Sikiliza Akili Matope tupu,
Sijaamanisha hicho ulichokiandika, nakueleza kuwa Madai ya kuwa kukosekana kwa transparency katika awamu hii kumeongeza rushwa si ya kweli, mbona katika awamu iliyopita mliyozoea kumtukana mkulu kama mlivyotaka bado rushwa,wizi na dili bado vilikuwa juu sana!, hivyo hiyo siyo hoja sana, Kimsingi sisi Watanzania(na mimi mmojawapo) tunapenda sana maisha ya dili dili, Awamu hii kidogo inajitahidi kupambana na rushwa, lakini si unaona ugumu uliopo toka kwa wananchi, malalamiko kila kona kwanini? kwasababu ya mfumo wa maisha tuliyozoea, ndiyo maana si ajabu unapokutana na watetezi wa wezi, watu wanaowaona wezi kama mashujaa, ndiyo jamii yetu ilipofikia, Tunawasifia na kuwaona mashujaa watu walioiibia serikali.
Nafikiri kidogo umenielewa Akili Matope tupu.