Kassim Majaliwa: Makontena ya Makinikia yanayosafirishwa nje ya nchi ni halali

Bunge rubber stamp la vibajaji na sukumagu halina ubavu wa kuhoji hayo madudu.

Sent from my G80 using JamiiForums mobile app
 
Yale mliyoyakamata ikasemekana yalikuwa na vito vingi vya thamani kubwam je yapo wapi? je vito hivyo vimeshachenjuliwa na kukutwa na thamani gani halisi?

Ni vema wananchi wakapata mrejesho !!
 
Halafu hajui hapa hapa kuna watanzania plant metallurgists....anatuchukulia laymen wote.

Huyu Majaliwa kisha zoea kutulisha matango pori haaminiki!! Jiwe alituaminisha kuwa ili kujua nini kimo kwenye makinikia ni lazima yapitishwe kwenye SMELTER ndio utayajua madini mengine yaliyomo zaidi ya dhahabu!! Sasa yeye kutuambia kuwa makinikia yanapimwa na kujua composition ya madini mengine huo ni utaalam tofauti na ule wa jiwe?

Moja ya sababu ya JIWE kuweka condition ya kuwa SMELTER lazima ijengwe nchini, ilikuwa ni kuweza kuthibiti wizi huo wa madini ambao Majaliwa anatuambia umehalalishwa sasa!!!
 
Kwenye hili la kusafirisha mchanga bila kujua kilichomo, take it from me, tunaendelea kupigwa!.
P
 
kwahiyo huyu ndo yule mzalendo anayepigiwa makofi kule fb baada la kuwasimamisha watumishi wa wizara ya fedha,kwamba ndo anamuenzi mwendazake
 
Halafu shida ni kwamba udongo wa Shinyanga hauna tu dhahabu kuna madini mengine(maana pale Bulyanhulu a.k.a Twiga ndo mabingwa wa kusafirisha makinikia), kama copper. Sasa yeye hata basics za chemical engineering anazo kutoa majibu ya harakaharaka hata bila kuwashirikisha wataalam?

Hivi kama makinikia content ya madini ni minimal, mbona kila siku migodi inapiga kelele kuhusu wavamizi wanaoiba 'vipiece' vya vifusi?
 
t
tumeanza kupigwa tukae mkao wa kulia.
 
Hakuna cha ajabu,makinikia hata Yale ya mwanzo yalishaondoka na hatuambiwi lini,yalipelekwa wapi,faida tuliyopata hadi sasa na pia smelters zipo wapi?Hivi sasa tunapeleka mchanga ghafi,vipi tumetosheka na ajira?
 
Hakuna cha ajabu,makinikia hata Yale ya mwanzo yalishaondoka na hatuambiwi lini,yalipelekwa wapi,faida tuliyopata hadi sasa na pia smelters zipo wapi?Hivi sasa tunapeleka mchanga ghafi,vipi tumetosheka na ajira?
 
nimependa mstari wa mwisho,jioni yangu itakuwa njema sana kwa kizungu wanasema you made my evening 😀 ....thanks Jasmoni Tegga
 

..Magufuli na Kabudi ndio walioruhusu makinikia kusafirishwa nje.

..Pia walikubali kuachana na madai ya usd 191 billion wakaamua tulipwe kishika uchumba cha usd 300 million, tena kidogo kidogo.

..Vilevile walisaini mkataba kuruhusu migogoro baina ya Tz na Barrick kuamuliwa na mahakama za nje ya Tz.

..Mnaomlaumu Majaliwa mnamuonea na kumsingizia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…