Kashfa ya Richmond: Lowassa, Karamagi na Dkt. Msabaha Wajiuzulu

Kashfa ya Richmond: Lowassa, Karamagi na Dkt. Msabaha Wajiuzulu

Alijua serikali ya CCM ingeanguka kama asingekubali kujitwisha msalaba wa ........ japo baadae alikuja kujutia uamuzi wake maana chama kiliamua kumsulubisha kwenye msalaba huo huo.

Unajua wenzetu walioendelea walishachana na hii biashara ya kumpa mtu mmoja mamlaka ya kuamua hatima ya maisha ya wananchi wake yeye peke yake maana wanajua huyo mtu akikosa akili tu basi na raia wengine wote wamekwisha.

Ndio maana katiba zao zinatoa mamlaka kwa vyombo vya kuendeshea nchi na sio kama hii ya kwetu inatoa mamlaka kwa mtu mmoja yaani just a single person!its a shame you know.

Nyerere alitunga katiba ya namna hii maana alijua uadilifu wake na udhaifu wa viongozi waliomzunguka na ndio maana alimudu ila kwa sasa hakuna tena mtu mwadilifu wa kuweza kutumia aina ile ya katiba na ndio maana mzee Warioba na tume yake walikuja na mabadiliko ya dhati kabisa kutupatia katiba muafaka kwa muda huu na aina ya viongozi tulionao ila CCM ikaamua kuichakachua kwa maksudi kabisa wakiwa wanataka kuturudisha kule kule maana wanajua wananufaika na mfumo uliopo.
 
Inamaana chama kilimtuma afanye manyanga then chama hicho hicho kikamgeuka?

Tafakari,
Acha kutumika kizembe kizembe. EL ni miongoni mwa watu hatari hapa nchini. Hafai na hasafishiki hata gharama yoyote.
 
Hakuna siri yoyote, alichosema Lowassa wakati anajiuzulu sioni kama kina tofauti na alichokisema Sospeter Muhongo wakati anajiuzulu juzi.

Hili la Muhongo ni kweli halina tofauti na ndo maana ile Akaunti ya Stanbic ni SIRI kama alivyosema Lowasa kwenye Richmond!
 
Ninajiuliza hili Swali sio mbaya kuwahusisha au kuwashirikisha na nyie mnaweza kunisaidia kupata jibu

Mheshiwa Lowassa aliachia ngazi kkukilinda Chama chake cha CCM, maana alitamka nang'atuka kwa masirahi ya Chama changu ambacho ni CCM, Je CCm alihusika katika Diri la RICHMOND au Dowansi? manaa hawezi kutamka maneno kama yale kama hakukua na kitu ambacho CCM wanajua walifanya,

Sitaki kuchanganya mambo swali langu ni hilo tu
Aksanteni
Ni wazi kama alikuwa akilinda chama basi chama ndicho kilihusika na huo ufisadi, hilo halina ubishi sana maana wote tunaujua mwenendo wa chama hicho katika ufisadi na hata ukiangalia taarifa zote za CAG zinaonyesha kwamba hata serikali inayosimamiwa na chama hicho ni ufisadi uliokithiri.
Nami nakuongezea swali, huyu alikuwa PM huku naye akiwa sehemu ya chama hicho hicho. Je, mtu anayeamua kujiudhuru kulinda ufisadi naye si ni fisadi!? Je, kuna haja ya mtu kama huyu kusamehema baada ya kuwataja alioiba nao!?

Kama Uwaziri Mkuu ulimshinda, ataweza kuwa Mkuu wa nchi?
 
Inamaana chama kilimtuma afanye manyanga then chama hicho hicho kikamgeuka?

Tafakari,
Acha kutumika kizembe kizembe. EL ni miongoni mwa watu hatari hapa nchini. Hafai na hasafishiki hata gharama yoyote.
Na hapa nakubaliana na wewe Mkuu
 
Richmond aikuwa na usajili tz wala marekani na tenda walipewa

Leo hii anataka Urais hata bila aibu
 
siku ulivoachia uwaziri mkuu ulikuja Arusha tukakupokea pale uwanja wa kisongo baada ya kushuka ulilia sana ukashindwa hata kuongea chochote....swali langu ulikua u alia nini? je ulikua unalia kukosa nafasi ya kula au ulililia watanzania kutoa mwanamaendeleo?
 
