Kashfa ya Richmond: Lowassa, Karamagi na Dkt. Msabaha Wajiuzulu

Kashfa ya Richmond: Lowassa, Karamagi na Dkt. Msabaha Wajiuzulu

Yaani kweli walikuwa hawaoni aibu? $152 million shillings per DAY? Hiyo hela ya siku moja tu si ajabu ingekuwa enough kuwalipa walimu wote kwa mwaka mzima
.

Maneno mazito haya lakini ebu tumsikie mwenyewe El anavyosema:- Bwana Lowassa aliongeza "ninafanya hivyo kwa moyo mweupe kabisa ili kuonyesha dhana ya uajibikaji na pia kutokukubaliana na utaratibu uliotumika kusema uongo ndani ya bunge kwa kumsingizia mtu."

Mkuu hi sio dhana tena ni wajibu uawajibike na haitaishia kujiuzuru kwako, wananchi tunataka ufikishwe mahakamani na hakuna kifungu chochote cha katiba kitakacho kulinda sasa hivi.

Wewe na wafuasi wako, Msabah na wakurugenzi wake, Karamagi, Mwanasheria wakati ule, Hosea, na wengine wote walioshiriki ktk njama hizi ni lazima wafikishe mahakamani na sheria mpya ya Uhujumu uchumi itumike mara moja....
 
Analalamika waziri mkuu kuwa hakupewa natural juctice kwani hakuitwa na anasema kuwa alikuwa tayari kwenda hata kwa miguu kwenye kamati husika za bunge.

Anasema kuwa ameonewa sana na amedhalilishwa sana na kamati na kuwa ametuhumiwa bila hata ya kuulizwa hata jambo moja.

Anasema kuwa yeye ameonewa na anasema kuwa kwenye taarifa yao hakuna hata taarifa moja iliyotoka kwenye ofisi ya waziri mkuu , na anasema kuwa ingekuwa heshima kama angepewa nafasi ya kujitetea.

Analaumu kuwa kama wanaweza kumponda waziri mkuu kiasi hicho je?mwananchi wa kawsaida anaweza kutendewa haki?

Kamati ya Dk. Mwakyembe imetumia hekima kubwa sana kutokumuhoji aliyekuwa waziri mkuu. Kwa upande mwingine imejitahidi kulinda heshima yake licha ya mazingira kuonyesha kuwa yeye mwenyewe alishajivunjia heshima kwa kutumia nafasi yake katika kulazimisha maamuzi yasiyo na manufaa kwa taifa kufanyika na kinyume cha taratibu za uma.

Kamati haijamuhukumu, bali imefanya uchunguzi na ikaridhika na ilichoweza kukipata bila kuongea nae na kukitoa hadharani. Kama alifikiri ana maoni yoyote ya kuweka sawa hapo bado alikuwa na nafasi ya kufanya hivyo.

Inaelekea kamati ilikusudia kumuachia nafasi ya kujieleza si kwa kamati tu bali kwa bunge au taifa zima na kwa muda wake mwenyewe iwapo anacho kitu cha kujieleza. Iwapo kamati ingemuhoji kulikuwa na nafasi kubwa sana ya kumvunjia heshima zaidi.

Hakukuwa na heshima kubwa zaidi ya kupewa nafasi ya kuamua mwenyewe kusuka au kunyoa.

Inakuaje anaona ajabu kurushwa na kamati bungeni wakati yeye mwenyewe alishawahi kuwafukuza watu kazi kwenye TV mbele ya watoto zao na wake zao bila kuwapa nafasi ya kujieleza!?
 
................Inakuaje anaona ajabu kurushwa na kamati bungeni wakati yeye mwenyewe alishawahi kuwafukuza watu kazi kwenye TV mbele ya watoto zao na wake zao bila kuwapa nafasi ya kujieleza!??

Exactly...........ujue ni jinsi gani huyu EL alivyo mbinafsi
 
Mnakumbuka EL kule Mwanza alimfokea Mkuu wa Wilaya naye akamdindia akamwambia ana uzoefu wa ukuu wa wilaya kwa miaka 25?

Sasa yeye anatoa hukumu hapo kwa hapo- kwa waliochini yake na kuwaambia 'waachie ngazi na taarifa zao anazikataa'

Sasa yeye kwa nini leo inamuuma kuanchia ngazi bila maswali?
 
