Bongolander
JF-Expert Member
- Jul 10, 2007
- 5,067
- 2,210
Hivyo kwa maoni yangu tunachotaka kuona wana JF na watz wenye mapenzi mema, ni kwamba mapendekezo yote kwenye repoti ya Mwakyembe yamefanyiwa kazi!! HAPO NDIPO TUTAHEMA KWA FURAHA KIDOGO
Mambo taratibu mzee, hujui hayo unayosema yatawagusa wangapi, one thing at a time. Ya kwanza ilikuwa ni kukata njia zinazotumiwa kutuibia, halafu tukiwa na ukakika wa hilo the next step will follow.
Si unajua tena yaliyosemwa na tume ya Mwakyembe ni mapendekezo, sio sheria kuwa ni lazima yatekelezwe, na bunge halina uwezo wa kutekeleza yote, kwanza inategemea kupenda kwa Sitta, Kikwete na wengine.
Kwa maoni yangu Lowassa anatakiwa kufikishwa mahakamani, lakini i do not see that coming, sioni mahaka yenye jeuri hiyo! mambo taratibu!