Kashfa ya Richmond: Lowassa, Karamagi na Dkt. Msabaha Wajiuzulu

Kashfa ya Richmond: Lowassa, Karamagi na Dkt. Msabaha Wajiuzulu

Mamlaka ya juu haikuwasiliana na lowassa ikaamua kuwasiliana na Mgonja na lowassa mzee wa maamuzi magumu akakaa kimya!

Sasa nimeelewa kwa nini Mgonja kashinda Kesi, wakati wakina Mramba na Yona- wameenda Jela. Nimesha connect Dots............
 
Muda huu katika kukakiribishwa na kukabidhiwa kadi MH.LOWASSA ndani ya CHADEMA ,ameulizwa swali moja kuwa

Swali: Mh. Edward Lowassa unazungumiaje kuhusu kashfa ya Richmond?

Majibu Lowassa:
Nipende tu kusema mimi kama waziri mkuu kwa kawaida ya sheria huwa ninaletewa mkataba muda wa mwisho kuupitia na kuupitisha huwa sihusiki na kuandaa mikataba,mwenye mamlaka ni waziri husika.

Hivyo baada ya kuletewa mkataba husika wa Richmond niliupitia na kiukweli niliuwekea shaka kwa sababu nilishawahi kuwa waziri wizara ya maji nina uzoefu na kuandaa mikataba, nilishauri mkataba huo uvunjwe lakini waziri wa nishati akawasiliana na "NGAZI YA JUU" na kulazimishwa kuupitisha mkataba huo.

Baada ya kugundulika kuwa mkataba huo ulikuwa na mapungufu mengi, "NILICHUKUA MAAMUZI MAGUMU KWA AJILI YA SERIKALI, na kubeba mzigo wote ndio maana hadi leo wanasema mimi ni FISADI WA RICHMOND, nipende kumaliza kwa kusema kwamba MWENYE USHAHIDI WA RICHMOND AENDE MAHAKAMANI AKANISHTAKI.

mwisho.

Sasa nimeelewa kwa nini Mgonja kashinda Kesi, wakati wakina Mramba na Yona- wameenda Jela. Nimesha connect Dots............
 
Kweli sie ni wadanganyika na si watanzania, MTU alieliibia taifa Mali ya uma leo hii tunasema anafaa!!!! Na kama ilikuwa ngaZi ya juu mbona hakusema kipindi hicho, na alikubali kujiuzuru ili iweje? Na bila aibu eti mbowe anasema chama chake kimefanya kaz kubwa kumconvice Edo ajiunge chadema, mie nasema na eti mwenyeushahidi aende mahakamani. While 2007 chadema ndio waliokuwa wakiombwa ushaidi kuthibitisha ufisadi Wa lowasa, Leo hii chadema nao wanaomba ushahidi!!!! Eeemola nusuru kizaz hiki cha nyoka. Lowasa hafai hata kuwa mjumbe Wa nyumba10.
 
Hivi mamlaka zinazoitwa za juu zimejibu nn kuhusu hii movie
 
Kweli sie ni wadanganyika na si watanzania, MTU alieliibia taifa Mali ya uma leo hii tunasema anafaa!!!! Na kama ilikuwa ngaZi ya juu mbona hakusema kipindi hicho, na alikubali kujiuzuru ili iweje? Na bila aibu eti mbowe anasema chama chake kimefanya kaz kubwa kumconvice Edo ajiunge chadema, mie nasema na eti mwenyeushahidi aende mahakamani. While 2007 chadema ndio waliokuwa wakiombwa ushaidi kuthibitisha ufisadi Wa lowasa, Leo hii chadema nao wanaomba ushahidi!!!! Eeemola nusuru kizaz hiki cha nyoka. Lowasa hafai hata kuwa mjumbe Wa nyumba10.

Ahahahaa
Acha wadanganyike tu tupate mijihelaa aisee ikulu tamuu!!!
 
ukimpiga kiongoz mstafu UNAPEWA UKUU WA WILAYA HII NDIO CCM.
kura yangu ni kwa lowassa hatakama mimi sio UKAWA
 
Huyo kanga tumenyoa sisi tena ni kibudu aka nyamafu. Kuleni uozo wa matapishi mnayomezeshwa na Mbowe.

Misukule siwashangai kwa kuwa kila mtakacholishwa kwenu ni hewala tu, hamna akili za kufikiri wenyewe, nnamshangaa Mbowe, haoni hata haya kula matapishi yake?

sanduku la kura litawapa majibu,kama mpo sahihi au la.
 
uki achana na mke mpe heshima yake usipo fanya hivyo ata kuumbua maana ana kufahamu.na lowasa ata wa anika msipo kuwa makini.
 
sanduku la kura litawapa majibu,kama mpo sahihi au la.

Matokeo yameshajulikana. hakuna Mtanzania ataempigia mtu kura kwa fedha zake, watu fedha watakula na Urais hawampi.

Nani ataekubali kuongozwa na mgonjwa asiyeweza hata kuweka maneno sawa? Labda ni misukule tu.
 
Mods naomba usifute
Tumeona Basiri mramba, Daniel Yona wakifikishwa mahakamani
Lowassa alijiuzulu kupisha uchunguzi wa mahakaman lakn hakuna kilichofanyika zaidi ya kumtuhumu tu
naomba sababu za kwa nn hakufikishwa mahakaman???
 
Naomba watanzania mniwie radhi kwa swali hili.Nimekuwa nikijaribu kuwauliza watu wengi wa kawaida wenye chuki kubwa dhidi ya mh Lowasa waniambie kidogo kuhusu kashfa ya Richmond.Wengi wanasema ni kampuni ya mh Lowasa ndio maana kaiita Richmond yaani kifupi cha "Richard Monduli"!!!Ukiendelea kuhoji,inaonekana wengi hawajui chochote kabisa na ingawa wana misimamo mikali sana dhidi yake!Sasa ningependa kujua hii Richmond ni nini katika nchi hii?Ina maana hakuna kashfa nyingine nzito kama hii nchi hii?Najua hicho kifupi ni uswahili tu wa watanzania na wengi wana tabia ya kukariri bila kufikiri,hivi ilikuwaje watu waelelewa kama baadhi ya viongozi wa ccm yenyewe wakimuita mzee huyu ati fisadi?
 
