Kashfa ya Richmond: Lowassa, Karamagi na Dkt. Msabaha Wajiuzulu

Kashfa ya Richmond: Lowassa, Karamagi na Dkt. Msabaha Wajiuzulu

hata mtuchape fimbo kutudanganya safarihii hatudanyanyiki tena hata angeingia na richimond 30 nizake lakini lazima ashinde urahic octobar penda mcpende

Swala la uraisi siyo mchezo wa kubashiri..."EL ni vigumu kuwa raisi wa tz mwaka huu" hii ni kwasababu ya mazingira ya siasa za mwaka huu hasa maandalizi hafifu ya vyama vya upinzani. Acheni ushabiki wa kujazana ujinga mitandaoni na ktk vijiwe vya kahawa. Kura za watu wa mijini haziwez kutosha kumuingiza mtu ikulu...."hii ni siasa sia soka" useme natabiri timu fulani itashinda.
 
Richmond bado yamwandama Lowassa

Na Jabir Idrissa - Imechapwa 16 March 2011

KATIKA kile kinachoitwa "maandalizi ya kuelekea ikulu," waziri mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya mkataba tata wa Richmond, Edward Lowassa ametungiwa kitabu cha kumsafisha. Kitabu hicho chenye kurasa 15 kinaitwa, "Roho ya Edward Lowassa ni nyeupe kama theluji." Mwandishi ni Ruth F. Levis Msuya.

Hata hivyo, kisichoweza kuleta ubishi ni kwamba nywele za Lowassa ndiyo nyeupe na siyo matendo yake, hasa ikizingatiwa nafasi yake katika kashfa ya Richmond. Kwenye jalada lake, kitabu kimebeba picha ya Lowassa iliyozungushiwa duara na sehemu ya nyuma kuna maneno yanayosomeka, "Lengo kuu la kazi hii ni kuonyesha ukweli juu ya mh. Edward Lowassa kuhusu upendo wake kwa Watanzania."

Hata hivyo, "kitabu cha Lowassa" hakionyeshi mchapishaji, wala hakina namba ya usajili kutoka maktaba ya taifa.

Naye, Ruth Msuya ambaye amejitambulisha kuwa ni mwalimu, hakuweka maeleo yake fasaha kuonyesha jinsi anavyofahamu Lowassa. Kinachoonekana ni neno "shukurani" na kuhitimisha kwa kushukuru familia yake kwa kumpa moyo ili aendelee "kusema ukweli daima mpaka mwisho wa maisha yake."

Kupatikana kwa taarifa hizi kumekuja wiki moja tangu gazeti hili kuchapisha taarifa zilizofichua uhamiaji rasmi wa mbunge wa Kilindi (CCM), Beatrice Shelukindo katika mtandao wa Lowassa. Akiandika kwa Pindi Chana, mbunge wa Viti Maalum (CCM), tarehe 14 Februari mwaka huu, Beatrice alimshawishi Chana kumuunga mkono Lowassa na kumweleza juu ya ulokole wake na "mtumishi aliyepakwa mafuta" kutoka Nigeria.

MwanaHALISI lilipowasiliana na Ruth Msuya kupitia simu yake ya mkononi Na. 0765 366222 ili kujua jinsi alivyomfahamu kwa undani Lowassa, haraka alijibu, "kijitabu kinajieleza." Alipobanwa kuwa kitabu hakina maelezo yanayojitosheleza jinsi yeye alivyomfahamu Lowassa, kwanza alisema, "Nakushukuru kwa kupata kitabu" na pili akasema, "…Ninakwenda msibani Morogoro." Kisha akakata simu.

Katika ukurasa wa nane wa kitabu cha Lowassa mwandishi anasema, "…Tatizo ni kwamba wale wanaomchafua wana wivu mkubwa sana na utendaji uliotukuka. Hii ni sawa na mwanafunzi aliye wa kwanza darasani, wale wanaowania nafasi ile mara nyingi wanajenga uadui na huyo mwanafunzi…" anaeleza.

Mwandishi anasema, "Ukiuliza kisa cha wale wanaomchafua utaambiwa hafai, ukiuliza kwa nini utaambiwa ni tajiri! Inashangaza, kwani kuna mtu aliyekuzuia usifanye kazi," anahoji. Katika ukurasa wa tisa wa kitabu hicho, mwandishi anasema Lowassa ni mnyenyekevu na unyenyekevu ni asili yake.

Hata hivyo, mwandishi hajaeleza mahali popote katika kitabu chake kuwa Lowassa alijiuzulu wadhifa wa uwaziri mkuu kwa tuhuma za kuipa kazi kampuni ya Richmond huku akijua kuwa kampuni hiyo haikuwa na uwezo wa kufanya kazi iliyoomba.

Wataalam wa vitabu wanasema kama mwandishi alilenga kumsafisha Lowassa ameshindwa, kwa kuwa maudhui ya kitabu hayana hoja yoyote ya kumjenga.

Wakati hayo yakiendelea, taarifa zinasema kambi ya Lowassa imepanga kila mkakati ili kumzidi kete Rais Kikwete.

Taarifa za ndani ya kambi ya Lowassa zinasema hatua hiyo inalenga kumuimarisha mwanasiasa huyo kati ya sasa na uchaguzi mkuu wa CCM wa mwaka 2012.

