Kassim Majaliwa amekutana na Waziri Mkuu wa Côte d’Ivoire, Robert Beugre Mambe Jijini Abidjan

Kassim Majaliwa amekutana na Waziri Mkuu wa Côte d’Ivoire, Robert Beugre Mambe Jijini Abidjan

President of China

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2018
Posts
34,781
Reaction score
94,550
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekutana na Waziri Mkuu wa Côte d’Ivoire, Robert Beugre Mambe na kujadiliana nae masuala ya kidiplomasia, kiuchumi, teknolojia, kilimo na michezo kwenye kikao kilichofanyika ofisini kwa mwenyeji wake, Boulevard Angoulvant Plateau, Jijini Abidjan.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema hayo leo May 14,2025 ambapo amesema lengo la kikao chao lilikuwa kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia lakini pia kuhimiza haja ya nchi hiyo kushirikiana na Tanzania kwenye masuala mbalimbali ikiwemo utafiti na teknolojia za kisasa kwenye kilimo.

“Côte d’Ivoire ina Wakazi zaidi ya milioni 81 na inaongoza kwa kilimo cha kakao, korosho na michikichi, hawa wanalima korosho zaidi kuliko Tanzania, na sisi tunalima korosho kwenye Mikoa ya Pwani na kakao kule Mbeya na maeneo mengine, tunaweza kujifunza kwao na sisi tunaiona hii ni fursa kwetu ya kuongeza uzalishaji kwenye mazao haya”

“Kakao ni zao kuu la biashara na linawaingiza fedha nyingi za kigeni, tumekubaliana kuwa Mawaziri wetu wa kilimo wakutane na waangalie ni maeneo gani ya kuweka mikataba ikiwemo utafutaji wa masoko na masuala ya utafiti”
 
Back
Top Bottom