Pre GE2025 Kassim Majaliwa: Tujiulize kwanini matukio ya uuaji na utekaji yanatokea karibu na uchaguzi

Pre GE2025 Kassim Majaliwa: Tujiulize kwanini matukio ya uuaji na utekaji yanatokea karibu na uchaguzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Watanzania badala ya kulilaumu Jeshi la Polisi kuhusika na matukio ya utekaji na mauaji, ni vema wakajiuliza kwanini matukio hayo yanatokea kila inapokaribia wakati wa uchaguzi.
Naye anatakiwa ajiulize...
•Jeshi la polisi toka lianzishwe limeshuhudia/kushiriki chaguzi ngapi?
• Je, kazi ya jeshi la polisi ni nini?
• Kama mheshimiwa Rais Dr Samia ameshazungumza kuhusu jeshi la polisi, yeye anazungumza vipi haya?
 
Inaskitisha kiongozi ambaye ndiye mtendaji washughuli zaserikali anatutaka ss wananchi kuanza kufikiri kwanini utekaji na mauwaji yanatokea kipindi Cha kuelekea uchagizi badala ya kukomesha vitendo hivi kwakweli watanzania tinachukuliwa poa kwa sabbu ya uoga wetu ktk nchi zenye uwajibikaji alitakiwa awe amekwisha kuachia ngazi
 
Mtuhumiwa kujikamata ni ngumu Sana. Tuazime vyombo vya uchunguzi nje ya nchi ili tuchunguzwe kuanzia raia, viongozi, vyama na vyombo vyetu vyote. Kati ya haya makundi Kuna mmoja anahusika moja kwa moja
 
Huyu alitakiwa kutupatia majibu, lakini naye anauliza maswali.

Mwaka 2020 kwenye jimbo la uchaguzi alilokuwa anagombea Majaliwa, mgombea wa CHADEMA na wapambe wake, walitekwa na kuumizwa vibaya, halafu mkurugenzi akamtangaza haraka kuwa yeye Majaliwa amepira bila kupingwa.

Atuambie kwa uzoefu wake, alifanyaje kuhakikisha wapinzani wake wanatekwa na kuumizwa. Atuambie kama alitumia polisi au aliwalipa majambazi ya mtaani.
 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Watanzania badala ya kulilaumu Jeshi la Polisi kuhusika na matukio ya utekaji na mauaji, ni vema wakajiuliza kwanini matukio hayo yanatokea kila inapokaribia wakati wa uchaguzi.

Waziri Mkuu amesema hayo leo Jumatatu Septemba 16, 2024 katika Baraza la Maulid lililofanyika kitaifa mkoani Geita.

Majaliwa amesema tangu awamu ya tatu, nne, tano na sasa awamu ya sita, matukio ya aina hiyo yamekuwa yakitokea hususan kipindi cha kukaribia uchaguzi na kwamba jamii inapaswa kujitafakari na kujiuliza kwanini matukio hayo hutokea kwenye kipindi kama hicho.

“Rais alitoa karipio juu ya yanayotokea, matukio haya yanatokea kila kipindi fulani, lazima tujiulize kwanini yanajitokeza hasa inapokaribia uchaguzi. Nani anafanya, ni rahisi kusema polisi, ni muhimu tukatafakari kwanini wakati huu na nani anafanya” amesema Majaliwa.

Majaliwa amesema Jeshi la Polisi pekee haliwezi kulilinda Taifa, hivyo ni wajibu wa kila mwananchi kulinda usalama wa nchi na kusema Serikali itaendelea kuhamasisha wanachi kulilinda Taifa na kuifanya nchi kuwa imara kwa kutambua viashiria vya matukio yanayovunja amani na utulivu.

PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atoa majibu ya matukio ya kupotea na utekaji watu yanaendelea Nchini

Si tuitishe uchunguzi huru kama lengo ni kujua shida ilipo?

Scotland yard mbona mapema asubuhi tu wanaruka na mtu?
 
kwanini matukio hayo yanatokea kila inapokaribia wakati wa uchaguzi.

Majibu yanaweza kuwa yafuayo :


DOLA KUGONGANISHA BONGO ZA RAIA KWA MAKUSUDI, KIASI KILA MMOJA ANAJIPINGA MWENYEWE NDANI YA NAFSI YAKE NA KUISHIA KTK MKWAMO
1726505809057.png


Kugonganisha maoni ya raia kwa kuwapa taarifa nzuri za mafanikio ya serikali kupata waliopotea na kuendelea kukanusha hakuna wanaoshikiliwa mikononi mwa vyombo vya dola vya serikali


NDIMI MBILI (Doublethink) ni mchakato wa makusudi kufanya raia ambapo wahusika katika nchi wanatarajiwa kukubali kwa wakati mmoja dhana mbili zinazokinzana kuwa ukweli, mara nyingi kinyume na kumbukumbu zao au hisia za ukweli.

Kufikiri mara mbili kunahusiana na matukio katika jamii, lakini wakati huohuo akili yako hutofautiana na, unachosikia kweli au si kweli hivyo kuishia kulipuuza jambo .

George Orwell alibuni neno doublethink kama sehemu ya lugha ya kubuniwa ya mkakati maalum waliobuni lugha yao ya kipekee yaani Newspeak katika riwaya yake ya dystopian ya 1949 ya Nineteen Eighty-Four . Katika riwaya, chimbuko lake lugha hii mpya ya walio katika mamlaka kwa,ndani ya raia halieleweki; ilhali inaweza kuwa kwa kiasi fulani zao la programu rasmi za mamlaka kufubaza bongo za raia Big Brother za uoshaji ubongo , [ i ] riwaya hiyo inaonyesha kwa uwazi watu wakijifunza kufikiri mara mbili wenyewe na lugha mpya ya Newspeak kutokana na shinikizo la mamlaka huwa taarifa zao ni za kweli na nia za "kufaa", au ukikubali basi kupata hisani ya hadhi ndani ya Chama—Tawala . kuonekana kama Mwanachama mwaminifu wa Chama.

Katika riwaya hii, kwa mtu hata kutambua—achilia mbali kutaja—mkanganyiko wowote ndani ya muktadha wa mstari wa msimano wa bunge, mahakama, serikali na Chama kongwe dola tawala ni sawa na kukufuru , na inaweza kumfanya mtu huyo kuchukuliwa hatua za kinidhamu na kutoidhinishwa papo hapo kijamii na Wanachama wenzake.
 
Taifa limepoteza mwelekeo...waziri mkuu amekuja na mdomo wazi hivyo
rasimi naunga mkono maandamano ya chadema
 
Ben Sa8, Azory Gwanda, Roma Mkatoliki, n.k walitekwa ama kuuawa wakati uchaguzi unakaribia?

Huyu pm Majaliwa hatoshi kabisa. Usikute kalikumbuka lile tukio lake la utekaji wa mgombea ubunge Jimbo la Ruangwa kwa tiketi ya chadema ili asirudishe fomu kwa wakati 2020 , ndiyo anadhani matukio yote yalitokea muda huo
 
Serikali kwanini hamtaki kufanya uchunguzi ikiwemo ni nani walimpiga risasi Tundu Lissu

16 September 2024
Dar es Salaam, Tanzania

'Matokeo ya Uchunguzi kuhusu kupigwa kwangu risasi bado mpaka leo'


View: https://m.youtube.com/watch?v=Wyj6BKIAWAs

Mwandishi wa BBC Leonard Mubali amefanya mahojiano na makamu mwenyekiti wa CHADEMA taifa mheshimiwa Tundu Lissu na kuzungumza masuala mbalimbali ikiwemo kushikiliwa kwa viongozi wao kinyume cha sheria, matukio ya utekaji pa moja na uchunguzi dhidi ya tukio la kuupigwa risasi miaka michache iliyopita huko Dodoma ktk nyumba za viongozi zinazolindwa saa 24 kwa siku ...
 
Back
Top Bottom