Kassim Majaliwa ameshindwa kumsaidia Rais?

Kassim Majaliwa ameshindwa kumsaidia Rais?

Status
Not open for further replies.

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Waziri mkuu Kassim Majaliwa amekuwa ni mtu mwenye kauli zenye makeke mengi lakini outcome ni kidogo sana.

Leo hii rais anazungumzia kuhusu madudu bandarini, lakini ikumbukwe kuwa yeye siyo wa kwanza kugundua madudu ya huko, infact hata Kassim Majaliwa kipindi cha Magufuli anrwahi kugundua ufisadi wa huko, na mbele ya Camera akaonyesha kukasirishwa sana na yanayotendeka huko. Je mbona madudu huko bandarini yanaendelea?
Je Majaliwa anataka milage ya kisiasa aonekane anafanya kazi lakini kumbe hakuna cha maana kinachoendelea?

Waziri Mkuu amewahi kutoa kauli za kuwajibishwa wale wote waliotajwa katika ripoti ya CAG, Je ni hatua gani zilichukuliwa, iweje leo rais aagize Takukuru kuchukua hatua wakati ni. jukumu lao?

Waziri mkuu amewahi kutueleza juu ya uchunguzi wa kuungua soko la kariakoo, Je ripoti iko wapi?, Nani anahusika na ni nani keshafikishwa mahakamani?

Mbona utendaji kazi wa Waziri mkuu kwenye Camera ni mkubwa kuliko. matunda halisi ya makeke yake tunayoyaona daily kwenye TV?

Je hii Tabia ambayo waziri mkuu aliianza ya kusema Samia ataendelea hadi mwaka 2035 ililenga kumfanya Samia asimuone kama mshindani wake wa kimyakimya na hivyo kurelax juu ya utendaji wake wa kazi(PM)?

Haiwezekani vitu vinapanda bei kila kukicha halafu waziri mkuu yuko yuko tu, haya ndiyo mambo tuliyopaswa kumuona waziri mkuu anahaingaika. Yuko wapi waziri mkuu kutoa briefings kwa umma juu ya mikakati ya kila siku ya serikali kupambana kupunguza ukali huu wa maisha?
 
Waziri mkuu yupo busy na ziara zisizo na manufaa labda kwa wengine mnaziona.

President mwenyewe ni safari nje ndani na hii ni Maana halisi ya Kazi iendelee.
 
Ila pm akiwa anasisitiza Jambo unaweza uombe ardhi ipasuke udumbukie!
Anatumia tekniki ileile ya Magufuli akiwa waziri, ufanyaji kazi mbele ya Camera ili upendwe na wananchi, kumbe bebind the scene misala tupu.
Ni tekniki pia iliyompa umaarufu mrema wakati huo akiwa waziri enzi za Mwinyi.

Mama aanze na kubwa lao, abadili PM Asap
 
Waziri mkuu yupo busy na ziara zisizo na manufaa labda kwa wengine mnaziona.

President mwenyewe ni safari nje ndani na hii ni Maana halisi ya Kazi iendelee.
Rais hajawahi fanya ziara zisizo na tija wala kufanya mazungumzo yasiyo na maana .

Alishazifanya Sana hizo ziara kabla ya kuingia Serikalini kwa hiyo sio mshamba kama wewe.

Moja ya matokeo ya ziara na Kazi za Rais ni haya hapa 👇

3016496_BA2BC087-B043-497B-92C5-82D5C04D74BD.jpeg

Screenshot_20211119-082914.png

3018505_Screenshot_20211201-065711.png
 
Kuna wale wa Wizara ya fedha walikula mamilioni kama sio Mabilioni Mei Mosi 2021, alifoka sana nikajua hela zitarudi kujengea Madarasa!! Hadi sasa funika Kombe mwanaharamu apite Lol!!!!
 
majaliwa ni kiongozi imara sana,shida ni back up.
 
Namshauri mama avunje baraza la mawaziri aanze upya...kuna team magufuri hii ndio inamnyima usingizi mama yetu...
 
TLS walimshauri na kutoa waraka unaothibitisha ushauri wao umo katika mafungamano ya katiba inambidi aunde baraza jipya la mawaziri. Yeye akaendelea na baraza alilorithi. Pengine alikuwa anasubiria wakati mzuri sijui.

