EPA kunasa wengi
na Mwandishi Wetu
Tanzania Daima~Sauti ya Wengi
UCHUNGUZI wa wizi wa fedha katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inazidu kuchukua sura mpya kila siku iendayo.
Siku chache tu baada ya wanaharakati na wanasiasa kuanza kuhoji kuhusu kurejeshwa kwa sehemu ya fedha zilizoibwa katika akaunti hiyo, suala hilo sasa linaanza kubeba sura nyingi mchanganyiko.
Katika hatua moja, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema, jana alikuwa kiongozi wa kwanza kuelezea kwa undani kile ambacho timu ya uchunguzi wa kashfa hiyo ambayo yeye ni mjumbe wake inakifanya.
Akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari, IGP Mwema alisema upelelezi wao sasa umekuwa mtambuka, akionyesha dhahiri kuvuka na pengine kuwagusa watu ambao wako nje ya orodha ya kampuni 22 ambazo ndizo zilizotajwa kuhusika na wizi wa fedha hizo za EPA.
Mwema aliwaambia wahariri hao kuwa, kazi inayofanywa sasa ni kufuatilia mlolongo wa fedha hizo, kutoka zilipoibwa BoT mpaka kwa mtu wa mwisho aliyezipokea.
"Sasa tumeshavuka corporate vein (wigo wa kampuni)… tunazikusanya fedha bila kujali kwamba ulikwenda benki kuchukua EPA au la. Hili si eneo dogo. Watu wengi wametupa taarifa na sisi hatujadharau hata taarifa moja," alisema.
Mwema alisema kuwa timu hiyo imelazimika kuchunguza zaidi kwa sababu kama ilivyo katika wizi mwingine, mali ya wizi inaweza kuuzwa kwa mtu zaidi ya mmoja na uchunguzi wa fedha za EPA unaonyesha kuwa mlolongo umekwenda mbali.
Katika hatua nyingine, suala hilo limeendelea kuonekana likizidi kuchukua mkondo wa kisiasa, hasa baada ya jana Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoa tamko lake la pili kuhusu suala hilo hilo.
Taarifa ya jana ya Kamati Kuu ya CCM iliyokutana juzi inaonyesha kuwa, hadi hivi sasa timu ya wataalamu inayochunguza sakata hilo la EPA ilikuwa tayari imefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 64.
"Hadi sasa tume imefanikisha kurejeshwa kwa jimla ya sh 64 bilioni. Aidha, tume inaendelea kuwabainisha wanahisa wote wa makampuni hayo na hasa wahusika wakuu wa uchukuaji wa fedha hizi," ilisema CCM katika taarifa yake hiyo iliyosainiwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa, John Chiligati.
Wakati CCM ikitoa taarifa yake hiyo ya pili katika kipindi cha siku moja, jana hiyo hiyo, kiongozi wa timu hiyo ya uchunguzi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika ambaye alikuwa akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari, alishindwa kusema kwa uhakika kiasi hasa kilichokuwa kimekusanywa.
Mwanyika ambaye kimsingi ndiye aliyepaswa kuwa na uhakika wa kiasi kamili kilichokusanywa, katika tamko lake hilo la jana, alisema mpaka wakati alipokuwa akija katika mkutano huo, kulikuwa na harakati za kukusanya kiasi kipatacho sh bilioni 60.
Hata hivyo, Mwanyika alisema hatua itakayofuata baada ya kukusanya fedha hizo, ni taratibu za kijinai ambazo alisema haziwezi kuanza kufanywa sasa kwa kutangaza majina ya watuhumiwa hadharani kwa sababu tu ya kuwafedhehesha.
Aliwataka wanahabari na wananchi kwa ujumla kutambua na kuiunga mkono tume yake, akisema taratibu za kijinani ili zifanikiwe zinahitaji hifadhi mpaka pale uchunguzi utakapokamilika.