Sakata la Richmond: LOWASSA KITANZINI Na Saed Kubenea

MAWAZIRI watatu katika serikali ya Rais Jakaya Kikwete, wanatarajiwa kujiuzulu wakati wowote kutokana na kashfa ya mkataba wa Richmond, MwanaHALISI limedokezwa.

Taarifa za kuaminika kutoka serikalini na ndani ya Bunge zinasema mawaziri hao watatu wanatajiuzulu katika kipindi cha mkutano huu wa Bunge. Tayari mmoja wa mawaziri anapitapita miongoni mwa wabunge mjini Dodoma akilalama kuwa ameponzwa na Waziri Mkuu Edward Lowassa. Haijafahamika ni kwa msingi gani.

"Ndiyo wapo mawaziri watakaojiuzulu wakati wowote kuanzia sasa. Sifahamu ni lini, lakini ni katika mkutano huu wa Bunge," kimeeleza chanzo cha habari cha gazeti hili. Chanzo hicho kimesema, "Inawezekana wakajiuzulu kabla ya ripoti ya Dk. Mwakyembe (Dk. Harisson Mwakyembe), kuwasilishwa bungeni, au baada ya kuwasilishwa na kujadiliwa. Lakini uhakika ni kwamba watajiuzulu."

Ripoti ya Kamati Teule ya Bunge kuhusu mkataba katiya serikali na kampuni ya kuzalisha umeme ya Richmond, inatarajiwa kuwasilishwa na kujadiliwa katika mkutano wa sasa wa bunge. Taarifa zinasema kujiuzulu kwa mawaziri hao kunafuatia shinikizo kubwa lililotokea ndani ya Kamati Kuu (CC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Imeelezwa kuwa baadhi ya wajumbe wa CC, walikuja juu, wakitaja majina na kushinikiza kwamba wote wanaotuhumiwa kwa ufisadi unaohusu Richmond waachie ofisi za umma "na bila mjadala." Imefahamika kwamba wajumbe waliokuwa wakishinikiza waliongozwa na Abdulrahaman Kinana na makamu mwenyekiti mstaafu wa CCM, John Malecela.

Taarifa zinasema walishinikiza kwamba rais Kikwete "awaondoe" mawaziri wake iwapo hawatakubali kujiuzulu kwa hiari. "Mjadala ulikuwa mkali.

Rais alikubaliana na hoja za wajumbe. Alisema kila anayetuhumiwa ni vema akaondoka, kabla hajaondolewa," alisema mjumbe mmoja wa CC, akimnukuu Kikwete. Mawaziri wawili wanaotajwa kuwa na uwezekano wa kujiuzulu ni Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi na mtangulizi wake katika wizara hiyohiyo, Dk. Ibrahim Msabaha. MwanaHALISI halikuweza kupata mara moja jina la waziri wa tatu anayetakiwa kujiuzulu. Dk. Msabaha ambaye sasa ni Waziri wa Afrika Mashariki, anasulubiwa kutokana na mkataba huo kusainiwa wakati wa utawala wake. Dk. Msabaha aliondolewa katika wizara hiyo Oktoba 2006 katika mabadiliko madogo ya baraza la mawaziri.

Karamagi amebanwa ajiuzulu kutokana na tuhuma kwamba aliongeza mkataba wa kampuni ya Dowans, bila kumshirikisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini. Dowans ndiyo iliyonunua mkataba wa Richmond ambapo kama ilivyokuwa kwa dada yake (Richmond), ilishindwa kukamilisha kazi kwa wakati. Wakati mawaziri wanajiandaa kujiuzulu kwa shinikizo, mmoja wa wabunge wa zamani katika CCM anasema kunaweza kuibuka mgogoro mkubwa iwapo mawaziri hao watakataa kushinikizwa na kutaka "waondoke na waliokuwa wakiwatuma."

