Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Nilimtajia mtu mmoja kuwa inawezekana kuwa hilo ni kumbatio la pole, lakini jamaa akasema inawezekana ni kumbatio la ushindi.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
UWT = Usalama Wa Taifa
Lakini si usalama wa taifa huwa hawana urafiki na viongozi wa kitaifa kwa vile mojawapo ya kazi zao ni kuwachunguza viongozi hao?
Mimi ninavyopenda kudadisi picha, kwenye mazingira kama hayo na kwa maumbo ya watu hao, mtu ambaye anamlaki mwenzake kwa kumpa pole,kwa wanaume hata wanawake ingelimbidi awe amefungua macho,ila mwombolezaji anayelakiwa anaweza kuwa amefumba au kufumbua macho.
Kumbatiano hilo mara nyingi kama linavyo onekana kwenye picha, inaonyesha hao watu wanafahamiana vizuri sana.
Kumbatiano hilo lina fanana sana na lile la kimapenzi au pia la kuoneana haya baada ya mmoja kati ya washiriki kushindwa katika shindano mojawapo(accepting defeat).
Lakini tafsiri nyingine kutoka katika picha hiyo ni kwamba,anayelaki anajikosha na kwa kufumba macho anafikiri hataonyesha mabaya yake(guilty consciousness) kwa mwenzake bila kujali watazamaji waliopo, kwani katika kulakiana vitu na watu wote waliopo huwa havina maana kwa waliopo au mashuhuda, kama kitu hicho kinatendeka kwa mapenzi ya mioyo. Haya ni mawazo yangu.
SteveD.
Lazima pia ukumbuke kuwa ile ilikuwa talaka moja, na ina maana yake. Yaani kwamba kuna kila uwezekano wa kurudiana tukimaliza tofauti zetu ama ukijirekebisha ama kwasababu moja au nyingine mume akibadilisha uamuzi wake. Kwa mfano, mwanamke wa Ki-Islam akipewa talaka moja haruhusiwi kuolewa ama kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mtu mwingine. Hiyo inaitwa kwa maneno ya mtaani, talaka rejea. Ukipewa tatu, ndio biashara imekwisha kabisa na hata mume akitaka kuwa na wewe tena haruhusiwi mpaka mwanamke awe ameolewa na kuachwa na mwanamme mwingine. Kwahiyo, hata kama ile talaka moja bado ilikuwa inasimama, bado mwanamme anatambuliwa kuwa mume wa marehemu!
Mwanakijiji,
Hili swala la talaka ni swala la Madhehebu kwa hiyo msitake kulivisha kofia na kuliweka kama ni swala la jumla ktk dini Islaam.
Swala la ndoa waumini wengi sana huchanganya pia na mila na sheria za nchi pia. Na kuna tofauti nyingi ktk tafsiri za baadhi ya aya kulingana na mapokezi ya hadithi yenyewe, iwe ktk Kuran ama Biblia..
Kwa mfano kuna wanao amini kuwepo kwa Muda wa seperation ktk talaka wakati mwanamke amekaa eda ya talaka. Kuna eda ya talaka na pia kuna eda ya kifo. Amina alikuwa bado hajamaliza muda wa eda yake ya ndoa!
Kwa hiyo muda wa seperation unapokwisha bila suluhu huyo mwananmke anaweza ku move on hakuna haja ya Talaka ama barua, wengine wanadai ni lazima kuwepo na talaka nyingine na wengine wanadai kuwa huyo mwanamke akiwa ktk eda bado ni mkeo kwa sababu ni seperation period... na wengine wanadai kuwa seperation ndio kuachana huko kinachosubiriwa hapa ni suluhisho.
All in all mjomba ukisha toa talaka mimi nadhani mtu unakuwa umesha amua. Tena basi kuna seperation period hata ktk ndoa za Kikristu, na hata serikali inazitambua sheria hizi sioni kitu cha ajabu hapa.
Iwe kiislaam ama Kikristu au kiserikali (inategemea nchi), kote kuna muda wa seperation kabla divorce haijatolewa. Can someone move on during separetion period?... Ooooh Yeah!.. dunia imebadilika.
Mkandara,
Hata mimi nadhani Barabaraya18 amekuwa too strict na talaka ya kiislamu. Nilikwishaona watu wanapeana hizo talaka moja na kurudiana kabla hata ya mwezi kupita bila fanfare yoyote. Sasa aliposema kuwa hawawezi kurudiana hadi mwanamke aolewe na mme mwingine na kuachika tena ndipo warudiane kweli ikanichanganya sana. Ndiyo maana hata baba yake marehemu ile siku ya tareher 8 May alifafanua kuwa bintiye alipewa talaka moja tu kwa hiyo haikuwa hitimisho la ndoa yao.Nadhani kuwa kanisa la katoliki halina talaka kabisa. Wana ule msingi unaosema "Akishaunganisha Mungu binadamu hawezi kutenganisha." Mkishindana katika ndoa yenu mnaweza kuachana kinyeji tu kila mtu akaenda kivyake lakini kisheria mtaendelea kuwa wanandoa.
... kabla hawajavunja muungano wao wa kifamilia na haswa katika talaqa ivunjikayo (ya kwanza au ya pili) ... hiyo eda ni kutoa fursa na muda kwa mume na mke baada ya talaka huenda kwa kipindi hicho wakamaliza tofauti zao na kurudiana na kuishi ...
kwa habari zaidi ya habari hii tembelea link hii ya kiswahili
http://www.alhidaaya.com/sw/search/node/talaka+katika+uislam
katika mada ya eda imeelezwa kwa urefu na ushahidi upo
cha msingi kuangalia dhehebu gani si kuja na ushabiki tu
Ninavyofahamu mimi kutokana na talaka ya kiislamu ni kuwa: Uislamu unaruhusu talaka moja, mbili mpaka ya tatu. Yaani mume akitoa talaka ya kwanza anaweza kumrejea mwanamke aliyemtalaka kambla ya kipindi kile cha eda hakijamalizika (mienzi mitatu), so ikiisha ile eda na mwanamume hajamrejea huyo mwanamke (kumrejea kwenyewe ni kwa huyo mwanamume kumtamkia mwanamke aliyemtaliki kuwa nimekurejea)basi itabidi kwa mwanamume kwenda kuposa tena na kulipa mahari tena kwa huyo mwanamke aliyemtaliki.
Ame akiwa amemaliza zote tatu basi hana haki tena ya kumrudia wala kumuoa tena unless aolewe na mwanamume mwengine then amuache ndio yule mwanamume wa kwanza (alyemtaliki talaka tatu) ataruhusiwa na sheria kumuoa tena.
NB:
kama muda wa eda umeisha na yule mwanamume aliyemtaliki hajamrudia basi mwanamke huyo atakuwa na ruhusa ya kuolewa na mwanamume mwengine, hata kama hajapewa talaka zote tatu na yule mwanamume wa kwanza.
hata hivo kama ilivyosemwa hapo juu kuwa kuna tofauti za madhebu juu ya hizo talaka tatu zitolewe vipi? yaani kama mwanamume atamuacha mwanamke talaka zote tatu kwa mara moja wengine wanasema inahesabika ni moja tu ama wengine wanasema ni tatu (Allahu aalam)
hivyo ndivyo ninavyoelewa mimi