Kashfa ya Richmond: Lowassa, Karamagi na Dkt. Msabaha Wajiuzulu

Kashfa ya Richmond: Lowassa, Karamagi na Dkt. Msabaha Wajiuzulu

JK huu ndio mwanya wa kurudisha imani safisha kabisa kila idara.
Hii isiwe ndio kulisahaulisha la BOT. bado kule tumeelekeza macho na masikio, Kuna issue ya import support, kuna issue ya Kiwira, kuna Nyumba za serikali, kuna issue ya Container Terminal jamani tutafika?

Naona mama Lowasa anatia huruma sana hapa kwenye picha. Mama pole sana kila kitu nitalipwa hapa hapa duniani.

http://haki-hakingowi.blogspot.com/

Anafikiria jinsi atakavyokosa shopping the Harrods, London.

Wakifika hapa wanatumia utafiri ni wake wa King wa Saudi Arabia,
kumbe wanatoka nchi ambayo zaidi ya nusu yao hawana uhakika na chakula cha kila siku.
 
Lowassa hakuitwa kwa sababu, according to Mwakyembe committee, wakati wa probe ya mzozo wa Malima na Mengi, zilitoka taarifa kuwa Lowassa katoa rushwa ya namna fulani, na kwa hiyo Spika akashauri wasimwite kumhoji kwa sababu ni kiongozi mwenye wadhifa nyeti, sasa kwa sababu hiyo hiyo hawakumwita kwenye mzozo huu wa Richmond. Na pia walizingatia kuwa ushahidi walionao unajitosheleza.
 
Hili la kumuomba EL asijiuzulu sijui linahusu vipi bunge. Barua ya kujiuzulu ameandikiwa rais, kwa hiyo sidhani kama bunge lina msingi wowote wa kumuomba asiachie ngazi.
 
1. Edward Lowassa ( 2006 - 2008 ) Down

2. Naziri Mustafa Karamagi ( 2006 - 2008 ) Down

3. Ibrahim Msabaha ( 2000- 2008 ) down

4. Basir Pesambili Mramba (1995 - date ) ?

5. Andrew Chenge ( 2000 - to date ) ?

6. Joseph Mungai ( 2000- do date ) ?

7. Zakia Hamdani Meghji ( 1990 - to date ) ?

8. John Pombe Magufuli ( 1995 - to date ) ?

9 ???

10. ???

11. ???

12.???
 
Lowassa hakuitwa kwa sababu, according to Mwakyembe committee, wakati wa probe ya mzozo wa Malima na Mengi, zilitoka taarifa kuwa Lowassa katoa rushwa ya namna fulani, na kwa hiyo Spika akashauri wasimwite kumhoji kwa sababu ni kiongozi mwenye wadhifa nyeti, sasa kwa sababu hiyo hiyo hawakumwita kwenye mzozo huu wa Richmond. Na pia walizingatia kuwa ushahidi walionao unajitosheleza.

Katika ripoti kuna maandiko kwamba, watu mbali mbali walialikwa kupeleka ushahidi kwa kamati teule kwa hiyari ili kuweka mambo hadharani na kurekebisha palipopinda! Sasa basi kwa mantiki ya hoja hiyo ni kwamba kama yeye Lowassa alikuwa na lake moyoni angejipeleka mwenyewe kwenye kamati na kuweka mambo sawa. Kama alitarajia wamwite basi aliula wa chuya. Kwani nani hajui kwamba jamaa ni mbabe sana na huwa anawatishia watu uhai?
 
Na hili ndilo tatizo.
Leo hapa tunajipongeza kwa Lowasa na wenzake kujiuzuru na tunasahau system nzima iliyooza tokea mesenja mpaka Rais mwenyewe kiutendaji.

Tuufurahie kuubadilisha mfumo mzima wa utendaji na uwajibikaji kila sehemu; kuanzia kwenye serikali za vijijini na kwetu sote binafsi.

Matatizo ni makubwa zaidi, na binafsi sina sababu ya kufurahia chochote hapa.

Kama huna cha kufurahia hapa mkuu basi wewe naona utafute nchi nyingine mbali na sayari hii ya dunia....haya sio mabadiliko makubwa lakini mkuu ni muhimu ukubali Taifa linapiga hatu taratibu...mabadiliko ya fikra hayaji overnight.
 
Kweli kabisa!
Lazima tuanzie hapa kwanza, kwani hata hao ambao tunafikiri nchi zao ni adilifu walianzia hapa!
 
