu, Mufti wetu, RPC (sorry, VPC) wetu, Askofu wetu, TAKUKURU wetu, Supika wetu. Vipi, mpe tundulissu aongeze kwenye Ilani yake, last time aliishia majimboni sasa twende vijijini kabisa, eh?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…