Baada ya hotuba ya Dr. Mwakyembe, EL alikuwa na wakati, nafasi na muda wa kuijibu hasa vifungu vinavyomhusisha yeye lakini badala yake amechagua kujiuzuru na kuendelea kudai ameonewa.. Ile hotuba haikuwa hukumu hata kidogo ila ni uchunguzi ulofanywa na hakuna hata sehemu moja iliyomtaka yeye ajiuzuru moja kwa moja.

Huyo Msabah ma Karamagi naona bangi zinawasumbua, kumwandikia JK barua ya kujiuzuru ndio nini wakati waziri mkuu kisha jiuzuru?...wao ni moja kwa moja wanapotez nafasi zao hadi pale rais atakapo tangaza baraza jipya na kwa nini wasiliandikie bunge kuomba nafasi ya kujieleza bali moja kwa moja wamewasilisha barua zao kwa rais?

Guys hawa jamaa wamekiona cha moto na badooo.

Walisema hayawi hayawi.. sasa yamekuwa na kama tuliyosema Mwanzo wa mwaka huu ni lazima JK atabadilisha baraza la mawaziri, iwe ni kupitia swala la Tanesco ama.

It was written!..na muda wake ndio hiyo umesha fika.
 
You are very right on that one Mkandara. Badala ya kulia lia kuhusu kuonewa, na hata huko kuonewa kwenyewe kwa kutoitwa tu kwenda kutoa ushahidi; nafasi yake nzuri ya kutoa cheche zake za mwisho ilikuwa ni hapohapo leo.

Angetumia muda wake vizuri kutoa 'summary' ya kipi hasa kilitokea na mchango wake katika sakata zima.

Bada ya kufanya hivyo, basi ndipo angetoa hiyo habari yake ya kujitoa.

He squandered his chance. Again, great leaders are rare, he is not one of them.
 
Wakuu wote JF nichukue nafasi hii kuwashukuru kwa kazi nzito ya muda mrefu, kuipigania Richimonduli mpaka leo kuuona mwisho wake. Wakuu naomba niseme kwa dhati kwamba nilikuwa ninaijua power ya JF, lakini sivyo kama ninavyojua sasa, Oh! my God jana sikulala, simu na messages kutoka kila kona ya dunia wananchi wanataka kujua kilichotokea, na huku JF kuna nini maana kulikuwa hakuingilinki kabisaa, siku nzima ya leo. JF kwa kweli ni political power kama sio tool, wakuu tuzidishe mapambano maana sasa tulipofikia ni pakubwa sana katika kuelimisha na kuwasilisha ishus muhimu kwa taifa.

Pia ningemuomba ndugu Robot Invisible, kwamba ajitahidi iwezekanavyo na hasa kwa kwa kusaidiana na sisi members kuuimarisha mtambo unaoisukuma hii JF maana ukweli ni kwamba bado kunahitajika nguvu zaidi ili uweze kubeba wananchi wengi kwa wakati mmoja, leo kuna wakati ilikuwa impossible kuingia, kulikuwa na wananchi 510 kwa wakati mmoja, sasa mkuu Robot tuwasiliane kuangalia nini kinaweza kufanyika ili kuongeza nguvu.

Waziri Mkuu wa zamani, Lowasssa, ameondoka, huu ni ushindi mkubwa sana kwetu wananchi na hasa JF, kwa sababu hakuondoka kwa wema, ameondoshwa na nguvu ya wananchi, yaaani sisi wanyonge. Hakupenda kuondoka, tunajua jinsi alivyojaribu ku-lobby sana kwa Muungwana, kwa visingizio kuwa hakupewa Due-Process, mimi ninasema kuwa hakukuwa na haja ya kupewa hiyo haki kwa kiongozi asiyekuwa muaminifu kama yeye, hiyo tunawapa wananhi au viongozi ambao wanaonekana kuwa ni waadilifu na labda kuna hisiaa za kuonewa katika tuhuma zao, lakini sio yeye, kwanza Mwalimu alisema na ushahidi akaonyeshwa jinsi alivyokula hela za magari ya wabunge akiwa waziri katika ofisi ya waziri mkuu, Muungwana akaombwa sana na viongozi wa juu wa CCM kuwa asimpe huyu u-PM, na sasa haya ya aibu, sasa huyu tunampa hiyo haki ya nini? Ukweli ni kwamba by now alitakiwa awe anongelea Ukonga au Segerea, lakini sio bungeni!

