Kassim Majaliwa: Watanzania tufanye maamuzi ya kuingia kwenye kilimo na mifugo

Kassim Majaliwa: Watanzania tufanye maamuzi ya kuingia kwenye kilimo na mifugo

Aisee...

Umasikini wetu, hautokaa ututoke..

1. Madini anaachiwa mzungu
2. Gas kapewa mzungu na mchina
3. Viwanda ni magodown na stand za mabus.

4. Reli anatafutiwa mwarabu.

5.Usafirishaji wanabaki DART, UBER nk.

Wakati viongoz wanaendelea kulima kwenye kodi zenu, sisi tukalime vumbi na kuchunga mbugani.

Mkuu, Kuna maeneo mahsusi ya Kilimo na Ufugaji yametengwa kwa kazi hiyo?

Kilimo cha mvua na ufugaji wa migogoro...

Au yale yale ya Bashe ya kilimo cha Hector 1 kwa dolla elf 8?

mtalia hadi mkome, nothing will happen.
 
Tokea tumepata hii nchi imepata uhuru watu wanalimaga tu.. ko muheshimiwa kinachohitajika ni kilimo cha kisasa serikali ifikirie kuwekeza kwenye kilimo na zana za kisasa sio hizi mboyoyo za Kilimo kwanza
Sijui kilimo ni uti wa mgongo sijui nini...
 
Sisi tujikite kwenye extractive industry, bandari wapewe waarabu.
Tukachunge ngombe na kufunga nguruwe waarabu wake mjini.
Good idea maana kwenye kilimo na ufugaji huwezi kufukuzwa kazi.
 
Asilimia kubwa sasa hivi wanafanya nini ?

Au na sisi twende tukafanye wanachofanya ? Nadhani ungewaambia hao wenzako wafanye maamuzi ya kuwatafutia masoko ya uhakika hawa wakulima
 
Stori zilezile za
Siasa ni kilimo
Kilimo cha kufa na kupona
Kilimo ni uti wa mgongo
Kilimo kwanza

Tukaja viwanda kwanza
Waziri mkuu anasema turudi kwenye kilimo.

Maneno meengi kwa miaka 60, utekelezaji Sifuri.
Tunaenda mbele tunarudi nyuma.
Safari hii Bandari kwanza.
 
hii kauli alitakiwa aiongee Pinda, amekuwa mkulima mzuri sana wa zabibu, maembe, samaki n.k, sio huyu katelefoni. muda ufike tu tusiwe tunamwona kwenye tv. astaafu tu na dp world yao.
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Watanzania kuingia na kubobea kwenye kilimo, mifugo na uvuvi, akisema kuwa hilo ndilo eneo litakaoleta uchumi wa mtu mmoja mmoja na wananchi wote kwa ujumla.

Kauli hiyo ameitoa jana Agosti 3, 2023 baada ya kukagua mabanda ya maonesho ya nanenane kitaifa kwenye viwanja vya John Mwakangale, jijini Mbeya, ambapo ameongeza kuwa ilani ya Chama cha Mapindunzi (CCM), imeagiza Serikali kuhakikisha inafanya kila namna ili kila Mtanzania akingie sekta ya uzalishaji kisha aamua kuzalisha ama kwa matumizi yake au kibishara.
Wenyewe walikimbilia siasa halafu wenzao ndiyo waende kwenye Kilimo?
Walitakiwa watengeneze mazingira na unafuu kwenye Kilimo, lakini si kuwaambia watu waende kwenye Kilimo.
Waanze klna wakulima waliopo , hawatatumia nguvu kushawishi watu kwenda
 
kubobea kwenye kilimo, mifugo na uvuvi, akisema kuwa hilo ndilo eneo litakaoleta uchumi wa mtu mmoja mmoja

Hatimaye shughuli za bodaboda, bajaji zilizokuwa vinapigiwa chapuo na viongozi wa chama kongwe dola CCM zimetambulika na kiongozi mkuu wa shughuli za serikali mheshimiwa waziri mkuu kuwa haziwezi kuwa ajiri za kuwakomboa vijana.

