Kibunango
Platinum Member
- Aug 29, 2006
- 8,468
- 2,349
Napenda kurudia tena kwamba kuundwa kwa serikali ya mseto hakumaanishi kufutwa kwa SMZ. SMZ itaendelea kuwepo ila katika mtazamo wa umoja zaidi. Uhuru wa mwaka 63 ulikuwa ni kwa faida ya wachache na ndio maana haukudumu. Na inapotokea kundi ama mtu kudai kuwa uhuru ule ulikuwa kwa manufaa ya wengi basi huyo atakuwa na walakini.
Makovu ya mapinduzi yale yalianzwa kufutwa tokea awamu ya tano. Nafikiri wengi mnakumbuka kauli ya Komandoo Salmin alipotoa ruhusa kwa sultan kulejea visiwani humo. Aidha royal family ya sultan imekuwa ikirudi zanzibar kwa muda mrefu sasa. Nimekutana nao na wala hawana tatizo na mapinduzi kwani ukweli wa dhuluma yao dhidi ya wengi wanaujua fika.