Kashfa nzito: Zitto vs Amina Chifupa

Kashfa nzito: Zitto vs Amina Chifupa

Status
Not open for further replies.
Jamani huyu mtoto wa kike tatizo lake ni kale kamchezo bado mwili mchanga unahitaji kale kamchezo lakini tatizo kuwa la hawa wanandoa wawili ni shule ndogo. Huyu mpakanjia kama angekuwa na upeo wa kufikiri wala asingeweza kuanika hadharani maana ni kuzalilika tuu yeye angemwaacha kama walivyooana. Swala la ndoa nadhani sio swala la kujadili bungeni, mimi sioni uhusiano wa swala la ndoa na matatizo ya watanzania. Yaani spika anaeongoza bunge la wawakilishi wa watanzania milioni 36 akajadili starehe za Chifuta na Zitto! Kweli sasa bunge letu limekuwa kama baraza la kupigia umbea. Pia hii inawezekana ni janja ya kisiasa tuu; watu wanaweza kupiga kwa staili hiyo kwa masilahi ya watu sisi tusubiri huyu bint alipue hilo Bomu.
 
USALAMA WA TAIFA wanafanya kazi gani ya kumlinda huyu Mheshimiwa MBUNGE wetu?

Je damu ikimwagika watasemaje? na waheshimiwa nao watasema nini?

Mheshimiwa Samvulachole,jukumu la kumlinda AC ni la polisi.Usalama wa taifa kazi yao ni exact that,polisi ni usalama wa raia,ila usalama wa taifa wana kitengo kinachoitwa PSU,(Presidential Security Unit),ndio ma-body guard wa rais,makamu pm na nk.
 
jokaKuu said:
samvulachole,
huyu Mama Amina Chifupa Mpakanjia alikuwa drama-queen tangu hajaingia bungeni. uwezekano wa huyu Mama kuwa a DISTRACTION bungeni ulikuwa mkubwa mno. Hili tukio/skendo limethibitisha wasiwasi huo.


Hapa naona umeegemea upande mmoja..."Uroda" kama kweli walipeana wanakula watu 2 na sio Amina peke yake...hata Zitto naye kama livyosema mwanasiasa ana tuhuma za kujibu..pengine hii ni tabia yake ambayo ndio sasa inajulikana adharani..wanasema za mwizi 40.

jokaKuu said:
Yebo Yebo,
Yeyote "aliyemchongea" Mama Chifupa kwa ajili ya malengo ya siasa kwa kweli ni mtu hatari sana.

Miaka ya zamani wabunge walikuwa wakiingia siasa kwa malengo mazuri tu. Walikuwa wakiharibika baada ya kuingia siasa, na siyo kabla. Miaka hii ya karibuni wabunge wanakuwa tayari ni wahuni-huni kabla hata ya kuingia siasa.

Huu ni muendelezo tu wa siasa za wanamtandao. Naamini sote tunakumbuka kampeni chafu dhidi ya Salim Ahmed Salim. Kampeni hizi za ajabu-ajabu ndizo zilizomuweka Raisi wetu madarakani. Je, sasa ana uwezo wa kusafisha hali ya hewa ya kisiasa Tanzania?


Moto huu hakuna anayeweza kuuzima..ni mabadiliko ya wakati na kizazi. Nasema siasa ya bongo imeingiwa na vijana...tena sasa hivi bado huu uchafu haujakolea maana bado wakina JM, Kingunge, Kawawa n.k wako hai na wananguvu za kama zile za Yesu aliponyoosha mkono mawimbi ya bahari yakapoa...hawa kwa siasa za bongo ndani na nje ya CCM wana nguvu hizo. Wanauwezo wa kupoza mawimbi ya siasa bongo; yeyote ndani ya Chama akiambiwa ujumbe kutoka kwa JM unasema usifanye hiki au kile basi hakuna kusema LAKINI..!! Unatiii

Siku ikifika Mungu akawachukua hawa Wazee ndio itakuwa mwisho wa CCM maana MOTO unakaowaka utavunja Chama....hebu fikiria Nchimbi atake kugombea Umakamu M/kiti wa CCM halafu aje na Kampeni Chafu kiasi hiki.

Mzee ES naomba mawazo yako hapa...CCM imeingiliwa na VIJANA HATARI?
 
Joka Kuu.. kumkatikia mtu kiuno inahusiana vipi na uongozi na utawala? hili la Chifupa siyo kubwa sana kama watu wanavyotaka tuamini. Ukubwa wake unatokana na mumewe kushindwa kulishughulikia jambo hili na pia haja ya baadhi ya watu kumuumbua Zitto na kumharibia Chifupa. Vinginevyo, kuna orodha ya viongozi wengi tu (upinzani na ccm) ambao wamekula na wake/waume za watu na inajulikana. Kuna watu ambao wamepigwa hadi picha ambazo zikiwekwa hadharani itakuwa ni varangati!! You are right.. hili ni suala la kampeni chafu!!!

Hata wengine tunaopiga kelele kuhusu "questionable morality" ya Bi. Chifupa tungepatiwa nafasi ya kuwa naye "katika sita kwa sita" wachache tungelazia damu!! Watu wanavyomhukumu huyu binti ni kwa vile yeye ni mwanamke. Viongozi wanaume waliovunja ndoa za watu au kula na wake za watu (na wengine hadi kuzaa nao) bado wapo wanatanua na kukenua!! let cut her some slack.. kama ndoa iliyovunjika ni ya kwake, na kama anahitaji msaada zaidi wa kutulizwa mizimu ya kikwao hili ni la kwake! Kama angekuwa mtoto mdogo au kama angefanya kwa kulazimishwa hapo ingekuwa issue, lakini kwa mtu mzima na akili zake it is naive to expect perfection among politicians and other leaders!!

Since the time of Solomon.. people in power have always taken sexual liberty to experiment with whoever they want.. as long as people don't find out.. Herod alichukua mke wa kakake, even the Prophet aliruhusiwa kuchukua mke wa mtoto wake wa kulelea!!! Is it wrong yes! is it immoral absolutely! does that mean these people should not be given any chance to serve? hell no!!!

Nitakubali kuongozwa na mtu mwenye udhaifu wa ngono kuliko mtu anayekula nchi bila kunawa, anayetafuna mali ya umma kama mchwa, mwenye kuficha ufisadi, anayechukua 20 percent ya mikataba, n.k...

Let put this in its proper context.. it is not as bad as some people would want us to believe!!
 
Yaani hapa ni kama nasoma Novel vile hebu weka haya mambo 3 pamoja uone MOTO utakaowaka....Money..Power...Sex..

Moto Mnene huu naona Mzee ES amechoka kabisa...uwiiiiii jamani BUSARA za huyu Spika zinagharimu sio Chini ya Milioni 100...chonde chonde jamani...SPIKA ANAHUSISHWA VIPI.

Nchimbi...Nchimbi...enzi za BCS; Sam aliweka vita dhidi ya Nchimbi wakati ule nilikuwa sielewi lakini sasa naona huyu jamaa ni HATARI kama UKOMA. Huyu Nchimbi anatakiwa kupingwa vita atoke kabisa katika siasa za bongo. Huyu anataka MADARAKA kwa GHARAMA yoyote.

Siasa za Bongo zimeingiliwa na VIJANA...ule mchanganyiko wa...Sex...Power...Money...ni hatari, hebu hapo weka 24/7 media, mtandao wa internet, sms, (nimesikia Mpakanjia ana Video..!!) yaani ni hatari kuliko Bomu. Huu ni mwanzo tuu...Yet to come.


KWENYE HILI NIKO NA WEWE MHESHIMIWA YEBO YEBO

NCHIMBI HAFAI NA TUNAMHITAJI SAM AJE NA MA FAILI YAKE ASAP
 
Mbona mnashangaa ya AC vipi JK kila kukicha tunaambiwa yeye ni moto wa kuotea mbali, Je, Bill Clinton ilikuwaje? THIS IS JUST STUPID AND NONE ISSUE WALA HUYO SPEAKER HANA HAJA YA KUFANYA CHOCHOTE. Hawa watu ni over 18 and AC pengine waliisha achana na mumewe kitambo sasa nini cha zaidi? Zito ni mwanaume kama wengine, Je ana mke? Wakulalamika ni mkewe kama yupo vinginevyo sioni hata sababu ya huu ujinga.