Sasa fedha zilizokuwa zinaelekezwa kama mikopo kwa bodaboda na bajaji zielekezwe kununua injini na boti za uvuvi za kisasa, matrekta madogo na makubwa kwa ajili ya kilimo kikubwa cha kisasa pia ufugaji wa kuku, mbuzi ngombe wa kisasa na viwanda vya kusindika mazao ya uvuvi, kilimo na ufugaji yasiharibike na pia kuongozewa thamani kwa masoko ya ndani na nje kwa bidhaa hizo na mazao yake.

Toka maktaba :

7 Oktoba 2022

Rais Samia kuchangia ujenzi ofisi za bodaboda​

Jumapili, Agosti 07, 2022
1691236917113.png

Rais Samia Suluhu Hassan
Rais Samia Suluhu Hassan ameahidi kuchangia fedha za ujenzi wa ofisi za uwakilishi wa bodaboda katika kila mkoa nchini kama ilivyo...

Mheshimiwa rsis Samia Hassan ametoa ahadi hiyo leo Jumapili Agosti 7, 2022 alipozungumza na wananchi wa Kiwira mkoani Mbeya katika ziara yake ya siku nne.

“Vijana wangu wa bodaboda mjipange vizuri muwe na ofisi yenu na ofisi yangu itakuwa tayari kuwachangia,” amesema.
 

Boda boda si kazi, ni laana na umaskini uliopitiliza - Godbless Lema, MP mstaafu, Tanzania​

"Mtoto wa mkubwa yupi anaendesha boda boda? Viongozi wa serikali achene kuwadanganya vijana wetu eti boda boda ni kama kazi nyingine…”​


• "Hiyo ni ajira la laana, ikemeeni. Hamuwezi kufanya ajira ya kukimbiza upepo kwa visenti vidogo kwa siku…." - Lema alisema

Mbunge wa Zamani wa Arusha Godbless Lema akemea bodaboda.

Mbunge wa Zamani wa Arusha Godbless Lema akemea bodaboda.


Mbunge mstaafu wa upinzani nchini Tanzania Godbless Lema amepasua mbarika kuhusu kazi ya kuendesha boda boda ili kujitafutia riziki, kazi ambayo imekuwa kimbilio la vijana wengi wasio na ajira maalum katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Lema ambaye alikuwa mbunge wa Arusha mjini na aliyekimbilia uhamishoni baada ya kutofautiana kisiasa na aliyekuwa rais wa taifa hilo hayati John Magufuli alirejea nchini kwa mara ya kwanza tangu kutoroka mnamo Novemba 2020.
Alitorokea uhamishoni Canada baada ya kudai kwamba maisha yake yalikuwa hatarini na Jumatano wiki iliyopita baada ya kurejea na kupokelewa kwa mbwembwe ya aina yake na maelfu ya watu akiwemo aliyekuwa mgombea urais Kenya, wakili George Wajackoyah, alizungumza.
Katika hotuba yake kwa umma, Lema alisema kuwa serikali imekuwa ikiwahadaa wananchi kwamba Boda Boda ni ajira nzuri tu, lakini kwa upande wake alisema hiyo ni laana kwani hakuna mtoto wa tajiri hata mmoja ambaye amewahi onekana akifanya boda boda kama ajira.


Mbnge huyo wa zamani alkitoa changamoto kwa viongozi wa serikali wanaowaambia vijana kujishughulisha na boda boda kama ajira kuanza na watoto wao kama kweli ni ajira nzuri.
“Sikiliza boda boda, wakati nyinyi mnanipokea kwa shangwe, moyo wangu ulikuwa unahuzunika. Boda boda sio ajira. Ni umaskini unaopitiliza. Hiyo ni ajira la laana, ikemeeni. Hamuwezi kufanya ajira ya kukimbiza upepo kwa visenti vidogo kwa siku…. Mtoto wa mkubwa yupi anaendesha boda boda? Viongozi wa serikali CCM achene kuwadanganya vijana wetu eti boda boda ni kama kazi nyingine…” Lema alifoka.


“Mbona watoto wenu nyinyi hawaendeshi boda boda? Nitajie kuongozi hata mmoja amabye mtoto wake ni dereva wa bodaboda, kama hakuna basi mfahamu kuwa hiyo si kazi ya heshima, ni laana,” Lema aliongeza
 
Back
Top Bottom