Kwa mujibu wa mawasiliano yaliyonaswa ndani ya mtandao wa Lowassa, "Kamati ya Mkakati" imekubaliana kuwa sasa ni wakati mwafaka kwa Lowassa kujitokeza hadharani na kuzungumzia masuala mazito ya kitaifa. Masuala ambayo yamekubaliwa Lowassa ayazungumzie, ni pamoja na yale yanayohusu uongozi wa umma ambayo yalistahili kuzungumzwa na rais.

"…Viongozi waandamizi wamekutana mjini Dodoma. Jambo kubwa ilikuwa mkakati makini wa kupata nafasi ya kulikamata Bunge ili kurahisisha mambo yaweze kwenda vizuri na bila upinzani mkubwa kama ilivyokuwa katika Bunge lililopita," inaeleza sehemu ya mawasiliano ya wajumbe wa kamati hiyo.

Sambamba na mkakati huo, kambi hiyo imeazimia kupata chuo ambacho wanafunzi wake watapatiwa kiasi cha fedha za kujikimu ili muda ukifika Lowassa aalikwe kuhutubia. Katika kutekeleza mkakati huo, mtandao wa Lowassa umepanga kupeleka kikundi cha waandishi habari kuripoti tukio hilo.

Mkakati huo unafichuliwa katika kipindi ambacho tayari mfululizo wa matukio umeanza kujidhihirisha kuwa Lowassa anapiga hatua kujiimarisha kisiasa kwa ajili ya kinyang'anyiro cha urais mwaka 2015. Mtoa taarifa alimnukuu mjumbe wa kamati akisema, hatua ya Lowassa kufanikiwa kupata nafasi ya kuongoza kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama "ni sehemu ya mafanikio" ya mkakati huo.

Anasema, "Tunataka Lowassa kukubalika upya kimataifa ili kurahisisha safari yake ya kuelekea ikulu," anaeleza mtoa taarifa gazeti hili. Wajumbe wamekubaliana kuongeza jitihada za kumweka karibu mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama ili apunguze "maumivu na hasira kutokana na kunyimwa nafasi yake ya kuwa naibu spika, baada ya baadhi ya taratibu kupindishwa."

Hofu ya kundi la Lowassa ni kwamba Jenista anaweza kutekwa na kundi pinzani. Kwa upande wa naibu spika, mbunge wa Kongwa (CCM), Job Ndugai, mtandao wa Lowassa umepanga "kumfuatilia sana nyendo zake" kwa kuwa anaonekana, "mtu anayeyumba kimsimamo na anatekeleza anayoagizwa kutoka juu kwa malengo maalum. Wanasema Ndugai ni mfuasi wa waziri mmoja mwandamizi" ambaye anatajwa kuwa anaweza kujitosa katika kinyang'anyiro cha urais katika uchaguzi ujao.

Waziri huyo ametajwa kama anayeshika moja ya wizara nyeti na ambayo inamjenga kisiasa na ambaye anaonekana na kundi hilo kama mtu wa karibu na kiongozi mkuu lakini pia kama mpinzani wa kundi lao. Mkakati wa kundi unakwenda mbali, hata kupanga kutumia vyombo vya habari kwa "gharama yoyote ile" ilimradi ikifika mwisho wa mwaka 2013 hatua nzuri ya kufanyiwa tathmini iwe imefikiwa.

Tathmini hiyo itafanywa kwa kuhusisha taasisi binafsi itakayotoa matokeo bila ya kusukumwa ili kupata sura halisi ya mambo inavyokwenda. Taarifa zinasema kwamba matukio yote yaliyokwishatokea na kumhusisha Lowassa na mfungamano wake na umma, ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati huo.

Miongoni mwa matukio yanayotajwa ni lile la Lowassa kuzungumzia harakati zilizofanikiwa kumlazimisha aliyekuwa rais wa Misri, Hosni Mubarak kuachia ngazi baada ya maandamano ya umma yaliyochukua siku 18."Kwa kujua watu wengi wanafuatilia na hilo ndilo tukio kubwa kwa wakati ule, Lowassa alitumia fursa hiyo kuonyesha kuwa yupo na wananchi kwa kupongeza wanaharakati na ubaya wa viongozi wa nchi kujilimbikizia mali," alisema mtoa taarifa wa gazeti hili.

chanzo Mwanahalisi
 
Richmond bado yamwandama Lowassa


Na Jabir Idrissa - Imechapwa 16 March 2011


KATIKA kile kinachoitwa “maandalizi ya kuelekea ikulu,” waziri mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya mkataba tata wa Richmond, Edward Lowassa ametungiwa kitabu cha kumsafisha. Kitabu hicho chenye kurasa 15 kinaitwa, “Roho ya Edward Lowassa ni nyeupe kama theluji.” Mwandishi ni Ruth F. Levis Msuya.


Hata hivyo, kisichoweza kuleta ubishi ni kwamba nywele za Lowassa ndiyo nyeupe na siyo matendo yake, hasa ikizingatiwa nafasi yake katika kashfa ya Richmond. Kwenye jalada lake, kitabu kimebeba picha ya Lowassa iliyozungushiwa duara na sehemu ya nyuma kuna maneno yanayosomeka, “Lengo kuu la kazi hii ni kuonyesha ukweli juu ya mh. Edward Lowassa kuhusu upendo wake kwa Watanzania.”


Hata hivyo, “kitabu cha Lowassa” hakionyeshi mchapishaji, wala hakina namba ya usajili kutoka maktaba ya taifa.

Naye, Ruth Msuya ambaye amejitambulisha kuwa ni mwalimu, hakuweka maeleo yake fasaha kuonyesha jinsi anavyofahamu Lowassa. Kinachoonekana ni neno “shukurani” na kuhitimisha kwa kushukuru familia yake kwa kumpa moyo ili aendelee “kusema ukweli daima mpaka mwisho wa maisha yake.”



Kupatikana kwa taarifa hizi kumekuja wiki moja tangu gazeti hili kuchapisha taarifa zilizofichua uhamiaji rasmi wa mbunge wa Kilindi (CCM), Beatrice Shelukindo katika mtandao wa Lowassa. Akiandika kwa Pindi Chana, mbunge wa Viti Maalum (CCM), tarehe 14 Februari mwaka huu, Beatrice alimshawishi Chana kumuunga mkono Lowassa na kumweleza juu ya ulokole wake na “mtumishi aliyepakwa mafuta” kutoka Nigeria.


MwanaHALISI lilipowasiliana na Ruth Msuya kupitia simu yake ya mkononi Na. 0765 366222 ili kujua jinsi alivyomfahamu kwa undani Lowassa, haraka alijibu, “kijitabu kinajieleza.” Alipobanwa kuwa kitabu hakina maelezo yanayojitosheleza jinsi yeye alivyomfahamu Lowassa, kwanza alisema, “Nakushukuru kwa kupata kitabu” na pili akasema, “…Ninakwenda msibani Morogoro.” Kisha akakata simu.


Katika ukurasa wa nane wa kitabu cha Lowassa mwandishi anasema, “…Tatizo ni kwamba wale wanaomchafua wana wivu mkubwa sana na utendaji uliotukuka. Hii ni sawa na mwanafunzi aliye wa kwanza darasani, wale wanaowania nafasi ile mara nyingi wanajenga uadui na huyo mwanafunzi…” anaeleza.


Mwandishi anasema, “Ukiuliza kisa cha wale wanaomchafua utaambiwa hafai, ukiuliza kwa nini utaambiwa ni tajiri! Inashangaza, kwani kuna mtu aliyekuzuia usifanye kazi,” anahoji. Katika ukurasa wa tisa wa kitabu hicho, mwandishi anasema Lowassa ni mnyenyekevu na unyenyekevu ni asili yake.


Hata hivyo, mwandishi hajaeleza mahali popote katika kitabu chake kuwa Lowassa alijiuzulu wadhifa wa uwaziri mkuu kwa tuhuma za kuipa kazi kampuni ya Richmond huku akijua kuwa kampuni hiyo haikuwa na uwezo wa kufanya kazi iliyoomba.

Wataalam wa vitabu wanasema kama mwandishi alilenga kumsafisha Lowassa ameshindwa, kwa kuwa maudhui ya kitabu hayana hoja yoyote ya kumjenga.


Wakati hayo yakiendelea, taarifa zinasema kambi ya Lowassa imepanga kila mkakati ili kumzidi kete Rais Kikwete.

Taarifa za ndani ya kambi ya Lowassa zinasema hatua hiyo inalenga kumuimarisha mwanasiasa huyo kati ya sasa na uchaguzi mkuu wa CCM wa mwaka 2012.


Kwa mujibu wa mawasiliano yaliyonaswa ndani ya mtandao wa Lowassa, “Kamati ya Mkakati” imekubaliana kuwa sasa ni wakati mwafaka kwa Lowassa kujitokeza hadharani na kuzungumzia masuala mazito ya kitaifa. Masuala ambayo yamekubaliwa Lowassa ayazungumzie, ni pamoja na yale yanayohusu uongozi wa umma ambayo yalistahili kuzungumzwa na rais.


“…Viongozi waandamizi wamekutana mjini Dodoma. Jambo kubwa ilikuwa mkakati makini wa kupata nafasi ya kulikamata Bunge ili kurahisisha mambo yaweze kwenda vizuri na bila upinzani mkubwa kama ilivyokuwa katika Bunge lililopita,” inaeleza sehemu ya mawasiliano ya wajumbe wa kamati hiyo.


Sambamba na mkakati huo, kambi hiyo imeazimia kupata chuo ambacho wanafunzi wake watapatiwa kiasi cha fedha za kujikimu ili muda ukifika Lowassa aalikwe kuhutubia. Katika kutekeleza mkakati huo, mtandao wa Lowassa umepanga kupeleka kikundi cha waandishi habari kuripoti tukio hilo.


Mkakati huo unafichuliwa katika kipindi ambacho tayari mfululizo wa matukio umeanza kujidhihirisha kuwa Lowassa anapiga hatua kujiimarisha kisiasa kwa ajili ya kinyang’anyiro cha urais mwaka 2015. Mtoa taarifa alimnukuu mjumbe wa kamati akisema, hatua ya Lowassa kufanikiwa kupata nafasi ya kuongoza kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama “ni sehemu ya mafanikio” ya mkakati huo.



Anasema, “Tunataka Lowassa kukubalika upya kimataifa ili kurahisisha safari yake ya kuelekea ikulu,” anaeleza mtoa taarifa gazeti hili. Wajumbe wamekubaliana kuongeza jitihada za kumweka karibu mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama ili apunguze “maumivu na hasira kutokana na kunyimwa nafasi yake ya kuwa naibu spika, baada ya baadhi ya taratibu kupindishwa.”


Hofu ya kundi la Lowassa ni kwamba Jenista anaweza kutekwa na kundi pinzani. Kwa upande wa naibu spika, mbunge wa Kongwa (CCM), Job Ndugai, mtandao wa Lowassa umepanga “kumfuatilia sana nyendo zake” kwa kuwa anaonekana, “mtu anayeyumba kimsimamo na anatekeleza anayoagizwa kutoka juu kwa malengo maalum. Wanasema Ndugai ni mfuasi wa waziri mmoja mwandamizi” ambaye anatajwa kuwa anaweza kujitosa katika kinyang’anyiro cha urais katika uchaguzi ujao.


Waziri huyo ametajwa kama anayeshika moja ya wizara nyeti na ambayo inamjenga kisiasa na ambaye anaonekana na kundi hilo kama mtu wa karibu na kiongozi mkuu lakini pia kama mpinzani wa kundi lao. Mkakati wa kundi unakwenda mbali, hata kupanga kutumia vyombo vya habari kwa “gharama yoyote ile” ilimradi ikifika mwisho wa mwaka 2013 hatua nzuri ya kufanyiwa tathmini iwe imefikiwa.


Tathmini hiyo itafanywa kwa kuhusisha taasisi binafsi itakayotoa matokeo bila ya kusukumwa ili kupata sura halisi ya mambo inavyokwenda. Taarifa zinasema kwamba matukio yote yaliyokwishatokea na kumhusisha Lowassa na mfungamano wake na umma, ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati huo.


Miongoni mwa matukio yanayotajwa ni lile la Lowassa kuzungumzia harakati zilizofanikiwa kumlazimisha aliyekuwa rais wa Misri, Hosni Mubarak kuachia ngazi baada ya maandamano ya umma yaliyochukua siku 18.“Kwa kujua watu wengi wanafuatilia na hilo ndilo tukio kubwa kwa wakati ule, Lowassa alitumia fursa hiyo kuonyesha kuwa yupo na wananchi kwa kupongeza wanaharakati na ubaya wa viongozi wa nchi kujilimbikizia mali,” alisema mtoa taarifa wa gazeti hili.


chanzo Mwanahalisi

Kumbuka mahamuzi yalitoka ngazi za juu kusaini mkataba kwa hiyo lowassa ni mtu mdogo ukizingatia alikuwa na wakubwa zake hapo juu.


swissme
 
Lowassa ameshafunguka kuwa Richmond ni ya baba miraji!

Kilichopo ni Baba Mwanaasha naye kutoka hadharani kukanusha, ili Lowassa afafanue!
 
Mjadala wa Richmond bado haujafungwa

source: MWANAHLISI BY KUBENEA 2010

MJADALA juu ya mkataba wa kuzalisha umeme wa dharura kati ya serikali na kampuni ya kitapeli ya Richmond Development Company (LLC), ungali mbichi.
Pamoja na Bunge kutangaza kufungwa kwa mjadala mwishoni mwa mkutano wa 18 uliomalizika wiki iliyopita, kila mwenye nia njema kwa taifa hili anajua kuwa utata ungalipo na mjadala unaendelea.
Mjadala ungali hai kwa kuwa mambo ya msingi katika sakata hili hayajapatiwa ufumbuzi. Kuukatisha ni sawa na kusaliti wananchi na taifa kwa jumla.
Jumatano iliyopita, Spika wa Bunge, Samwel Sitta alitangaza bungeni "kufungwa kwa mjadala wa Richmond," kwa kile kilichoitwa, "Kuachia mamlaka ya juu ya nchi kuchukua hatua."
Alisema Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeridhishwa na utekelezaji wa serikali kwa yale maazimio 23 ya Bunge kuhusu Richmond.
Bunge lilisema badala ya kubaki kama maazimio yake, taarifa za utekelezaji ambazo zitafanywa na serikali, sasa zitapelekwa kwenye kamati husika za kisekta.
Mwaka 2006, serikali, kupitia Shirika la Umeme nchini (TANESCO), iliingia mkataba wa kufua umeme wa dharura na Richmond ambayo tayari ilithibitika kuwa ni kampuni hewa.
Kugundulika kwa kashfa hiyo ya kutoa zabuni kwa kampuni isiyo na uwezo kifedha, kiufundi na hata kimaadili ndiko kulisababisha kujiuzulu kwa aliyekuwa waziri mkuu, Edward Lowassa na waliokuwa mawaziri wa nishati na madini, Dk. Ibrahim Msabaha na Nazir Karamagi.
Katika hali hii, Spika Sitta na wenzake hawawezi kufunga mjadala huu bila ya kwanza kujibu hoja 19 za msingi kwa nini mjadala usifungwe.
Kwanza, yako wapi mamilioni ya shilingi ya wananchi ambayo bunge limekuwa likisema zimelipwa kwa kampuni feki kama sehemu ya malipo ya "Capacity Charge" na gharama nyingine?
Katika mkataba huo kati ya serikali na Richmond, serikali ilikubali kuilipa kampuni hiyo Sh. 152 milioni kwa siku hata kama haikutumia umeme kutoka kwake.
Si mara moja wala mbili, wajumbe wa Kamati Teule ya Bunge waliochunguza mkataba huo, akiwamo mwenyekiti wake, Dk. Harrison Mwakyembe wamenukuliwa wakisema pamoja na kwamba kampuni hiyo ilishindwa kutekeleza mkataba wake na TANESCO, lakini serikali ililipa Richmond mamilioni ya shilingi.
Pili, mjadala hauwezi kufungwa kama mmiliki halisi wa kampuni iliyotia doa serikali hajajulikana; na nakala halisi ya mkataba haijatoka hadharani.
Kwa mujibu wa taarifa za ndani ya serikali, Dk. Msabaha ndiye alikuwa na nakala halisi ya awali kabisa, yenye majina ya wakurugenzi wa kampuni hiyo feki; nakala ambayo hata Kamati ya Bunge iliyochunguza kashfa hiyo haikuiona.
Mjadala hauwezi kufungwa kama uhusiano wa kampuni ya Richmond na mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, haujawekwa wazi.
Kwa zaidi ya miaka mitatu sasa, Rostam amekuwa akikana umiliki wa Richmond, pamoja na kutajwa mbele ya Kamati Teule ya Bunge na mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais, Salva Rweyemamu.
Ni Rostam aliyeruhusu Richmond kutumia sanduku la barua, barua pepe na wafanyakazi wa kampuni yake iitwayo Caspian yenye makazi yake Barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam.
Tatu, mjadala hauwezi kufungwa wakati haijajulikana watendaji wa serikali na wanasiasa wote waliohusishwa na Richmond walilipwa nini na kiasi gani hadi kukubali kuvunja taratibu na sheria za nchi kwa kuipa kampuni feki kazi ya maana?
Wenye nia njema wanauliza na wataendelea kuuliza je, watumishi walilishwa nini hadi kukubali kutenda kazi kwa maagizo ya wamiliki wa Richmond badala ya serikali iliyowaajiri.
Nne, mjadala hauwezi kufungwa wakati hata Kamati ya Usalama na Maadili ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), haijamtaja mhusika mkuu wa chama hicho anayedaiwa kuwa alikuwa kiungo cha Richmond.
Tano, mjadala hauwezi kufungwa wakati kila mmoja anajua kuwa Dk. Msabaha alidaiwa kujiapiza kwa kusema, "…sitakubali kutolewa kafara, lazima nife na mtu." Bado Dk. Msabaha yuko bungeni na hajamtaja mtu aliyetaka kufa naye.
Sita, mjadala hauwezi kufungwa hivihivi tu wakati Lowassa hakuwa mmoja wa watu waliokuwa wametajwa na Kamati Teule, hakushauriwa kujiuzulu, lakini ilikuja kudhihirika kuwa alikuwa ameshiriki kushinikiza kampuni ya Richmond ipewe kazi ya kufua umeme wa dharura.
Saba, mjadala haujafungwa bila ya kwanza kumpa nafasi Dk. Msabaha kuwataja hata wale ambao hawakutajwa na Kamati ya Bunge – ambao walikuwa wazito zaidi, na ambao Lowassa alikuwa akiwalinda wasiguswe.
Madai kuwa Lowassa aliamua kujiuzulu ili kumfunga mdomo Dk. Msabaha asitaje hao waliokuwa wakilindwa, hayajawekwa wazi na hayajathibitishwa.
Nane, mjadala hauwezi kufungwa bila kujua kama ni kweli Rais Jakaya Kikwete alijua "kila kitu" kuhusu mradi huo na kwamba alipoona mambo yamekuwa magumu zaidi alimshauri Lowassa afanye uamuzi ambao usingefumua makubwa zaidi, hata kama ungemgharimu nafasi yake ya waziri mkuu?
Katika kikao chake Butiama, mkoani Mara, Kamati ya Usalama na Maadili iliitaarifu Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) juu ya mchakato uliokuwa umechukuliwa kuwalinda vigogo na kwamba katika orodha ya waliopaswa kujiuzulu, Lowassa hakuwamo.
Kamati ilisisitiza kuwa Lowassa alishinikiza wahusika katika wizara ya nishati na madini, wakati huo chini ya Dk. Msabaha, kuikubali Richmond kwa sababu ya maslahi ya waliokuwamo.
Tisa, mjadala hauwezi kufungwa bila ukweli kujulikana kuwa Dk. Msabaha alijua fika namna mkataba wa awali wa Richmond ulivyoandaliwa, na majina yaliyokuwamo katika orodha ya wamiliki wa iliyoitwa kampuni ya Richmond.
Kumi, mjadala hauwezi kufungwa kama nakala halisi ya mkataba haijatoka hadharani.
Kumi na moja, mjadala hauwezi kufungwa bila ya kwanza kupatiwa majibu ya kina kuhusu malalamiko ya Lowassa kwamba alisakamwa kwa hoja dhaifu na visasi vya uwaziri mkuu.
Kufunga mjadala huu bila ya kujulikana ukweli ni kuthibitisha kuwa wote waliohusika walikuwa na nia mbaya na Lowassa.
Kumi na mbili, huwezi kufunga mjadala wakati watendaji serikalini wamekiuka Sheria ya Manunuzi ya Umma (PPRA) ya mwaka 2004 tena kwa makusudi kwa lengo la kubeba Richmond.
Kumi na tatu, mjadala huu hauwezi kufungwa kwa utashi wa kikundi kidogo cha watu walioweka mbele maslahi yao binafsi au yale ya vyama vyao.
Kumi na nne, mjadala hautafungwa hadi baada ya umma kuridhika kwamba "serikali imetekeleza wajibu wake katika kuadabisha wote waliohusika kwenye mkataba huu."
Kumi na tano, mjadala hautaisha hadi wananchi waridhike kwamba Lowassa alijiuzulu ili kuepusha mawaziri kuanza kutajana.
Ingefikia hatua hiyo, Dk. Msabaha anadaiwa alikuwa tayari kuweka hadharani majina ya wakurugenzi halisi wa Richmond, akiwamo "mtoto mmoja wa kigogo mzito" serikalini.
Si kigogo wala mtoto wa kigogo anayejulikana kwa wananchi. Wanasubiri Dk. Msabaha amtaje au mtu mwingine ataje ndipo mjadala utamkwe umefungwa.
Kumi na sita, mjadala hauwezi kufungwa wakati mpaka sasa haijafahamika kinagaubaga, nini hasa ilikuwa dhamira halisi ya Rais Kikwete hadi kukubali Lowassa kujiuzulu.
Hili ni muhimu kujulikana hasa kwa kuwa ni Kikwete aliyemlinda, hadi mwisho, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Edward Hoseah na maofisa wengine wa taasisi hiyo waliotuhumiwa kuandaa taarifa isiyo sahihi juu ya Richmond.
Kumi na saba, mjadala wa Richmond hauwezi kufungwa kwa sababu Bunge, katika hatua ya mwisho, limejikunja katika shuka la aibu, kushindwa kutaja mkosaji na hatua zilizochukuliwa.
Kwa mfano, taarifa ya Kamati iliyosomwa bungeni na mwenyekiti wake, William Shelukindo (Bumbuli – CCM), ilisema, Azimio Na. 9 lililokuwa linataka Hoseah aondoke, halikujadiliwa kwa sababu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU huteuliwa na Rais na pia TAKUKURU inachunguza wabunge.
Sasa swali la kujiuliza: Nini kilianza kati ya bunge kutaka Hoseah aondolewe na hatua yake ya kuchunguza wabunge? Jibu ni kwamba lilianza azimio la bunge.
Je, sasa hoja kwamba wabunge wanachunguzwa na Hoseah ilitoka wapi? TAKUKURU si Hoseah, ni taasisi.
Serikali inaweza kumuondoa Hoseah na bado kazi ya kuchunguza wabunge ikaendelea. Ni kama vile mahakamani, kutuhumu hakimu au jaji, hakufanyi kesi kutosikilizwa au kusitishwa kwa utekelezaji wa hukumu.
Kama bunge lilijua kwamba Hoseah anateuliwa na rais kwa nini liliagiza aondolewe katika nafasi yake? Lilikuwa linamuagiza nani?
Lakini kuna jingine kubwa zaidi. Kama bunge liliweza kuchagiza serikali hadi Lowassa akajiuzulu, limeshindwaje kwa Hoseah?
Kumi na nane, bunge haliwezi kufunga mjadala wa Richmond maana ajenda ya Richmond haikuwa ya bunge. Ilikuwa ni ajenda ya wananchi kupitia vyombo vya habari na wabunge wa vyama vya mageuzi.
Kimsingi Sitta na wenzake wameegemea utetezi dhaifu na Sitta ameshindwa kusimamia kauli yake mwenyewe kwamba atakuwa "Spika wa kasi na viwango."
Sasa Sitta na wenzake, hasa wale walioitwa "Wapiga vita ufisadi," wanageuziwa kibao kuwa walijipachika katika hoja hii kwa lengo la kujitafutia umaarufu wa kisiasa. Mtu wa kuwatetea sharti awe na hoja kubwa zaidi.
Kumi na tisa, serikali imewafikisha Gray Mgonja na Basil Mramba mahakamani kwa tuhuma za kutumia madaraka vibaya. Je, kama hili limewezekana, serikali hiyohiyo imeshindwaje kufikisha mahakamani waliotia hasara kupitia Richmond?
Ni muhimu Sitta na wenzake wakaelewa kwamba kufunga mjadala, ni kukubali "kufunga ndoa na mafisadi."
Wananchi wanaona yote haya. Wananchi wataendelea kujadili. Wananchi wataamua.
 
NA HII ESCROW NIAJE?
WATU WALIZOA FEDHA KWA MAGUNIA

EPA INAENDELEAJE?

MEREMETA IKOJE?

BUZWAGI IMEISHA?

HII RICHMOND TUMESHAMJUA MHUSIKA WAKE.
ii
 
Lowassa aibu Mapya

Na Saed Kubenea - Imechapwa 21 July 2010

MADAI mapya ya Edward Lowassa, yule waziri mkuu aliyejiuzulu, kwamba hata kama angekuwa madarakani angeendelea kushirikiana na kampuni ya Richmond, yameibua mapya.

Akizungumza na kituo cha Televisheni cha TBC1 Ijumaa iliyopita, Lowassa alisema hajutii “uamuzi wa kuipa kazi Richmond.â€

Anasema hata kama angerudi leo madarakani, bado angeendelea na mpango huo uliozaa kashfa iliyommomonyoa kisiasa.

Lowassa alijiuzulu wadhifa wake, Februari 2007 baada ya kutuhumiwa kufanya upendeleo wa kuipa kazi kampuni ya Richmond Development Company (LLC) kutoka Marekani.

Kampuni hiyo ambayo ilikuja kuthibitika kuwa haikuwa na sifa wala uwezo wa kifedha na kitaaluma, ilipewa jukumu la kuzalisha megawati 100 za umeme wa dharura. Ilishindwa.

Wakati Lowassa akijitapa kwamba uamuzi wake ulikuwa sahihi, taarifa kutoka ndani ya serikali na Kamati Teule ya Bunge, zinasema Lowassa alitumia madaraka yake vibaya kwa kuagiza kufutwa kwa zabuni ya kufua umeme ambayo tayari ilipewa kampuni ya CDC Glogbeleq kutoka Canada.

Uamuzi wa Lowassa wa kufuta zabuni ya CDC ndio ulisababisha taifa kutumbukia katika giza na hatimaye kuingizwa kwa kampuni isiyokuwa na hadhi, sifa wala uwezo wa kufanya kazi iliyoomba – Richmond.

Uchunguzi unaonyesha kwamba tarehe 11 Januari 2006, serikali iliteua kampuni ya CDC kuingiza nchini mitambo ya kuzalisha umeme yenye uwezo wa kuzalisha megawati 74. Mitambo ya kampuni hiyo ilikuwa na vipengele vifuatavyo:

Kwanza, ikiwa mkataba wa ukodishaji utakuwa wa miaka mitano, serikali itatakiwa kulipa dola za Marekani 3.2 kwa kWh moja ya umeme itakayotumia.

Pili, iwapo mkataba wa ukodishaji utakuwa wa miaka mitatu, serikali italazimika kujikamua na kulipa kiasi cha dola 5.3 kwa kWh moja ya umeme.

Mkataba kati ya serikali na CDC ulikuwa na unafuu mkubwa kwa kuwa kilikuwapo kipengele kinachoelekeza kuwa mara baada ya mkataba wa ukodishaji kumalizika, mitambo iliyokodishwa inakuwa mali ya serikali.

Kwa mujibu wa mawasiliano ambayo gazeti hili linayo, baina ya TANESCO, serikali na kampuni ya CDC, mitambo ya kampuni hiyo ilitarajiwa kuwasili nchini Aprili 2006.

Kampuni ya CDC Glogbeleq ni kampuni tanzu ya kampuni inayofua umeme kwa kutumia gesi ya Songas.

Hadi sasa, hakuna anayefahamu kilichosababisha Lowassa kuingilia mchakato wa zabuni ulioiteua kampuni hiyo ya kimataifa na inayosifika kimaadili, uwezo wa kiuchumi na kiutaalam; na badala yake kuipa kazi hiyo Richmond.

Uchunguzi wa MwanaHALISI unaonyesha kwamba tarehe 20 Februari 2006, Lowassa kupitia kwa aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Dk. Ibrahim Msabaha aliagiza bodi ya zabuni ya Tanesco kuanza mchakato upya.

Mchakato huo ulioibua Richmond kutoka kusikojulikana, ulisimamiwa kwa nguvu zote na Lowassa mwenyewe. Tangazo la serikali la kuitisha zabuni mpya lilitolewa 23 Februari 2006, huku zabuni zikipangwa kufunguliwa 6 Machi 2006 na tathimini kwa wazabuni ikiwa tarehe 7 na 8, Machi 2006.

Hata hivyo, kabla Lowassa hajatekeleza mpango wake wa kuipa kazi Richmond, hapo tarehe 22 Februari 2006, mamlaka ya manunuzi ya umma (PPRA) iliandika barua mbili kwa Tanesco.

Barua zote mbili – ile yenye Kumb. Na. PPRA/Tanesco/41/16 ya tarehe 23 Februari 2006 na nyingine yenye Kumb. Na. PPRA/Tanesco/47/18 – zilikuwa zikitaka kusitishwa kwa zoezi la zabuni zilizozaa Richmond kwa kuwa ilikuwa kinyume cha sheria.

Aidha, PPRA ilitaka Tanesco kutafuta moja kwa moja mitambo kutoka kwa watengezaji kwa maelezo kuwa, katika mazingira yaliyopo nchini na kutokana na zabuni kwenda kinyume cha taratibu, zoezi hilo likiendelea litaingiza wazabuni feki
 
mambo ya richmond yalifanywa na serikali kwa ujumla, woooote. kama ni ubaya woote wamo kama ni uzuri woote wamo. el,jk waachwe, twende mbele...tusifanyie kampeni mambo ya richmond
 
EL alifanya Ufisadi kwa Maagizo ya Mkuu.YAani alitii Kufanya Ufisadi kama wajibu na utii maagizo ya mkubwa wake. El hakua na mamlaka ya kukataa.
Ni kawaida hata jeshini ambapo polisi anaweza kufanya uhalifu kwa Raia Wema katika utekelezaji wa Kutii alichoagizwa na mkubwa wake wa kazi.
Mfano: FFU wamekua wakipiga Raia na Wapinzani kwenye mikutano ili kutii maagizo ya watawala wa Chamadola.So utaona Tatizo sio Polisi na FFU bali Wakuu wa System ndiyo wenye Kutoa Maagizo. hakuna kitu El alifanya Mkuu wake hajui. Imeshakua wazi sasa. SISIEMu ndio Cancer inayoitafuna hii nchi. Twende kwenye MAbadiliko...
 
hah hah hah
daktari katupwa kavunjwa meno mabwepande kwa sababu ya lowassa?
ni juzi juzi mwandishi wa kiuchunguzi kapigwa moto kwa sababu ya lowassa?

lowassa ashasema haikuwa yeye mwenye richimond na kaweka wazi aliyeilinda, mpaka leo haijakanushwa

AKILI ZETU ZILIIBWA NA TUKAAMINISHWA....waliotuaminisha walifanya kazi nzuri kwa nafasi zao na nawapongeza.ILA UKWELI NI KWAMBA HATA WALIOZIVUJISHA HIZO TAARIFA kwa wale waliotuaminisha walivujisha taarifa za kupikwa kummaliza lowassa. NI MKAKATI WA KIUFUNDI NA NAMPONGEZA KUBENEA....waliotudanganya ni wale waliompatia KUBENEA taarifa pikwa ambao ni hawahawa waliokuwa wakiandaa mpango wa kumshusha lowassa
 
EL alifanya Ufisadi kwa Maagizo ya Mkuu.YAani alitii Kufanya Ufisadi kama wajibu na utii maagizo ya mkubwa wake. El hakua na mamlaka ya kukataa.

Ni kawaida hata jeshini ambapo polisi anaweza kufanya uhalifu kwa Raia katika utekelezaji wa Kutii alichoagizwa na mkubwa wake wa kazi.
Mfano: FFU wamekua wakipiga Raia na Wapinzani kutii maagizo ya watawala wa CCM.So utaona Tatizo sio Polisi na FFU bali Wakuu wa System ndiyo wenye Kutoa Maagizo. hakuna kiti El alifanya Mkuu wake hajui. Imeshakua wazi sasa. SISIEMu ndio Cancer inayoitafuna hii nchi. Twende kwenye MAbadiliko...

Hoja yako dhaifu na soma historia ya The Hague wanajeshi walioshiriki ktk mauaji ya kimbari ya Wayahudi katika Vita Vikuu vya Dunia walishtakiwa na kupatwa na hatia .. hii ya kufuata amri haikubaliki kwani unafanya kitu kwa dhamira. Ukiina dhamira yako inakusuta unaweza kuacha. Mfano ukiambiwa kumwua mama yako unaweza amua kufuata amri au kuacha. Hakuna atakayekushangaa.
Kama alipewa amri alikuwa na option ya hapohapo kujiuzulu na asingepata hatia yoyote. Ye alichagua kushiriki katika ufisadi na alichagua hili kwa utashi wake.
Tafuteni hoja nyingine hii haiuziki. Kukiri kuwa alishiriki ktk ufisadi ni kukubali ufisadi.
 
Saed Kubenea ameonesha unafiki wake.....kama una makala zake nyingine za kumhusu Lowasa zishushe humu.
 
Mmeshaambiwa mwenye ushaidi atangulie mahakamani tumeshachoka na maneno yasiyo na ushaidi ,nchi hii ina polisi,TAKUKURU UWTnk tangu2008 mnashindwa nn kumpandisha kizimbani? LOWASA ndiye raisi wangu mtarajiwa

Dr Slaa anao ushahidi
 
Hoja yako dhaifu na soma historia ya The Hague wanajeshi walioshiriki ktk mauaji ya kimbari ya Wayahudi katika Vita Vikuu vya Dunia walishtakiwa na kupatwa na hatia .. hii ya kufuata amri haikubaliki kwani unafanya kitu kwa dhamira. Ukiina dhamira yako inakusuta unaweza kuacha. Mfano ukiambiwa kumwua mama yako unaweza amua kufuata amri au kuacha. Hakuna atakayekushangaa.
Kama alipewa amri alikuwa na option ya hapohapo kujiuzulu na asingepata hatia yoyote. Ye alichagua kushiriki katika ufisadi na alichagua hili kwa utashi wake.
Tafuteni hoja nyingine hii haiuziki. Kukiri kuwa alishiriki ktk ufisadi ni kukubali ufisadi.
umetaja vita ya dunia, but
Mrema alijiuzuru Ccm na hakuna anayemwona mpinzani. Sanasana anaitwa pandikizi la ccm

History is the best teacher..

OK mkuu, binafsi naona kuna mapungufu mengi kwenye hoja yako na nikilinganisha na mazingira ambayo ccm ina operate. Hata hivyo to shortening the story kama Ana kosa, ccm wanangoja nini wasimpeleke mahakamani?. Istoshe ameshatoka kWenye system kitambo sana, sitegemei kusikia hoja ku analindwa na system. Na ameshasema mwenye facts aende akathibitishe. Simple and clear.
 
Nimesikia pombe anataka.kugawa laptop, nikilinganisha na umeme njaa kama huu hizo laptop zitasaidia nini?

Maduka ya wauza laptop yatauza nini kwa wateja kama serikali itaua soko.lao.

Teach a poor how to fish instead of giving him a fish.
 
Sita apinge humu kama hakuwa front kupuka habari iliyomshusha EL. Kisa alinyimwa Uwaziri Mkuu akapewa uspika wa bunge.
 
EL alifanya Ufisadi kwa Maagizo ya Mkuu.YAani alitii Kufanya Ufisadi kama wajibu na utii maagizo ya mkubwa wake. El hakua na mamlaka ya kukataa.
Ni kawaida hata jeshini ambapo polisi anaweza kufanya uhalifu kwa Raia Wema katika utekelezaji wa Kutii alichoagizwa na mkubwa wake wa kazi.
Mfano: FFU wamekua wakipiga Raia na Wapinzani kwenye mikutano ili kutii maagizo ya watawala wa Chamadola.So utaona Tatizo sio Polisi na FFU bali Wakuu wa System ndiyo wenye Kutoa Maagizo. hakuna kitu El alifanya Mkuu wake hajui. Imeshakua wazi sasa. SISIEMu ndio Cancer inayoitafuna hii nchi. Twende kwenye MAbadiliko...

duh kutetea uwongo ni shida kwelikweli, nini majukumu ya waziri mkuu kikatiba? huna hoja mkuu rudi darasani
 
Back
Top Bottom