Kashfa ya Vitol (2026): Inahusu tuhuma za ufisadi na upandaji holela wa bei za mafuta nchini Tanzania. Inadaiwa kuwa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) lilipewa zabuni na kisha kuikabidhi kampuni ya Uswisi ya VITOL katika mazingira ya utata, na kusababisha nchi kulipa gharama kubwa zaidi ukilinganisha na nchi jirani. Hii nayo inaenda kuwa moja ya kashifa kubwa kuwahi kutokea nchini ambayo inahusisha familia ya Rais mstaafu na aliyepo madarakani.
Kashfa ya Richmond (2006): Ilitikisa nchi baada ya kubainika kuwa kampuni hewa ilipewa mkataba wa kuzalisha umeme wa dharura na kusababisha hasara kubwa, jambo lililosababisha aliyekuwa Waziri Mkuu wakati huo, Edward Lowassa, na mawaziri wengine kujiuzulu.
Kashfa ya Escrow (2013): Ililenga uchotaji wa zaidi ya Shilingi bilioni 300 kutoka kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ikihusisha viongozi mbalimbali wa serikali na wafanyabiashara.
Kashfa ya EPA - Tangold (2006): Wizi na ufisadi mkubwa uliofanywa na wafanyabiashara kupitia Akaunti ya Malipo ya Nje (External Payment Arrears) iliyokuwa Benki Kuu.
Kashfa ya Rada (1999): Ilihusu ununuzi wa rada ya kijeshi kutoka kampuni ya Uingereza ya BAE Systems kwa gharama ya dola za Marekani milioni 40. Ununuzi huu ulikuwa na utata mkubwa tangu mwanzo kufuatia mashirika kama Benki ya Dunia kuonya kuwa rada hiyo ilikuwa ya gharama kubwa na isiyofaa kwa matumizi ya kiraia.
Kashfa ya Lugumi (2016): Sakata lililohusu mkataba tata wa vifaa vya utambuzi wa alama za vidole katika vituo vya polisi uliohusisha mabilioni ya fedha za walipa kodi.
Kashfa ya Makinikia (2017): Inahusu mzozo mkubwa wa kiuchumi na kisheria kati ya Serikali ya Tanzania na kampuni ya madini ya Acacia Mining (kwa sasa inamilikiwa na Barrick Gold Corporation) kuhusu usafirishaji wa mchanga wenye madini (makinikia) nje ya nchi.
Kashifa zingine kubwa kwa Tanzania ni BOT Twin Towers, Loliondo.