Pre GE2025 Kassim Majaliwa: Tujiulize kwanini matukio ya uuaji na utekaji yanatokea karibu na uchaguzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
CCM wana vituko

CCM wanaviuko sana...walikuwa wanamfagilia mama haui watu kama Magufuli, sasa mama anafanya ya Magufuli eti wanajifanya kushangaa nani anafanya vitendo hivi....Tanzania nzima inamjua anayehusika na huu unyama
 
Sijamwelewa Kabisa Waziri Mkuu.
1:Hivi Maswali haya ya kutuuliza sisi Wananchi Kweli Wakati yeye ndiye Mtendaji Mkuu wa Serikali?
Haijalishi ni Wakati Gani, Serikali inatakiwa kuchukua hatua na kukomesha matukio ya Utekaji na Mauaji bila kujali nani kafanya hivyo kwakuwa huo ni ukiukwaji wa Sheria za nchi
2:Serikali inatakiwa kuhakikisha kuwa Watu,vikundi au magenge yanayofanya uhalifu huu yanabainika na yanakemewa na hatua zichukiliwe, Waziri Mkuu anatakiwa kusimamia hilo kwakuwa ndiye Mtendaji Mkuu serikalini
 
Tangu aliposema Rais ni mzima na anachapa kazi kumbe si kweli, huwa simuelewi kabisa Mtu huyu. Halafu anataka kuendelea 2025 badala kuwaachia vijana nafasi yeye akalee wajukuu.
 
..Na kwanini wanaouawa ni wapinzani, Ccm wao hawauwawi?

..Pia kwanini jeshi la Polisi huwa halichunguzi, au kukamata wahusika?
Wake kumi kwa mganga dodoma walikua wapinzani?.. wapinzani wangapi wameuawa?
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Watanzania badala ya kulilaumu Jeshi la Polisi kuhusika na matukio ya utekaji na mauaji, ni vema wakajiuliza kwanini matukio hayo yanatokea kila inapokaribia wakati wa uchaguzi.
Kama yeye anajua uhusiano wa uchaguzi na vifo jeshi lake limefanya nini kukabiliana na hali hiyo?
 
Duh,kwamba chadema wanauana kisa madaraka? Hii nchi kweli mtihani basi
 
wanauana wenyewe kwa wenyewe
 
Wake kumi kwa mganga dodoma walikua wapinzani?.. wapinzani wangapi wameuawa?

..tunapozungumzia utekwaji na mauaji ya wanasiasa.

..kwanini wanaotekwa na kuuwawa ni wapinzani peke yao?

..Na siku zote, wanaotekwa, na kuuwawa, ni wale wanakotokea chama cha upinzani chenye nguvu ktk kipindi husika.

..wakati Cuf wana nguvu, makada wao wengi walitekwa, na kuuwawa. Cuf ilipodhoofika hali ikawa Shari.

..kipindi hiki ambapo Chadema ndio chama cha upinzani chenye nguvu, tunashuhudia matukio ya utekwaji,na mauaji, yakikiandama chama hicho, kuliko vyama vingine.
 
Huyo ndio prime Minister. Ukiona kwenye familia mtoto analalamika, Mama analalamika na baba nae analalamika

Ujue hiyo familia haina dira

Anyway …. Watanzania mtajua wenyewe na nchi yenu ; Napenda kuwafahamisha Rasmi nimepata uraia wa Canada

Nilipewa machaguo mawili yaani niikane nchi moja wspo ; wala sikufikiria mara mbili …. Nimeipiga chini Tanzania.

Pambaneni kuijenga nchi yenu, mm kwa sasa ni mtz kiasili tu lakini sio mtanzania Tena.
 
Huyu jamaa kachoka kuwaza, kumbe ndiyo maana kaletewa naibu. Kati ya wananchi na Jeshi la Polisi, ni nani anayetakiwa kujiuliza kwanini matukio ya mauaji huongezeka nyakati za kukaribia chaguzi?

Jeshi la Polisi halikutakiwa kujiuliza sasa, ila ilitakiwa kutumia swali hilo kama njia ya kutafuta suluhu. Siyo kutaka wananchi wawaonee huruma Jeshi la Polisi. Wao ndiyo wazuiaji uhalifu kwa mafunzo na zana.

Sasa huyu jamaa anasema hivi ili iweje? Wananchi wasilalamike na wakubali tu kupoteza wapendwa wao kwa kuwa ni kawaida nyakati za chaguzi matukio ya mauaji huwa yanaongezeka?

Ova
 
Ukisubiri Majaliwa aongee kitu cha maana utakuwa disappointed.

Huyu jamaa hata sijui ilikuwaje kuwaje!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…