connections
JF-Expert Member
- Apr 27, 2013
- 2,190
- 3,039
Ila kiukweli pesa tamu. Hata ungekua wewe misafari Kama yote. Pesa zinaingia kwenye akaunti tu nyie Ni Ku-Withdraw Tu na kuzipangia matumizi.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Pesa zisizo na mwenyewe. Ni kubunya tupesa a.k.a fuba a.k.a ankara a.k.a chapaa!
Hv Gidabuday mbona kimya ameanza kula mema ya Uongozi wa Riadha? Maana jamaa alikua anachonga balaa.Kwa Kweli Inawezekana!
ila Gidabuday ni M Barbaig au Datoga, na Bayi ndiye Wairaq.
Ila Hawa wangepata Vizuri, wangeweza kusogeza Riadha mbele
Sawa, Filbert Bayi aachie ngazi sasa....wapewe wengineIlisharuhusiwa na chifu kuwa kila mtu atakula kwa urefu wa kamba yake
Hii nchi ina operate chini ya mfumo wa uzembe, wizi, ubadhirifu na ufisadi, yaani kuanzia pale kwenye utosi hadi kwenye unyayo, ndio maana hamna anayewajibishwa kwasababu ndio mfumo ulioasisiwa na ulioratibiwa na chama tawala na katiba ya mwaka 1977Ndg FILBERT BAYI ndiye Katibu Mkuu wa sasa wa Kamati ya Olimpiki Tanzania, tangu achaguliwe kushika wadhifa huo ametumia nafasi yake katika KAMATI YA OLIMPIKI TANZANIA kupata zabuni zote, mikataba ya ugavi, na shughuli nyingine za manunuzi zinazodhaminiwa na Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki Duniani (IOC) kwa ajili yake mwenyewe, familia yake na marafiki wa karibu kinyume na Kanuni za Uadilifu ya IOC.
"RAIS NA KATIBU MKUU WA KAMATI YA OLIMPIKI TANZANIA WAMEONGOZA TOC TANGU 1/1/2002, HIYO NI ZAIDI YA MIAKA 22.
2002 WAKATI WANASHIKA MADARAKA HAPAKUWA NA SHULE MKUZA KIBAHA; JE NI LAZIMA UWE NA DIGIRII NGAPI UJUE KWAMBA FEDHA ZA IOC NDIZO ZIMETUMIKA KUJENGA HIYO SHULE?"
Katibu Mkuu huyo na familia yake wanamiliki Shule iliyopo Mkuza Kibaha iliyopewa jina la FILBERT BAYIINTERNATIONAL SCHOOLS, anapanga shughuli zote za TOC zinazofadhiliwa na IOC na zote zinafanyika katika Shule yake Mkuza Kibaha Mkoani Pwani.
Hii ina maana, malazi kwa washiriki katika shughuli zote kama vile chakula, usafiri, stationary na upishi wote ni mkataba na shule yake, (Milo inayotolewa na huduma za upishi ni kampuni inayomilikiwa na marehemu mke wake), hivyo viwango vyote vya kulipwa vinapangwa na mwenyewe kwa pesa alizonazo yeye mwenyewe zinazotoka IOC, hivyo kupitia vyombo vinavyomilikiwa na familia yake ananufaika moja kwa moja na wadhifa alionao kama Katibu Mkuu wa TOC.
Fikiria mpangilio huu;
1) Ndg Bayi anaamua ni shughuli gani itafanyika chini ya ufadhili wa IOC
2) Ndg Bayi huandaa hafla hiyo katika Shule yake iliyopo Mkuza Kibaha
3) Ndg Bayi na familia yake hutoa huduma zote zinazohitajika kwa shughuli hiyo (Milo, Ukumbi wa Mikutano na vifaa vingine, usafiri na malazi inapobidi)
4) Wote kwa pamoja; Bw Bayi mwenyewe, Rais wa TOC ndg Gulam Rashid na Makamu Rais wa TOC ndg Henry Tandau ndio wawezeshaji wa shughuli zote; mfano(Semina, kozi fupi, warsha n.k) na inasemekana wanajilipa mara kadhaa ya kiasi kinacholipwa kwa wanachama wengine ikiwa ni pamoja na Wajumbe wa Tume ya Wanariadha (Athletes Commission).
Malipo haya mara nyingi ni nyongeza ya kile wanachojilipa kwa mahitaji ya kila siku wakiwa viongozi wa TOC. Pia kuna swala hili la Olympic Solidarity na Athletes Support Funds, Wanariadha wa Tanzania hawana ufahamu wa kutosha jinsi hii inavyofanyika, lakini tunaelewa kuwa kuna fedha zinazotolewa na IOC kusaidia Olympians katika maandalizi ya Michezo ijayo ya Olimpiki. msaada unakwenda pamoja na WANACHUO kwa maana ya ufadhili wa kimasomo yaani (Schorlaships).
