Nimekuwa nikipiga kelele humu JF serikali ianzishe kitu kinachofanana na EWURA kwenye maji na nishati kwa masuala ya ELIMU lakini serikali imekaa kimya kwa kuwa miradi hii ya shule binafsi ni ya kwao. Sekondari ya Baobab iliyoko nje kidogo ya Jiji la Dar, barabara ya Bagamoyo, imepandisha KARO kwa zaidi ya 30% kutoka shs 2,600,000.00 tulizolipa mwaka huu hadi shs 3,375,000.00 kuanzia January mwakani.
Wamefanya hivo bila kutujulisha wazazi tujiandae kwa badiliko hili na baadhi yetu tuna watoto wanaingia kidato cha nne mwakani hivyo ni vigumu sana kuwahamisha watoto hawa. Elimu sasa imekuwa ni BIASHARA kubwa. Elimu sasa itabaki kwa WATANZANIA wachache!
Kibaya zaidi wameagiza karo hii mpya ilipwe kwa awamu mbili tu. January tulipe milioni mbili( 2,000,000.00) na June tulipe shs 1,375,000.00. Tunaiomba serikali sikivu ya JK iingilie kati suala hili. Wakati huohuo nawaomba wazazi/walezi wenzangu tukutane haraka ili tulijadili ongezeko hili ambalo ni wizi wa mchana.