Mwanyika kama ilivyokuwa kwa IGP Mwema, aliwaambia wahariri kuwa, hivi sasa timu hiyo imeelekeza juhudi zake kwa kampuni hizo 22 pamoja na kwingine ambako wameweza kuzifuatilia fedha hizo.
Wakati huo huo, kwa mara nyingine tana, Mwanyika alikataa kujitoa katika timu hiyo na kujiuzulu wadhfa wake kutokana na kutuhumiwa katika ripoti ya Kamati teule ya Bunge, iliyochunguza mkataba wa kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Richmond.
Mwanyika alisisitiza mbele ya wahariri kuwa, hawezi kujiuzulu kwa sababu yeye ni mtu safi na akabainisha kuwa, tangu aajiriwe serikalini Machi 10, 1973 hajajihusisha na masuala ya rushwa.
Alisema watu wengine waliojiuzulu nyadhifa zao kutokana na kashfa ya Richmond, walifanya hivyo ili kuwajibika kisiasa, lakini yeye hawezi kuwajibika kwa sababu taasisi anayoiongoza ni ya kitaalamu.
Kwa mara nyingine tena, timu hiyo ilikataa katakata kutaja majina ya watu au kampuni ambazo hadi sasa zimesharejesha fedha hizo, kwa madai kuwa kufanya hivyo kutaharibu upelelezi unaoendelea.
Katika hili, IGP Mwema alitetea utaratibu unaotumiwa na timu hiyo na kufanya uchunguzi kabla ya kuwakamata watuhumiwa kwa maelezo kuwa, hiyo ni moja ya mbinu za kipolisi katika kufuatilia masuala ya kihalifu.
Akifafanua, alisema kuwa, yapo matukio ambayo polisi wanaweza kumkamata mhalifu na kufanya uchunguzi baadaye, kutegemea mazingira ya kosa lenyewe na kutaja tukio lililomhusisha aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ditopile Mzuzuri anayetuhumiwa kumpiga risasi dereva wa daladala kuwa ni moja ya matukio hayo.
Timu ya Mwanyika, inayohusisha pia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) iliundwa na Rais Jakaya Kikwete, baada ya kupokea ripoti ya kampuni ya kimataifa ya ukaguzi wa mahesabu ya Ernst & Young, iliyobainisha kuwa kampuni 22 zilitumika kuchota fedha zinazofikia shilingi bilioni 133 kutoka EPA katika mazingira yenye utata mkubwa.
Baada ya kuwasilishwa kwa ripoti hiyo, Rais Kikwete alichukua hatua kadhaa, mojawapo ikiwa ni kutengua uteuzi wa aliyekuwa Gavana wa BoT, Daudi Ballali ambaye hadi hivi sasa haijulikani alipo.
Maoni ya Wasomaji
Maoni 32 yameshatolewa. (Nawe toa maoni yako!)
Nadhani bwana Mwanyika hajaelewa ni kwanini jamii inamtaka ajiuzulu. si kwa sababu nafasi yake kama mwanasheia mkuu wa serikali ni nafasi ya kitaalam na siyo ya kisiasa la, swala zima linalozungumzwa hapa ni uwajibikaji. Uwajibikaji haumhusishi mwana siasa tu, bali mtu yeyote aliyepewa dhamana kwa manufaa ya umma na nchi kwa ujumla. kwahiyo bwana Mwanyika anatakiwa kuwajibika kwasababu ofisi yake ilishiriki katika kupitia mkataba wa kifisadi wa Richmond, tunataka aelewe hilo. Hata kama alimuasign mtu mwingine, yeye ni mkuu wa idara anapaswa kuwajibika.
na Chiumbati MA, Dar , - 13.03.08 @ 10:10 | #1944
Nampa pole ndugu yangu Mwanyika, maana hata kujieleza hawezi!!Kumbe Tanzania kupata madaraka makubwa haitegemei uwezo wa mtu kiakili? (Sijasema Mwanyika hana akili) Lakini atasema nini? Waandishi, maswali mnayomuuliza hayana majibu, hata mngekuwa nyinyi ndo Mwanyika mngejibu nini? Mngemtaja nani? Mmiliki wa Deep Green au? Kama kawa tunaendelea na mazingaombwe, yetu macho. Watanzania ni nani ameturoga?
