Kashfa nzito: Zitto vs Amina Chifupa

Kashfa nzito: Zitto vs Amina Chifupa

Status
Not open for further replies.
Nyani angalia hii thread ilianzishwa na nani....? utapata jibu wengine tulishajua penye moshi....

Ni kweli aliengoea kuwa Zitto anafukuzia wanawake walewale na CCM wakti wa Bunge ni Mugongonwa Mungongo. aliandika hapa. Inaelekea alikuwa na taarifa kamili ya mambo haya ndiyo maana alikuwa miongoni mwa wanaforum wa kwanza kwana kuipata stori hii. Forum hii nzuri kweli; mtu unapata mambo live hata yale yasiyopatikana magazetini.
 
Mugongo Mugongo ni mtu hatari sana njua Mwanakijiji unafahamu undani wake ila sidhani kama unajua in details. Kwa taarifa yenu mgongo mugongo na mwenzake mmoja ndiyo walionifanya nipunzike kidogo kwani niligundua kuwa napambana na taifa kubwa. Hebu mugongo mugongo tupe motive ya Nchimbi kufanya aliyofanya ni chama kimemtua au kundi fulani la watu. Amina amesema haogopi kufukuzwa chama kwangu mimi huo ni ujumbe mkubwa sana. Pia amesema yeye siyo kiongozi wa ndiyo mzee. Mugongo mugongo tupe details.
 
AC amebore!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Anatudhalilisha bwana....sasa nitagombeaje ubunge??? (Si Mr ataclaim kwamba na mimi nitaenda kugawa???????????? (joking)
Hii kali, na inatisha ila haka kabinti kamenibore kwa nini kanaendesha ndoa na magazeti...
Umaarufu anaoutaka utammaliza!
 
Mama Lao tafadhali ungombee ili ukawe "Matron" wa mabinti hawa uwafundishe maadili yanayowataka "kubana mapaja" yao kulingana na nyadhifa walizo nazo.
 
Saa nyingine wanawake tunajidhalilisha wenyewe.....hivi chupi lazima akavulie bungeni??? To so many people?????????????????? Lakini she is still a young girl sasa sijui jamaa walikuwa wanavaa C au kavu kavu. Ukimwi utaisha kweli???
Kwa kweli "amebore" ametupaka matope sana. She is setting a bad precedent to other young women who would like to be politicians in future!!!
Na babake naye....ahaa..ndoa ya mwanao ukatangaze gazetini. I think the family needs counselling they are taking this too far!!!
 
With due respect, Mugongomugongo anasema kweli.

Mzee Chifupa ni bogus kama alivyo mwanae. Wanapenda publicity sana. Ni ukosefu wa shule ndio unawagharimu, kuanzia mama Chifupa, Mpakanjia, AC na Mzee C. Wooote shule zero!!!!

Safi sana Nchimbi!!

Naona tunarudia rudia tuuu mambo hamna jipya, hii topic ningependa iende kwenye UDAKU.

FD
 
hakuna anayemtetea zitto kama mbunge...lazima tumtendee haki,ushahidi uliopo HAPA hautoshi kumtia hatiani...ni ushahidi wa kusikia .unless yeye mwenyewe atakuja hapa akiri au akikataa kukiri tupate evidence nzito....
sasa nashangaa sana unless kama "ndugu yangu" wewe ndio ulimshikia ZITTO miguu....
hapa kuna option hizi:-
labda ukweli wametifuana kweli,kwa hiyo nchimbi kaumia kwa sababu
kashawahi kula au mabosi zake
labda ni mbinu ya kumaliza zitto
au mbinu ya kumzuia amina asigombee uchairperson
pia inawezekana meddy nae alikuwa akimtafutia sababu baada ya kusikia
mengi...

so lets be fair and take this issue under careful scrutiny...
 
