Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Usafiri wa dalaldala ndio usafiri mkubwa na unaotumika na kundi kubwa la raia katika nchi yetu ya uchumi wa kati na hivyo huwakutanisha watu wa aina mbalimbali pamoja kwa muda fulani iwe ni kuelekea kazini, nyumbani, hospitalini, kwenye usahili, kwa michepuko, kwa marafiki n.k
Kwa sababu ya kuwakutanisha watu wengi tofauti pamoja, kuna watu ni wastarabu sana na hujitahidi kusafiri bila kuleta karahaa na makwazo kwa wengine ila pia kuna wasio wastaarabu, mateja na walevi ambao huweza kuleta kero na kuifanya safari fupi kuwa yenye kuchosha sana, hawa ni wale ambao huongea kwa sauti kwenye simu gari zima, kulalia mabega ya abiria wenzao, wasiotaka kusogea kabisa wakiwa wamesimama, wabambiaji, madereva wanaofungulia mahubiri ya dini zao bila kujali kwamba watu katika gari lake ni wa dini tofauti
Watu wanaokutana katika daladala inabidi kuvumuliana sana wakati mwingine. Kuna mtu akikanyagwa kidogo tu ananuna, anasonya au kufoka bila kujua wote ni maskini na mafukara ndio maana mko wote hapo.
Kero, adha, vimbwanga na vituko gani vingine vya daladala umewahi kukutana navyo kutoka kwa abira mwenzako,kondakta au dereva mwenyewe?