Kassim Majaliwa: Wanasiasa waeleze yale watakayoyafanya kwenye kampeni na sio kubeza yaliyofanywa na wengine

Asipangie watu cha kuongea kwenye kampeni. Kila siku tunasikia rais wetu akibeza mambo ya hovyo yaliyofanyika awamu zilizopita, ni kwanini yeye awazuie watu wengine kuyasema ya hovyo ya awamu hii? Inaonekana awamu hii inataka kampeni zifanyike kwa utashi wa rais aliye madarakani.
Niupumbavu sana watawala kutaka wote tuipe pambio zao
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wanasiasa kufanya kampeni za kistaarabu mara kampeni za uchaguzi mkuu zitakapofunguliwa ili kuepuka vurugu zinazoweza kusababisha uvunjifu wa amani nchini.

Akizungumza katika ibada ya siku kuu Eid Al Adha Jijini Dar es Salaam, Majaliwa amesema kuwa ni muhimu kwa wanasiasa kueleza yale waliyopanga kuwasaidia wananchi kuliko kubeza yale yaliyofanywa na wengine na kukashfu.

“Tujiepushe na lugha za uchochezi, tujiepushe na lugha za bezo, tujiepushe na lugha za kashfa kazungumze kile ambacho utawatendea wananchi” amesema Majaliwa

Waziri Mkuu pia amewashukuru viongozi wa dini kwa kuendelea kuimarisha amani na mshikamano nchini kwa kutoa mawaidha mazuri yenye lengo la kujenga jambo ambalo limekuwa msaada mkubwa kwa Taifa.

Akielezea kuhusu hayati Benjamini Mkapa ,amesema kuwa waislamu watamkumbuka kwa kuanzisha Chuo Kikuu cha waislamu kwa kutoa majengo ya Serikali na kukabidhi kwa waislamu na hivyo kuanzishwa kwa Chuo Kikuu hicho kilichopo mjini Morogoro.

Ippmedia.com
mmechota hela za umma mmenda kununua korosho,،halafu mkala hasara ,hizo bilioni 600,zingetosha kupeleka MADAWA nchi nzima,mmezitupa kwenye korosho nyinyiiiiiiiii
 
Wacha wabeze mkuu...kiongozi gani wa siasa hapendi criticism?
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wanasiasa kufanya kampeni za kistaarabu mara kampeni za uchaguzi mkuu zitakapofunguliwa ili kuepuka vurugu zinazoweza kusababisha uvunjifu wa amani nchini.

Akizungumza katika ibada ya siku kuu Eid Al Adha Jijini Dar es Salaam, Majaliwa amesema kuwa ni muhimu kwa wanasiasa kueleza yale waliyopanga kuwasaidia wananchi kuliko kubeza yale yaliyofanywa na wengine na kukashfu.

“Tujiepushe na lugha za uchochezi, tujiepushe na lugha za bezo, tujiepushe na lugha za kashfa kazungumze kile ambacho utawatendea wananchi” amesema Majaliwa

Waziri Mkuu pia amewashukuru viongozi wa dini kwa kuendelea kuimarisha amani na mshikamano nchini kwa kutoa mawaidha mazuri yenye lengo la kujenga jambo ambalo limekuwa msaada mkubwa kwa Taifa.

Akielezea kuhusu hayati Benjamini Mkapa ,amesema kuwa waislamu watamkumbuka kwa kuanzisha Chuo Kikuu cha waislamu kwa kutoa majengo ya Serikali na kukabidhi kwa waislamu na hivyo kuanzishwa kwa Chuo Kikuu hicho kilichopo mjini Morogoro.

Ippmedia.com
Mheshimiwa tunaelekea kubaya,nasema kubaya iwapo mwanasiasa mpinzani anachaguliwa jambo la kusema na mtawala,kusema azungumzie atakayofanya bila kubeza yaliyofanyika imekaakaaje hii?nitasemaje nitaboresha shirika bila kueleza kasoro kwa aliyetangulia kujenga shirika?nitajengaje SGR vizuri bila kuonyesha kasoro kwa huyu aliyejenga hii SGR?au si ndio kubeza huko?
 
Back
Top Bottom