Tunajua kuwa toka juzi usiku, alikuwa ameshambiwa wazi uso kwa uso na Muuungwana kuwa atoke mwenyewe, kabla hajamtoa, ndio maana jana hakuwepo pale airport, na pia tunajua kuwa ilikuwa atoke toka pale aliponyimwa u-makamu wa CCM, na kwamba ana mkono kwenye umwagiwaji waaandishi wa habari tindikali, kwa sababu wale waandishi walikuwa tayari wameshapata habari kuwa anatakiwa atoke wiki ile ile aliyowamwagia hiyo sumu, akafanikiwa tu ku-delay the process. Wakuu JF hebu fanyeni kazi ya utafiti wa kweli mjue mali alizojilimbikizia huyu mkuu in the last two years, maana wengi wetu hapa inaonekana hatujui how much damage the man amefanya kwa taifa, angalia mtoto wake asiyezidi umri wa miaka hata 30, mali alizokusanya in the last two years, hayo maneno ya kunyimwa haki anayatoa wapi? Hivi hana aibu? Kwa nini mwishoni mwa ripoti Mwakyembe anawapa pole waandishi wa habari waliomwagiwa acid? Ninasema huyu fisadi belongs to prison na sio kupewa haki, hao waandishi anatakiwa awalipe makovu na majeraha na vilema aliyowapatia, Yes I said it I do not care anymore huyo ni jambazi, he belongs to prison kama sio Rumande, lakini sio haki ya sheria zetu, absolutely NO!

Enough!, sasa tumejua kuwa nguvu ya wananchi haiwezi kuchezewa na majahili, hata kama ni marafiki wa rais, they all fall kama panzi and that is what they deserve, kuondoka kwa nguvu ya wananchi, tena wapigwe mrufuku kuingia tena kwenye siasa hawa maana ninajua kuwa sio wajinga hao wana plan B hao, they are not done hawa, sasa hivi mtawasikia Yes I said kwa sababu I know it kuwa hawawezi kukubali kutoka hivi hivi tu, lazima watakufa na wengi very sooon, and wakifanya hivyo itakuwa ni kuvuja kwa pakacha furaha yetu wananchi! Sasa wataingia kwenye vyama au watajificha nyuma ya vibaraka wao na baadaye watajitokeza mbele, Yes ndio tabia ya fisadi hiyo huwa hawatosheki.

Lakini for now heshima mbele kwa wananchi wote hapa JF kwa kazi nzito, na bado wakuu mbele kuna kazi zaidi, ninasema kuwa bado kuna viporo vingi sana havijamalizwa, ninasema kuwa Hosea naye aondoke, huko Usalama atueleze alikuwa wapi haya yakitendeka? kama hana ya kutosha naye aende sasa, mwanasheria mkuu naye alikuwa wapi, kama hana maelezo naye aende, waziri wa polisi alikuwa wapi? Ubalozi wetu DC walikuwa wapi? Halafu huyu Lowassa na wenziwe wapelekwe kwenye mkono wa sheria, na pia Mwakyembe apewe new assignment ya kumfuatilia Rostam na kuweka mambo yake wazi, anafanya nini? Mbona yuko kila kona ya nchi yetu yeye ni nani? Halafu Spika naye ana mengi ya kujibu huyu naye, maana haeleweki kabisa.

Wakuu heshima mbele tena, tusilale, ujumbe kutoka hapa unafika panapotakiwa, salaam kwa wajumbe wote JF wembe ni ule ule, tumejionea wenyewe kuwa inawezekana, sasa kazi!

Ahsante Wakuu!

Mzee Mkapa kaachonjo, wananchi wanakuja haoooooooo!
 
Lowassa ameonewa na nani? Alipewa wito wa kwenda kujieleza (wote tulipewa huo wito) na hakutaka. Kamati ilitaka WOTE wenye habari zinazohusu jukumu walilopewa waende kuieleza.

