Pre GE2025 Kassim Majaliwa: Tujiulize kwanini matukio ya uuaji na utekaji yanatokea karibu na uchaguzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Matukio haya yanatokea ni kwa sababu Wananchi wengi zaidi katika nchi hii hawaitaki CCM, na kwa upande mwingine CCM nayo ilazimisha kupendwa kwa lazima baada ya kugundua kwamba imepoteza mvuto wa kuweza kuendelea kupendwa na Watu.
 
Ni Majaliwa huyu huyu aliyekuwa anavikwa cheo cha 'ajaye' ndiye katamka haya maneno toka kinywani pake!

Yaani raia tujiulize badala ya kupewa taarifa mahsusi za kweli za kiuchunguzi juu ya tuhuma nzito zinazoelekezwa kwenye Serikali yake kama boss wake alivyoagiza, leo yeye anakuja na hoja muflisi za namna hii kweli!

Jukumu la Polisi ni lipi kikatiba?

'Wananchi kujilinda na kulinda' kauli hii inamaanisha nini kimantiki?

Katika viongozi pendwa wa moyo wangu katika Serikali ya awamu ya 5 alikuwa ni huyu jamaa, lakini katika awamu hii kila mTz anamshangaa kala maharage ya wapi yaliyombadilisha hadi haiba!

Sipendi kusikiliza hotuba yake yoyote, hata hii clip sijaifungua kujiepusha kujazwa jazba na chuki kutokana na matamshi yake ya uongo na yenye muelekeo wa kutetea Polisi watekaji na wauaji.

Angalao angelikuja na blah blah kama za Nchimbi kidogo angelishusha kwa asilimia fulani kiwango cha hasira za raia wanaoendelea kupotea na kupoteza ndugu na marafiki zao kila siku iitwayo 'leo' bila ya Serikali kutoa majibu ya suluhisho la tatizo hilo.

Lakini kwa upande mwingine nina shaka sana na kauli yake hii kuitoa kwa kipindi hiki, maana kiongozi mwandamizi wa ngazi yake ni lazima awe anawajua wauaji kwa majina na aliyewatuma.

Nadhani kaja kwa nia ya kukoleza hasira mioyoni mwa watu huyu.

Iweje kauli yake kimantiki ipingane na kauli ya katibu mkuu wake wa Ccm tena kaitoa juzi tu?
 
Kuna mtu naona kaweka X kwamba itakuwa ni vizur Sasa tupate ukwel kutoka kwa wachunguzi huru wanaoaminika..

Kwenye kujiuliza majibu ni muhim na yatoke kwenye chanzo huru..

Kauli nzuri sana Muheshimiwa
Ni nani ameyatamka hayo?
 
Huyu naye ni mbumbumbu.
Hivi polisi wameshindwaje kutoa ripoti ya watu kutekwa, kupotea na kuyawa?.
Kwani wanaowatuma polisi si ndio hao hao walioko madarakani na wengi wao wanagombea nafasi mbalimbali?.
Sijaona waziri mkuu mwenye IQ ndogo kama huyu.
 
Camouflage kwa sana tu. Kuna watu wanafanya kwa maslahi yao wakijua lawama itabebeshws serikali
Na serikali inashindwa kung'àmua hilo? Na kwa nini inashindwa kuleta wachunguzi huru wachunguze bila kuegemea upande wowote. Inasita sita WHY? Jaribu kufanya wewe kwa maslahi yako kama hujakamatwa ndani ya 24hrs, sasa hili kwa nini halitatuliwi, kesi ya lisu kwa nini inashindikana? Jibu. mpaka hapo nani kafanya ulishalipata.
 
Huyu naye ni mbumbumbu.
Hivi polisi wameshindwaje kutoa ripoti ya watu kutekwa, kupotea na kuyawa?.
Kwani wanaowatuma polisi si ndio hao hao walioko madarakani na wengi wao wanagombea nafasi mbalimbali?.
Sijaona waziri mkuu mwenye IQ ndogo kama huyu.
Kuhamisha magori uwanjani si kazi ndogo.
 
Serikali ndio wanao watuma hao wanao teka watu na kuuwa kila uchanguzi unapo karibia . Halafu badae wanauda tume kuchuguza kazi ilivyo fanyika. Report wanakaa naye ile wahusika wapandishwe vyeo.
 
Badala ya kuja na majibu, naye kwa level yake anataka wananchi tujiulize. Siangejiuzulu tu kama hawezi kuwalinda raia?
 
Majaliwa angetueleza kwanza nani alimteka mgombea Ubunge wa Chadema jimbo la Ruangwa wakati anarudisha form hadi ikapelekea yeye Majaliwa akakosa mpinzani na kupita bila kupingwa? Huyu naye ni mhalifu kwani yeye ndiye alikuwa mnufaika wa utekaji huo hivyo Polisi kama wangekuwa fair wangeanza na yeye.
 
Nani alitekwa cuf?
 
Siasa za wanasiasa!
 
Kwanini mnawatafuta watu wema miongoni mwa waliooza?
 

Uchaguzi ulopita jimboni kwake Ruangwa palikuwa na tukio la Kutekwa na kuteswa kwa mgombea wa ACT wazalendo, alitupwa maeneo ya Rufiji porini akiwa na Hali mbaya.

Mgombea alikuwa kutoka Kijiji Cha Nangumbu,alisoma Secondary ya Kigonsela alimaliza kidato Cha 4 mwaka 1980.
Mwaka ambao Mh Waziri Mkuu alimaliza pia kidato Cha nne,yawezekana alikuwa class mate wake, na Kuna uwezekano ni kabila Moja anaitwa Mmuya.


Mpaka Leo watekaji haeajulikani.

Kubwa zaidi alikataa msaada wa matibabu Kwenda India.

Mwamba Mmuya anaishi DSM!! Ndugu zake wamemwambia aache Siasa.
 
Yaani anataka tujiulize ili iweje sasa! badala ya kuunda tume huru ya kuchunguza na kuwabaini wahusika wote wa hivyo vitendo!
Ajabu kweli hata hawajitambui kwamba majukumu yao ni yapi na hiyo mishahara yao wanapokea ili iweje badala yake ni kama genge fulani hivi teuliwa!
 
Hapo hata kwa akili ndogo tu kama ya Lucas Mwashambwa unaweza kutambua ni nani aliwatuma watekaji ili apite bila kupingwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…