Taarifa za kuaminika ni kwamba IOC inafadhili Shule ya Filbert Bayi kama Kituo cha OLYMPAFRICA kwa maana inapaswa iwe mali ya serikali wala siyo taasisi ya mtu binafsi, mpango huo ni wa kuwafadhili Wanamichezo wa Kitanzania lakini ndg Filbert Bayi inasemekana kaifanya mali yake. Huu ni ukiukwaji mkubwa wa maadili ya IOC pia maadili ya Tanzania kwa mujibu wa Sheria na pia naweza kusema ni Uhujumu Uchumi.
Shule ya Filbert Bayi inatoza wanafunzi ada kubwa, wakati huko IOC wanapeleka ripoti kwamba wanafunzi wanapatiwa ufadhili, lakini cha kushangaza ni kwamba IOC ilishaweka kituo cha Olympafrica DOLE Zanzibar (japo usajili wake unadaiwa kuwa kwa jina la GULAM RASHID) ambaye ni Rais wa TOC. Ndg Bayi inasemekana akafanya ujanja wa kusajili Shule yake kwenye program ya Olympafrica na hivyo kile cha Zanzibar kikibakia kuwa GOFU lisilotumika sababu program zote zinaelekezwa Kibaha.
Usajili wa Olympafrica shuleni kwa Bayi ulifanyika kwa taswira ya rushwa baada ya Msenegali ndg Ollasane Thierno Diack kuja Tanzania kisirisiri na kukamilisha usajili na kuondoka. Baadae viongozi wakuu wa TOC ambao ni wanufaika wakuu wa ujanja ujanja uliodumu tangu January Mosi 2002 tangu Bayi, Gulam na wenzao walipochaguliwa.
Katika utangazaji inasemekana Wazazi wanaombwa kupeleka watoto wao huko kwa ahadi ya matarajio ya kuchaguliwa kufaidika na ufadhili wa masomo wa IOC, inasemekana IOC wanapokuja kwa ukaguzi kuna (MABANGO MAALUM) yanawekwa kwa muda ili IOC waamini kwamba shule inatekeleza masharti yao, ila wakaguzi wakiondoka mabango hayo yanaondolewa, kwa kifupi kuna mambo mengi hayaendi vizuri pale Tanzania Olympic Committee. Inasemekana watu hawa ni wazuri sana wa kutoa taarifa nzuri, lakini kikubwa tunaamini ni uzushi, tunaambiwa kuna baadhi ya viongozi wa juu wa IOC wanaaminika kuwa ni washirika wa makampuni ya FilbertBayi na ndiyo maana haogopi hata serikali.
Mambo ya kutisha ni pamoja na yafuatayo;
1) Kuna ruzuku ya Wanariadha ijulikanayo kama (Athlete's Support Funds) hazijawahi kutolewa kwa Wanariadha na TOC wananufaika na uelewa mdogo wa wanariadha
2) Kuna ruzuku ya Covid-19 iliyotakiwa kupewa wanariadha kutokana na kuahirishwa kwa Tokyo Olympics pia hazijawi kutolewa
3) Kuna fursa za kimasomo (Schorlaships) ambazo inasemekana zinatolewa kindugu ama kirafiki ama kwa njia ya rushwa
4) Kuna taarifa kwamba milioni 27 za Olympafrica zilitumika kwa mradi wa kuku DOLE Zanzibar, mradi huo una utata
5) Makamu Rais anadaiwa kutengeneza risiti za kuchonga za milioni 25 kufuatia seminar ambazo washiriki walikuwa wanajiljpia kila sessions na thesis book zao wenyewe
6) Juzi January 20/2022 magazeti kadhaa (tunahifadhi majina) yaliripoti habari za miaka minne iliyopita kwamba Filbert Bayi, Henry Tandau na Irene Mwasanga wameteuliwa ANOCA; wakati hayo yalifanyika January 2018; pongezi hizo feki zilizotolewa na Rais wa TOC Gulam Rashid zililenga kupambaza umma wa Watanzania
7 ) Kuna Mashindano yanayodhaminiwa na OLYMPIC SOLIDARITY ambayo yalipaswa kuzunguka nchi nzima kama Michezo ya Olympics inavyozunguka katika miji na nchi tofauti; lakini haya ya Karatu yamefanyika kwa miaka 13 Karatu pekee ambapo ndiyo nyumbani alikozaliwa ndg FILBERT BAYI.
Swali la kujiuliza je Mtwara, Mwanza, Singida, Rukwa, Kagera, Kigoma na Mikoa mingine haipaswi kutafuta vipaji kwa udhamini wa Olympic Solidarity?
"OMBI LANGU NI KWAMBA MAMA YETU MPENZI SAMIA SULUHU HASSAN NA MPENDA MICHEZO UWAFUKUZE HAWA WAZEE ,WAHUNI WAMEILA SANA HII NCHI"