Lowassa hakwenda. Hapo ni kosa tayari kwani alikuwa na habari husika. Sasa alitaka aandikiwe barua ya KUMLAZIMISHA kwenda kujieleza? Na kwa KUTOLAZIMISHWA ameonewa?

Lowasa hajui maana ya neno UONEVU. Mtu anayemfukuza kazi Mhandisi wa Manispaa (badala ya contractor) kutokana na kuanguka jengo mahali anajua kweli uonevu ni nini?

Lowasa amelitia taifa hasara kubwa sana. Tuwafanyeje yeye na mafisadi wenzake? Naona kwa kuanzia, tuteme mate kila watakapopita (kuonyesha kwamba kuna uchafu umepita mbele yetu).
 
Mzee es, sikuwezi, picha nzima iko hapo btn the lines. ahahaha

Jk alisema EDO usiwe na pressure PM anakuwa member wa cc automatic, knowing well in advance kuwa atampiga chini upm na cc itaseize.

Sasa EDO analalamika kuhusu report, ashangai spika ilikuwa vipi nov 15, 2007 ndio kamati iuendwe/// Sitta alipewa amri na JK, na hata walipotaka kuleta usanii wa Sitta kwenda us ili adai amekwama us/europe mpaka end of next week bunge liishe bila huu mjadala, JK alimwita Sitta pale dsm na kumwambia rudi upesi Dodoma na nakuja huko Jumatano.
 
spika anakataa kuwa baraza zima haliwezi kujiuzulu , mpaka apate barua ya rais.

Hivi huyo Spika hajui kuwa kuna barua nyingine inazobidi zisomwe ni zile zilizotoka kwa wananchi wenye uchungu na nchi yao?

Hajui kuwa huyo raisi ni sisi tullimchagua, kwa hiyo tuna mamlaka juu yake? Hajui hilo? Mawaziri wajiuzulu, umma wa watu unataka hivyo, as long as JK is concerned, he also knew about Richmond- he should resign.

And if he didnt know about it, how many things doesnt he know? and if he doesnt all those stuff, why in this fucking hell is he a president? Whom does he preside on?

Money from Bot should be returned to Tanzania. as far as we are concerned that JK should FIND that money and bring it back to the people.

We want that money, its ours. we also need good housing and services like health same as you guys when you go to abroad just to get medication for your un-full-filled stomach aches
.
 
Mkuu ES,

Well said. Sishangai kumuona EL anachukua wadhifa mwingine baada ya wananchi kusahau ya RICHMOND.

Swali ni kwamba huyu fisadi mwingine GRAY MGONJA mbona amekaa kimya tu. Na yeye inabidi awajibishwe mara moja kwani JIKO lote la TANZANIA limenuna kwa ajili ya UJINGA WAKE NA TAMAA. Asijifanye kuwa kimya kwasababu yeye sio Waziri. Wengine pia wachunguzwe mara moja kama wakina MRAMBA, MEGHJI, MAGUFULI, ..... The list is long kwani hakuna wa kusalimika.

Hii ni aibu sana kwa serikali ya Kikwete kwani mambo yote haya yako wazi ila yeye na waziri wake mkuu waliyafumbua macho.

PONGEZI ZANGU ZA DHATI ZIENDE KWA KAMATI YA MWAKYEMBE KWA KAZI NZURI WALIOIFANYA BILA KUJALI WADHIFA WA MTU YEYOTE NA HASA KWA KUJALI MASLAHI YA WANANCHI NA TAIFA KWA UJUMLA.

PIA NAWAPONGEZA WABUNGE WA VYAMA VYA UPINZANI HASA DR. SLAA, ZITTO NA WENGINE KWA KUWA MSTARI WA MBELE KUTETEA MASLAHI YETU WANANCHI NA TAIFA ZIMA.

HILI PIA LIWE FUNDISHO KWA SPIKA WA BUNGE KATIKA UTENDAJI WAKE WA KAZI ILI AONDOE KASUMBA YA KULINDA HAWA MAFISADI WA CHAMA CHAKE/TAWALA.

FURSA HII NI YA RAIS KIKWETE KUONYESHA WANANCHI KUWA ANA NIA YA KWELI YA KUSAIDIA UMMA. IMEKUWA MUDA MREFU HADI KUFIKIA HAPA.
 