MwanaHALISI inazo taarifa kwamba kuna malalamiko mengi miongoni mwa watuhumiwa ambao wanadai kuwa walikuwa wakipokea amri "kutoka juu" katika kutekeleza mkataba wa serikali na Richmond. "Iwapo watakuwa jasiri na kumtaja huyo aliyeko juu na ambaye alikuwa akiwaamuru au kuwaelekeza, basi watakuwa wamepona na yeye atalazimika kujiuzulu kwa aibu kubwa," kimeeleza chanzo cha gazeti hili.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, mkataba kati ya serikali na Richmond ulisainiwa bila kufuata taratibu, ikiwamo kutofikishwa katika kikao cha makatibu wakuu (AMTC).

Kikao hicho kinachokuwa chini ya Katibu Mkuu Kiongozi, ndicho chenye jukumu la kujadili jambo lolote ambalo litatakiwa kufikishwa katika Baraza la Mawaziri.

Kutokana na hali hiyo, mkataba wa Richmond haukifikishwa katika kikao cha Baraza la Mawaziri, ambacho mwenyekiti wake ni rais wa Jamhuri. Vyanzo vyetu vya habari vinasema, mkataba kati ya serikali na Richmond ulijadiliwa na Dk. Msabaha kama waziri mwenye dhamana ya umeme, Waziri wa Fedha, Zakia Meghji na Waziri Mkuu Lowassa.

"Mkataba haukufikishwa katika kamati ya makatibu wakuu. Wala haukufikishwa katika Baraza la Mawaziri," waziri mmoja mwandamizi ndani ya serikali aliliambia MwanaHALISI. Alisema, "Wakati mkataba unasainiwa, rais Jakaya Kikwete alikuwa ziarani Marekani. Aliporudi nchini akakuta tayari kila kitu kimevurugika.

Ndipo alipoamua kufuatilia ili kujua ukweli wa suala hili." Bunge katika kikao chake kilichopita, liliunda Kamati teule kuchunguza mkataba kati ya serikali na kampuni Richmond. Kamati hiyo iliongozwa na mbunge wa Kyera (CCM), Dk. Harrison Mwakyembe.

Taarifa za ndani ya kamati zinasema, pamoja na mambo mengine, Kamati imeridhika kwamba Richmond haikuwa kampuni yenye hadhi, uwezo, wala heshima ya kupewa kazi iliyoomba.

Inaelezwa kwamba, Kamati ya Bunge, imeridhika kwamba Richmond nchini Marekani, ni kampuni inayojishughulisha na vifaa vya ofisini, wakati nchini Tanzania inajishughulisha na utoaji huduma za intaneti. Mjadala wa Richmond tayari umepamba moto kila pembe ya nchi, huku wabunge waking'ang'ana kutaka kuwatoa macho wote wanaohusika.

"Kama mjadala utakuwa umekwenda kwa usawa, hakuna mwenye uhakika wa kubaki. Hata Lowassa, anaweza kung'oka," alisema mbunge mmoja wa CCM. Katika hali inayoashiria kwamba mambo yameiva, mwishoni mwa wiki iliyopita, wabunge waligomea semina iliyoandaliwa na Wizara ya Nishati na Madini kwa ajili ya kuwaelimisha kuhusu muswada wa Sheria ya Umeme na Biashara ya Mafuta ya Petroli.

Kwa kauli moja wabunge walishinikiza kwanza waletewe ripoti ya Richmond ili waijadili kabla ya kupitisha mswada huo. Aidha, wabunge walisikika wakisema kwamba hawana imani na uongozi wa wizara hiyo na Tanesco kwa vile "vimejaa uchafu," na kwamba hawawezi kujadili mambo mengine hadi "wahusika wajisafishe."
"Zile za jana (Jumapili iliyopita) zilikuwa salamu za rasharasha.

Kazi kamili inakuja wakati wa kuwasilisha hoja. Safari hii hatutaki tena kutumiwa kama mihuri," alisema mbunge mwingine wa CCM, ambaye alitaka jina lake lisitajwe gazetini. Kujiuzulu kwa mawaziri kutapunguza shinikizo la wanachama wa CCM kwa viongozi wakuu wa chama hicho, hasa rais Kikwete ambaye amekuwa akituhumiwa kulinda mawaziri wake walioboronga.

Naye mbunge wa Karatu (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, akizungumzia mvutano kati ya wabunge wa CCM na mawaziri wao, alisema kwamba kama Karamagi anasoma nyakati alipaswa kujiuzulu mapema. "Kama kujiuzulu, alitakiwa ajiuzulu tangu siku ya semina.

Sura za wabunge zilionyesha wazi kuwa hawamtaki," alisema Dk. Slaa.
 
Nasikia kahamia CHADEMA, huenda kule akausema ukweli woteee
 
conc acid 10:24 Today
Jikumbushe
Lowassa Ngoyai Edward 2008.

"Mheshimiwa Spika, kwanza napenda. kuchukua
nafasi hii kukushukuru sana kwa kunifanya
msemaji wa kwanza katika hoja hii.
Lakini la pili, nimpongeze Dk. Harrison
Mkwakyembe, Mwenyekiti wa kamati Teule kwa
kuwasilisha kwa mbwembwe nyingi sana taarifa
yake, mbwembwe zilikuwa nzuri kweli.

Kwa kazi nzuri kwa maoni yao, wamewasilisha
vizuri. Lakini nimesimama kuweka kwenye
kumbukumbu kutoridhika kwangu na jinsi kazi
hiyo ilivyofanywa.

Mheshimiwa Dk. Mwakyembe
ni Mwanasheria, tena Daktari alikuwa anafundisha
Chuo Kikuu. Moja ya vitu alivyokuwa anafundisha
ni "Natural Justice".
Mheshimiwa Spika, wewe ni Mwanasheria
unafahamu suala la Natural Justice. Kwamba
Kamati Teule imesikiliza watu wengine wote
pamoja na wanaoita minong'ono ya mitaani,
wamesafiri mpaka Marekani kutafuta mashahidi,
lakini mimi ambaye ni mmoja kati ya
watuhumiwa mle hawakunihoji hata siku moja.

Mheshimiwa Spika, nimesimama kueleza
masikitiko yangu. Ofisi ya Bunge mpaka ofisini
kwangu hata kama wangeniita ningekwenda kwa
miguu kama hamna gari na nilikuwa tayari
kufanya hivyo.

Hawa ni watu makini sana siwezi kuamini
kwamba wanaweza wakafanya oversite kama
hiyo. Kwa sababu katika kila hoja walizojenga
wamesema Waziri Mkuu ilikuwa hivi. Kulikuwa na
shida gani kuja kuniuliza Waziri Mkuu wanasema
uliotoa dokezo hili ni sawa sawa kweli? Kulikuwa
na shida gani kwa mfano kufuata utaratibu wa
Westminster kuthibitisha hapo unaposema
mwenye Richmond ni fulani uka-lay on the table
records na ushahidi kuwa ni fulani.

Mheshimiwa Spika, Taifa letu ni Taifa changa,
lakini chombo hiki ndiyo mahali pa demokrasia
pakubwa katika nchi pote, hapa ndipo penyewe.
Kama katika chombo hiki haki haitaonekana
kutendeka nchi yetu haitakwenda vizuri. Hapa
ndipo tunategemea tuwaonyeshe umakini wetu,
umahiri wetu katika mambo ya demokrasia.

Kwa
nhiyo nilichofanyiwa napenda kuweka
kumbukumbu sawa kwamba naona si sahihi,
nimefadhaika sana, nimedhalilishwa sana,
nimeonewa sana katika hili.
Maana zimechukuliwa tuhuma zikaelezwa hapa
kwamba hivi ndivyo ilivyo. Mimi sijauliza.
Kulikuwa na shida gani kuniuliza, kwa nini
muamini minong'ono ya mitaani kuliko maelezo
yangu. Sisi wote hapa ni wanasiasa tukianza
kuamini minong'ono ya mitaani niambieni
mwanasiasa atakayesimama. Hatuwezi, Tume
imepewa muda wa kutosha lakini inashindwa
kumuona mtu ambaye wanamtuhumu na
wanamsema kwa kirefu sana.

