Kashfa ya Richmond: Lowassa, Karamagi na Dkt. Msabaha Wajiuzulu

Kashfa ya Richmond: Lowassa, Karamagi na Dkt. Msabaha Wajiuzulu

Kithuku,

..Balozi Kazaura alinukuliwa nje ya kiapo akisema kwamba Richmond ilitokana na shinikizo la "BWANA MKUBWA" na mshirika wake wa kibiashara.

..Hivi ktk Tanzania, bwana mkubwa ni Kikwete au Lowassa?

..Je, ripoti ilielekeza huyu "bwana mkubwa" anayezungumziwa ni nani?

..pia haiwezekani mambo yote haya yakafanyika bila Raisi kuwa na habari nayo.

.. huu ni wizi mkubwa sana wa fedha za umma. nashindwa kuamini Waziri Mkuu atakiuka hata maagizo ya baraza la mawaziri bila "baraka" za Raisi.
Mbona hukumalizia ile paragraph? labda kwa kukumbusha tu ilisema ni mradi wa bwana mkubwa, akimaanisha PM na mshirika wake Rostam. Labda ungeniambia kuwa Balozi Kazaura kakataa kwa kuwekewa maneno mdomoni, otherwise stop that non sense talk about the issue.
 
Inaelekea kweli kuna ujanja hapa, kwa nini hakuhojiwa Lowassa? Kwa maelezo ya Dr Mwakyembe, hawakupata sababu za kumhoji Lowassa ati kwa kuwa waliomtaja walifanya hivyo nje ya kiapo! Lakini je, hao wote waliohojiwa ni kutokana na kutajwa ndani ya kiapo? Hakuna waliohojiwa kutokana na tetesi tu ili kuthibitisha madai yaliyotolewa? Ukisoma ripoti ile utagundua wengi tu walihojiwa kutokana na kutuhumiwa hata kama tuhuma hizo zilikuwa nje ya kiapo, na wengine ni kutokana na nafasi zao katika wizara na idara husika.

Nakuja na hypothesis hii: Dr Mwakyembe alikuwa na maelekezo rasmi kuwa asimhoji Lowassa. Dr Msabaha kasema "bangusilo", pengine Lowassa angekuja na neno lake la kimasai ambalo lingekuwa na athari zaidi?
Sina hakika na kauli yako. Unaweza ukajiuliza kwanini PM hakuitwa kwenye mahojiano na kamati. Lakini sina hakika kama unawezaje kuconclude kuwa PM kwa kuwa tu hakuitwa basi kaonewa?
 
Mbona hukumalizia ile paragraph? labda kwa kukumbusha tu ilisema ni mradi wa bwana mkubwa, akimaanisha PM na mshirika wake Rostam. Labda ungeniambia kuwa Balozi Kazaura kakataa kwa kuwekewa maneno mdomoni, otherwise stop that non sense talk about the issue.

I agree with you. ripoti imesema kabisa kwamba bwana mkubwa ni PM, na mshirika ni Rostam.

Rostam Rostam Rostam - hili ndilo fisadi kuu, kama Lowassa ni kichwa, Rostam ndiyo engine. Inabidi awajibishwe ipasavyo. tukimalizana na Richmonduli inabidi kuanza kumshughulikia Chenge, Yona, na swahiba wao "Mkapa" - Jambazi baba lao
 
Mimi siwaelewi wanaompongeza Lowasa kwa kujiuzulu. Fedha aliyoowaibia Watz ni nyingi. Hivyo badala ya kumpongeza Sheria ichukue mkondo wake ili angalau Walalahoi tupate nafuu ya bili ya Umeme. Karamagugu bado Mkataba wa Buzwagi ni jinamizi linalosubiri kukumeza, You have nowhere to run.
 
Mafuchila,

..OK..na-concede kwamba sikuisoma paragraph nzima. kwamba ilielekezwa kwamba "bwana mkubwa" ni Edward Lowassa.

..Lakini bado suala linabaki palepale. Hivi Lowassa na Rostam wataingilia suala nyeti kama hili bila Raisi kuwa na taarifa?

..Tume inaelekeza kwamba maagizo mengine yalikuwa yanakiuka maamuzi ya cabinet. sasa nani alikuwa anampa ruhusa Lowassa kukiuka maagizo ya cabinet?
 
Mbona hukumalizia ile paragraph? labda kwa kukumbusha tu ilisema ni mradi wa bwana mkubwa, akimaanisha PM na mshirika wake Rostam. Labda ungeniambia kuwa Balozi Kazaura kakataa kwa kuwekewa maneno mdomoni, otherwise stop that non sense talk about the issue.

Hapa JF hakuna non-sense wala sense.Tudhibiti jazba na tujibu hoja kwa hoja.

Nafikiri kwa mtu yeyote akiisoma hii ripoti lazima atabaini tu kuwa haiwezekani Mawaziri hawa wakiuke maagizo ya baraza la mawaziri bila ridhaa ya Rais.Kwa jinsi ninavyofahamu kikao cha baraza la mawaziri mwenyekiti wake ni Rais.

Pia huwezi kushindwa kuhusisha ikulu kwa vile kipindi hicho Rais mwenyewe aliwahi kusema katika kampuni zote zilizoomba tenda Richmond na Aggreko ndizo zilizokuwa bora maelezo ambayo kamati imebaini ni uongo.Haiingii akilini kwamba baada ya TANESCO,PPRA kukataa kwamba Richmond haina sifa yeye hakupewa taarifa.

Kitu kingine kinachomleta karibu Rais ni kuhusishwa kwa rafiki yake mkubwa Lowasa na Rostam Aziz.

Pia tukumbuke kuwa kuna gazeti la kenya liliripoti mapema kuhusika kwa Lowasa Richmond akishirikiana na mtoto wa Rais kwa hiyo kitendo cha Rais kufumbia macho Richmond inaweza ikawa sio bahati mbaya ingawa uchunguzi zaidi unahitajika.

Siku si nyingi tutafahamu zaidi kuhusu ushiriki wa watu hawa.
 
Sina hakika na kauli yako. Unaweza ukajiuliza kwanini PM hakuitwa kwenye mahojiano na kamati. Lakini sina hakika kama unawezaje kuconclude kuwa PM kwa kuwa tu hakuitwa basi kaonewa?

Sijatamka mie kuwa Lowassa kaonewa, hebu soma tena maneno yangu. Ninachosema ni kuwa nahisi kuna ajenda ya siri katika kutokuhojiwa kwake, pengine naye "bangusilo"!
 
Huu uwe ni mwanzo tu, sasa sheria ifuate mkondo wake! Ingekuwa ni vigumu sana kwa kamati kumuhoji PM ndio maana kila siku tunasema kiongozi yeyote akihusihwa na kashfa aachie ngazi ili kupisha uchunguzi.

Wengi tumekuwa tukilia na Mkapa, inaonekana JK anamuonea haya japokuwa madhambi yake anayajua sasa sijui hapa kwa swahiba wake itakuwaje? Kujiuzulu tu haitoshi, je ataweza kumkoma nyani giladi? Yangu macho.
 
Hapa JF hakuna non-sense wala sense.Tudhibiti jazba na tujibu hoja kwa hoja.

Nafikiri kwa mtu yeyote akiisoma hii ripoti lazima atabaini tu kuwa haiwezekani Mawaziri hawa wakiuke maagizo ya baraza la mawaziri bila ridhaa ya Rais.Kwa jinsi ninavyofahamu kikao cha baraza la mawaziri mwenyekiti wake ni Rais.

Pia huwezi kushindwa kuhusisha ikulu kwa vile kipindi hicho Rais mwenyewe aliwahi kusema katika kampuni zote zilizoomba tenda Richmond na Aggreko ndizo zilizokuwa bora maelezo ambayo kamati imebaini ni uongo.Haiingii akilini kwamba baada ya TANESCO,PPRA kukataa kwamba Richmond haina sifa yeye hakupewa taarifa.

Kitu kingine kinachomleta karibu Rais ni kuhusishwa kwa rafiki yake mkubwa Lowasa na Rostam Aziz.

Pia tukumbuke kuwa kuna gazeti la kenya liliripoti mapema kuhusika kwa Lowasa Richmond akishirikiana na mtoto wa Rais kwa hiyo kitendo cha Rais kufumbia macho Richmond inaweza ikawa sio bahati mbaya ingawa uchunguzi zaidi unahitajika.

Siku si nyingi tutafahamu zaidi kuhusu ushiriki wa watu hawa.

Wakati huo huo tunasahau kwamba huyo mwakilishi wa kampuni ya Richmond hapa Bongo ilibidi awe na mkutano na Rais mwenyewe ana kwa ana wakati mambo yalipozidi kuwa mazito. Hakuna msafi hapa, bali wanaoangukia kisu ndio hivyo tena, tunaendelea na safari.
 
1. Jamani wana JF, PM alijua kuwa alikuwa gumzo la nchi juu ya kuibeba RDC. na ndiyo maana, hata aliweza kulijibu gazeti la This Day juu ya story yao iliyokuwa based on PPRA findings bila hata yeye PM kuulizwa na gazeti.

2. Public hearing ya kamati ya Dr Mwakyembe iliitisha Public hearing kwa yeyote mwenye taarifa muhimu juu ya RDC.

3. Kufuatia hili, PM kama mtu anayekereketwa na haya mambo, ni wazi angekimbilia kutoa taarifa anazozijua juu ya RDC ili ajaribu kujisafisha. Hakufanya hivyo, akatulia tuli pengine akijua hii itakuwa utetezi wake.

4. Juu ya PM kufanya maamuzi juu ya Rais, ikumbukwe kuwa kiaina huyu jamaa yuko powerful zaidi ya JK kwa rungu la pesa. Alimsaidia sana wakati wa kampeni ya kumweka madarakani.
 
Wakati huo huo tunasahau kwamba huyo mwakilishi wa kampuni ya Richmond hapa Bongo ilibidi awe na mkutano na Rais mwenyewe ana kwa ana wakati mambo yalipozidi kuwa mazito. Hakuna msafi hapa, bali wanaoangukia kisu ndio hivyo tena, tunaendelea na safari.

Atajiju,kwani yeye hakujua kuwa hiyo kamati ipo wazi kwa ajili ya watu wote? Kama yeye alikuwa na taarifa kuwa ni "Bangusilo" alishindwa nini kwenda kutoa hayo maelezo.

Katika tarifa pia hakuna malezo yanayosema kulikuwa na vinote au simu au maelekezo toka ofisi ya Rais.

Tunajua JK si msafi lakini kwa mujibu wa ripoti hii hakuna muunganisho wa yeye kuhusika.
 
Swali langu kubwa kwa Kikwete ni kwamba - Je hakuyaona haya all this time? haya mambo yameanza since 2006. Wananchi na magazeti wamepiga kelele since 2006, yeye kama kiongozi aliyechaguliwa na watanzania alikuwa wapi? au aliamua tu kuangalia upande mwingine?
Kama angeyashughulikia haya mambo toka 2006 hao mafisadi wake aliowakumbatia wasingekuwa wameiba hela zote hizo. Hilo pekee ni kosa kubwa tu

Mawsali ya kujiuliza ni kwamba Kikwete alijua nini? Na wakati gani?

Kwa wachunguzi hii issue inamhusisha hata Kikwete naye, kwa sababu kama alijua imekuwaje akaiachia? Kama hakujua imekuwaje yeye kama Head of State na CEO wa nchi asijue?

Rais Harry S Truman wa Marekani alikuwa na kibao mezani mwake kimeandikwa "The Buck Stops Here" akimaanisha yeye ndiye lawama zote zinaishia kwake, Je Kikwete ilikuwaje upuuzi huu unaendelea bila wewe kujua? Au unahusika na wewe?
 
Rais akubali kuondoka kwa Waziri Mkuu

Taarifa za hivi punde kutoka Dodoma, mji mkuu wa Tanzania zasema Rais Jakaya Kikwete amekubali barua ya kujiuzulu kwa Waziri Mkuu Edward Lowassa kufuatia madai ya kashfa.

Akitangaza hatua yake katika bunge Alhamis asubuhi, Bwana Lowassa alisema: "Nimetafakari sana kwa niaba ya chama changu, kwa niaba ya serikali yangu, nimeamua kumwandikia Rais barua ya kumuomba niachie ngazi."

Mawaziri wengine wawili wamefuata nyayo zake Waziri Mkuu wa Tanzania Edward Lowassa na kuamua kujiuzulu baada kuhusisha na kashfa ya ufisadi mkubwa.

Sakata hiyo inahusu zabuni iliyotolewa kwa kampuni ya Richmond kuzalisha megawati 100 za umeme wa dharura.

Mawaziri wengine walioomba kujiuzulu ni Nazir Karamagi wa Nishati na Madini pamoja na mwenzake wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ibrahim Msabaha.

Bwana Lowassa aliteta kwamba kamati teule ya bunge iliyomhusisha na kashfa ya Richmond ilimnyima haki ya kujieleza.

Alisema alikuwa ametafakari kwa makini kuhusu shutuma hizo na kufikia uamuzi kwamba, "tatizo ni uaziri mkuu."

"Kwamba ionenekane Waziri Mkuu ndiye amefanya haya, tumwondolee heshima au tumwajibishe."

Akielezea hatua yake ya kujiuzulu, Bwana Lowassa aliongeza "ninafanya hivyo kwa moyo mweupe kabisa ili kuonyesha dhana ya uajibikaji na pia kutokukubaliana na utaratibu uliotumika kusema uongo ndani ya bunge kwa kumsingizia mtu."

Zabuni hiyo ilipewa kampuni ya Richmond Development group yenye makao yake nchini Marekani.

Kamati teule ya bunge kwenye ripoti yake iliyowasilishwa hapo Jumatano, ilipendekeza kujiuzulu au kuchukuliwa hatua kali kwa wahusika.

Ripoti hiyo iliwasilishwa bunge na Mwenyekiti wa kamati hiyo teule, Harrison Mwakyembe.

Kuhusu Waziri Mkuu, ripoti hiyo inasema: "Uamuzi wa serikali kuizuia Tanesco ( Shirika la umeme Tanzania) isivunje mkataba na kampuni hiyo licha ya sababu zote za kisheria kuwepo ni baadhi tu ya viashiria vya nguvu kubwa iliyojuu ya wizara ya nishati na madini."

"Kutokana na ushahidi wa kimaandishi, kimazingira na wa kimdomo inaiona nguvu hiyo kuwa ni Waziri Mkuu."

Kikatiba ndiye mwenye madaraka ya juu ya udhibiti, usimamiaji na utekelezaji wa siku hadi siku wa kazi na shughuli za serikali.

Yeye pia ndiye kiongozi wa shughuli za serikali bungeni.
"Kamati teule haikufurahishwa hata kidogo na taarifa hizo zinazomgusa moja kwa moja Mheshimiwa Waziri Mkuu katika kuipendelea Richmond."

Mawaziri wengine walioshutumiwa katika ripoti hiyo ni yule anayehusika na nishati na madini, Nazir Karamagi, mtangulizi wake Dr. Ibrahim Msabaha ambaye sasa ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa takukuru, ilikuwa motoni kwa kutoa maelezo ya uongo kwa kamati hiyo.

Mbunge Mwakyembe alisema kamati yake ilitaka kuweka wazi kwamba mchakato wa zabuni ya kuzalisha nguvu za umeme kwa dharura wa megawati 100 ulighubikwa na vitendo vya ukiukwaji taratibu, kanuni na sheria za nchi."