hizo ndizo politics za bongo mara zote huwa hazinyooki,lakini nyepesi nyepesi ni kwamba hiyo ni mfumo kuelekea uchaguzi wa uvccm 2008,kama mnakumbuka miaka sita iliyopita lile kasheshe la nchimbi na dada mmoja mwandishi wa habari aitwaye jane mihanji kule tabata,bado nasoma magazeti ya leo kuhusu sheshe hilo,lakini nitachangia mjadala baadaye.ebu someni habari hii ya majira

http://www.majira.co.tz/kurasa.php?soma=tanzania&habariNamba=2830
 
hizo ndizo politics za bongo mara zote huwa hazinyooki,lakini nyepesi nyepesi ni kwamba hiyo ni mfumo kuelekea uchaguzi wa uvccm 2008,kama mnakumbuka miaka sita iliyopita lile kasheshe la nchimbi na dada mmoja mwandishi wa habari aitwaye jane mihanji kule tabata,bado nasoma magazeti ya leo kuhusu sheshe hilo,lakini nitachangia mjadala baadaye.ebu someni habari hii ya majira

http://www.majira.co.tz/kurasa.php?soma=tanzania&habariNamba=2830

Twist nyingine iko hapa
 
Mswahili,

Brown alijiuzulu kwasababu kaidanganya mahakama. Blunkett pia alitumia
cheo chake kumpendelea house girl wa huyo kimwana wake.

Hizo ni cases tofauti kabisa na hii ya sasa. Hii haina public interests zaidi ya kujua wabunge wetu wanautumiaje muda wao wa zaida huko bungeni.

Kosa la kabwe hapa ni kutembea na mke wa mtu. Hili ni kosa lake na mume wa huyo mama na pia ni kosa lake na chama chake kama kinajua ethics kama alivyosema Mwanasiasa, vinginevyo tuendelee kufurahia huu udaku.

Ila kujitetea kwa Zitto kunatia walakini. Hakuhitaji kusema yote aliyoyasema.
Alitakiwa kukanusha tu na kuendelea na mambo yake.

Hili jambo linanuka uchafu wa siasa. Kila mtu anajua bungeni ngono ni kama kazi lakini hili la sasa nafikiri lengo ni kujaribu kummaliza AC. Na yeye kakosa mtu wa kumshauri, alitakiwa atulie mpaka siku yuko tayari kulipua bomu lake.
 
Siasa zaharibu ndoa ya Chifupa


*Kisa ni kuutaka uenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM
*Baba yake Amina amzuia kutoa siri kwa waandishi

Na Waandishi Wetu

TALAKA kwa Mbunge wa Viti Maalum-Chama Cha Mapinduzi (CCM) Amina Chifupa imeingia katika sura mpya baada ya kubainika kuwa kiongozi mmoja wa UVCCM, alikataa ombi la mbunge huyo kutaka ampigie debe katika nafasi ya Mwenyekiti wa umoja huo katika uchaguzi utakaofanyika mwakani.

Chifupa alikaririwa na vyombo vya habari jana akilalamika kuwa, kiongozi mmoja wa UVCCM ambaye pia ni Naibu Waziri na Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri ya CCM, alitumia ushawishi wake kwa mumewe hali iliyosababisha yeye kupewa talaka.

Taarifa zingine zilieleza kuwa, tukio hili la kupewa talaka linahusishwa na kitendo cha Mbunge huyo kuonyesha tamaa ya madaraka ya juu katika UVCCM. Hata hiyo, mbunge huyo alipoulizwa kufafanua ukweli wa dai hilo, hakupenda kubainisha wazi kuhusu dai hili.

Kilichobainika baadaye kufuatia uchunguzi wa gazeti hili ni kuwa, Chifupa amekuwa katika kampeni za chinichini zenye lengo la kutaka kuiongoza UVCCM.

Katika harakati za Mbunge huyo kusaka sapoti, alifika kwa kiongozi huyo wa ngazi ya juu katika UVCCM na kutaka baraka zake. Kiongozi mmoja wa UVCCM aliiambia gazeti hili kuwa, Chifupa alikataliwa bila kuelezwa sababu za kukataliwa kwake.

Habari zaidi zinasema kwamba kiongozi huyo alisema Chifupa hawezi kuwa kiongozi wa umoja huo, kwa madai kwamba hana uwezo wa kushika nafasi nyeti kama hiyo.

Kuna hali ya kuanza harakati za kutaka madaraka katika UVCCM. Kwa sasa makundi yameashaanza kujiandaa huku yakifanya kampeni za chini chini.

Hali hii, inaonyesha kuwepo uchaguzi mgumu kabisa mwakani katika UVCCM na kama utaratibu wa CCM utatumika, kuna uwezekano zoezi la kufungia makada kadhaa kutogombea likafanyika. Ni jambo la wazi kuwa kuna ushahidi wa makundi na baadhi ya makada kuanza kupiga kampeni.

