Kashfa ya Richmond: Lowassa, Karamagi na Dkt. Msabaha Wajiuzulu

Kashfa ya Richmond: Lowassa, Karamagi na Dkt. Msabaha Wajiuzulu

Na Mwandishi Wetu

SIRI nzito moyoni mwa aliyekuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Ibrahim Msabaha, ndiyo ililazimisha Edward Lowassa kujiuzulu Uwaziri Mkuu kutokana na kashfa ya Richmond, MwanaHALISI limegundua.

Habari nyeti zilizolifikia gazeti hili zinasema Lowassa alijiuzulu ili kuepusha mawaziri kuanza kutajana. Kama ingefikia hatua hiyo, Dk. Msabaha alikuwa tayari kuweka hadharani majina ya wakurugenzi halisi wa Richmond, akiwamo mtoto mmoja wa kigogo mzito serikalini.

Kwa mujibu wa habari hizo, Dk. Msabaha ndiye alikuwa na nakala halisi ya awali kabisa, yenye majina ya wakurugenzi wa kampuni hiyo feki; nakala ambayo hata Kamati ya Bunge iliyochunguza kashfa hiyo haikuiona.

Lakini kutokana na mambo kuwa mazito dhidi ya Dk. Msabaha, huku akishinikizwa na Kamati ya Uongozi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ajiuzulu, yeyé alisema “nimesikia.”

Kamati hiyo hiyo, ilimshauri aliyekuwa waziri wa madini, Nazir Karamagi, naye ajiuzulu ili kulinda heshima ya serikali, akakubali.

Kwa mujibu wa Kamati ya Usalama na Maadili ya CCM, ambayo nayo ilikuwa inajua fika sakata zima la Ridhmond, lakini inaogopa kuligusa kwa kuwa lilikuwa la wakubwa, baadaye Dk. Msabaha alisikika akijiapiza kwamba “sitakubali kutolewa kafara, lazime nife na mtu.”

Haikujulikana kama ‘mtu’ huyo alikuwa mtoto wa kigogo au kigogo mwenyewe; jambo lililoleta wasiwasi mkubwa na kulizimu ufanyike uamuzi mzito kuikoa serikali.

Lowassa hakuwa mmoja wa watu waliokuwa wametajwa na kamati hiyo, wala hakushauriwa kujiuzulu, lakini ilidhihirika kuwa alikuwa ameshiriki kushinikiza kampuni ya Richmond ipewe mradi wa kufua umeme wa dharura.

Kwa kuhisi kwamba Dk. Msabaha angeweza kuiumbua serikali kwa kuwataja hata wale ambao hawakutajwa na Kamati ya Bunge – ambao walikuwa wazito zaidi, na ambao Lowassa alikuwa akiwalinda wasiguswe – inasemekana aliamua kujiuzulu ili kumfunga mdomo Dk. Msabaha.

Habari nyingine zinasema hata Rais Jakaya Kikwete alijua ‘kila kitu’ kuhusu mradi huo, na kwamba alipoona mambo yamekuwa magumu zaidi alimshauri Lowassa afanye uamuzi ambao usingefumua makubwa zaidi, hata kama ungemgharimu nafasi yake ya uwaziri mkuu.

Habari za uhakika zinasema Kamati ya Uongozi nay a Wabunge wa CCM haikuwa imedhamiria kumtaka Lowassa ajiuzulu, lakini tishio la Dk. Msabaha dhidi ya vigogo ndilo lilimlazimisha Lowassa kuondoka.

Katika kikao chake cha majuzi Butiama, mkoani Mara, Kamati ya Usalama na Maadili iliitaarifu Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) juu ya mchakato uliokuwa umechukuliwa kuwalinda vigogo hao; na kwamba katika orodha ya waliopaswa kujiuzulu, Lowassa hakuwamo.

Hata hivyo, ilisisitiza kuwa Lowassa aliwashinikiza wahusika katika wizara ya nishati na madini, wakati huo chini ya Dk. Msabaha, kuikubali Richmond kwa sababu ya maslahi ya waliokuwamo.

Dk. Msabaha alikuwa Waziri wa Nishati na Madini wakati mkataba wa kufua megawati 100 za umeme wa dharura unasainiwa kati ya serikali na kampuni hiyo.

Taarifa zimesema kwamba Kamati ya Uongozi iliwahoji Lowassa, Karamagi, Msabaha na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, na uamuzi uliofikiwa ni kwamba watu wa kuwajibika walikuwa wawili tu, Karamagi na Dk. Msabaha.

“Wajumbe walifikia maamuzi yafuatayo:- Mhe Dk. Ibrahim Msabaha (Mb) Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mhe Nazir Karamagi Waziri wa Nishati na Madini wawajibike kwa kujiuzulu, kwa kuzingatia hali ilivyokuwa na kwa maslahi ya chama na Taifa.

“Viongozi hao waliitwa kwenye vikao na kuelezwa uamuzi wa vikao uliokuwa umefikiwa. Mhe. Karamagi alikubaliana na maamuzi na akaahidi kuandika barua ya kujiuzulu. Mhe. Dk. Msabaha alikijulisha kikao (kuwa) alikuwa amesikia na (kwamba) angekwenda kwenye mamlaka iliyokuwa imemteua,” inasema taarifa.

Kutokana na mlolongo huo wa mambo, kitendo cha Dk. Msahaba kutotamka kuwa tayari kujiuzulu, kilizusha hisia kuwa angekwenda kueleza kila anachokijua katika sakata zima la maandalizi na utiaji saini wa mkataba.

Vyanzo vya habari vinasema kutokana na Dk. Msabaha kusema tu ”nimesikia” bila kusema wazi kwamba angejiuzulu kama alivyofanya Karamagi, iligundulika kuwa jambo kubwa lilikuwa linakaribia kulipuka, hatua iliyomfanya Lowassa kuona umuhimu wa kuachia ngazi ilki walau kulinda mengine yasiibuke.

Habari zinasema kama kuna mtu anayejua fika namna mkataba wa awali wa Richmond ulivyoandaliwa, na majina yaliyokuwamo katika orodha ya wamiliki wa iliyoitwa kampuni ya Richmond, ni Dk. Msabaha.

Source:MwanaHalisi
 
Nimeirudisha hapa kwa sababu naona part two ya hii movie imeanza,kuna watu bado wanamuona EL kama presidential material.Sijui tuko serious kiasi gani na hili taifa letu
 
Dhana ya uwajibikaji mkuu....safi sana Lowassa....juzi mkuu wa usalama wa Obana alijiuzulu kisa mtu moja kapanda lift na Obana akiwa na silaa wenzetu washafikia hiyo hatua kitu kidogo lazima awajibike, na ndicho alichofanya Lowassa
 
Dhana ya uwajibikaji mkuu....safi sana Lowassa....juzi mkuu wa usalama wa Obana alijiuzulu kisa mtu moja kapanda lift na Obana akiwa na silaa wenzetu washafikia hiyo hatua kitu kidogo lazima awajibike, na ndicho alichofanya Lowassa

Wabongo hawawezi kukuelewa mkuu. Resgnation kama a form of accountability is beyond comprehension of many simple minds.
Wao wanajua ni admission of guilt and direct involvment.

Hapo huyo mama angejjiuzulu kwetu ungesikia ni kwa sababu alihusika na kutaka kumuua raisi! Tuko nyuma sana aisee.
WaTZ wenngi hawana elimu na upeo. Hii ndio itakua sababu kubwa ya kutomchagaua Lowassa. Lowassa anajua intellectually yuko above wengi sana CCM ndio maana analazimika kutumia basic tactics kama kutoa hela kukamata basic minds. Akitumia reasoning and debate hataweza kuwapata wabongo.

Mfano madudu yanayotokea muhimbili, mgonjwa wa kichwa afanyiwe operation ya mguu, ingetakiwa mkurugenzi kama sio naibu waziri au waziri ajiuzulu. Na kwa wenzetu ingekua hivyo. Lakini hakuna kati yao aliyekua chumba cha operation! Mswahili atakuelewa kwa hili unafikiri?
Kwanza daktari mwenyewe bado ana practice hadi leo!
 
Huu uzi ni moja ya njia ya kumsafishia njia huyu mh?
 
Lowassa ni fisadi tu kama mafisadi wengine ndani ya CCM. Ila naona hapa maelezo kibaao ya kumsafisha na kumtakasa na kuita watanzania watu wasio na elimu wala upeo. Ndio mlivyo nyinyi, kila siku kutukana watu wanaowapa kura wakati wa uchaguzi.
Ila msiogope, Bongo tambalale CCM hata ikimsimamisha Kingwendu watu wampigia makofi.
 
Hasafishiki kwa kujiuzulu haikuwa kwa ridhaa yake mpaka alishinikizwa mzee lazima uachie tu
 
Ninajiuliza hili Swali sio mbaya kuwahusisha au kuwashirikisha na nyie mnaweza kunisaidia kupata jibu

Mheshiwa Lowassa aliachia ngazi kkukilinda Chama chake cha CCM, maana alitamka nang'atuka kwa masirahi ya Chama changu ambacho ni CCM, Je CCm alihusika katika Diri la RICHMOND au Dowansi? manaa hawezi kutamka maneno kama yale kama hakukua na kitu ambacho CCM wanajua walifanya,

Sitaki kuchanganya mambo swali langu ni hilo tu
Aksanteni
 
Ninajiuliza hili Swali sio mbaya kuwahusisha au kuwashirikisha na nyie mnaweza kunisaidia kupata jibu

Mheshiwa Lowassa aliachia ngazi kkukilinda Chama chake cha CCM, maana alitamka nang'atuka kwa masirahi ya Chama changu ambacho ni CCM, Je CCm alihusika katika Diri la RICHMOND au Dowansi? manaa hawezi kutamka maneno kama yale kama hakukua na kitu ambacho CCM wanajua walifanya,

Sitaki kuchanganya mambo swali langu ni hilo tu
Aksanteni

Unfortunately watakaochangia hii thread yako watakuwa wachache sana,jamaa wa LUMUMBA wanalijua na kulifahamu hilo so hawatatia neno hapa
 
Hapa kna SIRI kubwa, na ndiyo maana inakuwa vigumu mno kujaribu kumtosa kada huyu Mkongwe wa chama cha Mapinduzi.

Nanukuu "Ndugu wajumbe hakuna nilichokifanya ambacho Boss wangu (Mwenyekiti ) hakukijua" Mwisho wa kunukuu!!
 
Hapa kna SIRI kubwa, na ndiyo maana inakuwa vigumu mno kujaribu kumtosa kada huyu Mkongwe wa chama cha Mapinduzi.

Nanukuu "Ndugu wajumbe hakuna nilichokifanya ambacho Boss wangu (Mwenyekiti ) hakukijua" Mwisho wa kunukuu!!
Hakuna siri yoyote, alichosema Lowassa wakati anajiuzulu sioni kama kina tofauti na alichokisema Sospeter Muhongo wakati anajiuzulu juzi.
 
Unfortunately watakaochangia hii thread yako watakuwa wachache sana,jamaa wa LUMUMBA wanalijua na kulifahamu hilo so hawatatia neno hapa
Hivi sifa za kijinga alizokuwa nazo wakati anajiuzulu si ndizo hizohizo anazotamba nazo kwenye kuusaka urais au? Mimi sasa ndiyo natambua kuwa kauli yake hiyo haikuwa na jipya zaidi kutafuta sifa.
 
Back
Top Bottom