Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Taarifa zetu za Uchunguzi zinaonyesha kwamba Chuo cha Ufundi cha Taifa (VETA), kwa sasa ndio Taasisi duni kabisa miongoni mwa Taasisi kongwe za serikali ya Tanzania, zipo habari kwamba kwa sasa VETA inaweza kuahirisha mitihani kutokana na kukatika kwa umeme tu, hii ni kwa sababu hawana jenereta au hawana hela ya kununua mafuta kwa ajili ya jenereta lao la kizamani walilonalo.
Kwa mfano, VETA CHANG'OMBE wanaongoza kwa matatizo , ambapo mtoa Taarifa wetu amedokeza kwamba ukiachilia mbali UKATA wa kushindwa kununua mafuta kwa ajili ya Generetor lao la kizamani lililopitwa na wakati, HATA WAFANYAKAZI WAO WANAWEZA KUTOKULIPWA MSHAHARA MPAKA UREFU WA MIEZI 6, ikumbukwe kwamba hii ndio taasisi inayofundisha hata wale malundo ya wanafunzi wanaodaiwa kulipiwa na ofisi ya Waziri Mkuu, Sasa kwanini wafanyakazi wao hawalipwi mshahara, ni nani anakula hela hizo, ni Mkuu wa Chuo au ni vigogo wa Wizara?
Taarifa mpya kutoka VETA CHANG'OMBE inadokeza kwamba kitengo cha wakufunzi wa shule ya Madereva , shule ya madereva iliyoheshimika Duniani kinazidi kupukutika baada ya Zaidi ya wakufunzi 6 kuondoka kwa mkupuo kutokana na kudhulumiwa hela zao za mshahara kwa miezi mingi.
Tatizo la Chuo cha VETA linatokana na Mkuu wa Chuo cha Chang'ombe au linatokana na Wizara?
Timu yetu ya Uchunguzi yenye watu zaidi ya 10 imeingia rasmi ndani ya Veta na itahakikisha kila uchafu unafukuliwa na kuanikwa hadharani, kama chanzo ni chuo chenyewe au kama chanzo ni serikali, basi kila kitu kitaaanikwa bila huruma.
ITAENDELEA...