Tukio hili la Chifupa kumhusisha kiongozi mmoja wa UVCCM linabainisha hali iliyopo ndani ya chama hicho. Kinachoelezwa sasa ni kuwa, uongozi wa UVCCM umekuwa ukitumika kama nguzo ya kusaidia kampeni za urais kupitia CCM. Zoezi hili mara kadhaa linawahusisha viongozi wa juu katika serikali na chama, kama inavyoanza kujionyesha sasa.

Mwananchi ilipowasiliana na Mwenyekiti wa UVCCM, Emanuel Nchimbi, ili kupata upande wa uongozi wa umoja huo, simu yake ilikuwa imezimwa. Lakini habari zaidi zinadai kuwa Nchimbi kwa sasa yupo Songea kikazi.

Vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti juzi na jana kuwa Amina alitalikiwa na mumewe baada ya kubainika kuwa na uhusiano na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe na kwamba mwanaume huyo alichukua uamuzi huo baada ya 'kuumwa sikio' na kiongozi huyo wa UVCCM.

Hata hivyo, Kabwe alikaririwa na gazeti moja jana akikanusha kuwapo kwa uhusiano huo, akisema amemzoea Amina kama Mbunge mwenzake, kuanzia siku walipoteuliwa kuhesabu pamoja kura za wabunge wakati walipokuwa wakithibitisha uteuzi wa Waziri Mkuu.

Wakati huo huo, Mbunge huyo jana alishindwa kutimiza ahadi yake ya kuzungumza na waandishi wa habari kumtaja Naibu Waziri katika serikali ya Awamu ya Nne anayedaiwa kuvuruga ndoa yake.

Badala yake, Baba mzazi wa Mbunge huyo, Luteni Mstaafu Hamis Chifupa, alifika katika Ukumbi wa Maelezo jijini Dar es Salaam na kutangaza kuwa amemzuia mwanawe kutangaza jambo hilo kwenye vyombo vya habari kwa kuwa ni suala la ndani ya familia.

"Kila jambo linapotokea lina taratibu zake, namna ya kulitatua hivyo hata mgogoro huu wa Amina na mumewe lazima ufuate taratibu zinazotakiwa katika kuusuluhisha, hata kama angekuja kuongea na ninyi angeongelea masuala mengine lakini siyo hili la kuachwa kwa talaka moja," alisema Chifupa.

Luteni Chifupa alikiri kuwa mtoto wake huyo ameachwa na mumewe, Mohamed Mpakanjia kwa talaka moja kwa kufuata misingi ya dini ya Kiislamu.

Hata hivyo, alikataa kueleza kwa undani sababu ya kuvunjika kwa ndoa hiyo.

Alisema kwa kuwa suala la kuachwa kwa mtoto wake ni jambo la ndani ya familia, wamemzuia Amina kulizungumzia suala hilo katika vyombo vya habari.

Mbunge huyo jana alikaririwa na vyombo vya habari akisema kuwa alitaka azungumze na waandishi wa habari kwa lengo la kutoa ufafanuzi wa kuachika kwake, lakini kinyume na matarajio ya waandishi waliokuwa wamefurika kumsuburi, alijitokeza baba yake na kutangaza kutokuwepo kwa mkutano huo.

Alisema ameamua kufanya hivyo kwa kuwa kigogo huyo wa serikali ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM, alikwenda kwa ofisi kwa mumewe na siku hiyo hiyo akapewa talaka, jambo analohisi kuwa lilichangia kuachwa kwake.

Alipoulizwa na waandishi wa habari mahali alipo mtoto wake, Kapteni Chifupa, alisema hajamuona tangu alipoachwa ili wamekuwa wakiwasiliana kwa njia ya simu.

"Kwa kuwa tuna ndugu wengi siwezi kujua anakaa wapi, licha ya kuwa kwa taratibu za dini ya Kiislamu anatakiwa kukaa eda huku akiendelea kuhudumiwa na mume wake," alisema Chifupa.

Alisema watoto ni sawa na pensheni kwa wazazi, hivyo wameamua kumlinda mtoto wao kwa kulizungumzia suala hilo wakati taratibu nyingine zinafanywa ili kuweka mambo sawa.

Alipoulizwa juu ya sababu iliyomfanya mtoto wake apewe talaka moja, alisema haelewi akisisitiza kuwa hayo ni mambo ya ndani ya familia.



Kutoka katika Gazeti la Mwananchi
 
Sam: kabla ya kumtaka JK amuondoa Nchimbi, inabidi kwanza tujiulize are they different?
 
Mwanasiasa ukigombea URAIS au UBunge nijulishe nikuchangie fedha ya Kampeni
wewe kwa fedha gani uliyonayo?Unapenda kuyavalia njuga ya wenzio mbona yako huyataji hapa ambayo ni machafu zaidi ya haya,wengine siwajui Lakini Kutokana ninavyomfahamu huyu bwana ninahakika wengi wetu tunamachafu yetu Lakini hatuyaoni tunaona ya wenzetu.Sitetei yaliyofanyika LAKINI sioni sababu ya wale wanayofanya kama hayo au zaidi ya hayo kushabikia hili badala ya kuomba msamaha kwa waliwatendea na kwa mungu muumba.Unapomnyoshea mwezio kidole basi ujue dole gumba nalo linakunyooshe wewe.Ni nani kati yetu aliyemsafi ainue kipande cha jiwe kuwatupia watuhumiwa hawa.
 
sam umesema Mugongo Mugongo ni mtu hatari sana ? hebu fafanua . najua kundi lake hapa ni lipi na uhatari wake naujua ila sikujua kama ni mtu hatari sana . Yeye na kundi lake wanalia na Chadema tu . Wameleta habari kwa shangwe bila ya kujiuliza kama ni faida kwa CCM ama hasara . Hawakuza kabla kuandika .
Lete file la Nchimbi na hasa kuu ya mauaji ya Ippy .
 
sam umesema Mugongo Mugongo ni mtu hatari sana ? hebu fafanua . najua kundi lake hapa ni lipi na uhatari wake naujua ila sikujua kama ni mtu hatari sana . Yeye na kundi lake wanalia na Chadema tu . Wameleta habari kwa shangwe bila ya kujiuliza kama ni faida kwa CCM ama hasara . Hawakuza kabla kuandika .
Lete file la Nchimbi na hasa kuu ya mauaji ya Ippy .
Wakuulizwa hili ni Mzee ES(A.K.A SAM ORIGINAL,Mh. Mbunge).
 
Ni kweli aliengoea kuwa Zitto anafukuzia wanawake walewale na CCM wakti wa Bunge ni Mugongonwa Mungongo. aliandika hapa. Inaelekea alikuwa na taarifa kamili ya mambo haya ndiyo maana alikuwa miongoni mwa wanaforum wa kwanza kwana kuipata stori hii. Forum hii nzuri kweli; mtu unapata mambo live hata yale yasiyopatikana magazetini.

kwa taarifa yako zilianzishwa TOPIKI NNE na zote ama zilifutwa au kuunganishwa kule kwenye ile thread ya MBOWE kwa kisingizio kuwa eti zinaendana

Of course wenye BARAZA LETU tukasema hii haiwezekani kuachwa ili hali ni muhimu..ndo waheshimiwa wakakubali kuirudisha hii topiki

unajua saa zingine haya mambo ya kuingiliwa wakati yanaboa cha muhimu walitakiwa waache tu watu waendelee na mambo yao hapa kijiweni
 
Wajumbe wa JF;Tuache longolongo....Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa CHADEMA na Mbunge wa Kigoma Kaskazini(2005-2010),anatakiwa ajiuzuru ili kulinda heshima ya Chama.Inakuaje asinginziwe yeye na sio wengine.Nyerere alisema hata kutuhumiwa tu ni kosa.
Naomba kutoa hoja.
 
Alles, Inategemea tuhuma zinaanzishwa na nani,unategemea CCM wamtuhumu kiongozi Chadema halafu kwa kuwa Nyerere alisema `hata kutuhumiwa ni kosa` basi aondoke. Mtiririko wa kihistoria unajionyesha wazi kuhusu tabia za wote wawili kimaadili.Mpeni nafasi Zito atuweke sawa ktk hili.
 
Kwa kupenda UDAKU.....

Mtu ajiuzulu kisa kuna udaku umeandikwa???!

FD
 
hahahah aisee hii tamu sana CCM 0 Chadema 1. Chifupa inaelekea kutoa game hana noma wacha na mimi nitafute ubunge wa songea mjini labda ntazimpompa pompa bi amina
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom