Karo ya shule baobab yapanda ghafla

Karo ya shule baobab yapanda ghafla

WildCard

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2008
Posts
7,505
Reaction score
2,416
Nimekuwa nikipiga kelele humu JF serikali ianzishe kitu kinachofanana na EWURA kwenye maji na nishati kwa masuala ya ELIMU lakini serikali imekaa kimya kwa kuwa miradi hii ya shule binafsi ni ya kwao. Sekondari ya Baobab iliyoko nje kidogo ya Jiji la Dar, barabara ya Bagamoyo, imepandisha KARO kwa zaidi ya 30% kutoka shs 2,600,000.00 tulizolipa mwaka huu hadi shs 3,375,000.00 kuanzia January mwakani.

Wamefanya hivo bila kutujulisha wazazi tujiandae kwa badiliko hili na baadhi yetu tuna watoto wanaingia kidato cha nne mwakani hivyo ni vigumu sana kuwahamisha watoto hawa. Elimu sasa imekuwa ni BIASHARA kubwa. Elimu sasa itabaki kwa WATANZANIA wachache!

Kibaya zaidi wameagiza karo hii mpya ilipwe kwa awamu mbili tu. January tulipe milioni mbili( 2,000,000.00) na June tulipe shs 1,375,000.00. Tunaiomba serikali sikivu ya JK iingilie kati suala hili. Wakati huohuo nawaomba wazazi/walezi wenzangu tukutane haraka ili tulijadili ongezeko hili ambalo ni wizi wa mchana.
 
Du asanteeeee kwani kuna tofauti gani ya kusoma baobab au st kayumba? Mbona sie tumesoma kayumba na tumepiga points za ukweli yani one za ukwenheee!! Ushamba tu wa wazazi wengine!! 2.6m??? Mie nitasomesha gov xul tu ada sh 70k kwa mwaka kula bure!!
 
Tulianza na shule hizi karo ikiwa milioni moja na ushei miaka minne iliyopita. Walimu wote wazuri wamehamia huko. Lakini kwa kuwa hakuna udhibiti wa aina yoyote kwenye shule hizi hali ndio hiyo. Karo zinapanda kila mwaka kwa viwango vya kutisha. Tunahitaji Regulatory Authority kwenye ELIMU ya NCHI hii.
 
Duh. 3.75 kwa elimu ya sekondari hii hii au? Bora nimpeleke akasome nje kupunguza gharama. Khaaaaaah

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Mi wanangu siwezi wapeleka kwenye mishule ya gharama kiasi hicho wakati kuna shule
za serikali mtoto akiwa serious anachomoka na matokeo mazuri tu,mi sijawahi kusoma shule ya private
hata moja,kuanzia nursery mpaka chuo na nimefaulu vizuri tu with flying colours.
Wazazi msiadaike na hizo private school,siku hizi watu wanafanya business,kama mtoto ana akili
ana akili tu
 
Pole mkuu, its too much. Na si vyema kumtoa shule 'nzuri' kumpeleka ya kawaida
 
Nakuelewa mkuu Wildat kwamba inauma hela ndefu hivyo kukutoka ghafla lakini kumbuka siku hizi biashara ni huria na kama mtu huna uwezo kwanini kumpeleka kule Baobab? Unapoamua kumpeleka mtoto shule binafsi jipange sababu jamaa wanapandisha kadri wanapoona inafaa!! Nakushauri usimpeleke huyo wa pili kule tena. Pole sana lakini mkuu!!
 
Mi wanangu siwezi wapeleka kwenye mishule ya gharama kiasi hicho wakati kuna shule
za serikali mtoto akiwa serious anachomoka na matokeo mazuri tu,mi sijawahi kusoma shule ya private
hata moja,kuanzia nursery mpaka chuo na nimefaulu vizuri tu with flying colours.
Wazazi msiadaike na hizo private school,siku hizi watu wanafanya business,kama mtoto ana akili
ana akili tu
Enzi hizo kweli shule za SERIKALI zilikuwa nzuri sana. Ilikuwa ni AIBU kubwa mtu kufeli mtihani wa darasa la saba. Ilikuwa ni aibu pia kwenda kusoma private schools. Ulionekana mjinga. Sasa ni vice versa. Kwenda kusoma shule ya serikali ni adhabu. Shule hizi ziko hoi bin taaban. Hazina WALIMU, hazina MADARASA ya kutosha, haziina mabweni, haziina VITABU, haziina MAABARA, haziina MAKTABA, hata VYOO hakuna!

Hali hii imefanywa makusudi kabisa ili WAZITO wa NCHI hii wafanye BIASHARA ya ELIMU. Shule hizi za PRIVATE zinamilikiwa na WANASIASA wetu, Wakuu wetu wa TAASISI za UMMA na madhehebu ya DINI.
 
Nakuelewa mkuu Wildat kwamba inauma hela ndefu hivyo kukutoka ghafla lakini kumbuka siku hizi biashara ni huria na kama mtu huna uwezo kwanini kumpeleka kule Baobab? Unapoamua kumpeleka mtoto shule binafsi jipange sababu jamaa wanapandisha kadri wanapoona inafaa!! Nakushauri usimpeleke huyo wa pili kule tena. Pole sana lakini mkuu!!
Kwa nini tuna-regulate:
-Mawasiliano(TCRA);
-Nauli(SUMATRA);
-Mifuko ya Jamii(SSRA);
-Maji na nishati(EWURA);
Tumeshindwa ku-regulate ELIMU? Hivi kati ya vyote hivyo kuna kilicho muhimu kuliko ELIMU nchi hii?
 
watoto wangu wapo nursery, teacher anataka pesa ilipwe yote 1.6 kwa mtoto mmoja bila installments. remeber nina twins! hataki kuongea, hataki kumsikiliza mtu, ni mama wa kighana! kwa kweli serikal iingilie kati, laasivyo twafwa!!
 
Mi wanangu siwezi wapeleka kwenye mishule ya gharama kiasi hicho wakati kuna shule
za serikali mtoto akiwa serious anachomoka na matokeo mazuri tu,mi sijawahi kusoma shule ya private
hata moja,kuanzia nursery mpaka chuo na nimefaulu vizuri tu with flying colours.
Wazazi msiadaike na hizo private school,siku hizi watu wanafanya business,kama mtoto ana akili
ana akili tu

Umesoma miaka ipi? Shule gani? Maana kama ni Kibaha, Ilboru, Kilakala, Mzumbe una haki ya kusema hivyo. Kwa mtoto wa kijijini per se na shule za Kata forget about flying colours! Kama ni kata za mjini, it is possible maana unaweza kupata supplement baada ya kutoka shule, siyo kijijini per se ambapo watu wanafanya mambo as if hakuna serikali!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! watu wanajua mpaka leo kuwa Nyerere bado anatawala!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
cacico watoto wetu wako shule moja nini? Hili balaa sasa
 
Last edited by a moderator:
mkuu sii rahisi kusikilizwa kilio chako,watoto wa JK,BILAL wanalipa 4m feza primary,wa RAGE wote wapo australia,usa
 
Elimu hatuwezi regulate maana nyingi ni za hao hao wa Wizara ya Elimu au pia kuna shareholding!!! Ilishapigiwa kelele na hakuna jipya!!! Kila shule ni inajiamlia inavyotaka yenyewe tu. Serikali sikivu!! Feza boys/Girls hivi siku hizi haijafika 10m kweli?
 
watoto wangu wapo nursery, teacher anataka pesa ilipwe yote 1.6 kwa mtoto mmoja bila installments. remeber nina twins! hataki kuongea, hataki kumsikiliza mtu, ni mama wa kighana! kwa kweli serikal iingilie kati, laasivyo twafwa!!

Aisee pole sana!!! Kuna moja inalipwa 2.4 Nursery, bado uniform!!!! Kweli serikali sikivu au dhaifu!!! Huwezei kufanya market mechanism kwa kitu muhimu kama elimu!!!! Ni mwiko!! Matokeo yake ndo kama hivi sasa!! Tunalia na hakuna wa kutusikiliza.
 
Back
Top Bottom