Mfa maji haishi kutapatapa, na safari hii mpaka kieleweke hapendwi mtu hapa ni haki tu itendeke Tanzania, wakati ni huu.
Analalamika waziri mkuu kuwa hakupewa natural juctice kwani hakuitwa na anasema kuwa alikuwa tayari kwenda hata kwa miguu kwenye kamati husika za bunge.

Anasema kuwa ameonewa sana na amedhalilishwa sana na kamati na kuwa ametuhumiwa bila hata ya kuulizwa hata jambo moja.

Anasema kuwa yeye ameonewa na anasema kuwa kwenye taarifa yao hakuna hata taarifa moja iliyotoka kwenye ofisi ya waziri mkuu , na anasema kuwa ingekuwa heshima kama angepewa nafasi ya kujitetea.

Analaumu kuwa kama wanaweza kumponda waziri mkuu kiasi hicho je?mwananchi wa kawsaida anaweza kutendewa haki?
 
Mkuu moelex,

You got it right, majuz Kikwete alimuuliza Sitta eti unakwenda wapi? Mkuu maneno yote yalimuishia, kwani wakati anaenda Dodoma muungwana likuwa hajui kuwa kuna nini kwenye ripoti? Mkuu tunajua kuwa Muungwana likuwa na hii ripoti hata kabla Mwakyembe, hajapewa kamati, Muungwana hataki lawama akaamua kuwatafutia kitanzi kamati ya Mwakyembe,

Tunajua kuwa wakati Msabaha na wenziwe wanacheza the game, Masha hakukatiwa, na alikuwa ameshaonywa na wakulu wengine kuwa akae chonjo, akawa anawafuatilia kwa karibu na kuweka ripoti yake pembeni, siku moja Muungwana, alimuita na kumkaripia kuwa hata wewe nilikuwa ninakuamini, Masha akatoa ripoti yake aliyokuwa ameichimbia na kumwambia Muuungwana, nilijua Msabaha ni rafiki yako nikimchongea nitajichongea mwenyewe, lakini mkuu ninayo ripoti yangu hiii hapa ya kila kitu walichofanya, ndio akapona kwenda uhamiaji,

Mambo yote yalianzia na kuishia hapo, Lowasssa asidanganye wananchi aliambiwa toka juzi kuwa atoke, Karamagi alijua hili linakuja kwa sababu majuzi tu alisikika akidai kuwa siasa inamharibia biashara zake afadhali arudi kwenye biashara, kumbe aliijua kuwa panga linakuja maana yale mambo ya kukutana na Muungwana na Rostam, mara kwa mara saa za usiku Muungwana aliyakata, na yeye Karamagi kwa mra ya kwanza kukutana uso kwa uso na Muungwana, ilikuwa wiki iliyopita kwenmye ziara yake huko West, ambapo aliweza ku-read clear usoni kwa Muungwana kuwa something is coming, mbona toka Jumatatu alikuwa akihamisha vitu toka ofisini kwake kulikoni?

Waende salama ila ikibidi warudishe mali zetu!
 
Last edited by a moderator:
Kazi inaendelea , ushindi wa kwanza wa wananchi na sasa ni karibia na half time, naamini kuna haja ya wananchi kujipanga ili kukikabili kipindi cha pili .
 
This is the best time in Tanzania history, as my dad said "it is right time, at the right place".

Mwalim Nyerere aliwa toa worn kuhusu muheshimiwa Lowassa kwamba "he is corrupted". Hawa watu wamelitia taifa kwenye damage nzito sana. I expect JK will do few things in order to restore our confidences.

1- Kuwafikisha mbele ya sheria wote ambao wamelitia taifa kwenye hasara kubwa sana. Hii ni pamoja na Rostam Aziz, Patel, Balali, Karamangi, Hosea, Lowassa, na wengine wengi sana. We need answers for all the questions we have.

2-JK anatakiwa apunguze baraza la mawaziri kati ya 15-30, this will be easy for him to control. The next thing ni kwamba tuna expect mawaziri watakuwa wapya who never been in his cabinet at all.

3- JK anatakiwa ajue kwamba hili tatizo sio juu tuu, bali system nzima imecorrupted. So, i expect makatibu wote kuwa fired au relocated and this is only for the sake of the nation. Clean every corner of the government is the only options.
 
