Na bado anataka Ubunge kuna usalama huko ??Kasimu Majaliwa alishiriki kuteka kila Mgombea wa Upinzani 2020 ili kujihakikishia Kupita bila kupingwa, Mmoja wa wagombea wa Jimbo lake aliokotwa Mkuranga akiwa Hoi huku anavuja damu, Nani amesahau mambo haya na nani atamsikiliza na kumwamini?
Toa mifano miwili tu tuone unachosema kama ni sahihiChadema wamesababisha maumivu kwa watu wengi tu mifano ipo labda unaamua kupotezea au hufahamu ila wenzako wanafahamu.
Naye anatakiwa ajiulize...Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Watanzania badala ya kulilaumu Jeshi la Polisi kuhusika na matukio ya utekaji na mauaji, ni vema wakajiuliza kwanini matukio hayo yanatokea kila inapokaribia wakati wa uchaguzi.
Na yeye anashangaa na sisi tunamshangaaSasa kama ana jibu kwanini asilete jibu badala ya kutuongezea maswali
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Watanzania badala ya kulilaumu Jeshi la Polisi kuhusika na matukio ya utekaji na mauaji, ni vema wakajiuliza kwanini matukio hayo yanatokea kila inapokaribia wakati wa uchaguzi.
Waziri Mkuu amesema hayo leo Jumatatu Septemba 16, 2024 katika Baraza la Maulid lililofanyika kitaifa mkoani Geita.
Majaliwa amesema tangu awamu ya tatu, nne, tano na sasa awamu ya sita, matukio ya aina hiyo yamekuwa yakitokea hususan kipindi cha kukaribia uchaguzi na kwamba jamii inapaswa kujitafakari na kujiuliza kwanini matukio hayo hutokea kwenye kipindi kama hicho.
“Rais alitoa karipio juu ya yanayotokea, matukio haya yanatokea kila kipindi fulani, lazima tujiulize kwanini yanajitokeza hasa inapokaribia uchaguzi. Nani anafanya, ni rahisi kusema polisi, ni muhimu tukatafakari kwanini wakati huu na nani anafanya” amesema Majaliwa.
Majaliwa amesema Jeshi la Polisi pekee haliwezi kulilinda Taifa, hivyo ni wajibu wa kila mwananchi kulinda usalama wa nchi na kusema Serikali itaendelea kuhamasisha wanachi kulilinda Taifa na kuifanya nchi kuwa imara kwa kutambua viashiria vya matukio yanayovunja amani na utulivu.
PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atoa majibu ya matukio ya kupotea na utekaji watu yanaendelea Nchini
Na hilo nalo mkalitizameYaani anataka tujiulize ili iweje sasa! badala ya kuunda tume huru ya kuchunguza na kuwabaini wahusika wote wa hivyo vitendo!
Yaan tuwalipe mishahala halafu inapotokea kazi wanataka tufanye woteViongozi wetu bwana .
Yaani hapo anataka sisi wananchi tukae tujulize wakati hapo tayari anayo dhamana yetu ya ku act.
kwanini matukio hayo yanatokea kila inapokaribia wakati wa uchaguzi.
Kwa hii kauli yake ndugu yangu PM alipaswa awe ameachia ngazi ama kwa kuondoshwa ama yeye mwenyewe kujiuzulu.Jukumu la serikali ni kulinda usalama wa raia wake..serikali lazima iwajibike
Usipende sana kuishi kwa mifano ;Toa mifano miwili tu tuone unachosema kama ni sahihi