Anachonishangaza analia lia jambo ambalo naona ni upuuzi. Kama yeye haiwezi hiyo kazi awape watu hizo kazi yeye asubiri matokeo tu.
 
tatzo kaingia kibusura wakt nchi ilikuw inapelekwa kisugu na mzee baba , kwahyo watu hawana cha kuogopa tena nazn mama anahitaji afanye mapinduz ya kimfúmo wa viongz

Apge chin wotee na katb mpy n muhm

Sent from my vivo 2015 using JamiiForums mobile app
 
Waziri mkuu Kassim Majaliwa amekuwa ni mtu mwenye kauli zenye makeke mengi lakini outcome ni kidogo sana.

Leo hii rais anazungumzia kuhusu madudu bandarini, lakini ikumbukwe kuwa yeye siyo wa kwanza kugundua madudu ya huko, infact hata Kassim Majaliwa kipindi cha Magufuli anrwahi kugundua ufisadi wa huko, na mbele ya Camera akaonyesha kukasirishwa sana na yanayotendeka huko. Je mbona madudu huko bandarini yanaendelea?
Je Majaliwa anataka milage ya kisiasa aonekane anafanya kazi lakini kumbe hakuna cha maana kinachoendelea?

Waziri Mkuu amewahi kutoa kauli za kuwajibishwa wale wote waliotajwa katika ripoti ya CAG, Je ni hatua gani zilichukuliwa, iweje leo rais aagize Takukuru kuchukua hatua wakati ni. jukumu lao?

Waziri mkuu amewahi kutueleza juu ya uchunguzi wa kuungua soko la kariakoo, Je ripoti iko wapi?, Nani anahusika na ni nani keshafikishwa mahakamani?

Mbona utendaji kazi wa Waziri mkuu kwenye Camera ni mkubwa kuliko. matunda halisi ya makeke yake tunayoyaona daily kwenye TV?

Je hii Tabia ambayo waziri mkuu aliianza ya kusema Samia ataendelea hadi mwaka 2035 ililenga kumfanya Samia asimuone kama mshindani wake wa kimyakimya na hivyo kurelax juu ya utendaji wake wa kazi(PM)?

Haiwezekani vitu vinapanda bei kila kukicha halafu waziri mkuu yuko yuko tu, haya ndiyo mambo tuliyopaswa kumuona waziri mkuu anahaingaika. Yuko wapi waziri mkuu kutoa briefings kwa umma juu ya mikakati ya kila siku ya serikali kupambana kupunguza ukali huu wa maisha?
Hawa watu wanatofautiana msimamo. Mfano ile issue ya sukari, PM na Waziri wake wanaweka misimamo wanaambulia kuitwa nonsense.
 
Wanakuambia kuna Majaliwa wawili katika mwili mmoja.

Kuna Majaliwa wa serikali ya awamu ya5, ambaye kila ziara za kikazi alizozifanya popote, mafisadi na watendaji wa hovyo aliwaacha na majeraha yasiyopona na aliogopeka na kuheshimika sana!

Watu walikuwa wanasema, ni aheri kwenye ziara ukutane na Magufuli na siyo Kassim, simba dume likiunguruma hadi nyasi zinapeperuka, akisema amesema na hatua madhubuti za kinidhamu na kisheria zinachukuliwa kweli!

Majaliwa wa pili kaanzia figisu kwenye ugonjwa wa hayati kutuhadaa raia kwamba mwamba yupo "fisically fit" anachapa tu mzigo hataki maneno na mtu, kumbe...!

Sasa tangu awamu ya6 ishike madaraka, amekuwa ni mtu wa kufoka tu bila kuchukua hatua yoyote ile.

Na awamu hii ziara za mfululizo ni za Ruangwa, kunani Ruangwa!

Alivyofariki Magufuli hatukukufuru Mungu tukisema hajatuacha pabaya, tunalo jembe letu litakalotusukuma mbele, kumbe tulikuwa tunajidanganya pakubwa, binadamu siyo wa kuwaamini hadi ukabweteka, wa kumwamini ni Mungu pekee!

Kwenye awamu ya5 ilikuwa kila ukipima mawazo ya watu kuelezea nani anaweza kuwa chaguo sahihi baada ya rais Magufuli kumaliza muda wake, wengi walikuwa wanajibu kwa matumaini makubwa kwamba ni Majaliwa!

Ninadhani kuna agenda ya siri iliyopo moyoni mwake kwa sasa iliyombadilisha ghafla kumgawa na kutokea Majaliwa wawili wenye sura moja na mwili mmoja, ambayo sisi raia hatuwezi kuijua!

Lakini uzuri ni kwamba, jambo lolote la hila lifanywalo na mtu hata kwa kuigiza wema, binadamu werevu hulihisi na kuling'amua haraka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom