WILLIAM MARCONI
JF-Expert Member
- Apr 2, 2015
- 2,108
- 878
Jamani wacheni maneno ya kitoto msiwafanaye Watanzania kuwa ni taahira. Kama Lowassa - Mzee wa maamuzi magumu - angeona kuwa huu mkataba ni mbovu, angeuvunja. Alipokataliwa na "Mamlaka ya Juu" - kama kweli alikataliwa - basi angejiuzulu hapo hapo. Mbona ni juzi tu "Mamlaka ya Juu" imemuengua Lowassa kwenye kinyanganyiro cha Urais: kama kweli anatii Mamlaka ya Juu au analazimishwa nayo, mbona amejiuzulu na kwenda CHADEMA? Kwa nini hakuenda CHADEMA wakati huo huo wanamwita fisadi?
Sitegemei kama Kikwete kama mtu binafsi angeweza kuamuru Mkataba ufanyike, alisema "alishauriwa na Makatibu wakuu" kuwa uendelee. Lowassa anaposema Mamlaka ya Juu ilisema "mkataba uendelee" hatuambii kila kitu. What were the exact words and what was the context? Je, Mamlaka labda ilisema "kama ni shida ya kampuni kutoonekana, watafuteni zaidi" (maana Mwakyembe alisema walienda Texas wakakosa ofisi yao); au kama ni shida ya gharama basi "tafuteni uwezekano wa kupunguza". Au kitu kama hicho.
Rais ni mtu mmoja hawezi kusema "mkataba uendelee' hivi hivi. Au labda Lowassa anasema kuwa Rais "alijua kuwa najua kuwa anajua"? Yaani ulikuwa na "mradi" wao wote wawili? In that case wote ni majambazi, washitakiwe; haimaanishi kuwa kama Rai anajua kwa hiyo Lowassa ndiyo awe msafi.
Kumhusisha Rais na ufisadi wake haiamaanishi yeye ni msafi. Kumbuka kuwa Lowassa ana tabia ya kujificha mgongoni mwa watu wengine. Nani asiyejua kuwa ni majuzi tu alimhusisha Makamu wa Rais na ufisadi wake. Alienda Arusha kuhonga Msikitini akidai "amesaidiwa na marafiki zake". Marafiki hawo hajawataja hata siku moja, lakini siku hiyo haraka haraka akasema "marafiki wangu kama Makamu wa Rais" kwa vile alimtuma akamuwakilishe.
Hapo si anatumia vibaya jina la Dr Bilal ambaye hata siku moja hajafuatana na Lowassa kwenda kwenye hizi hongahonga zake Makanisani na kwenye kwaya na Misikitini?
Simtetei Rais lakini naona wazi kuwa Lowassa anatafuta pa kujificha - sasa anataka kuhusisha na Rais kwa jambo ambalo hatuambii ukweli wote. Hii huitwa MONEY LAUNDERING, yaani anamtumia Makamu wa Rais kufua nguzo zake chafu. Unaweza ukaenda mahakama yoyote utaambiwa kuwa "ushahidi" wa fisadi dhidi ya mafisadi wenziye huwa haupewi uzito wowote.
Lowassa hawezi kujitoa kwenye ufisadi hata iweje. Hata hii Richmond si ufisadi pekee anaohusishwa nao, wala si ufisadi mkubwa zaidi, ZIPO FISADI NYINGI. Wananchi wanamjua vizuri na watamjua zaidi; watamtosa asiweze kurudi tena. RM