Kashfa ya Richmond: Lowassa, Karamagi na Dkt. Msabaha Wajiuzulu

[h=1] Mzee Ngoyai kawaambia kwamba yeye ni Mkristo, na Neno la Mungu linanena waziwazi kuhusu kutii mamlaka iliyojuu:

Warumi 13
: 13

Kila mtu hana budi kutii serikali inayotawala. Kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na serikali zote zilizopo zimewekwa na Mungu.
[/h]
 
Lowasa hawezi kukwepa kashifa hii hata akiogamaji ya baarini.


Kushabikia tuhuma ambazo huna ukweli nazo juu ya mtu mwingine huo ni 'upumbavu' kwa maana ya kuwa unajua unachokifanya sio sahihi lakini utabaki kushupalia mpaka mizizi inakutoka...

Ameshasema mwenye ushahidi ampeleke mahakamani tofauti na hapo mkae kimya.Pia kumbuka siasa ni maisha yako ya sasa na ya baadae ,hivyo usiifanyie ushabiki kama wa mpira.Hapa tunaizungumzia Tanzania na mustakabali wetu ...
 
Mlitaka aseme alihusika ili akatwe tena? kashfa aliyotuhumiwa sio ya siasa ya chama bali ni maslahi ya umma na alipaswa kuulizwa na mamlaka ya serikali(mahakama) ikizingatiwa kuwa wanaomuuliza ndio waliomtuhumu kuhusika! au chadema wamekuwa mahakama?

Hivi mamlaka ya juu iko karibu na waziri mkuu au au na mwanasheria wa serikali.? Inauhakika gani kama mwanasheria hakupiga simu kwa mamlaka ya juu kisha kumuongopea.au kushauriwa vibaya na mwanasheria.ili hali yeye lowasa alikuwa karibu sana na mamlaka za juu za maamuzi kwa nini hakuongea yeye na mamlaka ya juu
 

Angejiuzuru hapo hapo.
 

Kwenye siasa watu hawazungumzizungumzi tu. Kila kauli ina sababu na maana kubwa.

Ukiangalia jitihada za Lowassa kutaka kuzungumzia sakata la Richmond kupitia TBC lilivyozuiwa kabla, yaliyomkuta Tido Mhando, ukifautilia kauli na mashaka ya viongozi wengi wa CCM dhidi ya mwanachama 'mwenzao' wa zamani Lowassa na hali ya hofu ya watu kusema atalipiza kisasi, mtu mwenye akili ata-conclude kuwa kuna kitu chini ya kapeti hatukijui kuhusiana na ufisadi au usafi wa Lowassa.
 

Si katika uovu.Huwezi tii mamlaka inayokutuma ufanye uovu.Mamlaka ya juu ikisema lete mkeo tumlale utaitii?
 
Katika majibu yake aliwahi kusema, tatizo halikuwa Richmond tatizo ilikkuwa uwaziri mkuu, na aliendelea kusema mkataba wa Richmond haukuwa na kasoro yyte,
 
mngekalia kumpigia debe mgombea wenu mngemsaidia sana,kwani ana wakati mgumu sana kupambana na tingatinga

Kibaraka hawezi kuwa tingatinga katu! Labda kama unazungumzia tingatinga kwa maana ya aina ya nguo ya batiki.
 
Wapendwa tambueni yakwamba Mungu ni MKUU hata kama lowasa hataingia ikulu ila tayari ukweli tumeujua
 
Mlitaka aseme alihusika ili akatwe tena? kashfa aliyotuhumiwa sio ya siasa ya chama bali ni maslahi ya umma na alipaswa kuulizwa na mamlaka ya serikali(mahakama) ikizingatiwa kuwa wanaomuuliza ndio waliomtuhumu kuhusika! au chadema wamekuwa mahakama?

Hapo penye red, Sasa kwanini mamlaka hiyo miaka nane(8) yote haijamuuliza, na amesha sema si jana tu kuwa mwenye ushahidi apeleke mahakamani. miaka nane yote mamlaka ilikuwa wapi?
 

Save that bullcrap to some CDM kid not me please.

Yani unataka mtu aliyeficha uovu wa CCM kwa miaka 8 baada ya kufahamu,if that was the case anyways,ndio apewe nchi?do u even listen to yourself?

Wakati slaa anamwita Lowassa Fisadi hakujua haya unayobwabwaja hapa?wakati viongozi wenu wakuu wooote walipotumia kodi zetu kuzubguka jukwaa baada ya jukwaa kumuambia Lowassa na marafiki zake hamkuyajua hayo?what changed?

Msifanye watu hatunazo.
 

Unajua mamlaka ya mwanasheria mkuu lakini?

Unajua anaripoti wapi?

Unajua hawezi kuhojiwa wala kushtakiwa kwa ushauri wake?
 
Ni kosa kutoa siri za vikao vya baraza la mawaziri,lowassa haaminiki, kama anaweza kutoa siri za vikao, tutawezaje kumwamini kwa kumpa nchi yetu aisimamie, akamatwe na kushtakiwa kwa kuyaleta mambo ya vikao katika public;
 

What changed is that ...Kwa sasa Tunaye Lowasa huku CHADEMA
Hata Dr Slaa alitoka CCM baada ya Kukatwa kwa tuhuma zake alizotungiwa na CCM...Its Just timing
This is Politics....Kule Field watu wanamwelewa sana Lowasa
 

Nasikia hakuna aina ya mganga wa kienyeji ambaye hajawahi kukanyaga jumba kuu. Kila siku ni dogoli tu linapigwa!
 

Unajua Richmond ndonini
 
CDM kweli akili ndogo.yani mnaaminishwa kabisa subordinate-mwanasheria mkuu,anaweza kutoa maagizo kwa senior wake,PM !

Hakuna ofisi duniani inafanya kazi kwa sampuli hiyo especially serikalini ambako ukikosea itifaki ya viti tu watu wanamind.

Katika mazingira ya kazi serikalini mwanasheria mkuu hawezi kumpigia simu Raisi kuomba Ushauri,hiyo ni kazi ya PM.the chain of command ni kuwa kwenye hicho kikao aliyeitisha sio mwanasheria mkuu,ni PM,ndio mwenyekiti.ndio alitakiwa apige simu kwenye mamlaka ya juu kama anavyoaminisha watu.

Huyu jamaa naanza kuamini kwa dhati aliyoyasema Mwakyembe kuwa bora akae kimya.
 
Lowassa kisasi hapana, lakini waliotenda maovu wawajibishwe, mzee wa "wapigwe tu" aende the haig
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…