Wanasiasa wengi hizi ndio zao au kwa sababu wengine hawajaandikwa?
 
Aibu CCM!

2007-05-07 17:43:59
Na Abdul Mitumba, Makumbusho


Chama cha Mapinbduzi Jijini Dar kimekumbwa na aibu kubwa kutokana na skendo ambalo makada wake wanadaiwa kukutwa wakilifanya usiku wa manane.

Taarifa za uhakika zilizolifikia gazeti hili zinadai kuwa kitendo hicho kinachofananishwa na kuwanga, huenda kikakifanya chama kuwapa adhabu kali wanachama wake kibao waliohusishwa.

Makada hao wanadaiwa kukutwa usiku wa giza nene wakilishwa pilau na wafadhili wanaodaiwa kuwa wanataka wagombea wao wa nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho waweze kupita kirahisi.

Baadhi ya wana CCM walio hatarini kuwajibishwa kutokana na tukio hilo la aibu ni wale wa Kata ya Makumbusho iliyopo manipsaa ya Kinondoni Jijini.

Taarifa zinasema wengine walikamatwa na wengine waliruka ukuta kukwepa kuwekwa chini ya ulinzi, wakati viongozi wa CCM ngazi ya wilaya walipowafumania katika ukumbi wa Chasimba uliopo Basihaya Campsite Boko ambako walifichwa wakijiandaa na uchaguzi wa viongozi wa matawi.

Inadaiwa kuwa viongozi na wanachama hao walipelekwa huko na viongozi wa CCM kata ya Makumbusho wakitumia basi dogo aina ya Toyota Coaster yenye namba za usajili T 415 ADK, ambapo baada ya kuwekwa chini ya ulinzi dereva wake amekiri na kwamba bado anadai malipo yake ya sh.80,000.

Tukio hilo lilitokea kati ya saa 4:30 hadi 6:30 usiku, ambapo kabla viongozi wa kata wa CCM wanaomuunga mkono katibu, waliwasiliana na katibu wa CCM Kinondoni, Bw. Abilahi Mihewa juu ya kuwepo kwa tukio hilo.

Bwana Mihewa naye aliwasiliana na Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Bw.John Barongo naye akamjulisha Mkuu wake, Luteni Yusuf Makamba, ambapo alimuagiza Bw. Mihewa kufuatilia kwa kina tukio hilo.

Akizungumza na Alasiri jana ofisini kwake, Bw. Mihewa, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa chama hicho wilaya ya Kinondoni, amesema baada ya kupewa rungu na Makamba, akiwa na vigogo wa CCM kata na wilaya, walikwenda hadi Boko kwa lengo la kuthibitisha kuwepo kwa taarifa hizo.

Akasema walipofika na baada ya mabishano ya dakika kadhaa na mlinzi wa ukumbi huo, hatimaye alikubali kufungua geti ndipo walipowakuta wanachama hao ambao ni wapiga kura na baadhi ya viongozi wanaogombea nyadhifa mbalimbali.

``Kwa kutambua wachofanya ni kosa, baadhi yao waliruka ukuta na kukimbia lakini wengi kati yao tulifanikiwa kuwaweka chini ya ulinzi na majina yao tunayo,`` amesema Bw. Mihewa.

Akaongeza kuwa ndani ya ukumbi huo, kulikutwa na masufuria matatu ya pilau lililokuwa tayari kuliwa na mmoja kati ya wanachama waliokimbia aliangusha bahasha ndogo 13 za kaki zinazoashiria kuwepo kwa mazingira ya kutembezeana mlungula mwingine wa fedha.

Kufuatia tukio hilo, Bw. Mihewa amesema alimpigia simu mkuu wa wilaya hiyo, Kanali Mstaafu Fabian Massawe ili akajionee tukio hilo na ikiwezekana awasiliane na vyombo vya usalama kwa hatua zaidi za kisheria.

``Kikatiba DC Massawe ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya na baada ya kufika katika eneo la tukio, aliahidi kulishughulikia kisheria na usalama zaidi kwa ajili ya kukisafisha chama,`` amesema.