na kukuz, singapore, - 13.03.08 @ 10:12 | #1945
.... Nadahni CCM ingeiachia tume ifanye kazi yake. Isituchangeye kwa kujifanya wao ni watoa taarifa. kwani wana wasiwasi gani? maji yakishamwagika hayazoleki... tuache tuone mwisho wake...
na Chiumbati MA, Dar, - 13.03.08 @ 10:14 | #1946
Nampongeza IGP kwa uwezo mkubwa alioonyesha katika kuelezea kinachoendelea (Simaanishi nimekubaliana na maelezo yake) Nachopongeza hapa ni uwezo wake na upeo alioonyesha. Angalau kaeleza kitu fulani kinachoweza kushawishi kihoja. HONGERA Mwema.
na kukuz, singapore, - 13.03.08 @ 10:19 | #1947
mwanyika ni sehemu ya wa2 wanajiona tanzania ni mali yao peke yao na familia zao.anadhana ya kuwa bila yeye hakuna AG ,na baraka za kiburi chote hiki anapata kwa mamlaka za juu.na shida yao hawasomi alama za nyakati na si muda mrefu watalia na kusaga meno hakitamfaa m2 chama chake wala cheo wala aina ya wapambe ama aina ya gari anayotembelea
na sadiki, mtwara, - 13.03.08 @ 10:35 | #1953
Mimi nafikiri taarifa tu haitoshi bali tunachotaka ni kuwa hawa waalifu ambao Memwa anawafananisha na Magaidi wanachukuliwa hatua hata kama ni nani? Kama wanashindwa kuwataja labda kwa nyadhifa zao basi watuambie sisi umma ili tuwaamue cha kufanya. Mkumbuke jamani nchi hii ni maskini tusiwape hawa waalifu nafasi ya kutumaliza. Manyika kama huwezi kujieleza basi waachie wenzio wanoweza.
na Musa Yamo, Tanzania, - 13.03.08 @ 10:40 | #1957
jamani mbona mwanyika anajivunjia mi sijaona lolote jipya na la maana alilosema,huyu jamaa nae inaonekana kapewa hii nafasi kishikaji tu na sijui taaluma yake ila nina wasiwasi ni mjanja mjanja ktk swala zima la taaluma,hata huyo mwema nae kasema ya kua sasa wamegundua ya kua mlolongo ni mrefu sana,na wanafanya uchunguzi kutoka kwa mtu aliepokea hadi wa mwisho kuzipata,sasa tumeshajua nani anazirudisha pesa kwa nini tusianze na huyo ili awataje wengine,km katumwa kuzirudisha aseme katumwa na nani na yuko wapi huyo aliemtuma,mi sijaona jipya vilevile kutoka kwa mwema mana kajikanyaga tu,unajua hawa wanajifanya km wamarekani kuona kwamba waafrika hawana akili so wanafanya mambo kisiri watanzania wanajua mambo tokea zamani ila tofauti ilikua ni ubabe tu wa mkapa ndio mana wengi walikua hawaongei kiwazi namna hii,na hao CCM mi sielewi, hivi na wao ni wanakamati inayochunguza mambo ya BOT ama vipi coz hukku mwanyika anasema mpk sasa kiasi cha bil.60 kimepokelewa chiligati anasema bil.64 mi naona mwema nae aongee na chiligati na kutwambia wanajua nini kuhusu hili swala,jingine ni kwamba mwanyika kasema ya kua mpk asubuhi akiondoka kazini zilikua bil.60mzimerudishwa mana yake ni kwamba wanajua leo,kesho na keshokutwa kuna fulani na fulani watarudisha pesa,jamani watanzania tuwaulize hawa watu maswali na watupe maelezo ya kina si upuuzi huu wa mwanyika na mafisadi wenzie,mi nina wasiwasi mwanyika anaambiwa kitu gani aseme ndio mana akifika mbele ya wahariri anapagawa,Mungu azidi kuwagonganisha wenyewe kwa nwenyewe wazidi kujichanganya na mwishoe wataanza kutaja majina bila kujijua wanachofanya sidhani km muumba anapenda ufisadi huu tena kwa nchi km tz.