Mheshimiwa Spika, lakini hata pale
uliponinong'oneza ukaniambia una ushahidi
wowote? Nilikupa ushahidi huo wa maandishi.
Katika taarifa yao hakuna hata moja ya ushahidi
ambao umetoka Waziri Mkuu. Kile kitabu cha
majedwali kimejaa majedwali mengi pamoja na
magazeti mpaka ya Udaku lakini maelezo ya
Waziri Mkuu hakuna hata moja.
Mheshimiwa Spika, naamini ingekuwa ni heshima
wangeiweka halafu wakasema tunakataa
kitambulisho hiki kwa sababu hii na hii, hiyo
ndiyo imejengwa hoja. Lakini kujenga hoja na
kuja hapa Bungeni tunahutubia nchi nzima na
kusema Waziri Mkuu amefanya hiki, amefanya
hiki bila ya kumsikiliza nachelea kuuliza hivi mtu
wa chini itakuwaje?

Mheshimiwa Spika, lakini nimetafakari kwa
makini sana jambo hili nikajiuliza hivi kulikoni
mpaka watu wazima wenye uwezo wao, watu
maarufu wenye heshima zao, mpaka wafike
mahali waache jambo la msingi kama hilo
kulikoni? Mimi nadhani there is a wish which I
am going to grant, ni Uwaziri Mkuu.
Nadhani
tatizo ni Uwaziri Mkuu. Kwamba ionekane Waziri
Mkuu ndio amefanya haya, tumuondolee heshima
au tumwajibishe.

Mheshimiwa Spika, nimetafakari kwa niaba ya
chama changu, kwa niaba ya Serikali yangu
nimeamua kumwandikia Rais barua ya
kumwomba niachie ngazi. Nafanya hivyo kwa
moyo mweupe kabisa ili kuonyesha dhana ya
uwajibikaji lakini kutokubaliana na utaratibu
uliotumika kusema uongo ndani ya Bunge wa
kumsingizia mtu.

Mheshimiwa Spika, nitumie nafasi hii
kumshukuru sana Rais kwa heshima aliyonipa ya
kutumikia nchi hii kwa Uwaziri Mkuu kwa miaka
miwili. Namshukuru sana Mheshimiwa Rais.

Nakushukuru wewe, nawashukuru Mawaziri na
Manaibu Waziri, nawshukuru Waheshimiwa
Wabunge na wanachama wa CCM tuliyosimamia
Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi.
Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo
nashukuru".
 
Too Late! Alishajiuzulu...no discussion!!
 
Hii hotuba haikuonesha kwamba Lowassa alikuwa defeated bali alionekana kutoridhishwa na mwenendo wa serikali nzima.. Vita rasmi kati ta Lowassa na KITENGO ilianzia hapPa.
 
Jamaa aliumia sana, kwa maelezo haya ni ngumu kuwasamehe!
 
Hotuba kamili

Lowassa Ngoyai Edward 2008.

Mheshimiwa Spika,
kwanza napenda kuchukua nafasi hii kukushukuru sana kwa kunifanya msemaji wa kwanza katika hoja hii. Lakini la pili, nimpongeze Dk. Harrison Mkwakyembe, Mwenyekiti wa kamati Teule kwa kuwasilisha kwa mbwembwe nyingi sana taarifa yake, mbwembwe zilikuwa nzuri kweli. Kwa kazi nzuri kwa maoni yao, wamewasilisha vizuri. Lakini nimesimama kuweka kwenye kumbukumbu kutoridhika kwangu na jinsi kazi hiyo ilivyofanywa. Mheshimiwa Dk. Mwakyembe ni Mwanasheria, tena Daktari alikuwa anafundisha Chuo Kikuu. Moja ya vitu alivyokuwa anafundisha ni "Natural Justice".

Mheshimiwa Spika,
wewe ni Mwanasheria unafahamu suala la Natural Justice. Kwamba Kamati Teule imesikiliza watu wengine wote pamoja na wanaoita minong'ono ya mitaani, wamesafiri mpaka Marekani kutafuta mashahidi, lakini mimi ambaye ni mmoja kati ya watuhumiwa mle hawakunihoji hata siku moja.

Mheshimiwa Spika, nimesimama kueleza masikitiko yangu. Ofisi ya Bunge mpaka ofisini kwangu hata kama wangeniita ningekwenda kwa miguu kama hamna gari na nilikuwa tayari kufanya hivyo.Hawa ni watu makini sana siwezi kuamini kwamba wanaweza wakafanya oversite kama hiyo. Kwa sababu katika kila hoja walizojenga wamesema Waziri Mkuu ilikuwa hivi. Kulikuwa na shida gani kuja kuniuliza Waziri Mkuu wanasema uliotoa dokezo hili ni sawa sawa kweli? Kulikuwa na shida gani kwa mfano kufuata utaratibu wa Westminster kuthibitisha hapo unaposema mwenye Richmond ni fulani uka-lay on the table records na ushahidi kuwa ni fulani.

Mheshimiwa Spika,
Taifa letu ni Taifa changa, lakini chombo hiki ndiyo mahali pa demokrasia pakubwa katika nchi pote, hapa ndipo penyewe. Kama katika chombo hiki haki haitaonekana kutendeka nchi yetu haitakwenda vizuri. Hapa ndipo tunategemea tuwaonyeshe umakini wetu, umahiri wetu katika mambo ya demokrasia. Kwa nhiyo nilichofanyiwa napenda kuweka kumbukumbu sawa kwamba naona si sahihi, nimefadhaika sana, nimedhalilishwa sana, nimeonewa sana katika hili.Maana zimechukuliwa tuhuma zikaelezwa hapa kwamba hivi ndivyo ilivyo. Mimi sijauliza. Kulikuwa na shida gani kuniuliza, kwa nini muamini minong'ono ya mitaani kuliko maelezo yangu. Sisi wote hapa ni wanasiasa tukianza kuamini minong'ono ya mitaani niambieni mwanasiasa atakayesimama. Hatuwezi, Tume imepewa muda wa kutosha lakini inashindwa kumuona mtu ambaye wanamtuhumu na wanamsema kwa kirefu sana.

Mheshimiwa Spika,
lakini hata pale uliponinong'oneza ukaniambia una ushahidi wowote? Nilikupa ushahidi huo wa maandishi. Katika taarifa yao hakuna hata moja ya ushahidi ambao umetoka Waziri Mkuu. Kile kitabu cha majedwali kimejaa majedwali mengi pamoja na magazeti mpaka ya Udaku lakini maelezo ya Waziri Mkuu hakuna hata moja.

Mheshimiwa Spika, naamini ingekuwa ni heshima wangeiweka halafu wakasema tunakataa kitambulisho hiki kwa sababu hii na hii, hiyo ndiyo imejengwa hoja. Lakini kujenga hoja na kuja hapa Bungeni tunahutubia nchi nzima na kusema Waziri Mkuu amefanya hiki, amefanya hiki bila ya kumsikiliza nachelea kuuliza hivi mtu wa chini itakuwaje?

Mheshimiwa Spika,
lakini nimetafakari kwa makini sana jambo hili nikajiuliza hivi kulikoni mpaka watu wazima wenye uwezo wao, watu maarufu wenye heshima zao, mpaka wafike mahali waache jambo la msingi kama hilo kulikoni? Mimi nadhani there is a wish which I am going to grant, ni Uwaziri Mkuu. Nadhani tatizo ni Uwaziri Mkuu. Kwamba ionekane Waziri Mkuu ndio amefanya haya, tumuondolee heshima au tumwajibishe.

Mheshimiwa Spika,
nimetafakari kwa niaba ya chama changu, kwa niaba ya Serikali yangu nimeamua kumwandikia Rais barua ya kumwomba niachie ngazi. Nafanya hivyo kwa moyo mweupe kabisa ili kuonyesha dhana ya uwajibikaji lakini kutokubaliana na utaratibu uliotumika kusema uongo ndani ya Bunge wa kumsingizia mtu.

Mheshimiwa Spika,
nitumie nafasi hii kumshukuru sana Rais kwa heshima aliyonipa ya kutumikia nchi hii kwa Uwaziri Mkuu kwa miaka miwili. Namshukuru sana Mheshimiwa Rais. Nakushukuru wewe, nawashukuru Mawaziri na Manaibu Waziri, nawahukuru Waheshimiwa Wabunge na wanachama wa CCM tuliyosimamia Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi.

Mheshimiwa Spika,
baada ya kusema hayo nashukuru".
 
Back
Top Bottom