Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Watanzania badala ya kulilaumu Jeshi la Polisi kuhusika na matukio ya utekaji na mauaji, ni vema wakajiuliza kwanini matukio hayo yanatokea kila inapokaribia wakati wa uchaguzi.
Waziri Mkuu amesema hayo leo Jumatatu Septemba 16, 2024 katika Baraza la Maulid lililofanyika kitaifa mkoani Geita.
Majaliwa amesema tangu awamu ya tatu, nne, tano na sasa awamu ya sita, matukio ya aina hiyo yamekuwa yakitokea hususan kipindi cha kukaribia uchaguzi na kwamba jamii inapaswa kujitafakari na kujiuliza kwanini matukio hayo hutokea kwenye kipindi kama hicho.
“Rais alitoa karipio juu ya yanayotokea, matukio haya yanatokea kila kipindi fulani, lazima tujiulize kwanini yanajitokeza hasa inapokaribia uchaguzi. Nani anafanya, ni rahisi kusema polisi, ni muhimu tukatafakari kwanini wakati huu na nani anafanya” amesema Majaliwa.
Majaliwa amesema Jeshi la Polisi pekee haliwezi kulilinda Taifa, hivyo ni wajibu wa kila mwananchi kulinda usalama wa nchi na kusema Serikali itaendelea kuhamasisha wanachi kulilinda Taifa na kuifanya nchi kuwa imara kwa kutambua viashiria vya matukio yanayovunja amani na utulivu.
PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atoa majibu ya matukio ya kupotea na utekaji watu yanaendelea Nchini