na mstari wa mbele, calif/usa, - 13.03.08 @ 10:40 | #1958
CCM ni wezi mbona wanajishitukia!!Mwanyika anahitaji ujasiri wa hali ya juu sababu Deep Green ni mali ya CCM,KWANI MAMBO HAYA YANAFICHIKA?Tena ilichota fedha nyingi sana BOT 2005,tembelea mikoa yote Tanzania kuna magari yana rangi ya "deep green" yani kijani muivo,yanatumika na makada wa CCM,kwa nyuma yameandikwa "Mahindra"yalinunuliwa kwa kasi ya ajabu mwaka 2005,hayo ndo matunda ya Deep Green company!kampuni yenya jina linafanana na rangi ya magari yake!!kinachofanyika ni kuwaengua baadhi ya vigogo ili kupunguza mtiksiko wa nchi,yote kenda,kumi lazma kitaeleweka na!!!The day is coming when ze deep green will change to ze deep red?!!when ze sons and daughters of "deep peasants" will rise against ze sons and daughters of "deep greeners"!!days are numbered!!all of cote de voire and near by Kenya will be seen as "mvua za rasharasha"
na MDANGANYIKA, Tz, - 13.03.08 @ 10:44 | #1962
Angalau IGP Mwema katoa maelezo ya kueleweka, sio hao wengine. Halafu kitu kingine ningependa kuwahasa wana Chama Cha Mafisadi kuiachia Kamati teule kazi yake, sio wanaanza kuingilia kazi za wengine.
na Malisa David, Tanzania, Dar Es Salaam., - 13.03.08 @ 10:47 | #1965
Ningetegemea jana katika mkutano na wahariri. Mwenyekiti a tume angetaja akaunti Namba kwa ajili ya kurejesha fedha hizo EPA. Ni utamaduni wetu wakati wa majanga mfano janga la mafuriko. ofisi ya waziri mkuu hutangaza akaunti wananchi kuchangia. Wakati wa serikali awamu ya kwanza. Sakata la uhujumu uchumi Marehemu Sokoine aliwataka wahujumu kusalimisha mali katika maeneo yalitojwa hasa ofisi za serikali. mwenyekiti ataje tu akaunti hiyo ili fedha na mali zirejeshwe kwa urahisi kwa manufaa ya taifa. kazi kwako mwenyekiti.
na Yukundus paul mhonda, dar es salaam, - 13.03.08 @ 11:06 | #1974
Kwa kweli inasikitisha sana ,Sasa huu uchunguzi unaofanywa na TAKUKURU iliyotiliwa mashaka na kinamwakyembe tena kwa ushahidi wa wazi na zaidi ya yote walishauri kwamba huyu bwana hosea na mwanasheria mkuu wajiuzuru na bado serikali ambayo ndio mwajili wao imeamua kuyagomea maamuzi ya kamati, sasa mbona hii nchi haieleweki .Huu uchunguzi wa EPA utaleta majibu ya Kweli ,hawa watu ambao hatuna imani nao je wanaweza kueleza ukweli?Inaelekea siku hizi utaraibu wa kukamata wezi umeboreshwa maana mpaka mwizi afanyiwe uchunguzi kwanza akiwa nje ndipo baadae akamatwe ,je wale walioko keko waliopokoea rushwa ya elf 10 na wizi mdogo ndio wanaostahili kudhalilishwa??????
Mwizi ni mwizi tu na mtu anapoiba anakua ameamua tokea ndani ya moyo wake kujidhalilisha sasa nivema kuwaanika labda itasaidia sisi wananchi kuwachukulia hatua kwa sababu vyombo husika vimeshindwa.
Wapinzani endeleeni kuiamsha serikali bado ipo kwenye usingizi mzito na inaota ndoto za alinacha,februali maka huu ilikua inajigeuza ubavu tukadhani imeamka kumbe bado please help!.
na queen, Dar, - 13.03.08 @ 11:10 | #1975
Kama hii deep green ni ya CCM na ushahidi wa wazi upo, wanaweza kutueleza fedha hizo wamepata wapi? Tumeona CCM wamekodisha Chopper(helcopter) wakati wa kampeni kule Kiteto, wanaweza kutuambia pesa walizipata wapi? Kwahiyo hawa ndo wezi wenyewe na wanajifanya kutoa taarifa za kamati wao ni akina nani ktk hili? wanachojaribu ni kuharibu ushahidi wa wao kuhusika mojakwa moja na ndio maana wanaendelea kumpa kiburi Hilo fisadi linajiita manyika. Mwema anadai eti wanaogopa kuwakamata eti wataharibu ushahidi, jamani mtu akiiba kuku hata kama hajaiona kuku yenyewe ila manyoya tu ya kuku huyo yakikutwa kwa mtu, basi huchukuliwa na kuwekwa police eti kusaidia police. sasa hawa wanaorudisha pesa hizi si manyoya yanayoweza kuwapeleka police kuisaidia.Tuache uppuuzi huu tunajua mtu ankua suspect under castody and to jail if proven guilty by the court, sasa wanafanya nini huku nnje hamuoni wataharibu ushahidi?
na minako, bukoba, - 13.03.08 @ 11:13 | #1977
HIVI HUKU NI KUCHANGANYIKIWA AU NI KUTUJUA MAJUKUMU? NI NANI ANAYETAKIWA KUTOA TAARIFA ZA KISERIKALI, NI CCM AU SERIKALI HUSIKA? HIZI TOFAUTI ZA MAREJESHO (bil 64 na 60) ZINAZOTOLEWA NA CCM NA SERIKALI TUZIAMINI ZIPI? HII NI SERIKALI YA NANI, NI YA WATANZANIA AU NI YA CCM? Kwanini ccm hupenda kujibu masuala ya kiserikali?
na Chirwa - 13.03.08 @ 11:16 | #1978
Mwanyika anaposema kuwa yeye ni mtu safi, eti wale waliojiuzulu ni kwa sababu ni political, hivi anatuona sisi hamnazo?eti anasema anaongoza ofisi ya wataalam, wataalam gani hao wasiojua wajibu wao?wataalam gani wasiojua kulinda maslahi ya nchi?wataalam gani hao wanaoshindwa kutambua hata forgery ndogo tu ya richmond?wataalam wanaokubali kuwa richmond ana makubaliano ya kikazi kwa kutumia business card!?Huyu mwanyika si ndiye alikuwa naibu mwanasheria mkuu wa serikali wakati wa awamu ya tatu ambayo ilivunja rekodi kwa kuingia mikataba mibovu kuliko mkataba wowote tunaoufahamu?Ukweli ni kuwa mwanyika si mtu safi hata kidogo, uchafu alionao pamoja na ofisi yake unatosha kumfanya aone kuwa sasahivi watanzania hawana imani naye tena hata kama atajaribu kulazimisha usafi. Hata ofisi yake imepoteza heshima yake mbele ya watanzania.