Jamani tuipitieni vizuri hii hotuba yake ya mwisho el kama waziri mkuu.

Hivi kwa nn hawakumfuata? Au ndio lilikuwa lishapikwa kama alivyoonyesha, kuwa lazima upm auachie?

Au ndio anaeuwa kwa upanga hufa kwa upanga?

Maana salim nnaamini anaangalia wabaya wake wanavyoumbuana.

Chama cha walevi hakina mwisho mwema


lowassa alia na kamati ya mwakyembe
habari zinazoshabihiana
• kamati ya richmond 'yahamia' marekani 14.12.2007 [soma]
• walioipa tenda richmond kuhojiwa 28.11.2007 [soma]
• richmond aibu! *lowassa, karamagi, msabaha, mwanyika, hosea mh! 07.02.2008 [soma]

na mwandishi wetu, dodoma

jana waziri mkuu, bw. Edward lowassa, alikuwa kiongozi wa kwanza kati ya watatu, kutangaza nia yake ya kujiuzulu kutokana na taarifa ya kamati teule ya kuchunguza mkataba wa richmond.

Katika hotuba yake bungeni, bw. Lowassa alionesha kutoridhishwa na taarifa hiyo na yafuatayo ni maneno yake aliyoyasema wakati akitangaza azma yake hiyo:

"mheshimiwa spika, kwanza napenda kuchukua nafasi hii kukushukuru sana kwa kunifanya msemaji wa kwanza katika hoja hii.

Lakini la pili nimpongeze dkt. Harrison mwakyembe, mwenyekiti wa kamati teule kwa kuwasilisha kwa mbwembwe nyingi sana taarifa yake, mbwembwe zilikuwa nzuri kweli.

Kwa kazi nzuri kwa maoni yao, wamewasilisha vizuri. Lakini nimesimama kuweka kwenye kumbukumbu kutoridhika kwangu na jinsi kazi hiyo ilivyofanywa.

Mheshimiwa dkt. Mwakyembe ni mwanasheria, tena daktari alikuwa anafundisha wanafunzi chuo kikuu. Moja ya vitu alivyokuwa akifundisha ni natural justice.

Mheshimiwa spika, wewe pia ni mwanasheria unafahamu suala la natural justice. Kwamba kamati teule imesikiliza watu wengine wote pamoja na wanaoita minong'ono ya mitaani, wamesafiri mpaka marekani kutafuta mashahidi, lakini mimi ambaye ni mmoja katika watuhumiwa mle, hawakunihoji hata siku moja.

Mheshimiwa spika, nimesimama kueleza masikitiko yangu. Ofisi ya bunge mpaka ofisini kwangu, hata wangeniita ningekwenda kwa miguu kama hamna gari na nilikutwa tayari kufanya hivyo.

Hawa ni watu makini sana, siwezi kuamini kwamba wanaweza wakafanya oversight kama hiyo. Kwa sababu katika kila hoja walizojenga wamesema waziri mkuu ilikuwa hivi.

Kulikuwa na shida gani kuja kuniuliza waziri mkuu, wanasema ulitoa dokezo hili ni sawa sawa ni kweli? Kulikwa na shida gani kwa mfano, kufuata utaratibu wa westminster, kuthibitisha hapo unaposema mwenye richmond ni fulani uka-lay on the table records na ushahidi kuwa ni fulani.

Mheshimiwa spika, taifa letu ni taifa changa, lakini chombo hiki ndiyo mahali pa demokrasia pakubwa katika nchi pote, hapa ndipo penyewe. Kama katika chombo hiki haki haitaonekana kutendeka, nchi yetu haitakwenda vizuri.

Hapa ndipo tunategemea tuwaoneshe umakini wetu, umahiri wetu katika mambo ya demokrasia. Kwa hiyo nilichofanyiwa napenda kuweka kumbukumbu sawa, naona si sahihi, nimefadhaika sana, nimedhalilishwa sana, nimeonewa sana katika hili.

Maana zimechukuliwa tuhuma zikaja zikaelezwa hapa kwamba hivi ndivyo ilivyo. Mimi sijaulizwa. Kulikuwa na shida gani ya kuniuliza, kwa nini muamini minong'ono ya mitaani kuliko maelezo yangu.

Sisi wote hapa ni wanasiasa, tukianza kuamini minong'ono ya mitaani, niambieni mwanasiasa atakayesimama. Huwezi tume imepewa muda wa kutosha lakini inashindwa kumwona mtu ambaye wanamtuhumu na wanamsema kwa kirefu sana.

Mheshimiwa spika, lakini hata pale uliponinong'oneza ukaniambia una ushahidi wowote? Nilikupa ushahidi huo wa maandishi. Katika taarifa yao hakuna hata moja ya ushahidi ambao umetoka kwa waziri mkuu. Kile kitabu cha majedwali kimejaa majedwali mengi pamoja na magazeti mpaka ya udaku, lakini maelezo ya waziri mkuu hakuna hata moja.

Mheshimiwa spika, naamini ingekuwa ni heshima wangeiweka halafu wakasema tunakataa kitambulisho hiki kwa sababu hii na hii na hii, hiyo
ndiyo imejengwa hoja. Lakini kujenga hoja na kuja hapa bungeni tunahutubia nchi nzima na kusema waziri mkuu amefanya hiki, amefanya hiki bila ya kumsikiliza, nachelea kuuliza hivi mtu wa chini itakuwaje?

Mheshimiwa spika, lakini nimetafakari kwa makini sana jambo hili nikajiuliza hivi hasa kulikoni mpaka watu wazima wenye uwezo wao, watu maarufu wenye heshima zao, mpaka wafike mahali waache jambo la msingi kama hilo kulikoni?

Mimi nadhani there is a wish which i am going to grant, ni uwaziri mkuu. Nadhani tatizo ni uwaziri mkuu. Kwamba ionekane waziri mkuu ndiye amefanya haya, tumwondolee heshima au tumwajibishe.

Mheshimiwa spika, nimetafakari sana kwa niaba ya chama changu, kwa niaba ya serikali yangu nimeamua kumwandikia rais barua ya kumwomba niachie ngazi. Nafanya hivyo kwa moyo mweupe kabisa, ili kuonesha dhana ya uwajibikaji, lakini na kutokubaliana na utaratibu uliotumika kusema uongo ndani ya bunge wa kumsingizia mtu.

Mheshimiwa spika, nitumie nafasi hii kumshukuru sana rais kwa heshima aliyonipa ya kutumikia nchi hii kwa uwaziri mkuu kwa miaka miwili. Namshukuru sana mheshimiwa rais.

Nakushukuru wewe, nawashukuru mawaziri na naibu mawaziri, nawashukuru waheshimiwa wabunge na wanachama wa ccm tuliosimamia ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi. Mheshimiwa spika baada ya kusema hayo nakushukuru.

chanzo: majira
 
Mtu wa Pwani nadhani Lowassa anataka SYMPATHY ya watanzania which he doesnt deserve. Lowassa new the problem with the whole issue of Richmond na akiwa kama mbunge wakati Mwakyembe na watu wake wanapewa jukumu la kuichunguza hii kashfa alikuwepo, na ALIJUA kwamba ANYBODY (unless yeye huyuko kwenye hiyo list ya anybody!) ana haki ya kwenda mbele ya kamati kuelezea anything anachokijua, jamani mbona hakwenda?

Asitufanye wajinga! Infact hii report imemtaja kwamba alikuwa na influence katika maamuzi haya na wala HAIJAMTUHUMU.

Narudia kusema kwamba Lowassa anataka SYMPATHY na wananchi tumeshaling`amua hilo. Asitufanye mabangusilo wasioelewa.

Mwisho napenda kumkaribisha mtaani aje aangalie na kushudia effect ya maamuzi yake. Iam sure now he will appreciate the effectiveness of "THREE LANE SYSTEM", aone FOLENI za magari zilivyo na karaha....and on and on.....It is a good ride waone the impact of their decisions while seated on the other side of the fence!

MWISHO NADIRIKI KUSEMA KUWA MWAKYEMBE KWENYE ILE REPORT ALIONGOZWA NA UZALENDO WA MALI YA TAIFA LETU.

Very few people have that courage and to that I say he will go down in history with this report as one of the best son of our mother land who did a favour to his compatriots when we most needed his services!! Kudos Harrison.
 
Lowasa hana haja ya kulalamika kuwa hajatendewa haki. Milango ya Kamati ilikuwa wazi kwa yeyote yule ambaye alikuwa na taarifa yeyote kuhusu RICHMOND kuwasilisha taarifa hiyo mbele ya Kamati. Watu hawakuitumia nafasi.

Lowassa kama Kiongozi mkubwa Serikali na kwa kuzingatia ushiriki wake wa karibu katika suala hilo, ilitarajiwa awe mtu wa kwanza kutoa taarifa ama maelezo juu ya mchakato wote wa utoaji wa tender hiyo mbele ya Tume. Kwa ujeuri na kiburi chake alijua tume haitathubutu kuhusisha mambo yanayomhusu kwenye taarifa yao.

Alijua wazi kulikuwa na mawasiliano ya moja kwa moja kati ya ofisi yake na ofisi ya wizara ya nishati na madini na hilo lingemsukuma kwenda mbele ya tume kueleza kile alichokuwa anakifahamu, hakufanya hivyo na sasa anamlalamikia Dr. Mwakyembe kuwa ripoti ameiwasilisha kwa mbwembwe, hii sio hoja kwa sasa.

La msingi ni kuwa ni kweli aliweka shinikizo la utoaji wa tender hiyo kwa ujeuri na nguvu binafsi. Asionewe huruma, alishawafanyia wengi mabaya kwa kutumia madaraka yake.

Alikuwa anawakebehi Watanzania kuwa kasungura ni kadogo tugawane kwa makini kumbe yeye na walafi wenzake wachache wanajineemesha kwa ming'ombe ilhali wananchi wengi wakiumia.

Wananchi wanalazishwa kila siku kuchangia ujenzi wa madarasa, zahanati na kununua madawati kwa kunyang'anywa hata vitu vya ndani kumbe fisadi huyu na wenzake wanajichotea mabilioni ya shilingi kwa faida yao binafsi na wake zao, (ati mama Regina anaingia bungeni na kuanza kulia, huu ni uchuro, alitakiwa afukuzwe).

JK asiishie kuwakubalia kujiuzulu tu, sheria ichukue mkondo wake, mali haramu walizojichotea zichukuliwe zirudishwe kwa wananchi, akaunti zao kwa sasa zifungwe tena kwa haraka ili wasije wakahamisha.

Wananchi tusichoke, tuendelee kupiga kelele kila mara na kama JK atawaonea huruma tufanye kila jitihada hata kwa kufanya hujuma kwa mali zao.

"MAPAMBANAO NDIYO YAMEANZA TUSIKUBALI KUCHOKA WALA KURUDI NYUMA"
 
Mafuchila,

..OK..na-concede kwamba sikuisoma paragraph nzima. kwamba ilielekezwa kwamba "bwana mkubwa" ni Edward Lowassa.

..Lakini bado suala linabaki palepale. Hivi Lowassa na Rostam wataingilia suala nyeti kama hili bila Raisi kuwa na taarifa?

..Tume inaelekeza kwamba maagizo mengine yalikuwa yanakiuka maamuzi ya cabinet. sasa nani alikuwa anampa ruhusa Lowassa kukiuka maagizo ya cabinet?
Naamini wewe ni muumini wa moja kati ya hizi dini mbili "kuu" za kigeni,Uislam na Ukristo,katika kitabu cha Mwanzo kwenye Biblia inasemwa kuwa Adam na Eva walikiuka maagizo ya Mungu kutokula lile tunda la mti wa katikati,walipokula na baadae Mungu kuwahoji Adam akasema ni Eva na Eva akasema ni Nyoka (Shetani), na tunaambiwa kuwa shetani alikuwa malaika na hivyo mshirika wa karibu wa Mungu katika uumbaji.

Kama wote Mungu na Shetani (Lucifer ambaye likuwa malaika) walikubaliana waumbe binadamu na kisha Lucifer kwenda kuwashawishi Adamu na Eva kula lile tunda,je Lucifer alitumwa na Mungu?

Kwa kifupi ni hivi ebu tuambie ni nani alimwagiza Lucifer awashawishi Adamu na Eva kutotii amri ya Mungu?
 
Back
Top Bottom