"Na hivyo kujenga kiwingu cha mashaka ya upendeleo, ubadhirifu na rushwa ambavyo vimechangia kumwongezea mwananchi mzigo wa gharama za umeme."

Taifa lilikuwa limetumbukizwa kwenye hasara kubwa kutokana na mkataba huo wa Richmond kinyume na taarifa iliyotolewa na Takukuru (taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa).

Kwa nini kamati ya wataalamu haikuihoji Richmond kuhusu uongo huo bayana? Ilishutumiwa kwa kujiharibia sifa yenyewe baada ya kutoa ushahidi wa uongo ikisema mchakato wa zabuni hiyo ulikuwa wazi, shirikishi na ulizingatia kanuni na kwamba dosari zilizojitokeza hazikuhitimu kuiletea taifa hasara.

"Taarifa hiyo imemong'onyoa kwa kiasi kikubwa hadhi na heshima ya chombo hiki muhimu cha kitaifa kilichopewa dhamana ya kupambana na rushwa na siyo kuipamba ili kurejesha heshima ya umma katika taasisi hiyo."

Mbunge Harrison alisema kwenye tovuti yake, kampuni ya Richmond "ilikuwa inajitangaza kimataifa kipindi hicho kuwa kampuni yenye miradi mikubwa Tanzania ya ujenzi wa kiwanja cha kisasa cha michezo, ujenzi wa bomba la mafuta la kilomita 1150 na ukarabati wa viwanja kadhaa vya ndege nchini."

Kamati teule ilishindwa kuelewa "kwa nini kamati ya wataalamu haikuihoji Richmond kuhusu uongo huo bayana ambao uliokuwa ushahidi wa kutosha kuipotezea sifa za kuwa mzabuni?"

Chanzo: BBC Swahili
 
Siku za mwizi zikifika ndio hivyo tena. Tunataka serikali iwafikishe mahakamani kujibu tuhuma ambazo zinawakabili na wakiwa guilt wafilisiwe mali zao zilizo Tanzania na nje ya nchi ili iwe fundisho. Wachunguzwe kwa undani biashara zao na kuona kwamba wanalipia kodi kwa mujibu wa sheria. Hatuwezi kuwaachia wale keki ya taifa na kufaidi.

Kundi lote la mafisadi ni lazima liondoke hatutakubali waendelee kula pension yao wakati wametolewa au kujiuzulu kwa kulifilisi taifa ni wakati mzuri wa wabunge kubadili sheria kuwathibiti wezi ambao tumekuwa tunawasema kila siku, wezi wa kuku wanafungwa hawa Je? Vipi muuaji DITO? Nani anamlinda?

JK hakuwa hata na ubavu wa kuwafukuza inabidi Bunge liwe makini na viongozi kama hawa wenye uchu wa madaraka na kujitajirisha kwa haraka haraka kwa mgongo wa walipa kodi.

BRAVO JF BRAVO ALL MEMBERS KWA KUMKOMA NYANI GILADI BILA KUMWONEA HAYA.

NEXT IMPEACHMENT
 
Atajiju,kwani yeye hakujua kuwa hiyo kamati ipo wazi kwa ajili ya watu wote? Kama yeye alikuwa na taarifa kuwa ni "Bangusilo" alishindwa nini kwenda kutoa hayo maelezo.
Katika tarifa pia hakuna malezo yanayosema kulikuwa na vinote au simu au maelekezo toka ofisi ya Rais.
Tunajua JK si msafi lakini kwa mujibu wa ripoti hii hakuna muunganisho wa yeye kuhusika.

Kwa mtizamo wako, Rais kutomkemea au kutomwajibisha waziri mkuu wake anapomwona anafanya makosa, mpaka asubiri kamati ya uchunguzi; huo ni uongozi imara?
 
Mawsali ya kujiuliza ni kwamba Kikwete alijua nini? Na wakati gani?

Kwa wachunguzi hii issue inamhusisha hata Kikwete naye, kwa sababu kama alijua imekuwaje akaiachia? Kama hakujua imekuwaje yeye kama Head of State na CEO wa nchi asijue?

Rais Harry S Truman wa Marekani alikuwa na kibao mezani mwake kimeandikwa "The Buck Stops Here" akimaanisha yeye ndiye lawama zote zinaishia kwake, Je Kikwete ilikuwaje upuuzi huu unaendelea bila wewe kujua? Au unahusika na wewe?

Swali gumu sana hili ndugu yangu...

tik tak tik tik tak................
 
Kwa mtizamo wako, Rais kutomkemea au kutomwajibisha waziri mkuu wake anapomwona anafanya makosa, mpaka asubiri kamati ya uchunguzi; huo ni uongozi imara?

Hiyo ndiyo demokrasia...Innocent until proven guilty.
 
Mawsali ya kujiuliza ni kwamba Kikwete alijua nini? Na wakati gani?

Kwa wachunguzi hii issue inamhusisha hata Kikwete naye, kwa sababu kama alijua imekuwaje akaiachia? Kama hakujua imekuwaje yeye kama Head of State na CEO wa nchi asijue?

Rais Harry S Truman wa Marekani alikuwa na kibao mezani mwake kimeandikwa "The Buck Stops Here" akimaanisha yeye ndiye lawama zote zinaishia kwake, Je Kikwete ilikuwaje upuuzi huu unaendelea bila wewe kujua? Au unahusika na wewe?

Pundit,

JK yote anayajua but he decided just kwenda through Tume ya Bunge ili kutafuta sababu ya kumtema! Inaonekana JK anajua mengi hata ITPL na EPA ila naona hataki tena haya mambo yaendelee- analeta mabadiliko bila yeye kuonyesha directly anahusika! Wengi wa CCM wanahusika -ila anaona aende taratibu!

Yawezekana JK kama yeye sii fisadi, ila system na waliomzunguka siyo safi, na wengi ni rafiki zake anawaonea huruma!

At the end may be JK ana nia njema- maana angalia ni yeye alisema repoti ya CAG ijadiliwe, ni yeye aliruhus EPA BoT ichunguzwe n.k.

Ni tofauti na Mkapa! Huenda JK ana nia njema! Taabu yake ni urafiki na ushkaji saa ingine vinamfanya anashindwa chukua hatua za haraka!

Pia anataka harmony ktk nchi na haswa CCM. Unajua ukianza kukamata watu wengi sana wakati mmoja- then unajenga maaduai na kushindwa kuongoza!

We wait and see!
 
Siku za mwizi zikifika ndio hivyo tena. Tunataka serikali iwafikishe mahakamani kujibu tuhuma ambazo zinawakabili na wakiwa guilt wafilisiwe mali zao zilizo Tanzania na nje ya nchi ili iwe fundisho. Wachunguzwe kwa undani biashara zao na kuona kwamba wanalipia kodi kwa mujibu wa sheria. Hatuwezi kuwaachia wale keki ya taifa na kufaidi.

Kundi lote la mafisadi ni lazima liondoke hatutakubali waendelee kula pension yao wakati wametolewa au kujiuzulu kwa kulifilisi taifa ni wakati mzuri wa wabunge kubadili sheria kuwathibiti wezi ambao tumekuwa tunawasema kila siku, wezi wa kuku wanafungwa hawa Je? Vipi muuaji DITO? Nani anamlinda?

JK hakuwa hata na ubavu wa kuwafukuza inabidi Bunge liwe makini na viongozi kama hawa wenye uchu wa madaraka na kujitajirisha kwa haraka haraka kwa mgongo wa walipa kodi.

BRAVO JF BRAVO ALL MEMBERS KWA KUMKOMA NYANI GILADI BILA KUMWONEA HAYA.

NEXT IMPEACHMENT

Impeachment inaandaliwa na inaonekana Lowasa ndio atawasilisha mswada bungeni ili amwage mboga baada ya wao kumwaga ugali..
 
Back
Top Bottom