Ni vita ya kuelekea ikulu baina ya CCM na Mbunge wa Monduli Mheshimiwa Edward Ngoyai Lowasa.
Kuna maswali mpaka sasa bado yanakosa majibu na hayako wazi na na hakika kama yangekuwa na majibu hakika kusingekuwa na vita baina ya Lowasa na Kikwete(CCM) kuelekea Ikulu apo mwezi wa kumi.
1) Kikwete na Lowasa walikuwa ni marafiki wakubwa sana, kipi kimewafanya mpaka urafiki uo uishe??
2) Kama Lowasa ni fisadi, Kuna mafisadi wangapi waliopita au waliopo kwenye chama cha CCM mpaka sasa??
3) Kwanini wakuu wachache wa chama wakiongozwa na Kikwete wamkatae sana Lowasa wakati wanachama wengi wa chama icho wakimkubali??
4) Kama kuna ufisadi mkubwa wa richmond unaodaiwa kuongozwa na Lowasa, Mbona hakuna ata mhusika mmoja alieshitakiwa kwa uo ufisadi??
Ayo ni baadhi tuu ya maswali machache ambayo yangekuwa na majibu bila shaka kusingekuwa na ushindani huu unaoenda kuelekea kwenye uchaguzi wa mwaka huu.
Bila shaka kuna mambo mengi yamejificha kutokana na ayo maswali na wawili hawa Lowasa na Kikwete(CCM) wanajua majibu (Wanajuana) either walikula wote au mmoja amemzidi ujanja mwenzie( hapa sizungumzii kuzurumiana kipesa bali kuzidiana ujanja uo ni mmoja kumtoa kafala mwenzie kama yeye ndo mhusika mkuu ili yeye awe safi) bila shaka watu baadhi wanaamini Lowasa ni mhanga tu wa ili swala.
Hali ilipo sasa si nzuri baina ya mafahali wawili hawa kiasi ambacho kila mmoja ameamua liwalo na liwe na kutunishiana misuli, kwa mfano kitendo cha raisi kikwete kutokea wakati wa magufuli kwenda kuchukua foarm Nec ghafla na kutoa kauli za majigambo uku akionyesha mwenye furaha usoni wakati mwili wake unaonesha ni mwenye woga moyoni ni ishara tosha kuwa sasa ni liwalo na liwe tu.
Wamasai ni watu wabishi sana nakumbuka nikiwa nafanya degree yangu ya Law nilikuwa nikisoma na mmasai yeye alikuwa ni mbishi na asiyependa kushindwa kuna wakati alisimama upande wa peke ake dhidi ya wengi akiamini yuko sahii na mara nyingi uwa anapandwa na jazba sana na mwisho wa yote anaropoka chochote kile ili tu aendelee na ushindi wake anao utaka, Kitendo cha Lowasa kuropoka maamuzi ya kuendelea na mkataba wa Richmond yalitoka ngazi ya juu ni ishara tosha ya kutojali na kuamua ule usemi wa liwalo na liwe tu.(Naambiwa lowasa si mmasai ila ni mmeru ila amekuria umasaini bila shaka ana ulka za kimasai apa namlinganisha na mmasai wa darasani kwangu wa mfano wa apo juu.
Kwenye ugomvi huu mpaka ilipofikia sasa Lowasa ndo mshindi.Mshindi kwa vipi:
1) Kikwete (CCM) walimuandaa Membe ndo achukue nchi ila kwa mchakato ulivyokuwa wa utata utata wakajikuta mtu wao Membe hajapata iyo nafasi na badala yake Mgombea Magufuri asie na uzoefu na chama wala asie na mvuto kwa watu amepata bahati ambayo ata yeye mwenyewe hakuitarajia( hapa ni sawa unalazimishwa kusikiliza mziki usioupenda)
Kwa mantiki iyo tu CCM kumpata mgombea asiye na nguvu yawezekana ilikuwa moja ya plan B ya Lowasa, kwamba kama akikatwa kama alivyokatwa na CCM ataenda upinzani na haakikishe mgombea wa CCM asiwe na mvuto ili apate mpinzani zaifu kama Magufuli na ilo ameweza na kwa akika kama mgombea wa CCM angekuwa Membe ali ingekuwa tofauti kidogo kuliko ilivyo sasa kwa Magufuli.
Wanatamani warudi Dodoma wamrudishe membe kwenye nafasi ya kupeperusha bendera CCM kwenye uraisi ila ndo haiwezekani tena kwa maana ata wao wanajua wanaupromote mziki wasioupenda kwa wengine ili waupende hakika ni jambo gumu watu kuwaelewa. Hapo bila shaka Lowasa ameshawapiga bao.
Kwa umri wa Lowasa na afya yake ana kila sababu ya kuamua alichoamua cha kuamua kwa vile hii ndo karata yake ya mwisho ya kuelekea Magogoni kama atapata iyo nafasi kwa vile HANA TENA CHA KUPOTEZA KWENYE MAISHA YAKE YA SIASA.
Mwisho wa siku sisi kama watanzania tuna maamuzi ya kuamua iyo mwezi wa kumi kila mtu ampime anayetaka kumpa kura yake kwa maana hakuna aliye mkamilifu kama ni suala la Ufisadi ata waliopo madarakani na waliotangulia ni mafisadi tu kwa mfano:
1) Wakati wa utawala wa mkapa wakati wa ubinafsishaji wa mashirika ya Uma, Viwanda vya sukari vya Kilombero vyote viwili viliuzwa kwa Bilioni 18 wakati kiwanda kimoja kibovu cha mtibwa kiliuzwa kwa Bilioni 21, Kumbe kiualisia pale kilombero kiwanda kiliuzwa kimoja cha Kilombero 1 na Kilombero 2 Mwenye nyumba wa wakati uo na watu wake wakakimiliki isivyo halali na pia kiwanda cha Mtibwa muulizeni Nasoro yule mwarabu wa Superdoll ni nani anakimiliki icho kiwanda atawapa jibu. Na walivyo na roho mbaya hawa watu mpaka leo tangia mwaka 2000 wafanyakazi waliokuwa wa kiwanda ivyo vya kilombero walioachishwa kazi hawajalipwa staiki zao mpaka leo na wengi wameshakufa kwa shida na dhiki. Hapa najaribu kuonyesha Ufisadi kidogo wa Utawala uliopia.
Moja ya kashfa kubwa zilizoikumba nchii hii ni ili sakata la TEGETA ESCROW, wabunge wa upinzani waliopeleka iyo Kashfa wakiongozwa na Kafurila wanazungumzia Bilioni 150 tu alizochukua Rugemalira ziko wapi zile Bilion zaidi ya 200 mbili zingine mbona hakuna anayethubutu kuzizungumzia??? ata Kafurila alieibua iyo ishu ya Escrow mbona na yeye hata athubutu kuzioji zilipokwenda???. Hapa najaribu kuonyesha ufisadi wa Serikali ya awamu hii bila Lowasa.
Mtazamo tu: maamuzi ni yako mwenyewe.
 
Ndicho kilicho shindikana Dodoma, kwa kuwa Uchafu wa Kikwete Richmond anao Lowassa kwa kumbeba mwenyekiti wake, na angepitishwa ingebidi asafishwe. Na kumsafisha ni kukiri kuwa Richmond ni Bosi wake.
 
Back
Top Bottom