na nyahende thomas, tz, - 13.03.08 @ 11:34 | #1983
Tunaweza kuokoa Tanzania isikumbwe na balaa la mapigano kwa viongozi wetu ambao kwa njia moja wamehusishwa na rushwa kuwajibika.hii itajenga imani kwa wananchi na jamii kwa ujumla,pia itapunguza tofauti ambayo imekwisha kujitokeza ya kipato kwa kuwa waliopo madarakani wamekuwa wakitumia madaraka vibaya kwa nia ya kujilimbizia mali na kusababisha tofauti ya kipato kati ya wenyenacho na wasionacho
na Rodius isack ng'unda, Tanzania, - 13.03.08 @ 12:00 | #1989
IGP Mwema anawafananisha mafisadi na maharamia (hijackers) wa ndege. Anasema kwamba timu yake inabidi iwe makini katika katika majadiliano na hawa "hijackers" wasije wakalipua ndege na abiria na ndege yao wakapotea na kuagamia! Tumuulize Bwna IGP Hao mafisadi washikilia bomu lipi na ndege ipi? Hao mafisadi wakilipua hilo bomu ina maana Tanzania na wananchi wake wanaweza kuteketea? Atwambie.
Kwa Mwanyika nadhani upeo wake ni mdogo kiasi Tume ya Uchunguzi wa Richmond ilichosema kuhusu AG Chambers ni kwamba that office is incompentent under the stewardship of Mwanyika Ushiriki wa ofisi yake katika mkataba wa Richmond haukuwa na TIJA. Ina maana gan? Mwanyika kwa nini haelewi hili?
na Luteke, Dar Es Salaam, - 13.03.08 @ 12:04 | #1991
Watanzania wenzangu,mwenye macho haambiwi tazama.Kumbukeni BUNGE liliagiza nini wakati linaahirishwa.Mwanyika anasubiri KUAIBISHWA ndio ajiuzuru kwenye kikao kijacho cha BUNGE.Kwa sababu hajaelewa alama za nyakati zilizopo sasa azisubili azione.Vilevile urejeshwaji wa pesa hizi ni KIINIMACHO.Kama kweli zinarudishwa kwa nini hiyo account isitajwe?Hiyo ni danganya toto,Lakini serikali ya ccm ikumbuke kuwa Tanzania ya leo siyo ile ya 1961.
na Daud Juma, Kisesa- Mwanza),Tanzania., - 13.03.08 @ 12:16 | #1993
MIE SINA IMANI JINSI SWALA LA EPA LINAVYOSHUGHULIKIWA. KWANZA ASANTE SANA MTOA MAONI MMOJA HAPO JUU ALIETOA HABARI ZA DEEP GREEN KWAMBA NI YA CCM.HIVI WANANCHI KWA NINI TUSIUNGANE KWA PAMOJA KUONA KUBENEA ANALINNDWA? MBONA WEZI WA EPA NA RICHMOND WANAJULIKANA NA WANADUNDA MITAANI KUBENEA ANAE TUPA HABARI MUHIMU ANAISHI KWA WASIWASI?HIVI KUBENEA AKIDHURIKA TUTASEMA NINI?MAANA ANATUFANYIA KAZI SISI YEYE TAYARI ANAYAJUA.MIE NAFIKIRI HILI LA KULINDW KUBENEA ITUMIKE NGUVU YA UMMA.
na pendo daniel, tz, - 13.03.08 @ 12:29 | #1994
.....hivi huyu Balali yuko wapi???? Ningekuwa Mwanyika na wenzake, nisingepoteza muda sana wa kuhangaika na uchunguzi. Ningetumia fursa ya kuteuliwa kwenye kamati hii na kumfuata Balali anieleze hawa watu aliogawana nao hii hela yetu ni akina nani na kila mtu alipata bie gani, baada ya hapo nawabana watu hao warejeshe pesa kisha hatua zingine zinafuatia. Miezi sita waliyopewa akina mwanyika ni mingi sana.
na Rutta., Dar es salam, - 13.03.08 @ 12:33 | #1995
Naungana na wenzangu waliotoa maoni kwamba,hivi Tume ya EPA ni ccm? mbona taarifa inatolewa na ccm kwa niaba ya tume? hii ni kwamba heri kufa tu kuliko kuona ujinga unafanyika wazi namna hii. Ni wazi kuwa Deep green ni kitengo cha CCM,sasa hii bla bla ya Mwanyika Na mwema itatufikisha wapi? why buying time? Mwanyika ni MCHAFU,PAMOJA NA HOSEA,hamwoni aibu? inaonekana hata aliye wateua ni mchafu pia,mbona wanaongea kama vile wamelishwa maneno nini waseme? Hivi watanganyika wenzangu mnafikiri CCM walipata wapi fedha ya kufanyia kampeni 2005 baada ya mgombea mwenza wa CHADEMA kufariki?hii ni kiini macho twachezwa,Tuamkeni ni heri kuvaa bomu la muhanga kuliko kuona watu wanatufanya sisi mazuzu...Aluta.
na Ng'ombe yapi, Arusha, - 13.03.08 @ 13:07 | #2004
Mizengwe tu! ndani ya ccm mizengwe,rushwa na chuki je nje ya CCM?ubabe,mikwara na vitisho-siasa imewashinda ndiyo maana mmeingiza wa fanyabiashara ndani ya siasa.Fedha hizo bilion 64 kuna kila dalili zina rudishwa na CCM,sawa malizieni zilizobaki jambo hili liishe.
Mlitaka kufanya maandamano nchi nzima Mhe Rais akawazua... jumlisha hapo.
na mlowe richard, dsm, - 13.03.08 @ 13:41 | #2009
Haya marejesho ya CCM na marejesho ya KAMATI mbona tofauti. Tuiamini CCM au KAMATI. Halafu hivi JK aliteua Kamati mbili? Hii Kamati ya CCM nani kaipa uwezo wa kuisemea EPA?
na Bubu Msemaovyo, Dar es Salaam, Tanzania, - 13.03.08 @ 13:51 | #2010
Nafikiri ccm wanachofanya nikuendelea kutudanganya sisi wananchi, hilo wanalifahamu ndiyo maana wameanza kujikita vijijini ambako wanajua watu mbumbumbu maana mjini tumesha washitukia. hivi kwanini kila anayevaa hiyo suti yao ya green ghafla tumbo linakuwa kubwa? kama siyo ufisadi ni nini? Niko radhi kufa kuliko kuona ccm wanaiba kura yangu 2010 bora tukose amani kuliko kuwa na amani kuwanufaisha deep greeners ili watafune nchi.
na mwijage, arusha, - 13.03.08 @ 13:54 | #2011
watazania nadhani tuwe wavumilivu, kamati imepewa miezi 6, na ndo kwanza hivi sasa ni miezi 2, imebaki 4, hivyo ni mapemz amno kuishinikiza tume kuweka wazi tuwache wafanye kazi than ukifika muda km hawataweka weka tuwasute na kuwasema. hata tume ya teule ya bunge ya Richmond ilipew muda na kuzidishiwa na matokeo yake tumeyaona, najua hofu yetu watanzania mambo mengine hayahitaji pupa hasa haya ya kisheria kwani ikifanyika pupa a kwanza pesa hazitopatika pili inaweza kusababisha hasara kubwa kwa serikali, katika hivi kesi za jinai na madai zinataratibu zake na ukimuhusisha mtu than ukampabublicize before ya ushahid than baadae ikabainika hajahusika anaweza kuipeleka mbele ya mahakama na kudai serikali fidia kubwa, uengereza kuna kesi iliyokuwa ikimhusisha Tonny Blair ya cash for honour, ktk kesi hiyo blair alituhumiwa kuwapa cheo baadhi ya watu kwasababu walikuwa wafadhili wake, wakatajwa majina na vyombo vya hanari kesi ikaenda mahakamani na matokeo yake walishinda na hivi sasa magazeti kadhaa ya nchi hiyo wanatakiwa wawalipe fidia.
na nda,br, Zanzibar, - 13.03.08 @ 14:26 | #2015
Viongozi wa serikali watambue kuna siku moto utawaka kuliko ilivyotokea Kenya na hakuna atakaeweza kuuzima sio Bush wala Koffi Annan watanzania wameamka kutoka kwenye usingizi mzito,sasa wamatambua Hata EPA,Deep green,Richmond,Iptl,Buzwagi,Anbem,Meremeta,Tangold, kila corneR ni Ufisadi mtupu je tutafika? ARI MPYA KASI MPYA SIJUI ITAANZIA WAPI.
na Casto Maiko, Dar-es-salaam, - 13.03.08 @ 14:30 | #2016
Mwanyika naye ni fisadi tu.Hafai kuwa
mwanasheria mkuu wa serikali.
na jane, tz, - 13.03.08 @ 15:29 | #2023
Chiligati nae fisadi, ndio maana umewasiliana na mafisadi wenzako wakakuhakikishia kuwa wangerudisha zifike bil 64 ndio ukaenda kutangaza, why the difference in figure between you and mwanyika, nyie nyie , tuvhezeeni tuu.
na kima, arusha, - 13.03.08 @ 15:35 | #2024
Mwakyembe bwana, acha kabisa. anasoma taarifa bila hata kunywa maji!!!!
mi sitaki kusema mengi, kwa aibu ya ndugu yetu Mwanyika, pole mzee, kazi unayo, watakuchambua wasome mpaka utajiuzulu tu. waachie wanaoweza mwanawane, cha kufia kwenye kiti cha moto kama cha jana. pole.
na mshikaji, Jiji la maraha-ARS, - 13.03.08 @ 15:53 | #2030
TAFSIRI ISIYO RASMI
DEEP GREEN = KIJANI KILICHOKOLEA!!!
na Quara, mwanza, - 13.03.08 @ 16:04 | #2032
hii inaonyesha dhahiri jinsi ya CCM na Serekali yake wanavyowahadaa wanyonge kwenye kura ili wawaibie mali zao za umma, CCM ( Chukuwa Chako Mapema ) , sasa itakuwa ( Chomoa Chako Mapema ) kwani wananchi wamekushtukieni wizi wa mali ya Umma
na kapucho, Zanzibar, - 13.03.08 @ 16:07 | #2033
mi nasema hii yote ni longo longo tu na upuuzi tu mtupu, ivi kna jambo gani la kuchunguza miezi 6 na kila kitu kiko wazi kabisa??
hosea na mwanyika kaeni pembeni kwanza ninyi ni mafisadi vile vile na mulitajwa waziwazi katika ripoti ya kamati teule ya bunge.
mwanike we!!! unajihashua bure kuita wanahabari wala huna mpya yoyote!!! kazi yako kupotezea watu muda bure na kujifanya kama una nyeti kumbe una pumba tupu, stupid wewe!!!!
na Vundo J.Vundo, bongoland, - 13.03.08 @ 16:41 | #2040
Mheshimiwa Mwanyika,
Pamoja na heshima zote, tunakuomba uache kujitetea kwa kutumia utaalamu na taaluma. Kuendelea kwako kufanya hivyo kunatufanya sisi wasomi na wanataaluma tujisikie vibaya!!
Swala hapa sio taaluma yako, swala ni uwezo wako wa kufanya kazi uliyopewa. Umeshindwa kufanya kazi ya Mwanasheria Mkuu kwa kushindwa kuishauri vizuri serikali. Basi!!! Unakubali, unakataa, huo ndio ukweli.
Acha kuchafua taaluma. Unataka watu waelewe kwamba wanataaluma wanaruhusiwa kuboronga na kuachwa tu? Tuamini kwamba ni wanasiasa tu wanaopaswa kuwajibika, wanataaluma hawapaswi kuwajibika. Hapana, hapana, hatukubaliani na wewe!! Umetuaibisha kiasi cha kutosha, ondoka waachie wenye uwezo.
Anagalizo: (Ushauri wa bure!!) Usiposhtuka sasa hivi ukajiondoa, unasubiri kuaibishwa punde Bunge litakapoanza. Kuna watu tunasubiri damu yako!!!
Mungu ibariki Tanzania, Mungu wasambaratishe mafisadi!!
na Amk, Dar, - 13.03.08 @ 17:34 | #2047