Kasi ya kuzaa kwa Wasichana wadogo Mkoa wa Lindi inahitaji Ufumbuzi kwani taifa linaangamia

Ukitoa Arusha na Kilimanjaro,jamii nyingine ndani ndani huko kumechoka saaaaana
Elimu inahitajika
 
Na wazungu wako hivo hivo hususani wingereza wanazaa mapema akifika 23yrs tayari hataki ndoa anataka kutalii tu.
Tofauti ya wao na sisi ni kipato. At 17 mtoto ameshaanza kuondoka nyumbani na kuwa na kipato ambacho ni sustainable, mtu ana career, ana kwake ana usafiri hata kama wa kawaida. Miaka 25-30 wanatafuta kukuza career au kubadili kabisa.

Njoo huku, miaka 27 watu wengi tu bado maisha hayaeleweki sembuse mtu awe mzazi na aweze kulea, kulipa ada etc 😅
 
Watoto wanautaka wenyewe...Huku Kusini sasa kama hujui watu hawazai watoto wengi ila Wanawake wanazaa mapema...akishakuwa na mtoto Mmoja basi hazai na wala haolewi...ndio muda wa kupiga show za Ndondo
Ni kweli na mimi nilitaka kusema hivyo hivyo kule wanazaa mapema lakini hawazai watoto
wengi na ndio maana population ya mkoa wa Lindi na hata Mtwara ipo chini.

Ni watumiaji wazuri sana wanjia za kisasa za uzazi wa mpango wengine tangu wakiwa
shule ya msingi nalo hili ni lakutazamwa.
 
Tanzania mzima hali ni hiyo hiyo aisee
Ni katika mazingira gan hasa hii hali ni serious? Rural context au urban slums?. Suluhu hapo ni kuongeza mikakati wezeshi kwa vijana mana iliyopo haitoshi na nina uhakika hili tatizo limefungamana na umaskini. Na kwa kawaida tatizo lolote likifungamana na umaskin haliomdoki mpaka umaskini uondoke (Norcela & Jamrozik 1998)
 
Lawama kwa vijana wenu wasiokuwa na maadili
Wanaharibu vitoto vya miaka hata 10 bila aibu
Msichana anapewa machungwa au mihogo akatembeze ( kosa) anakutana na jitu zima linataka mapenzi na katoto
Anakapa mimba kwa elfu 3 shame on you
Washenzi wasiokuwa na maadili
Usilaumu wasichana
 
Hao mbona wameelimika sana. Seems haujatembea vya kutosha katika hiyo nchi .
Hiyo nchi intervention zipo nyingi sana ila zinachangia kupofua macho jamii badala ya kuzielimisha, takwimu zinazotolewa ni za uongouongo tu kubabae (kumbe kbabae inaruhusiwa humu ndiy maana haiaweka vinyotanyota ili kuficha, sasa kuanzia sasa mtanikoma kubabae zenu) . Nenda Singida, maeneo wanaishi wasukuma. Huko mtoto wa miaka 13 hadi 15 mimba ni kitu cha kawaida sana.
Sijjauona huo uzi wa Arusha. Ningechangia kitu. Ila Arusha ni pkifala zaidi. Arusha watoto wa kike wapo salama mara 80 kuliko watoto wa kiume. Ukiwa una mtoto wa kiume Arusha hadi Moshi ni sawa na kulala mlango wazi wakati una mali ndani.
Kesi nyingi za ubakaji Arushi ni wanaum kulawitiwa, nadra kukuta mwanamke amebakwa, (sisemi wanawake wabakwe), Moshi hawabaki ila wanajilewea zao halafu wanaenda kupinduana.
 
Fanya utafiti wako vizuri,hii hali ya wasichana kuzalishwa ovyo kwa sasa ni karibu nchi nzima,na nina mashaka sana na hizi takwimu za Ukimwi za mwaka huu kama sio za kupika,zinaa inafanywa hovyo sana siku hizi na watu hawajali...
 
Utawala ndo shida na raia wamebweteka kwahiyo no body to blame
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…