Kama huna cha kufurahia hapa mkuu basi wewe naona utafute nchi nyingine mbali na sayari hii ya dunia....haya sio mabadiliko makubwa lakini mkuu ni muhimu ukubali Taifa linapiga hatu taratibu...mabadiliko ya fikra hayaji overnight.

Sina sababu ya kufurahi kwa Lowasa, Msabaha, Nazir Karamagi kujiuzuru kama hapatakuwepo na mabadiliko katika mfumo mzima wa utendaji na uwajibikaji; that is the fact you have chosen to ignore in my posting.

Na huko kutafuta sayari nyingine, hilo sahau!
 
Leo bungeni ilikuwa ni ile siku ambayo tulisoma kwamba:

Siku ilifika ya bubu kusema, viziwi kuona, mawe kuwa watu nk. nimesahau mengine.

Naona wabunge wametoa yote waliyokuwa nayo. Leo hakuna mbunge wa upinzani wala CCM. Wote ni Wabunge wa wananchi wa Tanzania.

Hivyo ndivyo ilitakiwa kuwa kila siku.

Vijana anzeni kuomba kazi maana kuna nafasi nyingi sana inaelekea zitakuwa wazi kwi kwi kwi!!!!
 
Si utani mkuu!
Huenda zikawa zimejazwa tayari kama ilivyo kwa TRA na BOT.
Yangu macho na masikio.
Laugh out Loud (lol)
 
Sina sababu ya kufurahi kwa Lowasa, Msabaha, Nazir Karamagi kujiuzuru kama hapatakuwepo na mabadiliko katika mfumo mzima wa utendaji na uwajibikaji; that is the fact you have chosen to ignore in my posting.
Na huko kutafuta sayari nyingine, hilo sahau!

Una kila sababu ya kutofurahia kujiuzulu kwao, kwani wakijiuzulu utakula wapi?
 
Mie nampongeza Edward Lowasa Kujiuzulu imgawa imemchukua muda mrefu sana. Pamoja na karamagi na msabaha. Congrats. Huko ndiko kuwajibika. Na Kikwete asiwe muoga awabariki waanze.

However issishie hapo Polisi sasa wafanye kazi yao vema kwania hujuma. Na Juu ya yote amali yote ya hao majamaa inabidi ipigwe mhuri vilevile.

Mwakyembe mwingine au huyohuyo original amepewe jukumu la kuwahoji majamaa hao na wengine ikiwa na Nkapa juu ya mali za za kifisadi, then Sheri aichukue mkondo wake. K wangu mie ni UPUUZI KUJIUZULU HALAFU UENDELEE Kutumia mali ya ufisadi ya wananchi.
 
Duh!! Mama Malecela ameshindilia zaidi na kuwaambia napokuja maslahi ya Taifa hana urafiki na mtu.
 
Anafikiria jinsi atakavyokosa shopping the Harrods, London.

Wakifika hapa wanatumia utafiri ni wake wa King wa Saudi Arabia,
kumbe wanatoka nchi ambayo zaidi ya nusu yao hawana uhakika na chakula cha kila siku.

Natamani siku moja ajitokeze mtu ambaye ataonesha receipts za credit card zilizotumika siku hiyo...... unaweza kukuta ni sawa au matanuzi hayo yanakaribiana na budget ndogo ya wizara mojawapo!!
 
Hii ni hatua kubwa kwa Tanzania. Ingawa Huko kujiuzulu kusiwe ndiyo their way out of this mess. Inabidi wananchi tupige kelele mpaka hawa mafisadi wahukumiwe kama wahujumu uchumi, na pia wafilisiwe mali zao zote.

Mbona wezi wadogo huwa wanapigwa na kuswekwa jela? kwa nini iwe any different from hawa ambao wametuibia watanzania hela yetu? Hii ni hela ya mlipa kodi, inabidi irudi.

Yaani kweli walikuwa hawaoni aibu? $152 million shillings per DAY?

Hiyo hela ya siku moja tu si ajabu ingekuwa enough kuwalipa walimu wote kwa mwaka mzima.

I hope wananchi wakimuona wamzomee na kumpiga mawe, kama wanavyopigwa wezi wengine
 
Swali langu kubwa kwa Kikwete ni kwamba - Je hakuyaona haya all this time? haya mambo yameanza since 2006. Wananchi na magazeti wamepiga kelele since 2006, yeye kama kiongozi aliyechaguliwa na watanzania alikuwa wapi? au aliamua tu kuangalia upande mwingine?
Kama angeyashughulikia haya mambo toka 2006 hao mafisadi wake aliowakumbatia wasingekuwa wameiba hela zote hizo. Hilo pekee ni kosa kubwa tu
 
Kuna maneno amezungumuza lowasa kama nimekosea naomba kusahihishwa"ni wivu na kuwa kuna watu wanautaka UWAZIRI MKUU".Kama ni kweli ,basi ni wakina nani hao.
 
Swali langu kubwa kwa Kikwete ni kwamba - Je hakuyaona haya all this time? haya mambo yameanza since 2006. Wananchi na magazeti wamepiga kelele since 2006, yeye kama kiongozi aliyechaguliwa na watanzania alikuwa wapi? au aliamua tu kuangalia upande mwingine?
Kama angeyashughulikia haya mambo toka 2006 hao mafisadi wake aliowakumbatia wasingekuwa wameiba hela zote hizo. Hilo pekee ni kosa kubwa tu

Kikwete ni mmoja wao. Ule wizi wa BOT ulikuwa ni kwa ajili ya kampeini yake kuwania upresident, jambo alilojiandaa kwa miaka kumi. Katika kusaini mkataba wa Buzwagi, Kalamagi alikuwa na Kikwete huko London; kwa hiyo alikuwa akiufahamu. Kwenye mkataba wa Richmond, Kikwete alikuwa na taarifa zote kuwa mshikaji kafanya vile, ila hakujua kuwa litakuwa bomu zito hivi.

Timu nzima ni kama mtoa rushwa na mpokea rushwa; wote wana makosa. hata hivyo huwezi kuwakamata wote mpaka pale utakampa kinga mmoja wao ili awe shahidi wako. Kwetu sisi inabidi tumwache Kikwete il awe shahidi wetu
 
Steve, mimi naona bado sana na natoa wito tuendelee kumuomba Mungu!

Dr. Mwakyembe amesema live kuwa Richmonduli ni mfano wa mikataba mingi mibaya kama vile IPTL, Agreko nk.

Hawa Richimonduli wanalipwa shilingi miloni 200 kwa siku! Wahta a shame na WaTz ndiyo wanaolipia!

Kama alivyosema EL mwenyewe, naungana naye kuwa hajatendewa haki na Kamati ya Mwakyembe maana hawakumuhoji (naamini asingewakwepa kama Mshirika wake wa Kibiashara- Rostam Azizi) maana Msabaha na wengineo walimtaja Waziri Mkuu kama ndiye Mshinikizaji; kwa nini hawakumhoji? LAbda naye angewataja wengine naamini kabisa kuwa angemtaja bosi wake maana vyanzo vyangu vinadai kuwa Richmonduli ulikuwa Mradi wa EL na Bosi wake! HAKI HAIJATENDEKA

Inaelekea kweli kuna ujanja hapa, kwa nini hakuhojiwa Lowassa? Kwa maelezo ya Dr Mwakyembe, hawakupata sababu za kumhoji Lowassa ati kwa kuwa waliomtaja walifanya hivyo nje ya kiapo! Lakini je, hao wote waliohojiwa ni kutokana na kutajwa ndani ya kiapo?

Hakuna waliohojiwa kutokana na tetesi tu ili kuthibitisha madai yaliyotolewa? Ukisoma ripoti ile utagundua wengi tu walihojiwa kutokana na kutuhumiwa hata kama tuhuma hizo zilikuwa nje ya kiapo, na wengine ni kutokana na nafasi zao katika wizara na idara husika.

Nakuja na hypothesis hii: Dr Mwakyembe alikuwa na maelekezo rasmi kuwa asimhoji Lowassa. Dr Msabaha kasema "bangusilo", pengine Lowassa angekuja na neno lake la kimasai ambalo lingekuwa na athari zaidi?
 
Kithuku,

..Balozi Kazaura alinukuliwa nje ya kiapo akisema kwamba Richmond ilitokana na shinikizo la "BWANA MKUBWA" na mshirika wake wa kibiashara.

..Hivi ktk Tanzania, bwana mkubwa ni Kikwete au Lowassa?

..Je, ripoti ilielekeza huyu "bwana mkubwa" anayezungumziwa ni nani?

..pia haiwezekani mambo yote haya yakafanyika bila Raisi kuwa na habari nayo.

.. huu ni wizi mkubwa sana wa fedha za umma. nashindwa kuamini Waziri Mkuu atakiuka hata maagizo ya baraza la mawaziri bila "baraka" za Raisi.
 
Back
Top Bottom