Kwa anayejua dhamana ya uongozi Lowassa hajajibu kitu. Kacheza na akili za wadanganyika tu. Eti simu ilipigwa kwa mwanasheria halafu akaja kusema uongozi wa juu umesema mkataba uendelee. Waziri mkuu anaongea utumbo kama huu halafu mnauita utetezi?
Kila nikitafakari sentensi hii naona kwamba Lowassa hafai kabisa kuwa rais. Kiongozi asiyejua mamlaka aliyonayo katika ofisi yake. Anayepokea maelekezo ya simu pasipo kuwapo ushahidi wa maandishi. Hiyo simu ilipigwa kwa mwanasheria, kwa nini maelekezo asipewe yeye moja kwa moja? Je alifanya juhudi gani kuthibitisha Kuwa kweli uongozi wa juu umeagiza hivyo?
Akiwa kiongozi mwenye dhamana na uchungu wa kuwatumikia watanzania, kwa nini hukuchukua jukumu la kujiuzulu nafasi yake ili kuepusha kujihusisha na kulihujumu taifa? Hii ingemjengea heshima kubwa pamoja na kuaminika na watanzania. Badala yake akaamua kutumikia maslahi ya uongozi wa juu. Hebu na atueleze yeye alinufaikaje na dili hilo. Ni wazi kwamba hakuishia kuidhinisha tu, kwa sababu alishaufahamu mchezo mzima.
Lowassa ni kiongozi dhaifu tofauti na baadhi ya watu wanavyomdhania. Hafai hata kidogo kupewa madaraka ya juu kabisa ya nchi
Tuanataka huo uongozi wa juu ukanushe kuwa haukuhusika.