Amefafanua kuwa kila mtu aliyeulizwa nani aliyewezesha wao kufika Boko, walidai ni viongozi wa CCM kata ya Makumbusho, akiwemo mwenyekiti na katibu mwenezi wa kata na diwani.

Alasiri ilipowasiliana na diwani wa kata hiyo, Bw.Christopher Mutayoba, alikiri kuwepo kwa tukio hilo, lakini akaruka kimanga kuhusika ambapo alisema wakati hayo yakiendelea, yeye alikuwa amelala nyumba kutokana na kuumwa.

Akizungumzia hatma ya uchaguzi huo, Bw. Mihewa amesema umesimamishwa hadi vikao vya kuwajadili wanachama hao ngazi ya wilaya na mkoa vikapofanyika na Kamati Kuu ya CCM Taifa itakapotoa uamuzi dhidi yao.

Uchaguzi huo wa marudio ungehusisha matawi matatu kati ya tisa ya kata hiyo, ambayo yalishindwa kutoa washindi wakati uchaguzi wa awali ulipofanyika wiki moja iliyopita. Matawi hayo ni Mchangani, Kisiwani na Minazini.

SOURCE: Alasiri


AMA KWELI SASA CCM MAMBO YAKO JUU
 
HATA CLINTON ALIKUWA AKIPEWA MA BLOW JOB NA MONICA KULE WHITE HOUSE LAKINI STILL UCHUMI WA USA ulikuwa maradufu wakati wake

Hii ni kampeni ya WAZEE DHIDI YA VIJANA na hiii mimi nitamtetea AC japo ana mushkeli kidogo lakini potelea mbali..Hawa wazee WASIONE KIJANA anataka kupata.

HIVI HUYO SAM YUKO WAPI NA MAFAILI YA NCHIMBI?
 
MKJJ kama uyasemayo ni kweli basi sakata la Zitto na Amina kuna zaidi ya hapo . Hii ndiyo awamu ya 4 wandugu na hiki ndiyo Chama cha mapinduzi . Je gari na simu vimechukuliwa na nani ? Simu ni mali uya CCM pia ? Je gari si ni mali yake kama Mbunge anakatwa mshahara ? Press conference imezuiwa kwa sababu gani ? Mwenye nyeti atueleze .
 
Lunyungu..hilo la simu ni kweli kabisa... gari.bado nafuatilia lakini sidhani kama wameweza kulizuia ila wamefanya iwe ngumu yeye kuamua kwenda anakotaka na kukutana/kuwasiliana na yeyote anayetaka. Msijekushtuka kuwa amelazwa mgonjwa.....
 
kama atakuwa smart atawaambia "mimi ni spika wa Bunge la Muungano, na siyo spika wa nyumba za watu!, hili ni suala la mashehe na wachungaji"!
 
Samvulachole,
Hivi Nchimbi ana uhusiano gani na Savimbi? Naona kama wanafanana vile.

Jasusi,

Inawezekana kabisa Nchimbi akawa alizaliwa na Savimbi!

Inasemekana Kabila ana watoto kibao BONGO!!

Vita ya NChimbi ni kama ya SAvimbi tusipokuwa makini atakuja kuwa rais wa Tanzania!


Ila tu inaonekana atashindwa kama Savimbi alivyoshindwa kuwa rais huko angola!!
 
Mimi naona hili swala la Amina na Zitto ni kubwa zaidi ya ngono .Maana yanayo jiri kwa Chifupa ni zaidi ya ugoni ama ngono. Mimi sina ka kusma kwa sasa ila najua kuna jambo kubwa zaidi ya haya watu kukubaliana pembeni kama kweli kuna ushahidi wa mambo na bado kuja Public sijaona maana yake maana ni mambo ya sirini kabisa haya .
 
Mzee Mwanakijiji acha kutunga uongo hapa. Umesema kwamba ile barua ya Mpakanjia kwa Spika imetungwa na Nchimbi (kwa maana hiyo Mpakanjia hakumwacha mkewe) lakini leo Mzee Chifupa kathibitisha kwamba ni kweli Amina kapewa talaka, lakini ni talaka moja.

Listen, it may be OK kwako kwa Mhe. Zitto kumla mke wa mtu (kisa eti Nabii Suleiman alifanya hivyo na kila mmoja Bungeni anafanya hivyo), lakini the issue hapa ni kwamba Mhe. Zitto has been holding himself to the highest ethical standards and this reveals hipocrisy. You are right kwamba wengi wetu, kama unavyodai, tusingemlazia damu Amina kama "tungekuwa ndani ya kumi na nane" (wacha sita), lakini hiyo hai-justify recklessness ya mtu kama Zitto ambaye ana a promising future kisiasa na tunaambiwa ni mtu makini. Yes, labda kula uroda is a universal aspiration, lakini cover your tracks basi hasa kama unajua uko kwenye public life.

Halafu hii habari ya ku-externalise weaknesses, therefore kutochukua responsibility, sijui wabongo tutaicha lini. Chupi uvue wewe, uroda ule wewe, leo unasema Nchimbi ndio a problem! Give me a break!
 
Mgongo2,
Leo nakuunga mkono kabisa kwa hili. Maajabu ya Musa kweli.
 
Mzee Mwanakijiji acha kutunga uongo hapa. Umesema kwamba ile barua ya Mpakanjia kwa Spika imetungwa na Nchimbi (kwa maana hiyo Mpakanjia hakumwacha mkewe) lakini leo Mzee Chifupa kathibitisha kwamba ni kweli Amina kapewa talaka, lakini ni talaka moja.

Mugongo.. barua ya Mpakanjia kwenda kwa spika imetungwa na Nchimbi..... na nimezungumza naye Nchimbi mwenyewe kuhusu suala hili... jibu lake litakulipua moyo!!!! (sileti habari zisizokuwa habari!)

Listen, it may be OK kwako kwa Mhe. Zitto kumla mke wa mtu (kisa eti Nabii Suleiman alifanya hivyo na kila mmoja Bungeni anafanya hivyo), lakini the issue hapa ni kwamba Mhe. Zitto has been holding himself to the highest ethical standards and this reveals hipocrisy. You are right kwamba wengi wetu, kama unavyodai, tusingemlazia damu Amina kama "tungekuwa ndani ya kumi na nane" (wacha sita), lakini hiyo hai-justify recklessness ya mtu kama Zitto ambaye ana a promising future kisiasa na tunaambiwa ni mtu makini. Yes, labda kula uroda is a universal aspiration, lakini cover your tracks basi hasa kama unajua uko kwenye public life.

Halafu hii habari ya ku-externalise weaknesses, therefore kutochukua responsibility, sijui wabongo tutaicha lini. Chupi uvue wewe, uroda ule wewe, leo unasema Nchimbi ndio a problem! Give me a break!

sijasema kuwa its ok.. ila kulifanya hili kama mbingu imeanguka na ardhi kupasuka si haki hata kidogo! maadili siyo mambo ya ngono peke yake.. Halafu kufanya kana kwamba Zitto ndiye kiongozi mkamilifu au amekufanya uamini kuwa ni mkamilifu it is not fair! Hakuna mkamilifu isipokuwa mmoja tu! So, wakati wewe unaangalia Zitto na kuwa disappointed, mimi naangalia issue na kusema, cut the young man some slack!!

Kama madai dhidi yake ni ya kweli, then it isimply due to "lapse in judgement" and "youthfull indiscretion" but that doesn't make him a bad leader not worthy of a second chance!. As long as he can demonstrate in the future that he has indeed learned from it this experience, nawakatia wote wawili some slack!! It is politics after all!
 
Kwamba Amina hafai kuwa mbunge sio jipya; hili tunalijua hata kabla hajagombea

Kwamba Nchimbi ni kilaza, mchafu na mpenda mambo ya usiku sio jipya pia; tunalijua siku nyingi na ni sifa ya uCCM.

Kinachonitisha mimi ni pale watu wanapojaribu kuonesha kwamba Zitto kula uroda wa Amina is a non-issue. Hii isingenipa taabu kama ingekuwa imetokea kati ya Nchimbi na Amina au mtu mwingine katika CCM na Amina maana hilo ni jambo la kawaida kwa wana CCM.

Tatizo hapa ni kwa Zitto kama kweli kafanya kinachoelezwa. Zitto ni rafiki yangu wa kisiasa kwa miaka mingi. Moja ya misingi yetu ni maadili. Kitu kimoja kikubwa ambacho tunapigania kujitofautisha na CCM ni maadili na misingi (principle and ethics). Ikithibitika kweli Zitto kala uroda wa huyu binti atakuwa amevunja principle yetu na ya chama chetu.

Kukosekana kwa maadili ndiyo chanzo cha uozo katika nchi yetu. Ni kwa kutokuwa na maadili ndiyo maana watu wanachelewa kazini. Wanasema uongo. Wanaiba. Wanapokea rushwa. Na kwa kukosekana maadili ndiyo taifa halioni ajaibu tena wanafunzi kuiba mitihani. Maadili ni msingi muhimu katika ujenzi wa taifa. Bila maadili hatuwezi kwenda.

Kama huoni shida kula uroda nje ya ndoa yako tena uroda wa mke wa mtu, tena mke mwenyewe malaya na amepata madaraka kwa umalaya, huwezi kuona shida kuiba, kula rushwa tukikukabidhi hazina. Huu ndio msingi wa tatizo hili. Ndio maana nasema kama kweli Zitto katenda hili, atoke hadharani, akiri, atubu na aombe msamaha kwa manufaa yake binafsi na chama chetu.

Kwamba hata viongozi wa mataifa ya magharibi kama akina Clinton huwakuta haya sio jambo jipya; tunajua hili na limeshasemwa na litaendelea kusemwa miaka nenda rudi. Kisichokweli ni kwamba eti wenzetu huko huwa wanadharau jambo la namna hii. Ukweli ni kwamba wenzetu huwa hawadharau jambo la namna hili. Likitokea wanachukua hatua. Clinton alitubu na akaomba msamaha. Kiongozi mahiri sana wa chama cha Liberal Democrats (jina limenitoka) alihisiwa kula uroda nje ya ndoa kwa muda mrefu. Hata hivyo alikanusha hadi tume ilipoundwa na kuthibitisha ukweli huo. Baada ya tume kuthibitisha alipatikana na hatia nyingine ya kusema uongo na ilibidi ajiuzulu. Mifano ni mingi.

Ok, hata kama nchi za nje wanafanya hayo hayo haiwezi kuhalalisha. Ushenzi ni ushenzi tu wala haubadiliki eti kwa sababu umefanywa na mtu anayeonekana wa maana.

Kama CCM wanachezeana kwa sababu zao za uchaguzi hiyo ni shauri yao na wala itakuwa haianzi leo. Ninachokataa mimi kama mwanachama wa CHADEMA ni kiongozi wangu kutumika hapa ama kwa kujua au kutokujua. Madamu habari yenyewe imeshakuwa in public domain, Zitto hana mbadala wa kulikanusha au kukiri jambo hili hadharani. Vinginevyo, reputation yake as an outstanding and credible poltical leader is very much in tatters!

Wakati tukiendelea kujadili jambo hili, sisi wana forum tufike mahala tuache tabia ya kuhalalisha yasiyohalalishika na kutetea yasiyoteteeka!
 
Huyu ndiye Mwanasiasa nimjuaye mimi, at his best! Take 5! bravo brother.

Bado napata tatizo nini niseme kuchelea kuwa jambo lenyewe halijathibitika, baya zaidi sidhani kama litathibitika unless wahusika waungame hadharani. Kwa mazoea ya wanasiasa wetu sioni kama hili litafanyika (afteall wote washakanusha)

Mwanasiasa time is running out kwa Zitto ku repair the damage ( if any), Amina mimi hanishughulishi sana kwani yawezekana ana enjoy publicity kama hizi.

Mwakjj

Historia za mitume na wengine hazi justify watu kutembea na wake za watu. Kama alivyosema Mwanasiasa ikiwa huwezi kuzuia zipu yako isishuke chini itakuwaje kama tutakupa hazina yetu ya taifa si utaimaliza? Maadili ni pamoja na hilo. Kama ni "lapse of judgement" au "youthfull indiscretion" Tunachataka aje open, otherwise utakuwa uvumi usio kwisha na sidhani kama itakuwa inamfanyia wema wowote Zitto
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom